Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Eti ni kweli nchi iko kwenye ‘auto pilot'?
ban.wazo.jpg

Juvenalis Ngowi

amka2.gif
KATIKA siku za hivi karibuni kuna msemo umeshika kasi baina ya watu wa kada ya kati. Huo msemo ni kwamba nchi iko kwenye ‘auto pilot'.
Huu ni msemo uliobuniwa na mwandishi nguli wa makala wa gazeti litokalo kila juma. Mwandishi huyu alimaanisha kwamba nchi inakwenda kama vile haina mtu anayeidhibiti huko inakoelekea.
Kimsingi hoja ya mwandishi huyu ni swali la msingi ikiwa tuna visheni (maono) kama taifa hasa kama hakuna kiongozi anayetupeleka kufikia hayo maono ya kitaifa.
Ukiangalia kwa makini matukio yanayotokeza, utajiuliza kama ina maono kuna juhudi za kweli zinafanyika kutufikisha katika maono hayo?
Hivi ni kiongozi gani anayeiongoza nchi kwa sasa? Huyo au hao wanaoingoza wanaidhibiti kwa kiwango gani tunachoweza kusema nchi haikuwa kwenye auto pilot? Tutafakari ili kujua nini cha kufanya ili kama taifa tufike pale tunapopahitaji.
Ni kweli kwamba moja ya malengo ya vyama vya siasa ni kukamata dola. Inawezekana ikawa hili ni lengo la kwanza la kila chama cha siasa. Lakini kukamata dola haipaswi kuwa ndio mwisho na mwanzo wa malengo ya kisiasa.
Tunakamata dola ili iweje? Hapa ndiyo inawezekana CCM inaelekea wametufikisha mwisho. Na lengo lao lilikuwa ni kushinda walikokuwa wakiita kuwa kwa kishindo huku malengo mengine yakiwa yamepotea.
Hiyo inadhihirisha kuwa kazi yao kubwa ndani ya chama imekuwa ni kupanga mikakati ya kushinda. Nilibahatika kumsikia mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu akisema, maono ya watu sasa yamekuwa finyu ni kuangalia uchaguzi mkuu. CCM baada ya uchaguzi mkuu, wanaangalia uchaguzi wa ndani ya chama. Hivyo wakati wote kila mmoja anaangalia uchaguzi unaofuata. Malengo na dira imekuwa ni kuangalia namna ya kuwabwaga wapinzani wa ndani na nje ya chama katika uchaguzi unaofuata.
Bahati mbaya sana ni kwamba chaguzi zetu zimetawaliwa na fedha.
Nimesikia kwamba hata hao walioko ndani ya chama wanaopinga malipo ya Dowans, hawafanyi hivyo kwa moyo mkunjufu kwamba wanalilia taifa na watu wao.
Habari zinasema kwamba vigogo wa chama hicho wanaopinga malipo ya Dowans wanalia kwa hofu kwamba fedha za malipo hayo zinaweza kutumika katika kuamua rais wa 2015. Tumefika hapo.
Mawazo yetu na mwelekeo wetu ni tufanye nini kushinda uchaguzi unaofuata. Fikiria fedha zilizotumika kuipa CCM ushindi. Sina hesabu ya fedha zilizotumika lakini kwa akili ya kawaida unajua si haba. Tumeona mabango, vipeperushi, misafara na hata takrima.
Hivi vyote ni gharama. Fedha zile zingewekezwa kwenye maendeleo tungekuwa tumeboresha maisha ya watu wangapi? Kuna mtu aliniambia nitazame yale mabango mengi yaliyotapakaa kila kona. Akaniambia kuna jambo moja la msingi.
Kwamba katika mabango yale yaliyokuwa na picha za Rais Jakaya Kikwete msisitizo ulikuwa kuchagua Kikwete na kuichagua CCM. Hayakuwa na ahadi au hayakutupa dira. Hatuna malengo thabiti.
Hata ukiangalia yale mabango yaliyokuwa yameandikwa hari zaidi, nguzu zaidi na kasi zaidi hayakujitosheleza wala hayakubeba ahadi yenye mashiko. Hari zaidi ya kufanya nini? Nguvu zaidi za kufanya nini? Kasi zaidi kuelekea wapi?
Kama ni kuongezeka kwa gharama za maisha kweli tumekwenda kwa kasi zaidi. Kama ni kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne kweli tumeporomoka kwa ari zaidi na kama ni kupambana na mabomu kweli tumeona nguvu zaidi. Dira yetu, mwelekeo wetu na maono yetu ni yapi?
Tumekuwa watu tulioamua kwamba tutavuka mto tukishaufikia. Tumekataa kuona kwamba mbele yetu kuna mto hivyo tutembee tukitafakari namna tutakavyouvuka pindi tukiufikia. Tumeamua kuwa taifa la dharura.
Angalia mahangaiko ambayo sisi kama taifa tunayapitia. Tatizo la umeme ni kituko. Hata niliposikia Kamati ya bunge ya Nishati na Madini ikizungumzia mbinu za muda mfupi za kumaliza tatizo la umeme nilijisikia kucheka.
Tatizo la umeme si tatizo la dharura. Matatizo hayo yalianza tangu miaka ya tisini nilishuhudia matatizo makubwa ya umeme. Kwa wale wenye umri mkubwa kuliko mimi huenda walishuhudia tatizo la umeme miaka mingi zaidi.
Hili halipaswi kuwa tatizo linaloshughulikiwa kwa dharura miaka zaidi ya ishirini! Tulilifahamu tatizo hili , tulikuwa na fursa ya kuingia mikataba inayoeleweka na wawekezaji lakini tukapoteza fursa hiyo.
Hatuna cha kujivunia ingawa tumekuwa na gesi ya songosongo. Umeme wa maji tuliambiwa unategemea mvua. Huu wa gesi tunasema nini? Tuna hazina ya makaa ya mawe. Pamoja na uwezo wa kuwalipa wawekezaji waliowekeza kwenye umeme lakini hatuna uwezo wa kuwekeza kwenye shirika letu la umeme.
Tunafanya vituko na viroja. Tunalenga nini? Sarakasi zote tunazoziona sasa ni vita ambayo sina hakika kama ni ya kumpigania mwananchi. Tunashuhudia kamati za bunge zikijaribu kujigeuza serikali badala ya kudhibiti serikali zinajaribu kuwa watekelezaji.
Yote haya ni ushahidi wa ombwe katika mfumo wetu wa uongozi na ndio maana watu sasa wanauliza; nchi iko kwenye auto pilot?
Hata maafa ya Gongo la Mboto nayo yanatuonyesha namna ambavyo hatuna mbinu na mikakati ya kujihami wakati wa maafa. Usiku ule wa maafa nakumbuka nilikuwa nikiangalia luninga ili kujua kama tutajulishwa chochote.
Nakumbuka niliona tangazo kwamba wananchi wameambiwa wakae sehemu za mabondeni! Hakuna maelezo yoyote na wala hakukuwepo msaada wa kuwapeleka huko "Mabondeni". Hata hospitali zetu hazikuandaliwa kujua namna ya kupokea wagonjwa wakati wa maafa.
Nimeelezwa na mwanaume mmoja aliyempeleka mke wake hospitali habari ya kusikitisha. Mke wake amekatika mkono, damu zinavuja. Mhudumu wa mapokezi anasisitiza lazima walipie kwanza fedha pale ya cheti ndipo huduma ziendelee.
Baba yule kwa bahati alikuwa na shilingi elfu mbili mfukoni kwake. Simlaumu sana yule mhudumu. Hii ndio namna tulivyowaandaa watu wetu. Hawajui tofauti ya heri na shari. Kama taifa hatujawapa maono ya kujua wafanye nini pindi ikitokea katika hali fulani.
Kwa mara nyingine tena tumepoteza uhai wa watu wasio na hatia kwa mlipuko wa mabomu na kuwapatia baadhi ya watu wetu vilema vya kudumu na wengine vilema vya muda. Tumeingia gharama kubwa ya mali. Lakini hakuna anayewajibika.
Hii nayo inaweza kushindilia hoja ya wanaohoji ikiwa nchi ipo kwenye auto pilot? Mamlaka ya nchi yalichukua tahadhari gani baada ya milipuko ya awali? Nani anawajibika katika kuhakikisha usalama wetu? Kama yupo mwenye dhamana ya kulinda usalama wetu, alitekeleza wajibu wake?
Nani anawajibika kwa matokeo mabovu ya kidato cha nne? Nani anawajibika kwa ukosefu wa umeme? Nani anawajibika matatizo ya elimu ya juu? Je, ni kweli tumepoteza mwelekeo?
 
Tatizo si kupungua kwa maji Mtera
ban.bamdogo.jpg

Innocent Nganyagwa

amka2.gif
HAIHITAJI nguvu kubwa sana na ushawishi wa hali ya juu ili mtu aifanye hoja ya kutaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ajiuzulu wadhifa wake kwa kushindwa kazi.
Haihitajiki nguvu au ushawishi mkubwa kwa sababu kwa utendaji wake wa miaka mItano iliyopita, Ngeleja ameshajianisha kuwa haiwezi kazi hiyo. Kama angekuwa anaimudu, leo hii tusingekuwa tuhangaishwa na mjadala kuhusu Dowans kiasi hiki.
Ikiangalia suala la Dowans ni kama nchi imesimama kufanya mambo mengine mengi. Ukisikiliza na kusoma maoni na hoja kuhusu Dowans, utadhani kana kwamba yenyewe ndiyo inayoshikilia siri ya upatikanaji wa nishati ya umeme Tanzania.
Waziri Ngeleja naye amezamishwa kwenye mjadala wa Dowans na kuacha uchumi wa nchi ukiungua kutokana na kukosekana kwa nishati kana kwamba hakuna njia nyingine mbadala za kuhakikisha umeme unapatikana zaidi ya Dowans.
Wakati alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri mwanzoni mwa awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, watu waliweka matumaini kwake na kwa kiasi kikubwa hii ilitokana na dhana tu kuwa ni kijana. Itakumbukwa kuwa wakati ule kulikuwa na vuguvugu la kuwataka wazee wawapishe vijana waiendeshe nchi kwa mwendo wa kupaa.
Wakati huo Ngeleja alikuwa ametoka kumshinda mkongwe katika medai za siasa nchini katika kuwania ubunge katika jimbo la Ukerewe. Haikuwa kazi ndogo kumwangusha wajina wake, William Shija, ambaye hivi sasa ni Katibu Mkuu wa chama cha mabunge ya Jumuiya ya Madola. Baada ya ushindi huo mzito, watu waliweka matumaini makubwa kwa Ngeleja kuwa ni mtu ambaye atafanya mambo makubwa.
Muda mfupi baadaye, Baraza la mawaziri lilipovunjwa, akateuliwa kuwa waziri kamili katika wizara ya Nishati na Madini. Baada ya madudu yaliyofanyika katika wizara hiyo, watu wakaona sasa wizara imepata kiongozi makini.
Tunakumbuka kuwa wakati baraza jipya linaundwa Februari 2008, kwa kuzingatia matatizo yaliyosababisha Baraza kuvunjwa, zilitolewa ahadi nyingi na kubwa kuhusiana na mikakati ya kuhakikisha nchi haiingii tena kwenye matatizo ya ukosefu wa umeme.
Huu ndio ulikuwa mkwara wa Ngeleja wakati anakamata usukani. Lakini kwa bahati mbaya sana, ukipima leo hii kilichofanyika, bado utabaini kuwa ahadi zilezile bado zinaendelea na hakuna jambo la maana sana lililofanyika kuhakikisha kuwa ile ahadi ya kuifanya nchi isiingie tena kwenye upungufu mkubwa wa umeme lililofanyika hadi hivi sasa.
Sijui ni kwa uvivu wa kufikiri, ubabaishaji, ubabe au ukosefu wa fedha lakini mikakati mikubwa ya kuondoa taifa katika janga la upungufu wa nishati haijatekelezwa hadi leo tangu Ngeleja aingie ofisini. Kwa bahati mbaya sana, hajakosa visingizio.
Kila lililoshindikana, anazo sababu zake ni kwa nini limeshindikana. Na kati ya sababu hizo, hakuna inayoonyesha kuwa yeye ni moja ya sababu za kukwama kwa utekelezaji wa mikakati hiyo. Hilo ndilo linalompa nguvu kuendelea kung’ang’ania madarakani.
Lakini kwa hali ilivyo sasa, hakuna tena haja ya kuendelea kushinikiza Ngeleja, au mtu mwingine yeyote yule, katika nafasi yoyote ile, ajiuzulu kwa sababu yoyote ile. Tanzania tumeshakuwa sugu wa majanga na si majanga ya asili kama sehemu nyingine, lakini hakuna anayeona kuwa anapaswa kuwajibika.
Kama watu kufa wameshakufa wengi sana kutokana na sababu ambazo hazipo mbali sana na uzembe lakini hakuna anayejiona kuwa anapaswa kuwajibika kutokana na uzembe huo.
Hakuna mwenye uhakika sasa hivi kuwa uchumi wa nchi unaumia kwa kiasi gani lakini hilo si jambo linalopaswa kuhangaisha nafsi zetu, achilia mbali nafsi za walio madarakani ambao wanapaswa kuhakikisha halitokei.
Watawala wanapoambiwa kuhusu mradi wa Stigler Gorge ambao utakuwa na uwezo wa kutoa megawati 3,000 kama mwarobaini wa matatizo ya umeme nchini kwa muda mrefu, wanakimbilia kusema kuwa mradi huo unahitaji mabilioni ya fedha kuutekeleza. Wanasema kuwa hatuna kiasi kama hichio cha fedha. Hivyo, wanaukwepa.
Lakini hapa katikati, wanakubaliana na vijimradi vidogo vidogo ambavyo gharama zake kwa pamoja ni zaidi ya kujenga Stigler Gorge.
Tumekubali mradi wa ujenzi wa mitambo ya kutumia mafuta mazito Mwanza huku tukijua kuwa hata Dare s Salaam upatikanaji wa mafuta hayo ni wa matatizo. Matokeo yake, mitambo inachakaa bila kuzalisha umeme.
Leo hii, ukipiga hesabu ya fedha zote ambazo serikali imeshazitumia kwa ajili ya kugharamia umeme wa dharura, ukijumlisha na gharama ambazo nchi inaingia kwa kukosekana umeme pamoja na gharama ambazo uchumi unateketea kutokana na mgawo wa umeme usiokoma, utabaini kuwa ni kubwa kuliko gharama za kujenga Stigler Gorge.
Hapa utabaini jambo moja tu kuwa kumbe haya matatizo ya umeme wala si ya bahati mbaya bali ya kutengenezwa mahsusi. Sasa ni dhahiri kuwa matatizo ya umeme nchi ni ni miradi ya watu ambao wanayatengeneza kwa makusudi ili waendelee kukinga mabilioni ya fedha. Ndio maana, kwa miaka mitano iliyopita, hatujatekeleza mkakati wowote wa maana wa kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa uhakika.
Katika kipindi hicho chote, tuliyoyafanya ni kuwa na mikakati ya kupata umeme wa dharura tu na kuendelea kuitegemea Mtera huku tukisali kuwa ikauke ili tulazimike kutafuta umeme wa dharura. Nadhani ni katika msingi huu ndio maana kuna baadhi ya watu werevu wanaoona kuwa ni heri tukae gizani kwa sababu tunachokifanya ni kuwanufaisha watu wachache tu.
Na ndio maana matatizo ya umeme hayaishi na hayatakuja kuisha kama tutaendelea kuchekeana hivi. Wapo watu ambao kazi yao ni kuchuma fedha kupitia miradi ya umeme wa dharura. Inavyoonekana, somo la 2008, lililosababisha serikali kuvunjika halikuingia akilini. Au, imepatikana njia ya kuwadhibiti wazalendo wachache ambao walitufikisha pale tulipofikia 2008.
Mwanamuziki maarufu wa rege, hayati Robert Nesta Marley, almaarufu Bob Marley, aliwahi kuimba kuwa huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote. Ipo siku Watanzania watashituka tu.
 
