kama hii ni fact.....rip mtu mzima muvungi..tutakuombea daima
It is a fact. He is no more.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kama hii ni fact.....rip mtu mzima muvungi..tutakuombea daima
Kwa kuwa ni lazima tufe basi kila mtu ataondoka kwa namna yake, yaliyobaki tunamuachia mola kwa misingi ya wale wanaoamini kuwepo kwa muumba mbingu na inchi
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka
Kitu ambacho siwezi kuafiki juu ya madhira yaliyomkumba Dr.Mvungi kuwa yote haya yalifanywa hili kukwapua simu na laptop au kopora fedha.Ni kitu ambacho kamwe sitokaa kuafiki,nadhani kuna motive kubwa zaidi ya vitu tajwa hapo juu,ukizingatia jukumu alilokabidhiwa lilikuwa ni muhimu na nyeti kwa mustakabali wa taifa letu.Kifupi waliotenda unyama huu walikusudia na inawezekana kuna mtu aliyesanifu na kufadhili unyama huu Kwa maslahi yake au taasisi aliyomo.RIP doctor.
Labda mimi nipingane na wewe kwa sababu nilishawahi kuwa muhanga wa yaliyomkuta mvungi ! Sema kwa kuwa wahanga wanakua ni watu wa kawaida polisi wanapiga kimya ,!! Nikiwa nyumbani kwangu kibamba nilivamimwa na majambazi wakatukata mapanga nyumba nzima, isingekuwa wazo la kuweka mikono kichwani basi ,probably nisingekuwa hapa kuandika posti hii hata hivyo nimepoteza vidole viwili mhimu mkono wa kulia .
Lakini kuna mazingira yanapromote sana aina hii ya ujambazi ,ikiwemo kujenga mbali na majirani au kujenga karibu na watu wanaomiliki maeneo makubwa bila kuyaendeleza,
dah?!
ccm ni zaidi ya shetani!
Kitu ambacho siwezi kuafiki juu ya madhira yaliyomkumba Dr.Mvungi kuwa yote haya yalifanywa hili kukwapua simu na laptop au kopora fedha.Ni kitu ambacho kamwe sitokaa kuafiki,nadhani kuna motive kubwa zaidi ya vitu tajwa hapo juu,ukizingatia jukumu alilokabidhiwa lilikuwa ni muhimu na nyeti kwa mustakabali wa taifa letu.Kifupi waliotenda unyama huu walikusudia na inawezekana kuna mtu aliyesanifu na kufadhili unyama huu Kwa maslahi yake au taasisi aliyomo.RIP doctor.
Maneno yako yana ukweli ulitulia 100% mkuu, heri kule kuliko huku kwenye mateso mengi hasa majeraha ambayo yangemsababishia depression.
Tangulia baba wengi tupo nyuma yako twaja! Yamekwisha!!
Msiba Tume ya Katiba: Dk. Sengondo Mvungi afariki Duania Afrika ya Kusini
R.I.P Sengondo Mvungi (PhD)Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia. -
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark. -
"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali. -
"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza. -
Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013. -
Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka