Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Kesho magazeti cjui yataandikaje..

Uhuru: NI MAGUFULI

Habari Leo: MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO

Tanzania Daima: LUBUVA ATETEMEKA WAKATI AKIMTANGAZA MAGUFULI KUWA RAIS

Jambo Leo: HAPA KAZI TU, MAGUFULI RASMI RAIS WA AWAMU YA TANO.

Nipashe: UKAWA WAPINGA MAGUFULI KUTANGAZWA MSHINDI. LOWASSA: NIMENYANG'ANYWA USHINDI
 
Pia suala la elimu naona ndo kipaumbele hapa Tanzania. Elimu iboreshwe, wasomi wawe na uwezo wa kuunda vikundi vya uzalishaji mali na kuweza kukopa mtaji kwa dhamana ya serikali.

Pia, kuna umuhimu mkubwa sana wa kuendeleza wajariamali na viwanda vya ndani kwa kutumia malighafi za ndani kuliko kuagiza nje. Pia, kodi inatakiwa iongezeke kwa bidhaa za nje pale zinapokuwa na uwezo wa kupatikana ndani ya nchi ili kukuza viwanda vya ndani na vya wazawa.
 
hongera sana Rais wangu John Pombe Magufuli, Mungungu akutangulie kwenye kila ulifanyalo. Mungu ibariki Tanzania.
 
Tumeridhika cc kulala sakafuni kuliko kuwapa wanafiki Nchi yetu, Tuliwagundua mlipokuwa mnakemea Ufisadi kinafki , Ngastuka.....
 
Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya 5 baada ya kuongoza kwa kupata kura 58.46%.

attachment.php


Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343.

Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba

  1. Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  2. Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza

===========

Kutoka kwa mwandishi wa FikraPevu

Mbona hiyo idadi ya kura za wagombea ni nyingi kuliko idadi ya kura halali kwa mujibu wa hiyo habari ya FikraPevu?..."mmepanga kuleta uchochezi"..."mmekosea bahati mbaya"...au ndo Lubuva alivotangaza hivyo?...(ukiwa mvivu kujumlisha zote basi jumlisha tu hata za Magufuli na Lowassa)
I stand to be corrected.
 
Uhuru: NI MAGUFULI

Habari Leo: MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO

Tanzania Daima: LUBUVA ATETEMEKA WAKATI AKIMTANGAZA MAGUFULI KUWA RAIS

Jambo Leo: HAPA KAZI TU, MAGUFULI RASMI RAIS WA AWAMU YA TANO.

Nipashe: UKAWA WAPINGA MAGUFULI KUTANGAZWA MSHINDI. LOWASSA: NIMENYANG'ANYWA USHINDI

Hiyo namba tatu naisubiria kwa hamu!!
Wanasema usianzise ugomvi wa mawe ikiwa unaishi kwenye nyumba ya vioo lakini hii minyumbu ina uthubutu, ina ujasiri kweli....
 
Dr. John Pombe Magufuli ametangazwa rasmi kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya 5 baada ya kuongoza kwa kupata kura 58.46%.

attachment.php


Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343.

Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba

  1. Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
  2. Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza

===========

Kutoka kwa mwandishi wa FikraPevu


Idadi ya kura zilizopo hapa zinakinzana na zilizopo ktk tovuti ya NEC. Je nani anatuvuruga?
 
Acha akili za kilofa ww.mm naamini katika denokrasia.watanzania walio wengi(majority) wamemuamini JPM kama mtu sahihi kwao wa kushughulika na shida zao.kwahiyo husijifanye unajua sana kuliko watanzania mil8 waliofanya maamuzi.na kujifanya unataka kukosoa maamuzi yao.piga kimya liache tingatinga lifanye kazi aliyopewa na watanzania
Kumbe tumechagua tingatinga! Ama kweli watanzania tuna bahati mbaya. Ina maana hakukuwa na watu mpaka tukaamua Tingatinga ndio lituongoze! Kweli hii ni nchi ya malofa.
 
Ikumbukwe kuwa LOWASSA alikatwa akiwa ndani ya ccm,pili alihama baada ya kukatwa huko alikoenda nako watanzania wamemfuata wakamkata tens je ni ishara kuwa wtz hawependi kuongozwa na LOWASSA?
 
EL ndo angeweza?? Kama vp hama nchi!
Yaani nihame kwenye ardhi ya mababu zangu toka kale eti kisa ninaikimbia CCM! Ndivyo mnavyojidanganya kwamba nchi hii ni mali ya wanaCCM peke yao ne wengine wote hawana haki ya kuendelea kuishi hapa. Kweli CCM ni chama cha Mashetani.
 
Na mimi ni mpongeze rais mteule wa JMT.

ilikuwa kwa makusudi na mie nianzishe uzi kama huu kwa minajili ya kumshauri mh rais mteule kama atakuwa ni msikivu na kuwasikiliza watu wake, sasa nitatumia uzi huuhuu.

na anza hivi:

1. Kila ulipoenda umeahidi jambo/mambo. ahadi zako ni nyingi mno, kwa maana halisi ya uwingi.

kwasababu hiyo vipaumbele vyako vitakuwa vingi mno. ili uweze kutekeleza vipaumbele vitakavyo leta tija haraka lazima uwe na vipaumbele vya vipaumbele nadhani nimeeleweka hapa.