Dowans: We are ready to forgive 94bn/-




By The guardian reporter



25th February 2011


email.png





headline_bullet.jpg
Tanesco officials yet to respond to offer?




At last Dowans -Tanzania yesterday succumbed to the countrywide public outcry and pressure and declared its intention to forgive the 94bn/- compensation, asking Tanesco to only pay UDS 24million being services-related debts.
The latest news signifies an end to the prolonged and complex multi-billion shillings legal dispute between Dowans and the state run power firm - triggered by the International Chamber of Commerce (ICC) ruling ordering Tanesco to pay Dowans 94bn/- in compensation for breach of contract.
Dowans Director of Finance, Stanley Munai told journalists that the private power firm reached the decision in the wake of Tanzanians' outcries.
"But Tanesco would be required to pay our debt of USD 24m being accumulated service charges for electricity they bought from us," he said during a visit by the Energy and Minerals parliamentary committee of the Independent Power Ltd (IPTL) gas-driven power plant.
However, it was not clear until yesterday whether Tanesco had accepted the Dowans offer or not so that negotiations between the two sides could start.
Officials of the power firm were not available to comment on the Dowans offer.
Munai told journalists who accompanied the parliamentary committee in the tour that they had no problem with forgiving the hefty compensation, but Tanesco has been reluctant to accept the offer.
If Tanesco and the government would not accept the out of court settlement, he said, Dowans would allow the law to take its course on the issue.
He clarified that the contract between the companies obliged them to respect decisions of the arbitration tribunal, and does not allow for any appeal.
"There is no room to appeal; Tanesco knows this part of the contract. I don't know if they are still unwilling to accept the compensation relief," said the Dowans official.
"We wrote a letter to Tanesco, expressing our readiness to forgive the hefty compensation, but they have not responded to date…just imagine, what should we do?" said Stanley.
The watchdog chairman, January Makamba questioned why the Dowans plants should not be transferred from Tenesco premises because they are not used. Responding, Dowans finance director, Stanley said they wanted to remove the generation plants but were prohibited by Tanesco officials.



SOURCE: THE GUARDIAN
 
kwa kweli sina imani tena na mkwere! ndo maana napata shida sana kuamini lolote ambalo ataliahidi,,,,,sina hata chembe ya imani na huyu mtu,,,hata akisema jambo ambalo kweli ni la kimaendeleo napata shida kubwa kumwamini!!!!!
 
PHP:
[B] [/B]

    kwa kweli sina imani tena na mkwere! ndo maana napata shida sana kuamini lolote ambalo ataliahidi,,,,,sina hata chembe ya imani na huyu mtu,,,hata akisema jambo ambalo kweli ni la kimaendeleo napata shida kubwa kumwamini!!!!!

On this you are not alone....................................
 
Umeme chanzo cha kupanda bei za bidhaa
ban.blank.jpg

Betty Kangonga

amka2.gif
WAKATI nchi ikikabiliwa na tatizo la mgawo wa nishati ya umeme, bidhaa muhimu kama petroli, dizeli na mafuta ya taa nazo zimepanda bei.
Hali ya kupanda kwa gharama za maisha inazidi kushika kasi huku hali ya kipato cha wananchi kikiwa ni chini ya dola moja kwa siku.
Hatua hiyo inamweka mwananchi katika wakati mgumu hasa katika kujihakikishia kupata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha ya kila siku yanayomkabili.
Wakati magumu hayo yakiwakabili wananchi, mwishoni mwa mwaka jana Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ilitangaza na kuruhusu Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari 2011.
Inawezekana kwa asilimia kubwa uamuzi huo umechangia na kufifisha ndoto za watu waliokuwa na malengo ya kuweka umeme katika nyumba zao kwa kuwa gharama za kuvuta umeme zitaongezeka maradufu.
Hali hiyo imesababisha gharama za chakula pamoja na vinywaji kuzidi kuongezeka kutokana na gharama za uendeshaji zimepanda hususan mazao ya nafaka
kama mahindi na mchele.

Kupanda huko kumetokana na gharama za ukoboaji na kusaga kuongezeka, kwa sasa mchele unauzwa kilo sh 1,350.
Bei ya vinywaji imezidi kupanda na baadhi ya maduka wanauza soda ya kampuni yoyote hadi sh 700 kwa chupa ambapo wananchi wengi hutumia vinywaji baridi.
Hali ya kupanda kwa gharama za umeme ni kuzidi kuongeza makali ya maisha kwa wananchi walio na kipato cha chini.
Ni vema upandishaji huo ungekwenda sambamba na maboresho ya shirika hilo hasa katika njia zake za kupitisha umeme.
Kabla ya kupandisha gharama hizo shirika hilo lilikuwa bado linatakiwa kufanya maboresho zaidi ya mitambo.
Kukatika kwa umeme mara kwa mara kumeleta madhara ikiwemo kuunguza vitu majumbani na maofisini, Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Felix Mosha, amewahi kusema kuwa ongezeko la asilimia 18.5 itapunguza ushindani wa kibiashara.
Anasema CTI kwa ujumla inatumia asilimia 15 hadi 40 za gharama za uzalishaji, hivyo ongezeko hilo litaathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji.
"Ongezeko hili litaathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya viwanda na kupunguza ushindani wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, kwa hiyo kitendo hicho kitaathiri uchumi wa taifa," anasema Mosha.
Anafafanua kwamba mwaka 2008 Ewura waliiambia TANESCO watimize masharti mbalimbali ili kuepuka tatizo la kupanda gharama za umeme mara kwa mara, lakini hadi sasa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na Ewura badala yake imeiruhusu TANESCO kupandisha gharama.
Wakati hali ikiwa hivyo, katika sekta ya umeme bado gharama za elimu nazo zimeendelea kuwa juu hasa kwa shule za watu binafsi.
Elimu ni suala muhimu na urithi kwa mtoto lakini kuwepo kwa ongezeko la gharama za elimu linaweza kusababisha nchi kukosa wasomi na huku hali ya idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika kuzidi kuongezeka hasa kutokana na gharama za maisha kuwa juu zaidi.
Kuna umuhimu wa elimu licha ya wananchi kutokuwa na kipato cha uhakika.
Watanzania wanafanya biashara ambazo hawana uhakika wa kupata fedha, kwa mfano fundi cherehani anakwenda kibaruani, hajui atarudi nyumbani na kiasi gani cha fedha, kisha bado anatakiwa kulipa ada ya shule kwa mwanaye.
Ukiangalia gharama za elimu kwa shule za binafsi ambazo ndizo zinazotegemewa kuwa zinatoa elimu bora, kutokana na kuingia kwenye ushindani wa kibiashara, ada ya mtoto mmoja kwa mwaka ni wastani wa sh 700,000 hadi sh 1,500,000.
Wakati vyuo vikuu karo ya mwaka, kwa shahada zote, zinaanzia sh 600,000 hadi sh 2,000,000. Je, mwananchi wa hali ya chini ataweza kumudu gharama hizo?
Pamoja na hali hiyo, hivi karibuni Chama cha Wamiliki wa Daladala (Dacoboa) na Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa) walipendekeza ongezeko la nauli za mabasi yao.
Wamiliki hao wamependekeza ongezeko la nauli ili kila msafiri alipishwe sh 51 kwa kilometa moja. Suala hili linaendelea kurindima huku Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imekwisha kupokea mapendekezo yao ili kufanya tathmini zaidi.
Ni wazi kuwa watendaji wa Sumatra watasimamia vema ili kuwanusuru wananchi kutoka katika makucha ya madalali wapandisha bei za magari hayo kiholela.
Kwa wamiliki wa mabasi yanayofanya safari zake mikoani na nchi za kigeni wanadai kwamba, ni lazima nauli ipandishwe hivyo abiria kulipa sh 69.86 kwa kilometa badala ya ile ya zamani ya 26.60.
Wanasema malipo haya yanapaswa kufanywa kwa kila abiria, hivyo malipo mapya yawe ya juu zaidi, kwani gharama za uendeshaji zimepanda.
Mathalani mabasi yaendayo Arusha kutoka jijini Dar es Salaam kwa sasa nauli yake ni shilingi 16,400 kwa mabasi ya kawaida.
Lakini kwa wale wenye kupenda kusafiri mabasi yenye vivutio pamoja na santuri za kileo wanatozwa nauli maradufu.
Kwa mantiki hiyo, nauli kutoka Dar es Salaam hadi Arusha kwa mujibu wa mapendekezo mapya ni sh 43,000. Hali hii inaweza kusababisha wananchi kushindwa kuwatembelea ndugu zao hasa nyakati za sikukuu ambapo watu wengi hufanya safari zake.
Na wale wenye kutaka kusafiri kwenda jijini Mbeya wanatakiwa kulipa nauli sh 58,000 badala ya ile ya zamani sh 22,000.
Lakini mapendekezo haya yanaweza kuwa kifo cha biashara za mabasi yenyewe na wamiliki wake.
Mbali na hayo, sukari inaongoza kwa kuuzwa bei ya juu, ambapo hadi sasa inauzwa sh 1,800 hadi sh 2,000 kwa kilo.
Hapa jijini imebainika bei ya mfuko mmoja wa sukari wa kilo 25 unauzwa kwa sh 80,000 kwa bei ya jumla kutoka sh 40,000.
Baadhi ya wafanyabiashara wanasema, kupanda kwa bei hiyo inatokana na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuficha shehena ya sukari ili kujipatia faida kubwa.
Inadaiwa kuwa hali hiyo ya kuwa na uhaba wa sukari kuna uwezekano wa viwanda nchini kuzalisha chini ya uwezo kutokana na ukosefu wa umeme.
Hata hivyo, serikali imewaagiza wenye viwanda vya sukari na wasambazaji kuisambaza bidhaa hiyo tani 61,000 zilizopo katika maghala, kwa wauzaji wa kati
na wadogo mara moja, ili kuondoa hofu iliyopo ya kupungua kwa ugavi na kusababisha kupanda bei.

