Dr. Slaa: Fungu la 23 la Ikulu halikaguliwi na CAG, tusipopiga kelele sasa milioni 150 keshokutwa itafikia bilioni 3

Kwenye mazungumzo yaliyofanyika club house Dr. Slaa amesema kwa utaratibu anaoufahamu Rais hana mafungu makubwa kiasi hicho (milioni 150) kwaajili ya eneo moja, na fedha hizi zinawekwa katika kifungu cha Ofisi ya Rais na balaa ni kwamba fedha hizi hazikaguliki kwasababu fungu la 23 la Ikulu halikaguliwi na CAG!

Kwa maana hiyo chochote kitakachofanyika inabaki kuwa siri ya Ikulu, siri ya Rais. Jambo hili kama ni kweli Rais ametoa mfuko binafsi hatuwezi kuziingilia lakini kama ametoa kwenye mfuko wa 23 (kama sijakosea) ni lazima watanzania tulipigie kelele, hili si sahihi huu ni wizi, huu ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kazi mambazo hazijaidhinishwa na bunge wala hazijawahi kuidhinishwa na bunge miaka yote tangu uhuru wetu mpaka leo, marais wamepita wengi hatujawahi kuona kitu cha namna hii.

Ni jambo la kusikitisha, tuendelee kulipigia kelele kwasababu tusipopiga kelele hii imeshapanda kuwa milioni 150, kesho itafika bilioni moja, kesho kutwa itafika bilioni 3!
Dr.slaa wacha unafiki bwana wako magufuli alichagia ujenzi wa msikiti dodoma na hatukusikia chochote kutoka kwako au kwa hao jamaa zao wanaokuunga mkono leo samia kuchangia kanisa imekuwa nongwa ,ingawa mimi kwa Imani yangu siungi mkono muislamu kuchangia kanisa lakini najuwa rais amefanya hivyo kisiasa tu.
 
Slaa kama muadilifu kweli aanze kupinga ule mkataba wa serikali na kanisa,aache unafiki.
 
Nani ana uhakika Vote 23 ndio imechangia milioni 150 Kanisani.
 
Kwenye mazungumzo yaliyofanyika club house Dr. Slaa amesema kwa utaratibu anaoufahamu Rais hana mafungu makubwa kiasi hicho (milioni 150) kwaajili ya eneo moja, na fedha hizi zinawekwa katika kifungu cha Ofisi ya Rais na balaa ni kwamba fedha hizi hazikaguliki kwasababu fungu la 23 la Ikulu halikaguliwi na CAG!

Kwa maana hiyo chochote kitakachofanyika inabaki kuwa siri ya Ikulu, siri ya Rais. Jambo hili kama ni kweli Rais ametoa mfuko binafsi hatuwezi kuziingilia lakini kama ametoa kwenye mfuko wa 23 (kama sijakosea) ni lazima watanzania tulipigie kelele, hili si sahihi huu ni wizi, huu ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kazi mambazo hazijaidhinishwa na bunge wala hazijawahi kuidhinishwa na bunge miaka yote tangu uhuru wetu mpaka leo, marais wamepita wengi hatujawahi kuona kitu cha namna hii.

Ni jambo la kusikitisha, tuendelee kulipigia kelele kwasababu tusipopiga kelele hii imeshapanda kuwa milioni 150, kesho itafika bilioni moja, kesho kutwa itafika bilioni 3!
Mkuu mmngeanza kuhoji wakati Magufuli alipoanza kutoa milioni tano tano barabarani kwa watu mbali mbali pamoja na kuchangia makanisa na misikiti.

Mwanzoni Rais Samia alisema yeye na Magufuli hawana tofauti, umoja wao ni kwa mambo ya namna hiyo. Bahati mbaya zaidi Magufuli alishaweka precedence mbaya matumizi ya namna hiyo!

Tusiangalie tulipo angaukia bali tulipo jikwaa. Kipindi hiko kila mtu alikuwa kimya pamoja na Dr. Slaa!
 
Hapa Slaa simuungi mkono kwa unafiki huo.

Michezo ya kugawa pesa na kutengeneza matukio kujiongezea umaarufu aliyaanzisha Magufuli ambaye Slaa alimuunga mkono na alikua kimya.

Samia alikua deputy wa Magufuli anapita alipopita boss wake japokuwa ni kosa ila pengine ameona ndio umaarufu wenyewe na Samia akaongezea mtindo wa kununua magoli ya Simba na Yanga.

Kwenye hili Slaa hana moral probity kulizungumza atamuonea Samia tu wakati kwa Magufuli aliufyata.
👏👏👏Dr. Slaa hapa kaonesha unafiki wake kweupeee!
 
Hapa Slaa simuungi mkono kwa unafiki huo.

Michezo ya kugawa pesa na kutengeneza matukio kujiongezea umaarufu aliyaanzisha Magufuli ambaye Slaa alimuunga mkono na alikua kimya.

Samia alikua deputy wa Magufuli anapita alipopita boss wake japokuwa ni kosa ila pengine ameona ndio umaarufu wenyewe na Samia akaongezea mtindo wa kununua magoli ya Simba na Yanga.

Kwenye hili Slaa hana moral probity kulizungumza atamuonea Samia tu wakati kwa Magufuli aliufyata.
👏👏👏Dr. Slaa hapa kaonesha unafiki wake kweupeee
Udini unamtafuna, ndiyo maana ilikuwa tatizo kwake kumpigania Lowassa.
Alikuwa tayari kusaliti Ukawa ili kumfanyia kampeni mkatoliki mwenzake.(Magufuli).
Magufuli alinyamazisha harakati za kisiasa, serikali yake ilimpoteza Saanane, ilimshambulia Tundu Lisu, lakini yote hayo aliyanyamazia.
Ati leo naye anajiona mzalendo!!
Mnafiki mkubwa
Mkuu usaliti wa Dr. Slaa haukuanza leo, ulianza toka utotoni! Kawaulize wazee zaidi yake huko kwao utapata full pdf la usaliti na unafiki wake na pia utaelewa chimbuko la usaliti wake! Ni Mnafiki mwenye cheo cha juu!
 
Mkuu mmngeanza kuhoji wakati Magufuli alipoanza kutoa milioni tano tano barabarani kwa watu mbali mbali pamoja na kuchangia makanisa na misikiti.

Mwanzoni Rais Samia alisema yeye na Magufuli hawana tofauti, umoja wao ni kwa mambo ya namna hiyo. Bahati mbaya zaidi Magufuli alishaweka precedence mbaya matumizi ya namna hiyo!

Tusiangalie tulipo angaukia bali tulipo jikwaa. Kipindi hiko kila mtu alikuwa kimya pamoja na Dr. Slaa!
Watu wote wakinyamaza sidhani km ndiyo maendeleo
 
Back
Top Bottom