Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...


Mkuu, realities ni kwamba hoja ya katiba mpya was a hard sell. Na sidhani wana CCM wanaifurahia kihiivyo.

Hao hao CCM na wingi wao wote ni kama bendera, upepo wa Mwenyekiti utakapopungia, wanafuata. Pia Mkuu wa Kaya kukubali ghafla na kuja haraka haraka na CRC hapo ndo kunakoibua maswali. Historia ya hizi kamati pia inajulikana, pale zinapokuja na mapendekezo yasiyowaridhisha wachakachuaji, zinatupiliwa mbali, na muda unakuwa umepotea.

Pamoja na uwingi wao, nani kati ya wabunge wa CCM waliokuwa na guts za kushikia bango marekebisho/katiba mpya? Si ndio hao tumewasikia (rejea--Celina Kombani, Chacha Werema, Nimrod Mkono) wakiangukia pua hadi JK kaja kuwashushua?

Hata hivyo, bado naamini utaifa unaweza kuzingatiwa. Kama wabunge wa CCM wenyewe waliweza kusimamia "utaifa" wakati wa mjadala wa Richmond (japo imekuja geuka shubili), sitaki kuamini wata-ichakachua hoja ya kuwa na Katiba inayokidhi matakwa ya sasa na kutoa mwongozo kuelekea taifa imara. Nadhani ndicho Dr Slaa anachopigania, Constitutional Assembly, licha ya kwamba anajua CCM ndio wengi bungeni, but the motion here is unique... Katiba...and so will be the tempo.
 

Ndugu William Machela sijaona sehemu ambapo CDM/Slaa wamesema ni lazima katiba ya chadema ifuatwe au kwa kila wanachosema CDM wako right! na wala sijaona hiyo katiba unayozungumzia yenye mawazo ya Dr Slaa pekee! naomba nikupe mfano mdogo tu wa hao wabunge wa CCM ni wazi kabisa unajua kuwa wapo ambao hawakuchaguliwa ila ni kwa wizi wa kura tu, hivi umejifunza kitu gani katika kuwania uspika wa bunge mwaka huu? ndio maana kuna members humu wanakwambia kwamba unaweza unaelewa lakini unajifanya huelewi ndio matokeo yake wengine wanakuwa kama unaona wanakutukana mkuu..
 

.....Huyu Mungu atafanya mangapi? ameshatupa akili, utashi, rasilimali, nguvu etc etc ajibu nini tena? kazi yetu ni kutumia rasilimali na nguvu na akili tulizopewa kupinga kila aina ya udhalimu wowote kwa bidii bili kuchoka.......!
 
LOWASA:urafiki wetu haukuanzia barabarani, HAIWEZEKANI HATA SIKU MOJA LOWASA NA ROSTAMU WANFANYE WIZI MKUBWA KIASI KILE KM WA RICHMOND HALAFU KIKWETE SWAIBA WAO ASIHUSIKE...KAMWE HAIWEZEKANI...KWANI URAFIKI WAO HAUKUANZIA BARABARANI KM MNAVYODHANI

HUYU NDIYE KIKWETE KIMBLIO LA WAHUNI NA MAFISADI
 
Wakuu hata mimi sina imani kabisa na mkwere naamini kwa asilimia zote hana nia na hayupo tayari kutusaidia kupata katiba ambayo itakidhi mahitaji yetu na sio wao mafisadi, nakubaliana na dr slaa.
 
"hata Bunge pia linaweza likatumbukia kwenye mtego wa kupitisha kitu kisichokuwa matakwa ya wananchi kwa sababu ya wingi wa wabunge wa chama kimoja."


You are missing nothing. Miaka nenda rudi wabunge wa CCM wakiwa na jukumu nambari wanu la kutetea maslahi ya wananchi waliowachagua wameshindwa kuona mapungufu makubwa ya katiba ya sasa. Harakati za kupata katiba mpya inaendana na Tanzania ya sasa itakuwa "still born" kama process ya kuipata utaongozwa na serikari ya sasa au bunge lililopo sasa. Njia sahii kwa hali tuliyonayo itakuwa ni kutumia tume huru inayojumuhisha stakeholders wote - ikusanye mawaidha ya wananchi - itengeneze draft - irudishe draft kwa wananchi kwa kura ya ndiyo au hapana. Kama wananchi walio wengi wameipitisha draft - basi ikabidhiwe kwa bunge kutengeneza sheria mama bila mabadiliko katika draft.
 