Aidha, inasema itaagiza tani 50,000 za sukari kutoka nje ya nchi kuanzia sasa hadi Mei 15, ili kufidia pengo la mahitaji katika kipindi cha Mei na Juni wakati viwanda vya ndani vitakapokuwa vinaanza uzalishaji wa sukari.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, anasema tani 61,000 zitatosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili kuanzia sasa hadi mwishoni mwa Aprili.
"Serikali imetoa tamko hilo kutokana na bei ya sukari kupanda kwa kasi katika baadhi ya maeneo nchini na hivyo kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wananchi," anasema Dk. Chami.
Anasema katika maeneo mengine, sukari haipatikani vya kutosha, hivyo kuifanya bei kupanda hususan katika maeneo ya pembezoni mwa nchi ambako inauzwa kwa sh 2,200, kwa kilo.
Dk. Chami anasema kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alikutana na wadau wa bidhaa ya sukari ili kulipatia tatizo hilo ufumbuzi, ambapo walibaini
kuwa bei ya sukari duniani imepanda mwaka huu hadi kati ya dola 850 na 900 za Marekani kwa tani tofauti na dola 235 hadi 400 za awali.

"Kwa viwanda vya Tanzania, hufungwa kati ya Februari na Mei kila mwaka, kwani si msimu wa kuvuna miwa, wenye viwanda hutumia fursa hiyo kukarabati mitambo yao wakisubiri msimu wa uzalishaji Juni," anasema na kuongeza kuwa mambo hayo yamesababisha wasiwasi wa wafanyabiashara wa sukari kuwa kungetokea upungufu mkubwa wa sukari nchini kuliko uliozoeleka katika kipindi hiki.
Anasema ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wazalishaji na wasambazaji kuhodhi bidhaa husika, ili bei ikipanda wanufaike na wakati mwingine huhodhi ili
kujilinda wasiishiwe wakati wa ushindani.

Dk. Chami anasema pamoja na maelekezo hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu itapeleka maelekezo mahususi kwa uongozi wa mikoa yote nchini kuhusu kuwapo sukari ya kutosha na wakuu wa mikoa wataelekezwa kuweka utaratibu wa kufuatilia upatikanaji na bei ya bidhaa hiyo mikoani mwao.
Kuhusu uagizaji wa tani 50,000 anasema, serikali imefuta ushuru wa forodha kwa sukari ya tani 37,500 itakayoagizwa kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na tani 12,500 kutoka nchi wanachama wa EAC, hazihitaji kufutiwa kodi maana ushuru wake ni sifuri.
Anasema serikali imeiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), kuweka utaratibu wa kutoa kipaumbele kwa meli zitakazokuwa zinabeba sukari hiyo
ili kupakuliwa haraka na kumfikia mlaji mara moja.

Kadhalika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) nayo imeagizwa kuchukua hatua za haraka kukamilisha taratibu za kutotoza ushuru wa forodha kwa sukari hiyo.
Dk. Chami anasema serikali itashirikiana na wadau ili wananchi wapate bidhaa hiyo kwa bei nafuu na utekelezaji utaanza mara moja, ambapo sukari itamfikia kila
mwananchi popote alipo na bei itashuka na kuwa chini ya sh 1,700 kwa kilo hata katika maeneo ya pembezoni.

Hata hivyo serikali imefikia hatua hiyo huku kukiwa hakuna mamlaka ya kudhibiti bei ya bidhaa za vyakula, kama ilivyo kwa bidhaa na huduma zingine kama vile nishati ya mafuta, umeme na maji na nauli za vyombo vya usafiri wa nchi kavu na majini.
Hatua hiyo ndiyo inayozidisha mwananchi wa chini kuzidi kuumia kutokana na kupanda kwa gharama za maisha huku kukiwa hakuna uwezo mkubwa wa kukabiliana na ongezeko la bei za holela zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wanaohitaji faida ya haraka.


h.sep3.gif

bkangonga2002@yahoo.com
0716730912


juu
blank.gif
 
Serikali na ahadi lukuki za miradi ya umeme
ban.blank.jpg

Asha Bani

amka2.gif
KUFUATIA mgawo wa umeme uliolikumbuka taifa takriban miezi mitatu sasa, serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, imetoa kauli ya utekelezaji wa miradi ya umeme katika kipindi kifupi na cha kati.
Nikiwa nafuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, waziri huyo mwenye dhamana alitoa mikakati mbalimbali itakayosaidia upatikanaji wa umeme ambao aliuita ni wa kipindi kifupi.
Hata hivyo wananchi mbalimbali ambao wengi wao ndio waathirika wakubwa wa mgawo huu unaoendelea wakiwamo wafanyabiashara walitoa maoni kwa kuitaka serikali kutolifumbia macho suala hili na badala yake kama kuna miradi imeanishwa basi ianze kushughulikiwa haraka iwezekanavyo ili suala hili lipatiwe unafuu.
Waziri Ngeleja anaanza na kutoa uwezo halisi wa uzalishaji umeme katika gridi ya taifa kuwa ni MW 1006, mitambo ya maji ikiwa na uwezo wa MW 561 na mitambo ya gesi asili na mafuta ina uwezo wa MW 445.
Hata hivyo anabainisha kuwa kutokana sababu mbalimbali za kiufundi, uwezo wa mitambo wa kuzalisha umeme katika gridi ya taifa bila kuwepo mgawo wa umeme ni MW 935 ambapo MW 523, sawa na asilimia 56 hutokana na maji MW 322 sawa na asilimia 34.4 hutokana na gesi asilia na MW 9.6 hutokana na mafuta mazito.
Anasema kina cha maji katika mhimili wa Bwawa la Mtera hadi kufikia Februari 14 kilikuwa kimeshuka hadi mita 691.31 juu ya usawa wa bahari, ikiwa ni mita moja 1.31 juu ya kina cha chini kinachoweza kuruhusu uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo ambacho ni mita 690.
Anasema mitambo inazalisha wastani wa MW 180 huku mafuta na gesi asili ikizalisha wastani wa MW 290 na kusababisha umeme wote unaozalishwa katika gridi ya taifa kuwa wa wastani wa MW 470, ambayo ni sawa na asilimia 67 ya mahitaji ya wastani ya umeme au asilimia 57 ya mahitaji ya juu katika gridi ya taifa MW 833 na kuleta upungufu wa wastani wa MW 230 kwenye gridi ya taifa.
Ngeleja anasema upungufu huo ndio unaosababisha mgawo wa umeme unaoendelea kwa sasa huku akisema serikali tayari imenunua mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL ili kuzalisha MW 80 kwa siku kutoka MW 10 kwa siku kama ilivyokuwa awali kabla ya kununua mafuta.
Kutokana na maelekezo hayo, hali ya umeme nchini imedhihirisha kuwa mbaya zaidi, hivyo kunatakiwa suala hili livaliwe njuga na kupatiwa ufumbuzi bila ya kutegemea Bwawa la Mtera.
Mbali na hilo, tunategemea katika Bunge lijalo serikali itatuambia imefikia wapi kuhusiana na miradi hiyo ya umeme.
Hatutarajii kuona katika Bunge jingine waziri tena baada ya kuanza na kwamba amefikia wapi katika utekelezaji, akaanza na kutoa tena ahadi za miradi mbalimbali.
Hata hivyo mbali na kutoa ahadi za miradi lakini Ngeleja ametoa mikakati ya dharura itakayochukuliwa ili kuhakikisha umeme unapatikana licha ya kuwa hautokidhi mahitaji ya watumiaji.
Hatua ya kwanza ya dharura Ngeleja anasema ni serikali kuhakikisha fedha za kununulia mafuta ya kuendesha kituo cha kuzalisha umeme IPTL zinaendelea kupatikana kwa wakati ili kituo kiweze kuzalisha katika kiwango cha MW 80.
Pamoja na kuhakikisha miradi ya kudumu ya kuzalisha umeme MW 100 itafungwa Ubungo Dar es Salaam itayotumia gesi asili na mitambo ya MW 60 itafungwa Mwanza itayotumia mafuta mazito (HFO) inakamilishwa kama ilivyopangwa na kukamilika Desemba 2011 au Januari 2012.
Aidha, anasema kutakuwa na mpango wa dharura utakaohakikisha Shirika la Umeme nchini (TANESCO) linasimamia mgawo wa umeme kwa makini zaidi na kuhakikisha kwamba umeme kwenye shughuli za uzalishaji na sehemu nyingine nyeti za huduma za jamii na usalama zinaendelea kupata huduma hiyo.
Hata hivyo mbali na mpango wa dharura, waziri hakusita kuwaambia Watanzania kuwa kuna utekelezaji wa miradi ya umeme kwa kipindi cha muda mfupi.
Anabainisha mpango huo ni pamoja na ujenzi wa mitambo ya kutumia gesi asili ya Songo Songo, Mnazi Bay MW 870 na Kinyerezi MW 240, utakaokuwa chini ya Japan Sumitomo Corporation utakaogharimu dola za Marekani milioni 510 na mchango wa serikali ni dola milioni 10, utakaokamilika mwaka 2013.
Mnazi Bay MW 300, nao anaahidi kukamilika mwaka 2013, utakaokuwa chini ya Kampuni ya China (CMEC) na kwamba mkataba wa EPC umesainiwa ambapo utagharimu dola za Marekani milioni 660 na mchango wa serikali ni dola za Marekani milioni 132 .
Mradi mwingine utafungwa Somanga Fungu, Kilwa MW 230 ukiwa chini ya ProEnergy Services, mradi utakaogharimu dola za Marekani 350.
Mradi mwingine ni wa makaa ya mawe wa Kiwira, Mchuchuma na Ngaka MW 1200 ambapo Kiwira MW 200 utakuwa chini ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mradi wa Mchuchuma MW 600 utakamilika mwaka 2015 na kwa mujibu wa waziri, mwekezaji ameshapatikana ambapo utagharimu dola milioni 1,000 na mchango wa serikali ni dola milioni 250 za Marekani.
Anabainisha kuwa mradi mwingine ni wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya upepo mkoani Singida MW 100 utakaokamilika mwaka 2012, utagharimu dola za Marekani milioni 250 na utaendeshwa na sekta binafsi bila mchango wa serikali huku wa Power Pool E.A MW 50 utakamilika mwaka 2013 kwa gharama za dola za Marekani milioni 123.
Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji inayohusisha kuongeza umeme wa MW 600 kupitia mradi wa Rusumo MW 20 anasema serikali imefanya upembuzi yakinifu ambapo kituo cha uzalishaji kitagharimu dola za Marekani milioni 85.65 na njia za usafirishaji umeme zitagharimu dola milioni 77.4.
Anasema kutakuwa na usambazaji na usafirishaji wa umeme ambapo sambamba na utekelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme wizara hiyo na TANESCO inaendeleza miradi ya kuimarisha na kupanua miundombinu ya kusafirisha umeme kwa lengo la kufikisha kwa wateja utakaozalishwa chini ya programu mbalimbali.
Anaahidi kuwepo na uendelezwaji wa mradi wa Iringa –Shinyanga na kwamba ujenzi wake umepangwa kuanza robo ya kwanza ya mwaka 2011 ambao umedhaminiwa na Benki ya Dunia.
Naamini kuna wafanyabiashara wanaotegemea umeme, wawekezaji wamekimbia kutokana na kukosa umeme na hata pato la Mtanzania wa kawaida pia limepungua kutokana na takriban robo tatu ya Watanzania kutegemea umeme.
 
