TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Sina uhakika kama kweli wewe akiri zako ni timamu.....utaendelea kuwa mpuuzi ktk maisha yako yote yaliyobakia hapa duniani.....try to hv a reasoning ability even though common sense z not common to every one like u......mnayo serikali mbona hamjawakamata hao cdm?

aheri mi nisiye na akili,kulikon ww mwenye nazo lakin umezikalia!!narudia tena kamwe hatutanyamazia upumbav na upuuzi mnaowafnyia wananchi.Chadema mauwaji yote yakutatanisha nyie ndo mnaohusika,na nawahakikishien hamtakaa muingie ikulu kuongoza nchi.mtaishia kwenda kunyw juice tu wauwaji wakubwa nyie.
 
Watu muhimu kama huyu wangehamishwa City centre kuna usalama sio mwituni. Wahindi sio wajinga kukaa jijini.
 
[RIP DoctorQUOuTE=Donyongijape;7801969]Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia. -

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark. -

"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali. -

"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza. -

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013. -

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.[/QUOTE]
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salaam za rambirambi ya kifo cha Dkt. Edmund Sengondo Mvungi, akitoa pole kwa familia, uongozi na wanachama wa NCCR-Mageuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na wananchi wote walioguswa na msiba huo.



Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wa chama hicho, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi, akimwelezea kuwa alikuwa mwanasiasa mwenye msimamo ambaye hakuwahi kutetereka kusimama na chama chake tangu alipojiunga nacho na kuanza kushiriki siasa za mageuzi nchini.



“Kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wetu nchi nzima, napenda kutoa salaam za pole sana kwa familia ya marehemu, mjane na watoto. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wa chama hicho, pia tunatoa pole kwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba na makamishna wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakifo cha Dkt. Mvungi. Tunaomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu sana wakati huu wa majaribu na majonzi makubwa.



“Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema.

"Mvungi pia alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa kupigania nchi yetu iwe na Katiba Mpya, ili hatimaye siasa zetu, hususan demokrasia ya vyama vingi nchini iendeshwe kwa misingi iliyo imara,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;



“Mwenyezi Mungu alimjalia marehemu akaweza kushiriki kutimiza ndoto hiyo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Mpya, kazi ambayo ameifanya hadi siku alipokutwa na tukio lililosababisha mauti yake.”



Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, amesisitiza kuwa kwa namna ambavyo Dkt. Mvungi alikuwa mstari wa mbele katika suala hilo, Tume ya Katiba Mpya inao wajibu wa kuthamini mchango wake katika hatua iliyofikia sasa ya mchakato huo nyeti hadi utakapofika mwisho.



“Wakati tukimwombea marehemu kwa Mungu, alazwe mahali pema peponi, ni matumaini yetu kuwa serikali kupitia vyombo vyake itahakikisha kuwa wale wote waliohusika katika tukio la lililosababisha kukatisha uhai wa Dkt. Mvungi wanapatikana na kuchukuliwa hatua zote zinazostahili kisheria,” amesema Mwenyekiti Mbowe.
 
Bila shaka Ccm ndo watakuwa wa kwanza salamu za rambi rambi! Tusisahau pia kuwa Ccm ni mabingwa wa kuhudhuria misiba ya watu maarufu.

Lakini je wanaweza kujinasua na kifo hiki? Kama mjumbe wa tume ya katiba anauwa na vibaka itakuwaje kwa raia wa kawaida? Wajumbe wa tume wamekuwa wakilindwa muda wote imekuwaje kwa Mvungi? Au ni baada ya kupendekeza serikali tatu?

Lakini uvamizi huu tunautofautishaje na wa Kibanda au Ulimboka? Je tunakumbuka maneno aliyosema Mbatia bungeni? Kwa nini haridhiki kwamba ule ni uvamizi wa majambazi kawaida?

Tutarajie mkanda wa mkenya mwingine kuhusishwa au mara hii atakamatwa mchina, maana juzi tuliona wa pembe za ndovu msishangae kuona wa mauaji!
 
Kanusu kakweli akili mgando" !Kwara nyingine jina lako linasadifu ulivyo.Kweli akili kanus
 
Tunamwombea marehemu Mvungi apumzike mahala pema peponi,Ameeen.
 
Kama ni wanangu, najua hawatakufa kwa kukosa chakula.
Wataishi, watakula na Watasoma...after all mke wangu yupo nao, atawatunza. Zaidi sana nina marafiki...hivi wanaweza kuninyanyapaa kisa nimehamia upande huu??, sidhani.

Nawaahidi kuwa Tanzania itapata Katiba nzuri tu, kuondoka kwangu kutalipia gharama ya katiba.

Jipeni moyo Watanzania.
Nawapenda sana.

Huku nilipo ni pazuri. Ni pazuri sana. Msinihofie mimi.
Angalieni zaidi mchakato wa Katiba.

Naamini siku isiyojulikana tutaunganishwa tena...sijui itakuwa katika umbo au hali gani, lakini ni ukweli dhahiri.

Ahsanteni.

Nimetokwa na machozi ndg, kwa kweli... Acha tu.
 
“Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema.


Hivi yule wa Arusha alikuwaga chama gani vile?? kwa hiyo Mbowe anatuaminisha Lema hakuwa na msimamo eeee??? ahsante Kamanda Mbowe kwa ufafanuzi huu

RIP dk Mvungi
 
very sorry Tanzania...........Nchi yetu imempoteza mtu muhimu sana katika wakati muhimu sana.......R.I.P Dr Mvungi
 
Back
Top Bottom