Dr Shein: Tunaandaa rasimu ya kuwatambua Watanzania wanaoishi nje kisheria, tutajenga Daraja la Zanzibar - Bara

Dr Shein: Tunaandaa rasimu ya kuwatambua Watanzania wanaoishi nje kisheria, tutajenga Daraja la Zanzibar - Bara

Kuna tofauti kati ya taa na mwanga bwashee!

Nimesema unaiona taa kwamba ni balbu, kibatali, chemli au mshumaa........uwe unaelewa!
Kwa hiyo mkuu at a distance of 20km unaweza kuiona taa na kujua ile ni 'balbu, kibatali, chemli au mshumaa'?
If that is the case then I commit to respect your ability!
 
Tiketi ya 50k bora uongeze 35k upande ndege
pale bandarini zanzibar pana mambo yanakera sana. Kuna uuzaji wa tiketi za ulanguzi kwa uwazi kabisa hasa tunaotaka usafiri wa Dar, hii inaumiza sana na ni kero mojawapo kwangu. Unaweza kulazimika kununua ticket kwa 50,000/= wakati ulitaka economy class 25,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo mkuu at a distance of 20km unaweza kuiona taa na kujua ile ni 'balbu, kibatali, chemli au mshumaa'?
If that is the case then I commit to respect your ability!
Ndio ujue Unguja ni karibu sana pengine pungufu sana ya 20km ukitokea Ununio!
 
Ni uzembe wako tu,tickets unatakiwa uwahi kabla hazijaisha,hizo za economy ya 25,000 unayouziwa ni ya watu walicancel safari zao na kuwapa walanguzi sasa kwasababu we umechelewa na unataka kusafiri inabidi wakuuzie maana kule ofisini nafasi zimeshaisha .

Kwahiyo hapo usimlaumu Dr Shein wala azam ni uzembe wako wa kutokufanya booking mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Epuka kutetea ujinga hata kama unafaidika kupitia ujinga huo. Utaratibu huo mbovu na unapaswa ukomeshwe mara moja. Cancellation ifanywe katika ofisi husika, si vinginevyo ili tiketi ziuzwe kwa mfumo wa wait list na kwa taarifa sahihi. Je John akinunua tiketi ya Juma then likitokea la kutokea, John ataweza je kuthibitishwa kama alisafiri? Kuuza tiketi kwa njia ya kulangua ni mfumo wa kijinga na wa kimaskini vilevile. Yumkini hiyo syndicated ni "formal", lakini kwa awamu hii itavunjwa tu. Ni suala la muda.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hatuna barabara hapa Zanzibar zaidi ya mashimo,usiombe ije mvua, kuna siku shein alisema serikali haina fedha za kuziba mashimo [emoji3]
Ni serikali maskini kupita zote afrika, ama pesa zipo zinaishia mikononi mwa vigogo
 
Kama nawaona TRA wakijipanga na hujuma dhidi ya Bidhaa ama chombo chochote kilicholipiwa ushuru Zanzibar kinapotumia hilo daraja na kufika upande wa pili wa "muungano"
 
Epuka kutetea ujinga hata kama unafaidika kupitia ujinga huo. Utaratibu huo mbovu na unapaswa ukomeshwe mara moja. Cancellation ifanywe katika ofisi husika, si vinginevyo ili tiketi ziuzwe kwa mfumo wa wait list na kwa taarifa sahihi. Je John akinunua tiketi ya Juma then likitokea la kutokea, John ataweza je kuthibitishwa kama alisafiri? Kuuza tiketi kwa njia ya kulangua ni mfumo wa kijinga na wa kimaskini vilevile. Yumkini hiyo syndicated ni "formal", lakini kwa awamu hii itavunjwa tu. Ni suala la muda.
Kununua ticket ya ulanguzi ni maamuzi ya mtu mwenyewe.

Ofisi za kukataka ticket zipo wazi kila mtu anaziona, na ticket zinazuzwa kwa bei halali iliotangazwa. Zinapokwisha ofisini, ndio zimekwisha tena, lakini kwa sababu wewe unataka lazima uondoke ndio unakutana na walanguzi, wanakulangua, wanakupa ticket ya Juma wakati unaitwa John, it was your choice, no one else to blame but yourself.

Cancellation hufanywa ofisini. Sasa kama wewe ulikata ticket, halafu hujacancel mwenyewe, hio sio kazi yao tena. Wewe ndio unajukumu la kwenda ofisini na ku cancel ticket yako. Wewe ukienda kumuuzia tickte yako mlanguzi kisa umeamua usisafiri tena, ticket hio inasoma kama bado valid na ndio anakuja kulanguliwa mtu hapo
 
chilubi,
Sijajua uzoefu ulionao kwenye eneo hilo la tiketi za kulangua. Tatizo watu mazowea yamewafanya muwe "rigid" hata kwa vitu vyenye kulenga kuboresha huduma na kuleta ustawi kwa wananchi. Kumbuka huyo John anayetumia tiketi ya Juma anapanda kwenye boti ya huyohuyo aliyetoa tiketi, na tiketi haikatwi mpaka pawepo na ID ya abiria, anapandaje kwenye boti hali ya kuwa yeye siye Juma? Kwanini uongozi wa boti usihusike? Kwanini maofisa wanaokagua abiria wasiwajibishwe?