Umeme wa uhakika hadi 2014


na Mwandishi wetu


amka2.gif
RAIS Jakaya Kikwete amesema mipango ya kulipatia taifa umeme wa uhakika itakamilika baada ya miaka miwili ijayo.
Akihutubia taifa katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Februari jana, Rais Kikwete alisema, "Waswahili wana msemo usemao, jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu. Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika.
"Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme," alisema Rais Kikwete na kuongeza:
"Naomba ndugu zangu muelewe kuwa miradi hii huchukua muda kukamilika. Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa kituo nao pia. Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta. Subira yavuta heri," alisisitiza.

Aidha, alisema makali ya mgawo wa umeme unaoendelea hivi sasa yatapungua hadi mwezi Julai mwaka huu, kwani tayari Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) limeagizwa na serikali yake kukodisha mitambo ya kufua umeme wa dharura wa megawati 260.
"Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011," alisema.
Alisema chanzo cha matatizo ya umeme nchini ni kupungua sana kwa maji katika bwawa kubwa la Mtera.
Hadi jana kina cha bwawa hilo kilikuwa kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7 na kwamba kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.
"Februari 15, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka bodi na menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi," alisema Rais Kikwete.
Akizungumzia sakata la milipuko ya mabomu nchini, Rais Kikwete alisema tume iliyoundwa kuchunguza suala hilo inaendelea na kazi yake na kwamba tayari serikali ya Marekani imetoa msaada kwa kutuma wataalam wake kuchunguza chanzo cha milipuko hiyo.
Akizungumzia fidia kwa wahanga wa milipuko hiyo, Rais Kikwete alisisitiza ahadi ya serikali ya kuwajengea nyumba wananchi hao.
"Tumeamua kuwa serikali ibebe jukumu la kujenga upya nyumba hizo kwa mujibu wa kiwango cha uharibifu. Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia shirika lake la Uchumi," alisema.
Akigusia njaa, Rais Kikwete alikiri kuwa baadhi ya mikoa nchini kuna njaa lakini alisema serikali yake itachukua hatua kuhakikisha hakuna mtu anayekufa kwa njaa, kwani bado ipo hakiba ya kutosha.
 
PHP:
RAIS Jakaya Kikwete amesema mipango ya kulipatia taifa umeme wa uhakika itakamilika baada ya miaka miwili ijayo.
 Akihutubia taifa katika hotuba yake ya kufunga mwezi wa Februari jana, Rais Kikwete alisema, "Waswahili wana msemo usemao, jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu. Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika.
 "Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme," alisema Rais Kikwete na kuongeza:

Hivi ukame unatuhusu ni nini katika kuzalisha umeme na sisi tuna malighafi kibao..........................kweli penye miti hakuna wajenzi..................................hivi hiyo gesi na makaa ya mawe nayo tunahitaki kudra ya Mwenyezi Mungu ili tuzalishe umeme????????????????
 
Mgawo wa umeme waleta hasara TTPL


na Neema Kishebuka, Tanga


amka2.gif
ZAIDI ya sh milioni 10 zimepotea katika Kiwanda cha Tanga Pharmaceuticals Limited (TTPL) mkoani hapa kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara na ukosefu wa miundombinu ya vyoo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Mohamed Raza, wakati alipokuwa kikabidhi zawadi kwa wafanyakazi bora kiwandani hapo.
Raza alisema kutokana na kiwanda hicho kuwa na mitambo ya kisasa yenye gharama kubwa, tatizo limekuwa ni kukatika kwa umeme ambapo mashine nyingi zinaungua unaporudi ghafla.
"Mashine zikiungua tunalazimika kuagiza spea zake kutoka nje ya nchi ambazo ni gharama na hii inaturudisha nyuma katika kuendeleza kiwanda hiki chenye wafanyakazi zaidi ya 900," alisema Raza ambaye kiwanda chake kinazalisha poda ya Vestilline na mafuta ya kupaka ya aina mbalimbali.
Aliongeza kuwa wakati mwingine umeme unakatika kiwanda kinakuwa hakizalishi huku wafanyakazi wakihitaji kulipwa, hali inayoongeza hasara kwa kiwanda hicho.
Tatizo jingine la kiwanda hicho ni ukosefu wa miundombinu ya kusafirisha maji taka, ambapo kiwanda hicho kina mashimo manne ya maji taka ambayo hayakidhi mahitaji ya wafanyakazi wake.
"Pesa tunayolipa halmashauri ya jiji ni nyingi, hivyo tunaiomba serikali kuliangalia suala hili, ikiwezekana uwekwe mtandao wa maji taka eneo hili la Duga," alisema.
Aliongeza kusema kuwa ukosefu wa miundombinu ya maji taka unasababisha kiwanda kutofikia lengo lake la kuajiri wafanyakazi zaidi ya 1,200 kutokana na kukosekana kwa huduma bora ya maji taka.
"Tunashindwa kufikia malengo ya ajira kutokana na kuwa hapa tunao wafanyakazi 900, lakini maji taka yanajaa haraka, sasa tukiongeza watu itakuwa hatari zaidi, kwani kila mtu kama atatumia lita 20 za maji kwa siku tutakuwa tunazalisha maji taka mengi zaidi na kushindwa pa kuyapeleka," aliongeza mkurugenzi huyo.
Katika sherehe za kukabidhi zawadi kwa wafanyakazi bora, kiwanda kimetumia zaidi ya sh milioni 50, zawadi zilizotolewa ni pikipiki 12 mashine za kupooza maji 21 na baiskeli 106.


h.sep3.gif
 
Tanesco: No Dowans letter




By Judica Tarimo



1st March 2011







Comments




headline_bullet.jpg
``We`re negotiating on switching on the Dowans power generation plant``



Dowawnsmitambo.jpg

Dowans power plant


Top management of Tanzania Electric Supply Company Limited (Tanesco) said yesterday it has received no letter from Dowans on the latter's intention to forgive the compensation award.
"Talks on the 94bn/- compensation offer are yet to start because we have not received any letter from Dowans on the subject," said Tanesco Managing Director William Mhando in an exclusive interview with The Guardian yesterday.
The latest statement by Tanesco's top official runs contra to the call by the Parliamentary Energy and Mineral watchdog on the power firm to respond to the Dowans offer.
Dowans said in a statement recently that it has already written to Tanesco expressing its intention to forgive the 94bn/- compensation.
In its verdict in November last year, the International Chamber of Commerce (ICC) ruled that Tanesco should pay Dowans the hefty amount for breach of contract between the two.
The decision has since then provoked a series of heated debates in both public and private circles, with many Tanzanians saying the penalty was unjustified.
Speaking to journalists recently during a tour by the Parliamentary Energy and Minerals Committee of the International Power Tanzania Limited (IPTL), Dowans finance director Stanley Munai said: "We have written to Tanesco regarding our intention to forgive the 94bn/- compensation, but the latter seems reluctant to accept the offer… they have yet to reply to our letter."
However, Tanesco managing director said the state-run firm is yet to receive the said letter from Dowans.
"It's good that you got Dowans version of the (compensation) story and contacted us for confirmation…let me insist that we have not received an official letter from them that they are forgiving the debt. There are no talks going on regarding the matter," Mhando said.
"So, what you heard or saw in the media is totally untrue…how could we dare refuse an offer?" Tanesco chief wondered without giving details.
Mhando, however said the two parties have started negotiations on switching on the power generation plant owned by Dowans.
This is seen as a strategic move by power stakeholders, industrialists, investors and ordinary people to mitigate the negative impact of the country's power crisis.
The question whether or not the Dowans power generation plant should be switched on would be determined by the outcome of the ongoing talks and the subsequent signing of the agreement.
"We may or may not sign a contract with Dowans to switch on the plant…but all this including the payment modalities would be decided by the talks. The public would be informed on the outcome today or tomorrow," he said.
In his statement last week, Dowans finance director said the private power firm reached the decision to forgive the 94bn/-, following outcries by Tanzanians, but wants Tanesco to only pay USD24m being services-related debts.
When reached for comment, The Parliamentary Energy and Minerals Committee chairman, January Makamba said the fact that Dowans had communicated, in writing with Tanesco on the 94bn/- offer was "public knowledge."
"But if Tanesco managing director says he has not received the letter, then that is something else…I have no comment on that. However, I am still of the view that the offer is a good opportunity," he said, adding: "We agreed that Tanesco should be the main speaker on this controversy."



SOURCE: THE GUARDIAN
 
Zigo la Dowans wabebe waliolileta na wanaolitetea
ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

