Wana JF na Watanzania wenzangu,
Uchaguzi mKUU 2015 ndiyo umemalizika hivo kwa kumpata Rais wa Awamu ya 5 Dr. John Joseph Pombe Magufuli kwa kupata kura 8,892,935 kati ya milioni 13+ waliojiandikisha kupiga kura sawa na asilimia 58 % huku mgombea wa Upinzani Edward Ngoyayi Lowasa akipata kura 6,022,848 sawa na asilimia 39.97% almost 40%.
Kulingana na Takwimu za Tume ya Uchaguzi NEC tuliambiwa Watanzania millioni 22.75 walijiandikisha kupiga kura kati ya Watanzania milioni 48+. Lakini walijitokeza kulingana na matokeo haya ni milioni kama 14.9 tu. Hapa kuna milioni kama 8 hawakupiga kura na milioni nyingine 30+ wala hawakuhangaika na kujiandikisha kupiga kura ukiondoa walio chini ya umri wa miaka 18 kama takwimu hizi ni za kweli!
Rais huyu wa awamu ya 5 lazima aelewe na ajue kuwa ana mzigo mkubwa wa kuliongoza Taifa hili kubwa lenye watu karibia milioni 50. Tunajua wengi waliompa kura ni aidha wafuasi wa CCM au wafuasi wa chama na wasio. Kwa mantiki hiyo Dr. Magufuli hatakuwa Rais wa Watu milioni 8 tu waliompigia kura au wana-CCM pekee wala Wasukuma kabila analotaoka D. Magufuli. Hivo Rais wa awamu hii ya 5 ajue kuwa Watanzania milioni karibia 40 hawakumchagua awe Rais wao na hivo basi hawezi kujisifu wala kujitapa kuwa amepata Ridhaa ya Watanzania wote.
Ushauri kwa Dr. Magufuli ni kwamba lazima afanye kazi kwa unyenyekevu mkubwa kwa kuwaheshimu Watanzania wote waliomchagua na wale ambao hawakumchagua wakiwemo Wapinzani wake Kisiasa. Kama atatumia busara na hekima basi awashirikishe Wapinzani kwa maana ya vyama vya siasa ambavyo wamepata kura zaidi ya milioni 6 kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayo saidia kuondoa manung'uniko, malalamiko na chuki za kisiasa ili nchi isonge mbele kiuchuni, kielimu na kiafya. Tanzania siyo ya Magufuli wala CCM ni ya Watanzania wote milioni 50!
Nawasilisha.