TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Ooh, Dr. Mvungi,
Uliponambia ndoto yako ya kuona taifa linakuwa na katiba mpya unaiona ikitimia wakati wa uhai wako, sikujua kuwa hayo ndio maneno ya mwisho kwangu kutoka kwako...
Machungu ya kukupoteza yananielemea. Nakuombea kwa Mungu akupe pumziko jema milele, amina.

Poleni wanafamilia,
Poleni Tume ya Katiba
Poleni Chuo Kikuu cha Bagamoyo
Poleni watanzania wenzangu wote.
 

Ningeomba umtoe Madelu katika Watanzania wote uliotutaja. Saa hizi linajipongeza kwa kumpanda Utaifakwanza. Shame on Taswira and Utaifakwanza.
 
Imeniuma sana,watu wamakatisha uhai wa binadamu mwenzao,Pumzika kwa amani Dr Mvungi,hakika damu yako haitapotea bure
 

Napingana na wewe juu ya hili, Mimi kwa mawazo na imani yangu binafsi naamini yaliyomkuta Dr. Mvungi sio Lack of security , it was politic mater
NALAANI KITONDO HICHO & R.I.P Dr. Mvungi
 
R.I.P. DK MVUNGI: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi aliyefariki leo alasiri A. Kusini alipokuwa akitibiwa,

James Mbatia, amethibitisha
 
RIP Dr. Mvungi Kapumzike salama na Mwanga wa Milele uangaziwe.Dunia cyo mbaya wabaya walimwengu.
 
Mimi bado niko na majambazi waliohusika:

Je watu walioshikwa ni wenyewe kweli?

Ni Watanzania wenzetu?

Nia yao ya msingi ilikuwa kuua au kuiba!?

Wanamtumikia nani?

Je tutaambiwa ukweli wa mkasa huu wa kikatili?

Je kuna tume imeundwa kufuatilia, au tuwaamini polisi wetu?

Wajumbe wa tume mnamsemeaje Mvungi kule kwenye tume?
Je alikuwa na misimamo hasi sana?
Je alikuwa Mwiba kwa mtu, chama au taasisi yoyote?

Mawasiliano yake ya mwisho aliongea na watu gani?

Samahani wadau, najua si muda muafaka, lkn imeniumiza sana kiasi naona majibu ya haraka yanatakiwa.

Haiwezekani tupoteze wasomi manguli wa aina ya Dr. Mvungi, halafu tuone kawaida tu!
 
aisee! Rest in peace Dr. Mvungi, watanzania tutakukumbuka daima, kifo chako ni rutuba ya katiba ya watanzania tuitakayo?
 
inaumiza sanaa, utaona sasa kwenye msiba wake siasa itapigwa hapo...mara tutawsaka mpaka, ...mara sijui nini kova na nchimb plus TISS poor wote... Walio sababisha haya nao ipo siku watarudi mavumbini imeniuma sanaaaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…