amka2.gif
LIPO zigo, zigo lisilobebeka, lipo zigo zigo lisilosogezeka, lipo zigo zigo lisiloachika! Zigo linaloelemea ambalo Watanzania wanaambiwa kwa kila maneno matamu kuwa wakiinama na kulibeba katika migongo yao iliyokunjika kwa kazi ngumu basi matatizo yao yatakwisha.
Naam! Zigo hili la Dowans ambalo limeingizwa kinyemela linazidi kupambwa kuwa ni suluhisho la matatizo yetu ya nishati ya umeme kwa wakati huu na sasa hoja imezidi kutiwa chumvi (baada ya kutiwa limau na mdalasini) kuwa ni suluhisho la matatizo yetu ya uchumi, na tukiendelea muda si mrefu tutasikia kuwa Dowans ndilo suluhisho la matatizo ya Gongo la Mboto, UKIMWI, watoto wa mitaani, barabara mbovu n.k.
Tukiendelea kuwachekea na kukumbatia zigo hilo tutajikuta tumeamini kabisa kuwa kakampuni ka Dowans ndiko dawa ya matatizo yetu yote.
Tatizo ni kuwa zigo lenyewe halibebeki, halitelekezeki, haliachiki na kwa hakika halilipiki!
Katika mazungumzo yake na wahariri mmiliki mmojawapo wa Dowans Tanzania Limited na aneyedhaniwa kuwa ni mmiliki wa Dowans Holdings S.A ya Costa Rica hakutaka kusema ukweli wote kwa Watanzania pale alipojitokeza siku chache tu zilizopita.
Katika mazungumzo yake ambayo yalikuwa na lengo la kuwafanya Watanzania wamuonee huruma kuwa anaonewa na kuwa kampuni yake ndilo suluhisho pekee la matatizo ya nishati nchini hakutaka kusema ukweli wote ya kitu gani kimemsukumua kujitokeza hadharani zaidi ya miaka mitano tangu alipojilengesha yeye na Rostam kujitengenezea utajiri wa haraka haraka wa kuongeza katika utajiri walio nao.
Mtu yeyote mwenye uwezo kidogo tu wa kufikiri na ambaye hahitaji hata kwenda Chuo Kikuu (anaweza kupita nje tu ya majengo ya chuo kikuu na kupata hekima) alihitaji kujiuliza swali moja muhimu tu baada ya Al Adawi kujitokeza na hasa baada ya jitihada zinazofanywa kwa kila namna na wasiasa wetu uchwara wa kulazimisha kampuni ya Dowans katika makoo ya watanzania ni hili: kwanini wameing'ang'ania Dowans kama suluhisho la mgao wa umeme nchini?
Ukiwasikiliza sana watetezi wa Dowans utaona kuwa kwa miaka yote hii hakuna kitu kilichobadilika. Kama hauna kumbukumbu unaweza kuamini kuwa wazo la Dowans kama suluhisho la umeme limekuja hivi juzi baada ya mgao kuongezeka.
Kama ndio leo tu umeanza kufuatilia sakata hili na ukawasikiliza hawa watetezi wa Dowans unaweza kuamini kabisa kuwa wanachopigania ni kuinua maisha ya Watanzania na kuwa wanataka kweli kabisa kupunguza ukali wa tatizo la umeme nchini.
Utaona kuwa hoja ya sasa hivi ambayo imepangwa vizuri sana inasikika namna hii: kwanza, tatizo la nishati ni kubwa sana na lina athari kubwa ya kiuchumi na pili kwa vile majenereta ya Dowans yapo tayari na katika hali nzuri basi tuyawashe tu hata kwa mkataba wa muda mfupi ili kupunguza makali ya mgao wa umeme.
Hoja hizi mbili ni hoja zenye lengo la kugusa hisia na vionjo. Yaani, zinataka watu wafikie uamuzi kwa kuangalia hisia zao na siyo akili zao.
Tatizo la hoja hizo mbili kwa kifupi ni kuwa tatizo la mgao wa umeme halikuanza leo na gharama yake katika uchumi wetu hazikuanza jana au mwaka huu. Kutokana na uongozi mbovu wa serikali ya CCM kwa karibu miaka ishirini Tanzania na Watanzania wamejikuta wakilipa gharama kubwa sana katika nishati ya umeme.
Kuanzia kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, manunuzi ya mafuta na majenereta na vipuri vyake Watanzania wamejikuta wakibeba mzigo ambao wengine wanauona wa kawaida kabisa.
Imefikia sasa hata watu wanaouza nyumba inabidi waoneshe kama nyumba ina jenereta! Hakuna mfanyabiashara ambaye atapanga biashara yake akitegemea umeme wa TANESCO. Hili ndugu zangu halikuanza jana au mwaka jana.
Tangu Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Madini alikuwa anajua tatizo hili na viongozi wote wa CCM ambao leo wanajipendekeza kuwa ni mashujaa wa kutatua tatizo la nishati walikuwa na miaka ishirni ya kufanya hivyo lakini wameshindwa.
Ukweli huu hakuna anayeweza kuupanga zaidi ya kutatufa maneno ya kutuelezea "nia nzuri, mikakati ya muda mrefu, mipango endelevu" na porojo nyingine ambazo zimekuwa kama wimbo uliokaririwa na kasuku kwa miaka karibu hamsini sasa.
Nitawaachia wengine waeleze kwanini uongozi wa chama na serikali ambayo kwa miaka hamsini imeweza kufikisha umeme kwa asilimia 14 tu tuamini kuwa leo ghafla wamepata uvuvio wa kutatua tatizo la kushindwa kwao ati kwa kwa mkataba wa muda mfupi au hata kwa mkataba mwingine wa muda mrefu.
Tatizo la pili hata hivyo ambalo linahusiana na Al Adawi ni kuwa hoja za kuwa "mitambo ya Dowans ipo na inahitaji kuwashwa" tu inapuuzia hoja zilizopo dhidi ya Dowans. Watetezi wa Dowans hawataki kuzungumzia tatizo la msingi la kimaadili na hata la kisheria ambalo lipo. Wako tayari kuzungumzia suala la hukumu ya ICC lakini hawataki kuzungumzia jambo ambalo ni kubwa zaidi ambalo hata Al Adawi hataki kulizungumzia. Kwamba, kampuni ya Dowans iliingia nchini kiulaghai, ikajirithisha mkataba kiulaghai, na kwa kutumia hadaa ikaweza kushinda kesi ya ICC.
Ndio maana nilijikuta nimefikia kilele cha dharau kwa waandishi wetu (wengine wanajiita wahariri) ambao walipata nafasi ya kumuuliza maswali makini Al Adawi na badala yake wakajiuma uma neno na kujivua nguo kiasi kwamba hawakuweza kurekodi sauti wala picha wala video! Na ndio maana kutokana na hilo nimefikia hitimisho kuwa hata waandishi wetu wanaopata nafasi ya kuwauliza maswali viongozi wetu iwe Rostam au Kikwete wanakwepda kuuliza maswali ya ukweli na badala yake wanauliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu. Na matokeo yake majibu wanayopewa hayasababishi maswali ya ziada ya kina.
Tulichokiona kwa wahariri wetu ni kuwa vipaza sauti vya Al Adawi kama ambavyo vimetumika kuwa vipaza sauti vya Rostam ambaye ameshindwa kujibu maswali ya msingi – kwa sababu hawakuulizwa. Hivyo, kwa manufaa ya waandishi hawa na watendaji wengine na wananchi wengine ambao bado hawajui tatizo la Dowans "ni nini hasa?' nimejitolea kuandika kwa kifupi sana suala hili tena kwani kwa miaka karibu mitano nimeliandika kwa kirefu sana!
Nikiwasamehe waandishi wetu kuwa walipitiwa na kuwa hawakujua cha kuuliza kwa sababu walipigwa na bumbuwazi naweza kusema kuwa inahitajika ujasiri wa pekee wa kuwauliza hawa waliolileta zigo hilo Tanzania na wakati umefika tuungane kwa sauti moja kukataa kuchezewa akili na kikundi cha watu wachache.
Inawezekana vipi watu wawili au watatu wawe na nguvu ya kuamua hatima ya taifa zima kwa namna hii? Kwanini Rostam Aziz hasemi ni nani huyo aliyemtuma kwenda kumuomba azungumze na Al Adawi.
Inawezekana ni kutokana na ukweli kwamba mtu aliyemuagiza amfuate Al Adawi ndiye mtu pekee ambaye anasema hamjui mmiliki wa Dowans? Yawezekana kuwa ni mtu ambaye kutaja jina lake na cheo chake ni tishio kwa watu wengine?
Vinginevyo tunaweza vipi kuelezea inakuwaje mtu pekee ambaye alikuwa anajua undani wa kampuni ya Dowans na ambaye kwa neno lake tu angeweza kuzuia TANESCO kuingizwa mkenge wa kihistoria hajawahi kuulizwa na chombo chochote cha usalama?
Inawezekana vipi mtu ambaye hakuwa tayari kujitokeza toka mwanzo hatimaye amepata ujasiri kuja hadharani na kuzungumza kuwa yeye ndiye mwakilishi wa Dowans na hakuna mtu hata mmoja aliyeapa kulinda katiba ambaye ameweza hata kumuuliza. Yaani, hata Rais wetu ameshindwa kumuuliza Rostam kuwa mmiliki ni nani!
Katika mazingira haya kweli mnafikiri kuna mtu ana uwezo au ubavu wa kuzuia mitambo ya Dowans isiwashwe? Mnafikiri katika safu ya watendaji wa vyombo vya sheria na usalama kuna yeyote mwenye ujasiri wa kusimama na kusema sheria kweli ifuatwe kama sheria hiyo inaweza kugusa wasiogusika? Jawabu la maswali hayo linajulikana katika mioyo ya Watanzania
Lakini zigo lisilobebeka, ni vipi watu wanaweza kutwishwa?
 
Makinda kutangaza mitambo ya Dowans iwashwe au la! Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 21:23 0diggsdigg

Sadick Mtulya
WAKATI suala la kuwashwa mitambo ya Dowans likiwa halijulikani, sasa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema taarifa ya mikakati ya muda mefu na mfupi kukabili kero hiyo, iliyopendekeza itatangazwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda.

Nchi ipo katika tatizo kubwa la mgawo wa umeme na kusababisha kuwapo kwa msuguano wa kutaka mitambo ya Kampuni ya Dowans, iwashwe kwa haraka kupunguza mgawo huo au isiwashwe.

Wafanyabiashara wengi, wamiliki wa viwanda na wasomi wanataka kuwashwa kwa mitambo hiyo, huku baadhi ya wananchi wakipinga hatua hiyo.

Hata hivyo, Kamati ya Bunge inayoongozwa na Januari Makamba iliyokuta jijini Dar es Salaam jana kwenye ofisi ndogo za Bunge na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ilikamilisha majuimuisho ya mapendekezo ya ripoti hiyo.

Jana, Makamba alisema kamati yake itakabidhi ripoti hiyo, ofisi ya Bunge na kwamba ndio itakayokuwa na mamlaka ya kutangaza au kutoitangaza ripoti hiyo.

"Pamoja na mambo mengine, kanuni za Bunge ndizo zinatutaka kufanya hivyo,'' alisema Makamba.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu huenda ripoti hiyo ikatangazwa leo.

Wakati huo huo, habari zimeeleza kuwa mitambo ya Dowans inaweza kuwashwa wiki hii.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #4 mkweli 2011-03-02 08:41 KWA VILE KIKWETE AMESAFIRI BASI JIBU LISHAJULIKANA, KWAMBA "MAKINDA TANGAZIA UMMA KUWA MITAMBO IWASHWE". UKWELI NI KWAMBA LOLOTE ATAKALOSEMA MAKINDA HILO NI AGIZO LA RAIS. MSITUDANGANYE MAKINDA NI KIVULI KISICHOELEWA CHOCHOTE.
Quote









0 #3 Vincent 2011-03-02 08:27 Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali ili itekeleze majukumu yake; kama inafikia Bunge ndilo linafanya maamuzi ya kiserikali hayo maamuzi yakiwa na dosari nani atahoji?
Quote









+1 #2 maharagejuma 2011-03-02 03:26 MITAMBO IO IMESHAWASHWA KWANI MAKINDA NDIO SEHEMU YA DOWANS UNATEGEMEA NINI. MAKAMBA KAZI ALIOTUMWA KAIMALIZA. ILA TUNAWAAMBIA NGUVU YA UMMA IPO NA ITAWAONYESHA KUWA NYIE MAFISADI HAMWEZI KITU. MAFISADI KIKWETE,ROSTAM MLICHOKITAKA MMEFANIKIWA ILA HUKUMU YENU INAKUJA SIO MUDA MREFU.
Quote









0 #1 DESRE 2011-03-02 02:40 huyu bibi atakubali tu iwashwe mie ananikera aaaah amechafua nafasi ya mr. six,kuongea hajui,sheria za bunge hazijui yaa yupo yupo tu
Quote

 
Makinda kutangaza mitambo ya Dowans iwashwe au la! Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 21:23 0diggsdigg

Sadick Mtulya
WAKATI suala la kuwashwa mitambo ya Dowans likiwa halijulikani, sasa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, imesema taarifa ya mikakati ya muda mefu na mfupi kukabili kero hiyo, iliyopendekeza itatangazwa na Spika wa Bunge, Anna Makinda.

Nchi ipo katika tatizo kubwa la mgawo wa umeme na kusababisha kuwapo kwa msuguano wa kutaka mitambo ya Kampuni ya Dowans, iwashwe kwa haraka kupunguza mgawo huo au isiwashwe.

Wafanyabiashara wengi, wamiliki wa viwanda na wasomi wanataka kuwashwa kwa mitambo hiyo, huku baadhi ya wananchi wakipinga hatua hiyo.

Hata hivyo, Kamati ya Bunge inayoongozwa na Januari Makamba iliyokuta jijini Dar es Salaam jana kwenye ofisi ndogo za Bunge na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ilikamilisha majuimuisho ya mapendekezo ya ripoti hiyo.

Jana, Makamba alisema kamati yake itakabidhi ripoti hiyo, ofisi ya Bunge na kwamba ndio itakayokuwa na mamlaka ya kutangaza au kutoitangaza ripoti hiyo.

“Pamoja na mambo mengine, kanuni za Bunge ndizo zinatutaka kufanya hivyo,’’ alisema Makamba.

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu huenda ripoti hiyo ikatangazwa leo.

Wakati huo huo, habari zimeeleza kuwa mitambo ya Dowans inaweza kuwashwa wiki hii.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #4 mkweli 2011-03-02 08:41 KWA VILE KIKWETE AMESAFIRI BASI JIBU LISHAJULIKANA, KWAMBA "MAKINDA TANGAZIA UMMA KUWA MITAMBO IWASHWE". UKWELI NI KWAMBA LOLOTE ATAKALOSEMA MAKINDA HILO NI AGIZO LA RAIS. MSITUDANGANYE MAKINDA NI KIVULI KISICHOELEWA CHOCHOTE.
Quote









0 #3 Vincent 2011-03-02 08:27 Kazi ya Bunge ni kuisimamia Serikali ili itekeleze majukumu yake; kama inafikia Bunge ndilo linafanya maamuzi ya kiserikali hayo maamuzi yakiwa na dosari nani atahoji?
Quote









+1 #2 maharagejuma 2011-03-02 03:26 MITAMBO IO IMESHAWASHWA KWANI MAKINDA NDIO SEHEMU YA DOWANS UNATEGEMEA NINI. MAKAMBA KAZI ALIOTUMWA KAIMALIZA. ILA TUNAWAAMBIA NGUVU YA UMMA IPO NA ITAWAONYESHA KUWA NYIE MAFISADI HAMWEZI KITU. MAFISADI KIKWETE,ROSTAM MLICHOKITAKA MMEFANIKIWA ILA HUKUMU YENU INAKUJA SIO MUDA MREFU.
Quote









0 #1 DESRE 2011-03-02 02:40 huyu bibi atakubali tu iwashwe mie ananikera aaaah amechafua nafasi ya mr. six,kuongea hajui,sheria za bunge hazijui yaa yupo yupo tu
Quote
 
Wafanyabiashara, wananchi wavutana kuhusu Dowans Send to a friend Saturday, 26 February 2011 21:43

Sadick Mtulya

WAKATI Wafanyabiashara nchini wakitaka mitambo ya Dowans iwashwe, wananchi wamepinga wakitaka itafutwe mitambo mingine kupunguza tatizo la umeme nchini.

Msimamo huo wawananchi ulijionyesha wazi jijini Dar es Salaam jana wakati wakichangia mada kwenye kikao cha wazi kilicholenga cha kukusanya maoni kuhusu suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini.

