TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

TANZIA Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Hii nchi sasa inatupa wasiwasi mkubwa kama msomi aliyetumia fedha nyingi za taifa kufika hapo alipokuwa anakuja kuuawa na vijana kwa gharama ya millioni mbili, laptop na simu ya mkononi.
 
Mungu ampokee mja wake... Mwenye sababu za kuvamiwa kwakwe atujuze kama kweli waliomvamia ni majambazi kweli au ni watu kutoka usalama wa ile taasisi

Yaani kiukweli mwanasiasa anapofariki huwa nasikitika kawaida tu, ila huyu imenipain, i dont know why kiasi hicho, pengine kwa sababu kuna mambo mengi sana sasa yanawapata watu mbalimbali haswa wanasiasa tena wa upinzani, na huyu ongezea alikuwa kwenye tume. Am not concluding anything, labda tu kama kuna anayefahamu hasa yatokanayo na kisa cha wauaji ni nini, haiwezekani iwe hamna sababu.

RIP Dr, huruma ya Mungu iwe juu yako, sote tu wadhambi, japo wengine sasa wamekuwa 100% wakala wa shetani
 
ndugu,jamaa,marafiki na watanzania wote tumehuzunika.kama taifa watawala kuna ufa mkubwa ktk ulinzi,ongezeni bajeti ya ulinzi.punguzeni magari ya kifahari,ongezeni magari,vipuri na mafuta kwenye ulinzi.sasa watu muhimu wanadhuliwa kina sisi je? mnaona fahari,kuonesha mapanga yalioua, badala ya bunduki , mbwa ,farasi, na askari waliozuia mauaji.hakika taifa lina mashetani.kiongozi unashupaa kuonyesha mapanga?

Mkuu si ndio watatumaliza kabisa mpaka huku vijijini wakiboreshewa usafiri? Ukisikia jambazi Tanzania ujue ni police au wanajeshi na ndio maana inakuwa vigumu kuwakamata, Na ukileta mchezo unauziwa kesi mara moja.
Na kubaliana na member aliyesema Tanzania sio sehemu salama ya kuishi hata kidogo. Ni heri ya vita ambavyo mtu unamfahamu adui yako na kuona namna ya kujilinda kuliko mtu unayemtegemea kama ndugu rafiki, jirani au mfanyakazi mwenzio anapogeuka kuwa mnyama wa ajabu.

Labda siku moja limtokee mtoto wa Rais ndipo tutakuwa na ulinzi wa raia na mali zao. Inasikitisha sana tena sana. Mauaji yalikuwepo tokea zamani lakini ukifuatilia kwa ukaribu utaona kwamba siku hizi za karibuni kuua imekuwa kama fashion.
Je rais wetu ni kwamba amechoka ama anaogopa kuwawajibisha wanausalama wetu na kuamua kuturithisha tabia za majirani zetu wa Burundi na Rwanda.
 
Ushasikia mtoto wa kiongozi kauliwa? Wao ndiyo wanasema nani auwawe na nani awe kiwete!
 
RIP Dr. Sengondo. Poleni familia na taifa Zima. Mungu ndie mfariji pekee
 
For Tanzania to progress we must apotheosize our
centripetal proclivities above our centrifigal
execrescence ,All hail the Legend!
Requiscant In Pace(R.I.P) Dr. Mvungi
 
Ni msiba wa taifa zima, poleni nyote mlioguswa na msiba huu.Bwana alitoa na Bwana ametoa jina la bwana libarikiwe. Amina
 
R.I.P Daktari, kwa kiasi kikubwa umetimiza wajibu wako wa kuishi.
 
Dah P.I.P. Lakini ingekuwa ni majambazi wangesikia kuwa umeuza gari au Shamba kwa Cash tungejua ni majambazi. Kwan cku hizi watu huhifadhi fedha benki, I think there is something wrong!!!!
 
Embu Dr. Hamza tusaidie wasifu wake kwa ufupi.
Mimi namkumbuka kwa umahiri wake wa kujenga hoja na kujieleza. Wakati wa Mazishi ya Prof. Mwaikusa yule ambaye alishambuliwa na Majambazi nyumbani kwake, yeye ndiye aliyesoma shairi la Shakespeare na MC alikuwa Prof. Palamagamba Kabudi.

May his soul rest in eternal life.Amen!

Kiukweli siwezi eleza lolote kuhusu wasifu wake kwani tulikuwa faculty tofauti mimi nilikuwa Biashara ila tulikuwa tunakaa hall moja. Labda niseme tu alikuwa mtulivu sana na mwenye kujenga hoja na mtu serious sana katika mambo ya msingi na alipenda sana vitu vya kitamaduni. Nimekumbusha kitu hapo alipokuwa mwaka wa tatu alifanya Birthday yake na badala ya kutuwekea keki alitulisha chakula cha kikwao (kipare) kinachoitwa KISHUMBA. Na ndio maana kila tulipokuwa tunakutana nilikuwa namwita Dr Kishumba au Mzee wa Kishumba.

Hakika Mola ailaze roho ya Mzee wa Kishumba pahala panapostahiki.
 
chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka
Hiyo ID yako inathibitisha akili yako ilivyo, Tangu uzaliwe ni MwanaCHADEMA yupi aliyekamatwa hadi sasa kutokana na kosa la Utekaji na kujerui au kuua? je Ramadhan Ighondu na Ahmed Msuya wote hawa ni CHADEMA? Je walipotajwa nagazeti la mwanahalisi kuhusiana na kutekwa kwa Dr. Ulimboka Serikali iliwachukulia hatua gani? na je yule dada wa kampuni ya TIGO anaesemekana kuhusika kutoa zile taarifa juu ya hizi No. za Ighondu na Msuya yupo wapi kwa sasa? na ni nani aliyemuangamiza? jitahidi kutumia akili unapoandika kama haujui ni bora kukaa kimya kuliko kuandika upuuzi huku maisha ya watu yanaendelea kupotezwa na hawa wajinga unaowaabudu.
 
Back
Top Bottom