Huo ndo uwezo wake afanye nini? Tulishauriwa tukapige kura na tuzilinde kwa yule atakayetufaa, sisi tukalemaa wachakachuzi wakafanya mambo yao. Watanzania tuamke na ku-riot kudai mambo yetu ya msingi. Tuache kudanganywa kuwa tuna amani hali tunaangamia sisi wenyewe na kuangamiza rasilimali za wajukuu zetu!
Aluta continua............
 

Mkuu, kalisema sasa kwa kuwa anaushahidi wa kutosha...Asingeweza wakati wa kampeni, ushahidi hakuwa nao na km mjuavyo Dr Slaa si mjinga!!!! Hao CCM wameambiwa wameiba kura,wamefyata........... Ndio, km hawajaiba mbona hawajamshtaki slaa kwa uzushi??? Someni alama za nyakati... CCM maji yamewafika kooni, muda si mrefu wataanza kunywa vikombe!!!!....
 

You said it all.

UKishaona mtoto mdogo anasema siri za nyumbani ujue ni za ukweli. Pinda ni mtoto ndani ya nyumba ya Jk na alidiriki kusema kuwa Lile ni genge la watu fulani basi huo ndio ukweli hata kama baba wa mji atasema vinginevyo. Mtoto huwa hasemi uongo lazima ameona kitu kinaendelea na ndiyo maana hata mahakama inaamini ushahidi wa mtoto pasipo kuhoji.

Baba wa mji anapojiumauma na huku watoto wanatoka nje na kusema hadharani, ujue kuna kitu na tena Baba anahusika. Mimi naamini baba anahusika japo inawezaikawa siyo diriect lakini lazima anahusika kupitia mabosi wake EL and RA. Akibanwa vya kutosha lazima atawatundika tu ndugu zake hawa. Anachokifanya sasa hivi ni kiburi cha Urais tu ila mambo yakienda kombo lazima atawatosa EL na RA wachukuwe msalaba wao.

Mimi naamini watanzanaia wakikomaa kwa mgomo bei ya umeme haitapanda na DOWNS hawtalipwa. Wanajua watanzania ni wapole na mbumbumbu hawataweza kung'amua kinachoendelea. kama vyama vya wafanyakazi na vya siasa vitaunga mkono maandamano basi haki yetu itapatikana. Tumeshuhudia kila wakati serikali haiwezi kuwapa haki wananchi wake wasipo idai haki hiyo kwa maandamano. Tumeshuhudia wanafunzi lazima wagome ndipo mambo yaende.

Nadhani imefika wakati watanzania tuige mtindo wa wanafunzi wakufanya maandamano tunapoona serikali haitutendei haki inaporuhusu bei ya vitu kupanda kihorerahorera tu ili watu wafaidike na mikataba mibovu kama ya Rich man from Monduli na Dowans. Tanzanians let's wake up and fight for our rights.
 
Kila mahali nawambia watanzania wamsitafute mchawi wa nchi yao, ila ni JK na genge lake.
 

hiyo kesi labda afungue yeye Slaa ya kudai mahakama iwalazimishe CCm wamshitaki maana CCM ipo busy kujijenga na kusimamia ilani yake, kesi na maandamano ni kazi ya vyama vya upinzani hasa vya ki afrika.
 

nakubaliana nawe mkuu
 

mwehu wewe!! umetumwa au umetoroka milembe!!
 
awali nilikwishasema mtu akiamua kutoona
ni vigumu sana kuona vile ambavyo wengine wanaviona.
angalia sasa umeamua kuona ccm ni wananch wote!
halafu pia umeamua kutoona hoja nyingine ya dr slaa ya kumhusisha
jk na dowans. endelea tu kuchagua vya kuona kwani nayo ni demokrasia

 


Tunamtukana huyu W.J.Malecela lakini kama utatafakari utaona kuna point anaiongea hapa ambayo ni yakutahadharisha na kututufanya tuwaeleze wabunge wetu wawemakini na suala la mabadiliko ya katoba kwa kupitisha maamuzi ya wananchi na sio ya chama. Jamaa anatupa tahadhari tuwe makini kwani kama likichukuliwa kichama zaidi CCM inaweza kuzuia mabadiliko yoyote yale yatakayokikandamiza kwa mtaji wa wabunge wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…