Hatua ya wananchi hao kupinga kuwashwa kwa mitambo ya Dowans kunafuatia wadau wengi hasa wasomi, wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kutaka mitambo hiyo iwashwe kama njia ya haraka na suluhisho la muda mfupi la kupatikana kwa umeme.

Hatua hiyo ililenga kuongeza kiwango cha nishati hiyo kilichopungua katika gridi ya taifa kutokana na kushuka kwa uzalishaji katika mitambo ya umeme Mtera kulikosababishwa na maji kupugua.

Mbali ya mitambo hiyo ya Dowans mitambo mingine inayotajwa kama suluhisho la tatizo la umeme ni ya IPTL iliyopo Tegeta na Songas iliyopo Ubungo.

Kwa sasa gridi ya taifa ina upungufu wa megawati 297 kufuatia vyanzo vilivyopo kuzalisha megawati 540 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 833 za umeme.

"Kwa kifupi Watanzania hatuko radhi mitambo ya Dowans kuwashwa. ikiwashwa itatuchefua na kutupandisha hasira zaidi kwa kuwa bado tunaugulia machungu ya kulipa deni la Sh 94 bilioni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha,'' alisema mmoja wa wananchi hao, Sajuki Thomas aliyejitambulisha ni mkazi wa Ubungo.

Thomas alisema wananchi watafurahi endapo serikali itatumia sheria ya uhujumu uchumi kutaifisha mitambo ya Dowans.

"Kama serikali itaitaifisha mitambo ya Dowans na kisha ikaamuru kuwashwa, wananchi wengi tutafurahia uamuzi huo kwani hautatuongezea gharama za maisha,'' alisema.

Alan Mwaigaga, mkazi wa Mbeya alishauri Tanesco lisiingiliwe katika masuala ya kitaaluma na akitahadharisha kuwa siasa ndio imeathiri utendaji wa shirika hilo.

Hata hivyo, kulingana na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati hiyo, alishauri kuwepo kwa kampuni nyingine zitakazozalisha umeme na kuiuzia Tanesco ambayo itafanya kazi ya kuusamabaza na kuuza kwa wananachi lakini sio Dowans.

Mkurugenzi wa Tanzania Investment ConsultancyAgency (TICA), Maliki Kasambala alipendekeza kuundwa kwa kamati ya wataalamu itakayokaa na kutoa mapendekezo ya muda mrefu na muda mfupi ya kutatua suala la umeme.

"Nchi nyingi zimetumia wataalamu wake waliobobea katika nishati ya umeme, wakajifungia kwa muda fulani na kutoa mapendekeo ya suluhisho la umeme, hivyo kamati itafute wataalamu hao na iwape siku sita au saba,'' alisema.

Akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba, alisema kamati yake imepokea maombi mbalimbali na itakutana na Tanesco Jumanne ijayo kufanya majuimuisho na kisha kuikabidhi Serikali mapendekezo ya muda mrefu na mfupi ya suluhisho la tatizo la nishati ya umeme nchini.

Awali, Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando alisema hadi kufikia Julai mwaka huu mgawo utakuwa umekwisha kufuatia kufungwa mitambo miwili mipya ya kuzalisha umeme katika Jiji la Dar es Salaama na Mwanza.

Mwanzoni mwa wiki hii Kamati ya Nishati na Madini ilikutana na menejimenti ya Tanesco kwa zaidi ya saa tano ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Januari Makamba alisema: "Tunataka kujua mgawo wa umeme utaisha lini na utaishaje? Katika hili muwe wazi na sisi tuweze kusaidia mawazo yetu kuondoa tatizo hili na pia tujue mnaendeshaje Tanesco ili tusaidie kwa manufaa ya Watanzania."

Hata hivyo, iliripotiwa kuwa katika kikao hicho kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya wabunge na viongozi wa Tanesco huku ikidaiwa kuwa imeshindwa kutoa mikakati yake ya kumaliza mgawo wa umeme kwa kamati hiyo.

Tanesco pia ilidaiwa kukataa kuzungumzia suala la Dowans nje ya Mahakama na kuwashwa kwa mitambo hiyo ili itoe megawati100 za umeme ili kupunguza makali ya mgawo wa umeme unaondelea sasa.

Hata hivyo akizungumzia hitimisho la kikao baina yao na Tanesco alisema wameliagiza shirika hilo kuhakikisha hakuna utata wowote wa kisheria iwapo wataamua kuingia mkataba na kampuni hiyo na kushauri uwe wa muda mfupi usiozidi miezi minne.

Alhamisi wiki hii Dowans iliripotiwa kuigeuzia kibao Tanesco na kulilaumu kwa mgao mkali wa umeme unaoendelea nchini ikisema imechangia tatizo hilo kwa kugoma kufanya nayo mazungumzo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania, Stanley Munai, alisema jijini Dar es Salaam kuwa pamoja na juhudi za kampuni yake kutaka mara kadhaa kuzungumza na shirika hilo nje ya mahakama lakini Tanesco imekuwa kimya.
Alisema bosi wao Al Adawi, anayeelezwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni hiyo ya Dowans, alikuja nchini na kuiandikia barua Tanesco kutaka mazungumzo nao, bado shirika hilo limekaa kimya bila kujibu.

Katika hatua nyingine, mgawo wa umeme unaondelea nchini kote, umeelezwa kuwa utapunguza pato la nchi(GDP) la mwaka, kwa asilimia 5 sawa na Sh1.75 trilion huku makusanyo ya mapato yatokanayo na kodi yakipungua kwa asilimia 30, ambazo ni zaidi ya Sh840 bilioni.

Akichangia mada katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Servacius Likwelile alisema endapo mgawo utaendelea Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka litapungua kwa asilimia 5 huku akieleza kuwa kwa sasa GDP ni Sh35 trilioni.

"Benki Kuu ya Dunia (WB) imeshatueleza kuwa mgawo wa umeme ukiendelea, asilimia kati ya tano na kumi ya pato la taifa kwa mwaka itapungua, jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa uchumi wa nchi,'' alisema Dk Likwelile.

Kufuatia hali hiyo, Dk Likwelile alishauri mfumo wa utoaji maamuzi ubadilike na kwamba taifa liwe na mikakati endelevu ya muda mrefu.

Alisema kulingana na hali halisi ilivyo mkazo mkubwa uelekezwe katika miradi ya maendeleo na kwamba ili kufanikiwa hilo kunahitajika msukumo wa utashi wa kisisasa.

"Ukweli ni kuwa imefika wakati matumizi ya Serikali yabadilike ikiwamo semina kupunguzwa,'' alisema.

Alisema pamoja na mambo mengine mgawo huo umesababisha mfumuko wa bei kwa asilimia 6.8

Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa Mamlaka ya Mapato(TRA), Tonedeus Muganyizi, alisema makusanyo ya mapato yatokanayo na kodi yatapungua kwa asilimia 30.

"Lengo la TRA kwa mwaka ni kukusanya Sh5.6 trilion lakini, kutokana na mgawo unaondelea uenda isikusanye mapato hayo na ikakusanya kwa asilimia 70,'' alisema Muganyizi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Sunday, 27 February 2011 09:15 Comments




0 #3 mpenda maendeleo 2011-03-01 14:17 Ndugu yangu tunatoa mawazo kwamba serikali itoe fedha za kutosha kununua mafuta ya katosha kuendesha mitambo ya IPTL kuanzia sasa mpaka hali ya umeme itakaporudi katika hali ya kawaida, kama mhando alivyosema kwamba mgao utaisha mwezi julai.basi wizara ya fedha toeni fedha za kuagiza mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL mpka mwezi julai.sio kutoa fedha za kununua mafuta ya mwezi mmoja na hali mkijua ugumu uliopo katika uagizaji wa mafuta hayo huchukua muda mrefu (miezi mitatu au zaidi)
Quote









0 #2 kisukulati 2011-02-28 00:13 Quoting salama:
IPTL imeshawashwa lakini haifanyi kwa uwezo wake kamili. Tatizo ni pesa ya mafuta. Mbona hawaongelei hayo, ni Dowans tu.

Salama, ni kweli kabisa unachosema kwa kua hamna vijisenti vya kununulia mafuta hayo, sasa hatujui hasa mipango yenyewe inavokwenda

Quote









0 #1 salama 2011-02-27 16:14 IPTL imeshawashwa lakini haifanyi kwa uwezo wake kamili. Tatizo ni pesa ya mafuta. Mbona hawaongelei hayo, ni Dowans tu.
Quote
 
Wafanyabiashara, wananchi wavutana kuhusu Dowans Send to a friend Saturday, 26 February 2011 21:43

Sadick Mtulya

WAKATI Wafanyabiashara nchini wakitaka mitambo ya Dowans iwashwe, wananchi wamepinga wakitaka itafutwe mitambo mingine kupunguza tatizo la umeme nchini.

Msimamo huo wawananchi ulijionyesha wazi jijini Dar es Salaam jana wakati wakichangia mada kwenye kikao cha wazi kilicholenga cha kukusanya maoni kuhusu suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini.

Hatua ya wananchi hao kupinga kuwashwa kwa mitambo ya Dowans kunafuatia wadau wengi hasa wasomi, wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kutaka mitambo hiyo iwashwe kama njia ya haraka na suluhisho la muda mfupi la kupatikana kwa umeme.

Hatua hiyo ililenga kuongeza kiwango cha nishati hiyo kilichopungua katika gridi ya taifa kutokana na kushuka kwa uzalishaji katika mitambo ya umeme Mtera kulikosababishwa na maji kupugua.

Mbali ya mitambo hiyo ya Dowans mitambo mingine inayotajwa kama suluhisho la tatizo la umeme ni ya IPTL iliyopo Tegeta na Songas iliyopo Ubungo.

Kwa sasa gridi ya taifa ina upungufu wa megawati 297 kufuatia vyanzo vilivyopo kuzalisha megawati 540 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 833 za umeme.

“Kwa kifupi Watanzania hatuko radhi mitambo ya Dowans kuwashwa. ikiwashwa itatuchefua na kutupandisha hasira zaidi kwa kuwa bado tunaugulia machungu ya kulipa deni la Sh 94 bilioni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha,’’ alisema mmoja wa wananchi hao, Sajuki Thomas aliyejitambulisha ni mkazi wa Ubungo.

Thomas alisema wananchi watafurahi endapo serikali itatumia sheria ya uhujumu uchumi kutaifisha mitambo ya Dowans.

“Kama serikali itaitaifisha mitambo ya Dowans na kisha ikaamuru kuwashwa, wananchi wengi tutafurahia uamuzi huo kwani hautatuongezea gharama za maisha,’’ alisema.

Alan Mwaigaga, mkazi wa Mbeya alishauri Tanesco lisiingiliwe katika masuala ya kitaaluma na akitahadharisha kuwa siasa ndio imeathiri utendaji wa shirika hilo.

Hata hivyo, kulingana na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati hiyo, alishauri kuwepo kwa kampuni nyingine zitakazozalisha umeme na kuiuzia Tanesco ambayo itafanya kazi ya kuusamabaza na kuuza kwa wananachi lakini sio Dowans.

Mkurugenzi wa Tanzania Investment ConsultancyAgency (TICA), Maliki Kasambala alipendekeza kuundwa kwa kamati ya wataalamu itakayokaa na kutoa mapendekezo ya muda mrefu na muda mfupi ya kutatua suala la umeme.

“Nchi nyingi zimetumia wataalamu wake waliobobea katika nishati ya umeme, wakajifungia kwa muda fulani na kutoa mapendekeo ya suluhisho la umeme, hivyo kamati itafute wataalamu hao na iwape siku sita au saba,’’ alisema.

Akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba, alisema kamati yake imepokea maombi mbalimbali na itakutana na Tanesco Jumanne ijayo kufanya majuimuisho na kisha kuikabidhi Serikali mapendekezo ya muda mrefu na mfupi ya suluhisho la tatizo la nishati ya umeme nchini.

Awali, Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando alisema hadi kufikia Julai mwaka huu mgawo utakuwa umekwisha kufuatia kufungwa mitambo miwili mipya ya kuzalisha umeme katika Jiji la Dar es Salaama na Mwanza.

Mwanzoni mwa wiki hii Kamati ya Nishati na Madini ilikutana na menejimenti ya Tanesco kwa zaidi ya saa tano ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Januari Makamba alisema: "Tunataka kujua mgawo wa umeme utaisha lini na utaishaje? Katika hili muwe wazi na sisi tuweze kusaidia mawazo yetu kuondoa tatizo hili na pia tujue mnaendeshaje Tanesco ili tusaidie kwa manufaa ya Watanzania."

