Mohamed Mbelwa
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 507
- 272
Poleni familia, wananccr, tume ya katiba, na watanzania wote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh kama ni kweli, R.I.P Dr. Mvungi
Wakuu Dr Mvungi amefariki nchini afrika kusini alilokopelekwa kwa matibabu zaidi, baada ya kuvamiwa na majambazi.
Bwana ametoa bwana ametwaa
Source: ITV
Mungu ampokee mja wake... Mwenye sababu za kuvamiwa kwakwe atujuze kama kweli waliomvamia ni majambazi kweli au ni watu kutoka usalama wa ile taasisi
Wakuu Dr Mvungi amefariki nchini afrika kusini alilokopelekwa kwa matibabu zaidi, baada ya kuvamiwa na majambazi.
Bwana ametoa bwana ametwaa
Source: ITV
Na wewe unataka uonekane umepost
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.
"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.
"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.
Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.
CHADEMA WATOA RAMBIRAMBI
Taratibu mkuu, hizi ni habari za kushtua harafu unaleta mambo sunshow!!Akina Thomas utawajua kuamini ni hadi aguse. Duh!