Na mimi ni mpongeze rais mteule wa JMT.
ilikuwa kwa makusudi na mie nianzishe uzi kama huu kwa minajili ya kumshauri mh rais mteule kama atakuwa ni msikivu na kuwasikiliza watu wake, sasa nitatumia uzi huuhuu.
na anza hivi:
1. Kila ulipoenda umeahidi jambo/mambo. ahadi zako ni nyingi mno, kwa maana halisi ya uwingi.
kwasababu hiyo vipaumbele vyako vitakuwa vingi mno. ili uweze kutekeleza vipaumbele vitakavyo leta tija haraka lazima uwe na vipaumbele vya vipaumbele nadhani nimeeleweka hapa.
2.ulijifunga kwa maneno ya kinywa chako,"utamtanguliza MUNGU mbele kwa kila jambo, haya maneno si ya mzaha hata kidogo. then utawatanguliza watanzania. Lazima na huna budi kuZingatia sana haya maneno ya kinywa chako kwa dhati ya moyo wako, vinginevyo......!
sasa na kuomba umtangulize Mungu katika kuunda serikali yako, ukikosea hapo ndio utakuwa mwanzo mbaya kwako.
najua kuna mashinikizo sana kutoka sehemu na watu mbalimbali, sikiliza ushauri kwa wanao kushauri, ufanyie kazi, take your time katika kunda serikali yako na maamuzi ya mwisho yawe yako.
3. tumesikia kwenye kampeni kuwa kuna kuhujumiwa, ukasema,"kuna watu mchana ccm usiku huko kwingine" lazima ushuhulike na hili tatizo haraka, tena mapema na kwa umakini wa hali ya juu sanq. kama kulikuwa na hujuma wakati wa kampeni ni dhari zitaendelea wakati wa uongozi wako ili ushindwe.
4. washauri wako.
najua unawashauri wako kwa mujibu wa katiba mbao wako katika nyanja, taaluma na sekta mbalimbali, wathamini sana hao na watumie vilivyo. katika kutumia ushauri wao tafuta sana hekima ya Mungu ili kuujua ni upi ushauri bora utakao lifaa taifa na wewe kama kiongozi.
lakini katika hili la washauri tafuta pia ushauri sehemu nyingine au kutoka kwa washauri wengine. ukiupata huo ushauri uje uwashirikishe wale wa team yako serikalini. Yale ambayo mtaona yana manufaa kwa ustawi wa taifa basi mnangalia jinsi ya kuyatekeleza.
vilevile kwa maoni yangu ni vizuri ukawa na washauri wa kiroho. ingawa wewe ni rais wa watanzania wote lakini si vibaya atleast ukapata washauri kutoka katika dini hizi mbili, uislamu na ukristo ili upate hekima ya washauri hawa hasa jinsi ya kuwaongoza watu kwa haki.
ila siku hizi za mwisho wako manabii wa uongo, angalizo usije kuangukia huko. uzuri tuna ambiwa tutawatambua kwa matendo yao, ya kiwemo yale ya kutumia neno la Mungu kujinufaisha wao.
5. Hili la kuhusu kuanzisha mahakama ya mafisadi.
ni kweli ufisadi ni tatizo kubwa kitaifa, ni janga.
lakini ningeomba ni kushauri jinsi ya kushughulika na hili tatizo.
mtazamo wangu ni kuwa, unge anza kushuhulika na ufisadi kwa kutunga sheria ya kuunda tume ya maridhiano kitaifa, maana ufisadi ni uhalifu ambao umeachwa kwa kipindi kirefu na una mizizi mirefu sana. kuwa wale watakao husishwa na ufisadi waje katika tume hiyo, wakiri, waeleze ukweli wao na jinsi walivyo jinufaisha na kuwa umiza wananchi wengine. warudishe sehemu ya manufaa yao kwa jamii iliyo adhirika kwa huo ufisadi. wakifanya hivyo basi wasamehewe kumbuka ulikuwa unasema,"samehe saba mara sabini kwenye kampeni". atakaye kataa sasa ndio aende kwenye hiyo mahakama kufuata mkondo wa sheria. hii ilifanyika huko SA kushuhulika na wahalifu wa ubaguzi wa rangi.
wakati hii tume ikifanya kazi, sambamba nayo taasisi za kupambana na rushwa ziimarishe na elimu kwa wananchi ya kuchukia na kupiga vita rushwa iimarishwe kwa kutumia raslimali za serikali sio wafadhili.
6. Katiba mpya.
Hili mimi sikukusikia ukilisemea kwenye kampeni.
lakini kama unavyosema,"ukweli lazima usemwe na msema kweli mpenzi wa Mungu" basi ukweli ni kuwa suala la katiba mpya haliepukiki, halipotelezeki. Hii ni changamoto ambayo utakutana nayo katika uongozi wako, upende usipende.
Ushauri wangu....
Itaendelea......!