TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Furaha ya milele uumpe ee bwana,
na mwanga wa wa milele umuangazie,
apumzike kwa amani ,
amen!
 
RIP Dr. Mvungi hata
mimi amenifundisha Jurispudence. Inabidi ulinzi uimarishwe pembenzoni
mwa Dar mfano Goba walimkata mapanga yangu mmoja kwa kuanza na mkato wa
msalaba kichwani, mguu na mkono walishindwa kuvitenganisha kasha
wakamalizia kwa kumng'oa meno manne (4). Mstaafu mmoja alilawitiwa mbele
ya familia na mkewe kubakwa hadharani. Miezi miwili imepita haijulikani
kama huyu Mzee amejiuwa au amehama jiji. Hii nguvu ya kung'oa kucha;
meno na jicho dhidi ya akina Dr. Ulimboka na Kibanda tungeilekeza huko
Goba; Mbezi Mpigi na maeneo yote hatarishi hapa Dar na kwingineko
nchini.

mmmm
tutahama majumbani mwetu sasa.. na sijui tutahamia wapi. hakuna kuliko salama. Ee Mungu utasaidie.
 
kuna mtu namweleza habari hata hampati mvungi so kama kuna mtu anapicha yake aiweke jamani ili nimweleweshe rafiki yangu amjue japo ameshatutoka

images
 
Sad! Too Sad!!! Pumzika kwa Amani Dr. Mvungi...Pole kwa wanafamilia na watanzania kwa ujumla
 
R.i.p Dr huu ndio mwisho wa kila binadamu! Hata walio kutenda nao wana siku yao!
 
Hao "Majambazi" ndio hao hao walitaka kutoa roho za Dr Ulimboka,Kibanda etc.

What a shame this country!!!
 
Upumzike pema peponi.Watanzania tuyaenzi mazuri yake yote.Tumepotelewa na Mtu mhimu sana hapa nchini
 
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka
 
Ooh my God! Aaah! Nimesonokeka sana. Watanzania tukatae ukatili huu,..
Pole familiya ya Dr Mvungi
pole NCCR Mageuzi
poleni watanzania.
R i p dr Mvungi
 
Mimi bado niko na majambazi waliohusika:

Je watu walioshikwa ni wenyewe kweli?

Ni Watanzania wenzetu?

Nia yao ya msingi ilikuwa kuua au kuiba!?

Wanamtumikia nani?

Je tutaambiwa ukweli wa mkasa huu wa kikatili?

Je kuna tume imeundwa kufuatilia, au tuwaamini polisi wetu?

Wajumbe wa tume mnamsemeaje Mvungi kule kwenye tume?
Je alikuwa na misimamo hasi sana?
Je alikuwa Mwiba kwa mtu, chama au taasisi yoyote?

Mawasiliano yake ya mwisho aliongea na watu gani?

Samahani wadau, najua si muda muafaka, lkn imeniumiza sana kiasi naona majibu ya haraka yanatakiwa.

Haiwezekani tupoteze wasomi manguli wa aina ya Dr. Mvungi, halafu tuone kawaida tu!

Na huu mtindo waliouanzisha police wakukamata watuhumiwa bila ya kuwaonyesha kwenye TV bado nakuwa na mashaka juu ya ukweri.
 
Ni huzuni kwa Taifa kwani masahibu yaliyopelekea umauti yanatokana na kazi ya kuhuisha roho ya Taifa (Katiba ya Nchi). Mungu ailaze roho yake mahala pema.

Ni huzuni kubwa sana Poleni wote mlioguswa na msiba huu
 
Allah ailaze roho yake mahala panapostahili....
 
Hawawataki Tume Ya katiba sasa wanauwa wajumbe. Mzee warioba Mungu akulinde
 
Bwana AMEETOA na Bwana AMETWAA.Polen ndugu,jamaa,marafiki.TUTAKUKUMBUKA DAIMA DR.MVUNGI
 
Bila Kumungunya MACCM wanahusika.
Kwa vyovyote vile.
Na sijuhi ni Intelejensia ya wapi inashindwa kuwapata hawa wauaji.

Tumushuhudia watalii wakiibiwa porini na chopa ikatumwa na wahalifu wakapatikana.

Tumeshuhudia Waziri Mzinzi akibiwa na Vibaka kushirikiana na Changudoa na wahalifu walipatikana.

Inakuwaje kwenye hili unaenda kukamata Wanywa Gongo alafu unasema wahalifu wamepatikana.

Nahisi mhusika ni yuleyule Rama.

Tenaaaaa
 
Neno la kwenye biblia limetimia.

"Kwa jasho la uso utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe ni mavumbi na mavumbini wewe utarudi" (Mwanzo 3:19).

"Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo" (Yohana 14:2)
 
Back
Top Bottom