Hata hivyo, iliripotiwa kuwa katika kikao hicho kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya wabunge na viongozi wa Tanesco huku ikidaiwa kuwa imeshindwa kutoa mikakati yake ya kumaliza mgawo wa umeme kwa kamati hiyo.

Tanesco pia ilidaiwa kukataa kuzungumzia suala la Dowans nje ya Mahakama na kuwashwa kwa mitambo hiyo ili itoe megawati100 za umeme ili kupunguza makali ya mgawo wa umeme unaondelea sasa.

Hata hivyo akizungumzia hitimisho la kikao baina yao na Tanesco alisema wameliagiza shirika hilo kuhakikisha hakuna utata wowote wa kisheria iwapo wataamua kuingia mkataba na kampuni hiyo na kushauri uwe wa muda mfupi usiozidi miezi minne.

Alhamisi wiki hii Dowans iliripotiwa kuigeuzia kibao Tanesco na kulilaumu kwa mgao mkali wa umeme unaoendelea nchini ikisema imechangia tatizo hilo kwa kugoma kufanya nayo mazungumzo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania, Stanley Munai, alisema jijini Dar es Salaam kuwa pamoja na juhudi za kampuni yake kutaka mara kadhaa kuzungumza na shirika hilo nje ya mahakama lakini Tanesco imekuwa kimya.
Alisema bosi wao Al Adawi, anayeelezwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni hiyo ya Dowans, alikuja nchini na kuiandikia barua Tanesco kutaka mazungumzo nao, bado shirika hilo limekaa kimya bila kujibu.

Katika hatua nyingine, mgawo wa umeme unaondelea nchini kote, umeelezwa kuwa utapunguza pato la nchi(GDP) la mwaka, kwa asilimia 5 sawa na Sh1.75 trilion huku makusanyo ya mapato yatokanayo na kodi yakipungua kwa asilimia 30, ambazo ni zaidi ya Sh840 bilioni.

Akichangia mada katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Servacius Likwelile alisema endapo mgawo utaendelea Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka litapungua kwa asilimia 5 huku akieleza kuwa kwa sasa GDP ni Sh35 trilioni.

“Benki Kuu ya Dunia (WB) imeshatueleza kuwa mgawo wa umeme ukiendelea, asilimia kati ya tano na kumi ya pato la taifa kwa mwaka itapungua, jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa uchumi wa nchi,’’ alisema Dk Likwelile.

Kufuatia hali hiyo, Dk Likwelile alishauri mfumo wa utoaji maamuzi ubadilike na kwamba taifa liwe na mikakati endelevu ya muda mrefu.

Alisema kulingana na hali halisi ilivyo mkazo mkubwa uelekezwe katika miradi ya maendeleo na kwamba ili kufanikiwa hilo kunahitajika msukumo wa utashi wa kisisasa.

“Ukweli ni kuwa imefika wakati matumizi ya Serikali yabadilike ikiwamo semina kupunguzwa,’’ alisema.

Alisema pamoja na mambo mengine mgawo huo umesababisha mfumuko wa bei kwa asilimia 6.8

Naye Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa Mamlaka ya Mapato(TRA), Tonedeus Muganyizi, alisema makusanyo ya mapato yatokanayo na kodi yatapungua kwa asilimia 30.

“Lengo la TRA kwa mwaka ni kukusanya Sh5.6 trilion lakini, kutokana na mgawo unaondelea uenda isikusanye mapato hayo na ikakusanya kwa asilimia 70,’’ alisema Muganyizi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Sunday, 27 February 2011 09:15 Comments




0 #3 mpenda maendeleo 2011-03-01 14:17 Ndugu yangu tunatoa mawazo kwamba serikali itoe fedha za kutosha kununua mafuta ya katosha kuendesha mitambo ya IPTL kuanzia sasa mpaka hali ya umeme itakaporudi katika hali ya kawaida, kama mhando alivyosema kwamba mgao utaisha mwezi julai.basi wizara ya fedha toeni fedha za kuagiza mafuta ya kuendesha mitambo ya IPTL mpka mwezi julai.sio kutoa fedha za kununua mafuta ya mwezi mmoja na hali mkijua ugumu uliopo katika uagizaji wa mafuta hayo huchukua muda mrefu (miezi mitatu au zaidi)
Quote









0 #2 kisukulati 2011-02-28 00:13 Quoting salama:
IPTL imeshawashwa lakini haifanyi kwa uwezo wake kamili. Tatizo ni pesa ya mafuta. Mbona hawaongelei hayo, ni Dowans tu.

Salama, ni kweli kabisa unachosema kwa kua hamna vijisenti vya kununulia mafuta hayo, sasa hatujui hasa mipango yenyewe inavokwenda

Quote









0 #1 salama 2011-02-27 16:14 IPTL imeshawashwa lakini haifanyi kwa uwezo wake kamili. Tatizo ni pesa ya mafuta. Mbona hawaongelei hayo, ni Dowans tu.
Quote
 
Mahakama yazuia mkataba wa Tanesco, Dowans Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 20:50

janmakamba.jpg
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini,Januari Makamba

Sadick Mtulya na James Magai
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imependekeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuingia mkataba mpya na Kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikiwa ni hatua za muda mfupi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Hata hivyo, Mahakama Kuu imeizuia Serikali na Tanesco kuchukua hatua yoyote inayohusiana na mazungumzo au mkataba wa aina yoyote baina yake na Dowans bila ridhaa yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Januari Makamba alisema: "Kamati imependekeza mambo 30 ikiwamo kuwashwa kwa mitambo ya Dowans haraka na serikali itoe fedha zaidi kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL. Hatua hii imefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.''

Makamba alisema pia kwamba kamati imependekeza kupunguzwa kwa megawati 50 kutoka katika migodi ya madini inayotumia umeme wa megawati 125 ili zipelekwe kwa wananchi.

Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga alisema mapendekezo hayo watayakabidhi katika Ofisi za Bunge na kwamba yatatangzwa na Spika, Anne Makinda

Lakini, wakati kamati ikitoa mapendekezo hayo, jana Jaji Emilian Mushi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam anayesikiliza maombi ya usajili wa tuzo ya Kampuni ya Dowans iliyoshinda iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara(ICC), dhidi ya Tanesco alitoa agizo kuwa lisifanyike jambo lolote kuhusu Dowans nje ya mahakama.

"Naagiza jambo lolote lisifanyike nje ya mahakama wakati ikiendelea na shauri hili. Kama kutahitajika kuwa na majadiliano yoyote basi pande husika zilete maombi mahakamani ili iweze kusimamisha kwanza mchakato huu kusubiri majadiliano hayo."

Jaji Mushi alisema: "Haitakuwa vyema mahakama kuendelea na mchakato wakati na huko nje majadiliano yakiendelea. Kama pande hizo zikiafikiana, basi zinaweza kuja ‘ku-withdraw' (kuondoa shauri) na kama zitashindwana basi ndipo tutakapoendelea na mchakato."

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Makamba zinasema kuwa mapendekezo ya kamati hiyo yamefikiwa kama suluhisho la muda mfupi la kupambana na mgawo.

Chanzo chetu ndani ya kamati hiyo, jana kiliiambia Mwananchi kuwa kamati imependekeza kabla ya kuwashwa mitambo hiyo, Tanesco liingie mkataba maalumu wa miezi michache usiokuwa na utata wa kisheria wa kuuziwa umeme na kampuni ya Dowans kulingana na mahitaji.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika mkataba huo kamati imependekeza Tanesco iuziwe umeme kwa uniti na kwamba iwe inalipa kila siku kulingana na kiwango inachouziwa.

"Kwa kuwa suala la gharama za uuzaji umeme kwa uniti ni la kitaalamu, kamati imependekeza Tanesco iingie mkataba maalumu wa miezi michache wa makubaliano ya kuuziwa nishati ya umeme na ilipe kulingana na uniti iliyouziwa,'' kilisema chanzo chetu.

Awali, kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati hiyo katika Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam, Makamba aliimbia Mwananchi kuwa: "Leo (jana) wajumbe wa kamati, tunakutana ili kusahihisha herufi, maneno pamoja na kuweka koma na nukta katika ripoti yetu ya mapendekeo ya suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini."

Mwenyekiti huyo alisema mapendekezo hayo yalifikiwa juzi katika kikao chao cha majumuisho na Tanesco kilichomalizika saa 2:00 usiku.

Tofauti ya wananchi na wafanyabiashara kuhusu Dowans
Hata hivyo, mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yametolewa kukiwa na msuguano kati ya wafanyabiashara na wananchi. Wafanyabiashara wanataka mitambo ya Dowans iwashwe huku baadhi ya wananchi wakipinga na kutaka itafutwe mitambo mingine kupunguza tatizo hilo.

Kwa takriban wiki mbili, kamati hiyo ilifanya vikao vya ndani na mikutano ya wazi na wadau mbalimbali kukusanya maoni kuhusu suluhisho la muda mfupi na mrefu la tatizo la umeme nchini.

Lakini Jumamosi iliyopita katika kikao cha wazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam baadhi ya wananchi walikataa kuwashwa kwa mitambo ya Dowans huku wasomi, wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara kutaka mitambo hiyo iwashwe ikiwa ni njia ya haraka na suluhisho la muda mfupi la kupatikana kwa umeme.

Hatua hiyo ililenga kuongeza kiwango cha nishati hiyo kilichopungua katika Gridi ya Taifa kutokana na kushuka kwa uzalishaji katika mitambo ya umeme Mtera kulikosababishwa na kupugua kwa maji.

Kwa sasa Gridi ya Taifa ina upungufu wa megawati 297 kwa kuwa vyanzo vilivyopo vinazalisha megawati 540 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 833 za umeme.

 
Kesi ya kupinga Dowans yanguruma


Na Waandishi Wetu

KESI ya kupinga serikali kulipa sh. bilioni 94 kwa kampuni ya Dowans imeanza kunguruma katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam jana huku ikielezwa
kuwa kelele za nje haziisumbui mahakama hiyo kuendelea kuisikiliza.

Kesi hiyo imefunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine 16 ya wanaharakati ikiwa na lengo la kupinga hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) iliyotolewa na Novemba 15, mwaka jana ikiliamuru Shirika la Umeme nchini (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kwa kuvunja mkataba baina yake na kampuni hiyo kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Mahakama hiyo, Gerald Aksen akisaidia na wasuluhishi, Swithin Munyantwali na Jonathan Parker.

Januari 25, mwaka huu Dowans iliwasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam maombi ya usajili wa tuzo yake hiyo kupitia kwa Wakili Kenedy Fungamtama, ili ulipwaji wa fidia yake hiyo ufanyike kwa mujibu wa taratibu, kitendo ambacho kinapingwa na wanaharakati, wakisema ni kinyume cha sheria.

Kesi hiyo jana ilitajwa ili kuangalia kama pande zote husika zimepatiwa nyaraka zote husika, na kubainika hazikuwa zimewafikia wote
mujibu wa sheria na taratibu za uendeshaji kesi, hivyo mahakama iliziagiza kupeana nyaraka hiyo.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju aliiomba mahakama kuu impatie siku 21 kujiandaa kwa ajili ya kujibu hoja zinazohusiana na kesi hiyo, huku Dkt. Mvungi akiomba siku saba kujiandaa baada ya hapo, kama kutakuwa na kitu chochote cha kujibu katika hoja hizo zitakazowasilishwa na upande wa serikali.

LHRC kwa niaba ya mashirika hayo wamewasilisha pingamizi lenye hoja saba kupitia Kampuni ya Uwakili ya South Law Chambers Advocates mbele ya Jaji Emilly Mushi.

Kwanza, wanadai kuwa hawakuridhika na tuzo hiyo iliyotolewa na ICC kwa Dowans kwani TANESCO ni shirika la umma linalomilikiwa na Serikali ya Tanzania na fedha zinazoiendesha zinatokana na Watanzania walipa kodi.

Katika hoja ya pili wanadai kuwa hakuna mkataba wa kisheria uliofungwa baina ya TANESCO na Kampuni ya Dowans uliosababisha kuwepo kwa mgogoro ulioilazimu ICC kutoa tuzo hiyo kwa kampuni hiyo.

Sambamba na hoja hiyo, wanaharakati hao wameambatanisha na mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond ambao Dowans iliurithi, unaodaiwa kuwa na mashaka kisheria, kama kielelezo.

Tatu, wanadai kuwa chini ya sheria za Tanzania, mkataba na tuzo hiyo kwa Dowans ni batili na umejaa dosari za kisheria.

