Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Elections 2015 Dr. Pombe Magufuli, Rais mteule wa Tanzania awamu ya 5

Niliisha andika huko nyuma kwamba CCM ikishinda ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu na Chadema chini ya Lowassa ikashindwa, hakuna kingine kitakachofuata na huo utakuwa ndio mwisho wa Chadema.

Kwa msingi huo itakuwa ni ndoto kwa Chadema kushika dola ndani ya miaka 50. Subirini muone.

Nadhani Lowasa kachanganyikiwa-kwani nimesikia anasema eti tume imtangaze yy kwani matokeo yake yanaonyesha kuwa kashinda kwa 62% huyu jamaa ni mbabe kiasi cha kuamuru tume imtangaze kwa data zake za nyumbani kwake.
 
Hongera Magufuli kwa zali ulilopata maana hakika ni zali. Kila la heri ktk kutimiza kauli mbiu ya HapaKazi Tu
 
Nitapiga kura kama kutakuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

+ uwezekano wa kuhoji matokeo mahakamani. Labda hapo nitashawishika. Ila CCM hii iliyorudi madarakani tena na wabunge wengi unafikiri kweli itatuletea hayo? Mie nadhani itapigwa photocopy katiba hii halafu iitwe katiba mpya. Maana mfumo huu ndio unawaweka madarakani.
 
uliwavumilia pindi walipoliondoa jina lako kwa hila ulipokuwa kwao,lakini ukukata tamaa kwa kuwa ulikuwa na lengo halisi la kuikomboa nchi yako,safari yako ya matumaini ikageuka kuwa safari ya mabadiliko lakini bado tena ulitukanwa,ukadhihakiwa mpaka na MATASA,wajinga,na vijana wenye ndimi za fila,ukavikwa joho la ufisadi kama yesu alivyovikwa taji la miiba lakini bado ulivumilia,kwa kweli ulivumilia,lakini cha kushangaza safari hii tena wamepola ushindi wako na wewe bado upo kimya?mpaka lini kipenzi chetu EDO?sema kitu basi nasi tutafanya,mbona European obsevers wamekuandalia njia?mbona US ipo upande wako?mbona kagame yupo upande wako?na zaidi ya hayo sisi vijana tupo upande wake?tunajua umeshinda lakini haki haiji bila ya upanga.sema kitu EDO,sema basi!!
Indeed
 
Usitukate stim acha tusheherekee tuliomchagua hayo mengine sio kazi yako ushauri wako kampe uiyempigia kura Magufuli anayo Ilani na itamwongoza kwa kuanzia. Ya Kitaifa ndio inayoleta shida Znz mwacheni Jembe ajiachie magogoni kama msuli alishatumia sana Ujenzi, Uvuvi na Ardhi.

Hapa kazi tu, ukitaka mabadiliko kzungushe mikono na Lowasa wenu aliyegawa Taifa hili kwa ubaguzi.
 
Alikwisha sema bana -- Matumaini-- Mabadiliko --- Monduli-- Labda kama hukumsikia
 
CHAMA TAWALA kinabeba lawama 80% (kinatumia madaraka yake kuzidi kuwafanya wananchi wewe misukule, tena makusudi, ili kitawale milele. Na hata pale ambapo wananchi wamebadilika na kuchagua upinzani, kinatumia vhyombo vyake vya dola kufanya uchakachuzi)
WANANCHI nao wanabeba lawama 15% ( sidhani kama wananchi wa Tanzania wana tofauti na wa Kenya au Zambia. Asilimia kubwa ni waoga wa mabadiliko. Na uoga huo unahusiana na propoganda za chama tawala)
UPINZANI unaweza kuwa nao unabeba lawama 5% (kwa hakika vyama vya upinzani kimoja kimoja na katika muungano wao wa UKAWA wamejitahidi sana kutoa elimu ya uraia na ushahidi ni ukombozi wa jiji mama wa majiji ya Tanganyika, DSM. Lakini hawajaweza kufanya kazi nzuri kuwafikia wananchi katika ngome za chama tawala kv mikoa ya kati na kusini. Pia hawakupaswa kupoteza majimbo ambayo tayari yaliishakuwa ngome zao. kulikuwepo na upungufu wa kimkakati kuhusu ushindi)

Sioni kitufe cha like
 
Nchi hii ina wajinga wengi sana unaomba chama cha upinzani kife ili iweje?vyama vya upinzani ndo vimefanya watz waijue serikali yao ilivyo ktk utendaji mimi kwa mtazamo wangu ningeomba viimarike ili serikali iwe makini.Nilikuwa na mengi ya kukuelimisha lakni muda sina ahsante

Asante. Bahati mbaya sana watz wengi hawajui hili wengine wanaombea vyama vya upinzani vife... Especially kwa nchi changa kama zetu -Ili chama tawala kifanye vizuri kinahitaji upinzani imara, na hapo ndo wananchi tunapata maendeleo! This is political ecology!
 
Chadema fisadi itakufa itarudi chadema Asili Nccr itabikia kusomwewa kipa imara
 
Lawama Kwa Hawa:-
Nec
Police
Ccm
Jk
Na Wote Waliounga Mkono Wizi Wa Kura Mpaka Uchaguzi Umekuwa Na Makando Kando
 
Cummon mods mbona mmeunganisha uzi ambao hauhusian ni hii mada, yaan hata baada ya matokeo bado mnaendelea kutunyanyasa na forum yenu
 
.huku vijana washaingia barabarani wanaimba " wamechinja KUKU, tumechinja NG'OMBE DUME" na zaidi kuna mmoja wao kapitiwa na gari, ndo anakimbizwa Hospitalini mda huu..

Pole yake na hivi hakuna dawa ndio atatia akili!
 
Alisema yeye ni muadilifu.Uadilifu wake u wapi wakati kaingia kwa wizi? Serikali ijayo itakuwa na
wizi kuliko zote zilizopita.
 
Hata Magufuli anajua kuwa hakushinda kihalali na asifikiri kuwa ndio imepita ,upinzani wa leo ni mkubwa sana na atakaposimama ,kwa kweli atakuwa hana nguvu ,kwani ukweli unajulikana kama hakushinda ,haya tusubiri ale hicho kiapo kwa Mungu wake ili aanza kupokea adhabu ya kuongopa mbele ya Mungu.

Unafikiri kiongozi aneshinda kwa hila atakuwa na habari na huruma na wewe ,hata kama upo CCM ,hivi anakujua wewe kama ndie uliempa kura ,marungu yanayokuja hayatawakumba wapinzani bali kwa kweli watakaoumia zaidi ni wale waliosheherekea ushindi usio wa kihalali. Hii ndio siri watakaoumia na kujuta ni ccm na mapolisi.

Magufuli kachaguliwa na watanzania walio wengi na wala hakukuwa na wizi wa kura. Au kwako wewe ushindi ni ule ti wa mgombea wako hata kama watu wamemkataa. Watanzania wasingempatia kura kwa kuwa wanapenda nchi yao. Fanyeni kazi acheni kushinda mitandaoni. Hapalipi na maendeleo utayaonea kwa jirani.
 
watatunyanyasa sana hawa jamaa m nawaza hadi naogopa yaan.

wala usiwaze mkuu great presidents never do that,,, utashangaa kawa rafiki wa ambao hawakumpigia kura zaid ya waliompigia.. mwisho wa siku ana nchi moja tu ya kujenga!
 
VIJANA wetu bado wanafanya tallying na kuandika historia ya nchi hii!
 
Back
Top Bottom