MjuviKitambo
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 711
- 811
RIP Dr. Mvungi hata
mimi amenifundisha Jurispudence. Inabidi ulinzi uimarishwe pembenzoni
mwa Dar mfano Goba walimkata mapanga yangu mmoja kwa kuanza na mkato wa
msalaba kichwani, mguu na mkono walishindwa kuvitenganisha kasha
wakamalizia kwa kumng'oa meno manne (4). Mstaafu mmoja alilawitiwa mbele
ya familia na mkewe kubakwa hadharani. Miezi miwili imepita haijulikani
kama huyu Mzee amejiuwa au amehama jiji. Hii nguvu ya kung'oa kucha;
meno na jicho dhidi ya akina Dr. Ulimboka na Kibanda tungeilekeza huko
Goba; Mbezi Mpigi na maeneo yote hatarishi hapa Dar na kwingineko
nchini.
kuna mtu namweleza habari hata hampati mvungi so kama kuna mtu anapicha yake aiweke jamani ili nimweleweshe rafiki yangu amjue japo ameshatutoka
pamoja na wale wote waliosuka njama hizo na vizazi vyao.
Mimi bado niko na majambazi waliohusika:
Je watu walioshikwa ni wenyewe kweli?
Ni Watanzania wenzetu?
Nia yao ya msingi ilikuwa kuua au kuiba!?
Wanamtumikia nani?
Je tutaambiwa ukweli wa mkasa huu wa kikatili?
Je kuna tume imeundwa kufuatilia, au tuwaamini polisi wetu?
Wajumbe wa tume mnamsemeaje Mvungi kule kwenye tume?
Je alikuwa na misimamo hasi sana?
Je alikuwa Mwiba kwa mtu, chama au taasisi yoyote?
Mawasiliano yake ya mwisho aliongea na watu gani?
Samahani wadau, najua si muda muafaka, lkn imeniumiza sana kiasi naona majibu ya haraka yanatakiwa.
Haiwezekani tupoteze wasomi manguli wa aina ya Dr. Mvungi, halafu tuone kawaida tu!
Ni huzuni kwa Taifa kwani masahibu yaliyopelekea umauti yanatokana na kazi ya kuhuisha roho ya Taifa (Katiba ya Nchi). Mungu ailaze roho yake mahala pema.
Bila Kumungunya MACCM wanahusika.
Kwa vyovyote vile.
Na sijuhi ni Intelejensia ya wapi inashindwa kuwapata hawa wauaji.
Tumushuhudia watalii wakiibiwa porini na chopa ikatumwa na wahalifu wakapatikana.
Tumeshuhudia Waziri Mzinzi akibiwa na Vibaka kushirikiana na Changudoa na wahalifu walipatikana.
Inakuwaje kwenye hili unaenda kukamata Wanywa Gongo alafu unasema wahalifu wamepatikana.
Nahisi mhusika ni yuleyule Rama.