Nne, wanaharakati hao wanadai kuwa chini ya sheria za Tanzania, Kampuni ya Richmond haikuwa na nguvu ya kisheria kuingia mkataba na Serikali ya Tanzania au na TANESCO, huku wakiambatanisha na kielelezo cha taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza uhalali wake.

Tano wameeleza kuwa kutokuwepo kwa mkataba hai kati ya Richmond na TANESCO, jukumu hilo lilitakiwa kutekelezwa na wajibu pingamizi wa kwanza na wa pili, ambalo ndilo lilisababisha kutolewa kwa tuzo hiyo kuwa batili, na hivyo tuzo iliyotolewa na ICC haiwezi kukubaliwa wala kutekelezwa na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Katika hoja ya sita ya pingamizi hilo, wanaharakati hao wanadai kuwa tuzo hiyo ilitolewa hata kabla ya mgogoro mwingine kutatuliwa katika mahakama nyingine ya Houston nchini Marekani, baina ya Richmond na Dowans Tanzania Limited juu ya umiliki wa mashine za kuzalishia umeme, ambazo zinahusiana na tuzo hiyo.

Katika hoja ya saba ya pingamizi hilo, wanaharakati hao wanadai kuwa maombi ya usajili wa tuzo iliyotolewa na ICC ambayo yamewasilishwa Mahakama Kuu hayapaswi kukubaliwa kwa kuwa imetokana na mkataba batili baina ya Richmond na TANESCO.

Kesi hiyo itaendelea tena Machi 30, mwaka huu, Jaji Mushi ataangalia kama taratibu na maamuzi aliyoyatoa yamezingatiwa na pande husika kama alivyoagiza.

 
Kamati ya Bunge yaamuru Dowans iwashwe
• Kesi ya fidia ya bilioni 94/- yasogezwa mbele Dar

na Betty Kangonga na Irene Mark


amka2.gif
KAMATI ya Nishati na Madini imeamuru kuwashwa mara moja kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans ili kupunguza tatizo la mgawo wa umeme.
Hatua hiyo ni kati ya maazimio na mapendekezo 30 yaliyofikiwa na kamati hiyo na huku ikisisitiza kuwa iwapo serikali itayatekeleza kwa haraka itasaidia kuiondoa nchi katika athari za kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika kwa muda wa siku 12, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), alisema kutokana na mitambo hiyo kuwepo nchini ni muhimu serikali iiwashe mara moja ili kuepukana na matatizo ya kiuchumi.
Alisema mapendekezo yaliyotolewa ni yale ya dharura, ya kati na ya muda mrefu ambapo katika moja ya mapendekezo ya dharura, kamati hiyo inataka kupunguzwe megawati 125 zinazotumika katika migodi 4 ya madini ili umeme huo uelekezwe kwa matumizi ya wananchi.
Makamba alisema migodi hiyo haijawahi kuathiriwa na tatizo la umeme hivyo kwa sasa inatakiwa ipunguziwe megawatts 50 na kusisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kufanyika hata sasa.
"Katika migodi hiyo hawajawahi kujua wala kuonja makali ya mgawo hivyo serikali ikiamua kulitekeleza hilo linawezekana hata leo hili megawat hizo zikafidie maeneo yenye mapungufu," alisema.
Alisema mbali na hiyo pia serikali inatakiwa kuhakikisha inatoa mafuta ya kutosha katika mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL ambapo hadi sasa inazalisha kati ya megawat 10 hadi 50 huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawat zaidi ya 80 hadi 90.
Alieleza kuwa iwapo serikali itashindwa kutekeleza mapendekezo hayo kuna uwezekano wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kupoteza kiasi cha sh bilioni 840 iwapo mgawo huo utaendelea katika kipindi cha mwaka huu.
Alisema mapato ya taifa yamepungua kwa asilimia tano ya pato la taifa ambayo ni sawa na dola bilioni 1.1.
"Mapendekezo na maazimio tuliyotoa ni yale ya kati, dharura na ya muda mrefu na iwapo serikali itatekeleza mapendekezo hayo basi tatizo la umeme litaisha katika kipindi cha wiki moja," alieleza.
Wakati huo huo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa siku 21 kwa pande mbili ambazo ni Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kupeana kwanza nyaraka za madai ya fidia ya sh bilioni 94 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kwa kampuni hiyo.
Aidha, mahakama hiyo imeamuru pia upande wa wapingaji wa fidia hiyo ambao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nao upewe nyaraka hizo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ombi hilo.
Ombi hilo lilifunguliwa mapema mwaka huu na Dowans ambayo inatetewa na wakili Kennedy Fungamtama dhidi ya TANESCO ambayo nayo inatetewa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Jamhuri Johnson, Dk. Angelo Mapunda na Florence Luoga.
Wapinga maombi ya Dowans ambao hawajaorodheshwa kwenye kesi hiyo ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinachotetewa na Dk. Sengondo Mvungi, Harold Sungusia na Francis Kiwanga na mwanahabari mkongwe ambaye hana wakili.
Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Emilian Mushi wakati kesi hiyo ya madai namba 8 ya mwaka huu ilipokuja kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kutajwa.
Alisema amefikia uamuzi wa kutoa amri hiyo baada ya wapinga maombi (LHRC na Timothy Kahoho) kueleza kuwa hawakuwa wamepatiwa nakala ya tuzo hiyo na wao hawajawapatia Dowans na TANESCO nakala za mapingamizi yao.
Jaji Mushi pia alikubaliana na maombi ya mawakili wa pande zote yaliyotaka pande zote katika kesi hiyo (Dowans na TANESCO) kuacha kufanya jambo lolote linalohusiana na masilahi ya pande hizo mbili hadi pale kesi hiyo itakapomalizika.
"Ila kama mlivyoomba nyie mawakili wa pande zote mbili kwamba endapo serikali kupitia TANESCO wakitaka kulimaliza jambo hili nje ya mahakama, mahakama hii inaziamuru pande hizo kabla ya kufikia uamuzi huo wa kumalizana nje ya mahakama au kuwasha mitambo, walete kwanza ombi mahakamani la kuomba kufanya hivyo.
"Na sioni haja ya kutoa amri ya kuwazuia wale wote wanaopiga kelele za Dowans, Dowans huko mitaani na kwenye vyombo vya habari kwa sababu sheria na utaratibu unaeleweka wazi kwamba kesi ikiwepo mahakamani ni marufuku kwa mtu au vyombo vya habari kuizungumzia …lakini mi nasema waache watu waendelee kupiga kelele zao huko mitaani kuhusu tuzo ya Dowans kwani napenda wajue kwamba mahakama hii haiyumbishwi na hizo kelele zao, kwani siku zote inafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria," alisema Jaji Mushi.
"Kwa sababu upungufu huo umejitokeza natoa siku 21, kwa pande mbili katika kesi hii na nyie wapingaji wawili, wenyewe kwa wenyewe muhakikishe mnapeana nyaraka mlizonazo na ninaiahirisha kesi hii hadi Machi 30 mwaka huu, ambapo kesi hii itakuja kwaajili ya kutajwa na kuangalia kama tayari mmeishapeana nyaraka hizo," alisema Jaji Mushi.
Awali wakili wa TANESCO, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju aliomba mahakama impatie siku 21 kujibu hoja za kutaka tuzo ya Dowans isisajiliwe. Naye wakili wa Dowans, Fungamtama pia aliomba mahakama impatie siku 21 kujibu pingamizi hilo litakalowasilishwa na TANESCO.
Kwa upande wake, wakili wa LHRC, Dk. Mvungi aliomba apatiwe siku saba kujibu hoja kama kutakuwa na cha kujibu.
Kahoho ambaye hana wakili, yeye alieleza kuwa kama maombi yake ya kupinga Dowans isisajiliwe yatawekewa pingamizi anaomba apewe siku 14 kujibu na kuiomba mahakama itoe amri ya kuzuia watu au vyombo vya habari kuchapisha habari ambazo zinaingilia mwenendo wa kesi hiyo.
Januari 25 mwaka huu, Dowans iliwasilisha ombi lake la kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania iisajili tuzo waliyopewa na Mahakama ya ICC na siku chache baadaye TANESCO, LHCR na Kahoho waliwasilisha hati ya nia ya kupinga ombi hilo la kutaka tuzo hiyo isajiliwe.
Mahakama ya ICC ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO, Novemba 15 mwaka jana, ambapo iliitia hatiani TANESCO kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans na ikaiamuru iilipe fidia ya shilingi bilioni 94.
 
Court issues stop order on Dowans plant Send to a friend Thursday, 03 March 2011 08:20

By Rosina Jn, The Citizen Correspondent
dowanssite.jpg
Dar es Salaam. The High Court yesterday issued an order barring the government and owner of the Dowans electricity generators from interfering with the plant, including switching it on to produce power, without the court's permission.

The order was given by Mr Justice Emilian Mushi following a request by lawyers that the status quo be maintained.

Dr Sengondo Mvungi, who was representing 16 human rights groups challenging the government's decision to pay Sh94 billion compensation to Dowans Holdings SA (DHSA) and Dowans Tanzania Limited (DTL), said there was too much interference, including the ongoing talks between Tanesco and the plant's owners on the possibility of switch the generators on.

He said it was against the law to continue discussing an issue that was already before the court.

Mr Justice Mushi said if there was issue regarding Dowans' operations, interested parties should file an application so that the court's process could be halted to enable the conclusion of that issue first.

He said if the parties would reach an agreement in the negotiations, the case would be withdrawn, otherwise the matter before the court would continue.

Mr Justice Mushi added that comments aired by other parties outside should not unsettle the court.

Court's order came at a time when negotiations have been going on between DTL and Tanesco on the possibility of reducing the compensation for breach of contract awarded to the latter by the International Chamber of Commerce (ICC) last November.

The two parties are also engaged in talks on the possibility of switching on the generators to obtain 100MW and ease the crippling power shortage in the country.

While the judge was issuing the order at the High Court, a few paces away at the parliamentary offices, the chairman of the Parliamentary Committee on Energy and Minerals, Mr January Makamba, asked the government to agree to proposals to have the Dowans turbines switched on to ease power rationing.

That was among 30 recommendations that the committee unanimously arrived at after 12 days of activities aimed to finding solutions to the power crisis.

And speaking in Dar es Salaam on Tuesday, Prime Minister Mizengo Pinda said the Dowans machines could be switched on to reduce the load shedding.

The objection by the Human Rights groups follows the filing at the High Court by Dowans Holdings SA (Costa Rica) and Dowans Tanzania Limited of an application seeking the registration of the ICC ruling.

The application came up for mention yesterday and the court wanted to confirm that parties were ready before hearing could begin.

However, it was established that some parties did not have relevant documents such as a copy of the ICC ruling and copies of objections raised by Tanesco and human rights groups.

The court thus directed parties having the documents to make them available to the other parties.

The court also gave the government 21 days to reply to Dowans' arguments in response to a request by Deputy Attorney General George Masaju, who is representing Tanesco.

For his side, Dr Mvungi asked for seven days to see if there was a need to prepare a response, while Mr Timothy Kahoho, who is representing ordinary wananchi, asked for 14 days to do the same.

In mid-November, last year, the ICC ordered Tanesco to pay Dowans tens of billions of shillings in damages resulting from a unilateral termination of a power generation contract.

The filing of the application to register the ruling has attracted several petitions to block the payment, with the Legal and Human Rights Centre (LHRC) asking the court not to register the award and instead refer the verdict back to the ICC for reconsideration of its legality.

The centre argues that the award was null and void on the grounds that it was improperly arrived at.

Tanesco has also filed a similar application in a bid to block the payments. Reports say some prominent lawyers will be joining Rex Attorneys to argue on behalf of the public utility in the petition.



UTILITY

CHRONOLOGY: TANESCO Vs DOWANS
November last year: ICC ordered Tanesco to pay Sh94 billion to Dowans in compensation for damages resulting from unlawful termination of a contract for power generation.

January 26: Dowans Holdings SA (Costa Rica) and Dowans Tanzania Limited filed application to the High Court seeking the registration of the award they won at the ICC.

January: Several petitions are filed to block the payment, with the Legal and Human Rights Centre (LHRC) asking the court not to register the award and instead order it be remitted to ICC for reconsideration of its legality.

February: Negotiations between Tanesco and Dowans over settlement of Sh94 billion arbitration award have officially started a move which may lead to switching on the emergency power firm's generators and ease power crisis in the country.

March: Parliamentary committee on Mineral and Energy advice the government to negotiate for switching on of Dowans generators to easy powe rationing.
 
Back
Top Bottom