TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Dah............. So sad. Rest In Peace Dr. Sengodo Mvungi. Poleni ndugu, jamaa na marafiki
 
Napingana na wewe juu ya hili, Mimi kwa mawazo na imani yangu binafsi naamini yaliyomkuta Dr. Mvungi sio Lack of security , it was politic mater
NALAANI KITONDO HICHO & R.I.P Dr. Mvungi

Who is against this?
R. I. P Dk
 
Mi nahisi siyo wenyewe. Watu watabambikiwa tu kesi hapo.

Polisi wanafanya siasa kwenye mambo ya usalama wetu alafu tunashinda humu tukipayuka na habari za akina Zitto na Mbowe! Tutumie forum kama hizi na taratibu nyingine kudai mabadiliko makubwa jeshi la Polisi.

Kwanza umuhimu wa vituo vidogo vya Polisi ambavyo havina uwezo kabisa wa kuzuia uhalifu tena wakikaa vibaya na wao wanatekwa!! Majambazi wanatamba,wanaua raia na kuzusha hofu mitaani! Hivi vituo vikae kijeshi haswa hasa kwa kuwa na askari walio stand by muda wote wakiwa na silaha na walau pikipiki.Unakuta kituo kina Polisi wawili wasio na silaha alafu usiku unakuta wamejibanza ndani wamepiga zao usingizi alafu tutasema mitaa itakuwa salama hapo kweli?
 
Sheria za zamani ifike mahali zipitwe na wakati.auae akatwekatwe vipande.tunafuga sana wauaji kwa kesi za muda mrefu.mauaji sasa hivi yameshamiri.bora umuogope binadamu kuliko simba.
 
Inasikitisha sana. Poleni Wafiwa na Mungu awatie nguvu
 
Waliomuua wamepata nini sasa?
Je Uhai wa Mvungi wataongezewa wao kwa kugawanagawana?
Nijuzeni walichofaidi!

RIP DR MVUNGI.
 
Mimi bado niko na majambazi waliohusika:

Je watu walioshikwa ni wenyewe kweli?

Ni Watanzania wenzetu?

Nia yao ya msingi ilikuwa kuua au kuiba!?

Wanamtumikia nani?

Je tutaambiwa ukweli wa mkasa huu wa kikatili?

Je kuna tume imeundwa kufuatilia, au tuwaamini polisi wetu?

Wajumbe wa tume mnamsemeaje Mvungi kule kwenye tume?
Je alikuwa na misimamo hasi sana?
Je alikuwa Mwiba kwa mtu, chama au taasisi yoyote?

Mawasiliano yake ya mwisho aliongea na watu gani?

Samahani wadau, najua si muda muafaka, lkn imeniumiza sana kiasi naona majibu ya haraka yanatakiwa.

Haiwezekani tupoteze wasomi manguli wa aina ya Dr. Mvungi, halafu tuone kawaida tu!

Sioni sababu ya kushupaa kwa kuwa amepigwa au amevamiwa Dr.Mvungi ,nionavyo kwa upande wangu Dr ni Mtanzania kama Mtanzania mwengine , Je ni waTanzania wangapi wanavamiwa na kupigwa na wengine kuuliwa on the spot na hakuna linal;ofanyika au kuona serikali inashtuka ,Je serikali inamjali Dr Mvungi kama nani ? Nikimaanisha inamjali kama Dr ,Mvungi mwenye heshima na kiongozi mchapa kazi aliekuwa hodari au inamjali kama Mtanzania ?

Kusema inamjali kama Mtz hio sio kweli ,serikali iliopo madarakani imeonesha dhahiri kushindwa kupambana na uharamia unaoota mizizi uharamia ambao utakuwa mzigo mzito kwa wengine watakaoitawala nchi hii ,iwe badala ya Kikwete au m'badala wa CCM , Hivi ndani ya Tz ni wangapi huuliwa na majambazi maharamia kila siku au kwa mwezi tu ? Je serikali iliopo madarakani inamthamini vipi Mtanzania huyu alieuliwa bila ya kosa lolote ? Na inamlindaje aliekuwa yupo hai dhidi ya vitendo hivi ? Ni mabodaboda wangapi wameuliwa ? Sasa inakuwaje majambazi au maharamia wanaowavamia viongozi na kuwajeruhi hukamatwa kabla ya alfajiri ?Na wanaouwa raia wakawaida huwa hawapatikaniki na hata kama wakiwapata huwa watu wameshasahau !

Natumai nimeeleweka.

Poleni wafiwa.
 
R.I.P Dr Mvungu.
Watanzania walikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi.
Uwasamehe wote waliokutenda maana hawajui walitendalo.
 
Eti nchi ya AMANI hii?mungu amuwepo mahali stahiki Dr.Mvungi
 
MUNGU ailaze roho yake mahali pema peponi Amina!!
poleni sana wanafamilia wote ndugu jamaa na marafiki wa DR.MVUNGI mungu awatie nguvu
 
So sad and very devastating !!

Mara ya mwisho tulionana Mtwara alikusanya maoni ya Katiba. Alikuwa mpendwa wetu sana! R.I.P Dr. Mvungi
 
This is sad news indeed. Tanzanians will miss his constructive contributions to National issues.

May the Almighty God rest Sengondo Mvungi's soul in eternal peace!! AMEN.
 
Back
Top Bottom