Sidhani kama zile tiketi zinazolanguliwa ni za abiria halisi waliocancel safari zao. Chunguza vizuri.
 
Mr What,
Nadhani unakosa uelewa wa 'kujengewa' na 'kujenga.'

Unataka akujengee daraja kama hilo wewe kama nani?

TAZARA was an exception; and that was then; this is now!
Kwani vingapi vimejengwa bwana Mbona una maswali ya ajabu ajabu, unapojenga nyumba yako, haina maana wewe mwenyewe ulishika tofali na uka jenga Bali uligharamia kila kitu... Hiyo ndiyo dhana ya kujenga haijalishi watajenga wachina au Taifa lingine lolote lile ili mradi Serikali yetu imegharamia hata iwe kwa mkopo basi IMEJENGA.....
 
Basi hukujua kujieleza katika bandiko lako la mwanzo.

Ni dhahiri unalo tatizo la kujieleza na kueleweka. Lifanyie kazi kulirekebisha hilo.

Hata nilipokupa mfano wa TAZARA, bado haukukusaidia kuelewa?
 
Sijajua uzoefu ulionao kwenye eneo hilo la tiketi za kulangua. Tatizo watu mazowea yamewafanya muwe "rigid" hata kwa vitu vyenye kulenga kuboresha huduma na kuleta ustawi kwa wananchi. Kumbuka huyo John anayetumia tiketi ya Juma anapanda kwenye boti ya huyohuyo aliyetoa tiketi, na tiketi haikatwi mpaka pawepo na ID ya abiria, anapandaje kwenye boti hali ya kuwa yeye siye Juma? Kwanini uongozi wa boti usihusike? Kwanini maofisa wanaokagua abiria wasiwajibishwe?

Sidhani kama zile tiketi zinazolanguliwa ni za abiria halisi waliocancel safari zao. Chunguza vizuri.
Sasa kwanini unalaumu Kampuni yenye Boti? Wao wameuza ticket kwa Juma.Wewe John unaenda kununua ticket ya Juma. Ukifika getini ukipita unaanza kulaumu watu wa getini kwanini wamekuruhusu upite kwa ticket ya Juma. Wakikuzuia usipite pia unaanza kulaumu kwanini wakuzuie wakati ticket umenunua kwa huyo Juma?

Hivyo ndio watu walivyo. Hakuna jema utakalolifanya wakakosa kulikosoa.

Haraka zako ndio zinakufanya uuziwe ticket za ulanguzi. Mimi kila siku naenda kwa aliekuwa authorized agent au ofisi zao wenyewe Azam. Sinunui ticket nje ya ofisi, kwanini wewe ununue nje ya ofisi inayotambuliwa? tuanzie hapo kwanza.
 
Itakuwa mzito kuelewa ndugu. Kwanini mfumo huo wa ulanguzi wa tiketi haupo kwenye ndege?

Shida haipo kwa anayeuza wala kununua tiketi ya ulanguzi (hawa hawana mfumo "authorized" wanaotumia,purely illegal). Shida ipo kwa watu waliowekwa rasmi (authorized) kuangalia kama sheria na taratibu zinafuatwa ikiwa pamoja na kuwabaini hao wenye tiketi feki.

Kimsingi, huwezi kuzuia watu wasivunje sheria au utaratibu isipokuwa anayebainika kuvunja sheria au utaratibu anapaswa achukuliwe hatua. Kwanini afisa wa kampuni anayekagua abiria wanaoingia kwenye boti amruhusu John ilihali tiketi imeandikwa Juma? Mamlaka zikiwazuia hao watu kupita, automatically ulanguzi hautakuwepo. In fact, hizo tiketi za ulanguzi nyingi si za abiria kwa maana ya abiria, ni walanguzi wanazinunua purposely.
 
Dan Zwangendaba,

Mkuu, usafiri wa ndege kwenda china na meli kuja dar ni vitu viwili havifanani zaid ya vyote kuwa unatoka upande mmoja kwenda wa pili.

Sio kila kitu ni mamlaka ifanye, kwanza uanze wewe kujirekebisha. Kwani hujui kuwa unatakiwa uwe na tiketi yenye jina lako?
 
UJENZI DARAJA LA DAR HADI ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani (TDC Global) Mhe Norman Jasson amesema kuwa Watanzania waishio nchi za nje (#Diaspora) wapo kwenye mkakati wa kujenga daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar na sasa wanasubiri baraka za serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa daraja hilo.

Daraja hilo litakuwa na njia tatu, moja ni kupitisha magari yanayotoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuja Dar es Salaam na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.

Mapendekezo matatu ya ujenzi wa daraja hilo yametolewa ambayo ni moja, kujenga daraja la kupita ndani ya bahari, pili daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa nchi Kavu na kusafirishwa na meli na kisha kuunganishwa.

Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji Dar hadi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko.

Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu.

Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.

Diaspora wameamua kujenga daraja hilo kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli ili kurahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar na watalii waweze kusafiri hata kwa baiskeli.

Mwandishi toka Zanzibar
IMG-20191222-WA0025.jpg
IMG-20191222-WA0021.jpg
IMG-20191222-WA0024.jpg
IMG-20191222-WA0022.jpg
IMG-20191222-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom