Sekenke
Senior Member
- Mar 3, 2008
- 132
- 30
- Mkuu sina tatizo na anybody ila ninajadili taifa langu kwa kuthamini realities na mazingara tuliyonayo kisiasa, hatuwezi kuunda katiba mpya ambayo haikubaliki na wananchi wote na hatuwezi kuunda katiba mpya kwa kuwasikiliza wananchi wachache, kama ni due process then CCM wanatakiwa na the upperhand kwa sababu ni wengi kwa uwakilishi bungeni,
- Unless tunataka kuunda katiba mpya nje ya katiba yetu ya sasa ya Jamhuri na kama hivyo ndivyo, ina maana tutafanya mabadiliko mengi sana kila kona ya taifa letu bila kupitia katiba yaani bungeni, eti mkuu unasema hilo linawezekana Tanzania ya leo?
William.
Mkuu, realities ni kwamba hoja ya katiba mpya was a hard sell. Na sidhani wana CCM wanaifurahia kihiivyo.
Hao hao CCM na wingi wao wote ni kama bendera, upepo wa Mwenyekiti utakapopungia, wanafuata. Pia Mkuu wa Kaya kukubali ghafla na kuja haraka haraka na CRC hapo ndo kunakoibua maswali. Historia ya hizi kamati pia inajulikana, pale zinapokuja na mapendekezo yasiyowaridhisha wachakachuaji, zinatupiliwa mbali, na muda unakuwa umepotea.
Pamoja na uwingi wao, nani kati ya wabunge wa CCM waliokuwa na guts za kushikia bango marekebisho/katiba mpya? Si ndio hao tumewasikia (rejea--Celina Kombani, Chacha Werema, Nimrod Mkono) wakiangukia pua hadi JK kaja kuwashushua?
Hata hivyo, bado naamini utaifa unaweza kuzingatiwa. Kama wabunge wa CCM wenyewe waliweza kusimamia "utaifa" wakati wa mjadala wa Richmond (japo imekuja geuka shubili), sitaki kuamini wata-ichakachua hoja ya kuwa na Katiba inayokidhi matakwa ya sasa na kutoa mwongozo kuelekea taifa imara. Nadhani ndicho Dr Slaa anachopigania, Constitutional Assembly, licha ya kwamba anajua CCM ndio wengi bungeni, but the motion here is unique... Katiba...and so will be the tempo.