2.ulijifunga kwa maneno ya kinywa chako,"utamtanguliza MUNGU mbele kwa kila jambo, haya maneno si ya mzaha hata kidogo. then utawatanguliza watanzania. Lazima na huna budi kuZingatia sana haya maneno ya kinywa chako kwa dhati ya moyo wako, vinginevyo......!

sasa na kuomba umtangulize Mungu katika kuunda serikali yako, ukikosea hapo ndio utakuwa mwanzo mbaya kwako.

najua kuna mashinikizo sana kutoka sehemu na watu mbalimbali, sikiliza ushauri kwa wanao kushauri, ufanyie kazi, take your time katika kunda serikali yako na maamuzi ya mwisho yawe yako.

3. tumesikia kwenye kampeni kuwa kuna kuhujumiwa, ukasema,"kuna watu mchana ccm usiku huko kwingine" lazima ushuhulike na hili tatizo haraka, tena mapema na kwa umakini wa hali ya juu sanq. kama kulikuwa na hujuma wakati wa kampeni ni dhari zitaendelea wakati wa uongozi wako ili ushindwe.

4. washauri wako.

najua unawashauri wako kwa mujibu wa katiba mbao wako katika nyanja, taaluma na sekta mbalimbali, wathamini sana hao na watumie vilivyo. katika kutumia ushauri wao tafuta sana hekima ya Mungu ili kuujua ni upi ushauri bora utakao lifaa taifa na wewe kama kiongozi.

lakini katika hili la washauri tafuta pia ushauri sehemu nyingine au kutoka kwa washauri wengine. ukiupata huo ushauri uje uwashirikishe wale wa team yako serikalini. Yale ambayo mtaona yana manufaa kwa ustawi wa taifa basi mnangalia jinsi ya kuyatekeleza.

vilevile kwa maoni yangu ni vizuri ukawa na washauri wa kiroho. ingawa wewe ni rais wa watanzania wote lakini si vibaya atleast ukapata washauri kutoka katika dini hizi mbili, uislamu na ukristo ili upate hekima ya washauri hawa hasa jinsi ya kuwaongoza watu kwa haki.

ila siku hizi za mwisho wako manabii wa uongo, angalizo usije kuangukia huko. uzuri tuna ambiwa tutawatambua kwa matendo yao, ya kiwemo yale ya kutumia neno la Mungu kujinufaisha wao.

5. Hili la kuhusu kuanzisha mahakama ya mafisadi.

ni kweli ufisadi ni tatizo kubwa kitaifa, ni janga.

lakini ningeomba ni kushauri jinsi ya kushughulika na hili tatizo.

mtazamo wangu ni kuwa, unge anza kushuhulika na ufisadi kwa kutunga sheria ya kuunda tume ya maridhiano kitaifa, maana ufisadi ni uhalifu ambao umeachwa kwa kipindi kirefu na una mizizi mirefu sana. kuwa wale watakao husishwa na ufisadi waje katika tume hiyo, wakiri, waeleze ukweli wao na jinsi walivyo jinufaisha na kuwa umiza wananchi wengine. warudishe sehemu ya manufaa yao kwa jamii iliyo adhirika kwa huo ufisadi. wakifanya hivyo basi wasamehewe kumbuka ulikuwa unasema,"samehe saba mara sabini kwenye kampeni". atakaye kataa sasa ndio aende kwenye hiyo mahakama kufuata mkondo wa sheria. hii ilifanyika huko SA kushuhulika na wahalifu wa ubaguzi wa rangi.

wakati hii tume ikifanya kazi, sambamba nayo taasisi za kupambana na rushwa ziimarishe na elimu kwa wananchi ya kuchukia na kupiga vita rushwa iimarishwe kwa kutumia raslimali za serikali sio wafadhili.

6. Katiba mpya.
Hili mimi sikukusikia ukilisemea kwenye kampeni.

lakini kama unavyosema,"ukweli lazima usemwe na msema kweli mpenzi wa Mungu" basi ukweli ni kuwa suala la katiba mpya haliepukiki, halipotelezeki. Hii ni changamoto ambayo utakutana nayo katika uongozi wako, upende usipende.

Ushauri wangu....






Itaendelea......!
 
kama mtu anakataa kupata elimu unategema nini hapo???,

1. Watu hao waliokataa elimu ya bure hawana hata uwezo wa kupata milo 3 kwa siku
2. ....................hawana hata nyumba ya tofali
3. ............................................wanakufa kwa kukosa panadol
4............................................hawana hata viatu vya kutembelea jambo ndala za tsh 1000
5.........................................wanakunywa maji machafu anayokunywa punda (mifugo)
6. ......................................................................................
7. ...................................................................
,...............................................................

Umaskini wa mwili na akili ndio mtaji wa ccm, ccm itatawala milele;
 
Mtu akizoea shida sanaa anakua rafiki wa shida, akipewa kitenge cha kijani, kofia, tishet na elfu kumi anauza utu wake..
 
Back
Top Bottom