Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kpifo hichi ni ngumu kikitenganisha na serikali! Dk Mvungi, profesa Mwaikusa, vifo vyao ni vya kuuliwa na majambazi... Tutakukumbuka Dk Mvungi..
Kuna habari za kutaka kupoteza ukweli juu ya kifo cha Dr Mvungi kwa kuhusisha na uporaji wa kawaida uliofanywa na vibaka.
Akili yangu inakataa kabisa ,huu ni mwendelezo wa tamthilia/hekeya ya jeshi la polisi kama ilivyo kuwa kwa Dr Ulimboka na Kibanda.Ni ngumu maelezo ya kamanda Kova kumuingia mtu akilini.
Katika mchakato wa katiba mpya kuna mengi tutayaona maana kama ni kupoteza maisha wapo wengi na Dr Mvungi yeye amekuwa wa kwanza tu,kuna wengi tutafuata hasa ikizingatiwa kuwa hapa kinachopiganiwa ni kukatisha ufalme wa baadhi ya watu waliozoea kuishi maisha ya pepo duniani kwa jasho la wenzao.
Ni kupingana na mfumo uliojengwa ktk misingi U-TWANA na U-MWINYI hivyo watu wote wenye nia njema ya kukomesha hizi ghiliba haina shaka kwamba ni lazima watambue kuwa njia aliyoipitia dr Mvungi bado inawangojea muhimu ni kuerejea mara kwa mara kauli ya Yesu kristo wakati akiwa msalabani"Mungu kutuepusha na Kikombe hicho".
Bahati mbaya ni kuwa mtu akifa huwa harudi hivyo hata sisi tunaoamini kuwa muda si mrefu ukweli utajulikana ila bado kwa Dr mwenyewe ,familia ,jamaa na wanamageuzi inabaki kutoleta jibu mbadala kwamba hatutakuona tena ktk mchakato huu wa Tanzania tuitakayo.
Pumzika kwa amani dr Mvungi u-playpart yako hakika historia itakukumbuka.
Angeuwawa TUNDU LISU sijui Makamanda na vyombo vya Habari vya kibongo wangesemaje?
R.I.P DOCTOR it is too sad but your ideas is still alive.Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.
"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.
Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
CHADEMA WATOA RAMBIRAMBI
Wakati tunafakari nyendo zetu hapa dunia wakati huu wa Msiba mzito kwa Taifa kutokana na kifo cha Dr. Mvungi (alikuwa mjumbe wa kuandaa rasmu ya katiba mpya ya Tanzania)....ebu tusikilize wimbo wa Mbaraka Mwinyishehe (R.I.P) alioimba baada ya kutokea kifo cha Dr. Kreluu...ni kuanzia dakika 0:00 mpaka dakika ya 4.30 katika link hii >>>>>>>>
>>>>>>>>>>Mbaraka Mwinshehe: Kifo chake Dr. Kleruu; Tunachogombea nini - YouTube
Recquiescas in pace et
in paradiso tecum rursus erimus.