Baba Sharon
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 372
- 253
R.I.P Mzee Sengondo Mvungi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mungu ampokee mja wake... Mwenye sababu za kuvamiwa kwakwe atujuze kama kweli waliomvamia ni majambazi kweli au ni watu kutoka usalama wa ile taasisi
ndugu,jamaa,marafiki na watanzania wote tumehuzunika.kama taifa watawala kuna ufa mkubwa ktk ulinzi,ongezeni bajeti ya ulinzi.punguzeni magari ya kifahari,ongezeni magari,vipuri na mafuta kwenye ulinzi.sasa watu muhimu wanadhuliwa kina sisi je? mnaona fahari,kuonesha mapanga yalioua, badala ya bunduki , mbwa ,farasi, na askari waliozuia mauaji.hakika taifa lina mashetani.kiongozi unashupaa kuonyesha mapanga?
Mkuu si ndio watatumaliza kabisa mpaka huku vijijini wakiboreshewa usafiri? Ukisikia jambazi Tanzania ujue ni police au wanajeshi na ndio maana inakuwa vigumu kuwakamata, Na ukileta mchezo unauziwa kesi mara moja.
Na kubaliana na member aliyesema Tanzania sio sehemu salama ya kuishi hata kidogo. Ni heri ya vita ambavyo mtu unamfahamu adui yako na kuona namna ya kujilinda kuliko mtu unayemtegemea kama ndugu rafiki, jirani au mfanyakazi mwenzio anapogeuka kuwa mnyama wa ajabu.
Labda siku moja limtokee mtoto wa Rais ndipo tutakuwa na ulinzi wa raia na mali zao. Inasikitisha sana tena sana. Mauaji yalikuwepo tokea zamani lakini ukifuatilia kwa ukaribu utaona kwamba siku hizi za karibuni kuua imekuwa kama fashion.
Je rais wetu ni kwamba amechoka ama anaogopa kuwawajibisha wanausalama wetu na kuamua kuturithisha tabia za majirani zetu wa Burundi na Rwanda.
Nadhani ulimaanisha hivi "Mkuu kwa wimbo huu tunaendelea kuwapoteza watu muhimu kwa taifa letu. Dr Mvungi (R.I.P)"Mkuu (R.I.P) Dr Mvungi kwa wimbo huu tunaendelea kuwapoteza watu muhimu kwa taifa letu.
Ushamba huu, google translate inawatia wazimu.
Embu Dr. Hamza tusaidie wasifu wake kwa ufupi.
Mimi namkumbuka kwa umahiri wake wa kujenga hoja na kujieleza. Wakati wa Mazishi ya Prof. Mwaikusa yule ambaye alishambuliwa na Majambazi nyumbani kwake, yeye ndiye aliyesoma shairi la Shakespeare na MC alikuwa Prof. Palamagamba Kabudi.
May his soul rest in eternal life.Amen!
Hiyo ID yako inathibitisha akili yako ilivyo, Tangu uzaliwe ni MwanaCHADEMA yupi aliyekamatwa hadi sasa kutokana na kosa la Utekaji na kujerui au kuua? je Ramadhan Ighondu na Ahmed Msuya wote hawa ni CHADEMA? Je walipotajwa nagazeti la mwanahalisi kuhusiana na kutekwa kwa Dr. Ulimboka Serikali iliwachukulia hatua gani? na je yule dada wa kampuni ya TIGO anaesemekana kuhusika kutoa zile taarifa juu ya hizi No. za Ighondu na Msuya yupo wapi kwa sasa? na ni nani aliyemuangamiza? jitahidi kutumia akili unapoandika kama haujui ni bora kukaa kimya kuliko kuandika upuuzi huku maisha ya watu yanaendelea kupotezwa na hawa wajinga unaowaabudu.chadema ndio wanaotakiwa kujibu issue ya dr kupigwa mapanga sha,wao ndo watakuw wahusika wakuu wa hili tukio!huu ni mwendelezo wa ile muvi ya kuteka watu na kuwatesa kama walivyofnya ulimboka
daa inasikitisha sana jamaa alikuwa mpambanaji sana