Mimi bado niko na majambazi waliohusika:
Je watu walioshikwa ni wenyewe kweli?
Ni Watanzania wenzetu?
Nia yao ya msingi ilikuwa kuua au kuiba!?
Wanamtumikia nani?
Je tutaambiwa ukweli wa mkasa huu wa kikatili?
Je kuna tume imeundwa kufuatilia, au tuwaamini polisi wetu?
Wajumbe wa tume mnamsemeaje Mvungi kule kwenye tume?
Je alikuwa na misimamo hasi sana?
Je alikuwa Mwiba kwa mtu, chama au taasisi yoyote?
Mawasiliano yake ya mwisho aliongea na watu gani?
Samahani wadau, najua si muda muafaka, lkn imeniumiza sana kiasi naona majibu ya haraka yanatakiwa.
Haiwezekani tupoteze wasomi manguli wa aina ya Dr. Mvungi, halafu tuone kawaida tu!