Wabunge wajadili mitambo ya Dowans gizani Send to a friend Monday, 14 March 2011 21:29
Leon Bahati
SIKU ya kwanza ya wabunge kujadili mpango wa kubadilisha sheria ya manunuzi ili serikali iruhusiwe kununua mitambo iliyotumika ilikumbwa na kioja cha aina yake baada ya umeme kukatika ghafla na giza kutanda ukumbini hali iliyowafanya baadhi ya wabunge kupiga kelele; Dowans! Richmond! Dowans! Richmond! Dowans na baadaye CCM! CCM! CCM!
Ikipitishwa, sheria hiyo itaiwezesha Serikali kununua mitambo ya Dowans ili kutatua tatizo la umeme linalolikabili Taifa.Kelele hizo zilizoandamana na kejeli za kuwasha kurunzi za simu za mikononi na kumtaka mtoa mada kuendelea kwa kutumia mwanga huo hafifu zilisikika katika eneo walilokuwepo wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Manunuzi ya Umma (PPRA), Dk Ramadhani Mlinga ndiye aliyekuwa akitoa mada juu ya taratibu za Usimamizi wa Mifumo ya Manunuzi Serikalini.
"Endelea! Endelea! Endelea!" Walisikika wabunge hao wakisema huku wakiwa wamewasha kurunzi za simu zao ambazo mwanga wake haukuhimili giza lililokuwepo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo, Dar es Salaam." Wabunge walibakia gizani kwa takriban dakika 10 kabla ya umeme kurejea.
Waandishi wa habari nao walitumia fursa hiyo kuwahoji baadhi ya wabunge na wakati wa mahojiano hayo, wabunge hao waliwasaidia wapigapicha za televisheni kwa kuwasha kurunzi za simu zao na kuwamulika usoni wale waliokuwa wakihojiwa ili waonekane vizuri.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema hayo ni matokeo ya Serikali ya CCM kukumbatia mikataba mibovu kama walioingia na kampuni ya Richmond Development LLC... "Mkataba huo ndiyo uliorithiwa na Dowans ambayo hukumu imetaka Tanzania iilipe kampuni hiyo Sh 94 bilioni."
Mbunge wa Viti maalumu (Chadema), Naomi Kihula alilibebesha mzigo wa lawama Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akisema kuzima kwa umeme huo ni ishara kwamba shirika hilo la umma haliheshimu hata Bunge.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tindu Lissu alisema kitendo ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa mjadala huo akidai kwamba Mkuu wa PPRA, Dk Milinga alipinga vikali utoaji wa zabuni kwa Richmond lakini vigogo serikalini wakashikilia msimamo wa kumpinga.
Alisema hakubaliani na mpango huo wa kubadili sheria hiyo ya manunuzi ili kuwezesha serikali kununua mitambo ya Dowans kama njia ya kutatua tatizo la umeme nchini.
Baada ya jenereta la hoteli hiyo kuwashwa, Dk Mlinga aliendelea na mada yake na kueleza kwamba kutatua tatizo la umeme nchini kwa kununua mitambo mipya itachukua muda mrefu. Lakini akasema sheria ya PPRA inayotumika sasa hairuhusu kununua mitambo iliyotumika jambo ambalo linaibana serikali kutafuta suluhu ya tatizo la umeme nchini kwa haraka.
Kwa mujibu wa Mlinga, siyo lazima sheria hiyo iruhusu moja kwa moja ununuzi wa mitambo iliyotumika, bali iwe ni mazingira magumu kama yalivyo nchini sasa na kwamba kutakuwa na vigezo.
"Taratibu (kwa sheria mpya) zitaandaliwa ili kukabiliana na mazingira ya kusaidia mitambo ikinunuliwa iwe na vigezo vya kitaalamu vinavyoonyesha uwezo wake wa kazi," alisema.
Lakini hakuna mbunge aliyechangia kwenye mkutano huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha, Dk Abdallah Kigoda aliyeonyesha wazi kwamba anaunga mkono mpango wa kubadili sheria hiyo ya manunuzi.
Hali hiyo ilimfanya Dk Kigoda kuwataka wawe makini kwa sababu kamati yake ilijadili kwa undani suala hilo na kubaini kwamba sheria hiyo ina upungufu... "Suala la manunuzi tulifikirie kwa umakini," alisema akieleza kuwa wabunge ndiyo wanaotarajiwa kuokoa jahazi la tatizo la umeme nchini.
Aliwataka wajaribu kufikiria njia fupi ya kulitatua ili kuokoa uchumi, maana hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa taifa iwapo litadumu kwa siku 100.
Awali, akifungua mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwataka wabunge hao kutumia fursa hiyo kuishauri serikali kuhusu utaratibu mzima wa usimamizi na mifumo ya ununuzi wa umma kwani hali ya nchi ni mbaya.
"Eneo la manunuzi ni changamoto kubwa kwa serikali. Bado kuna udhaifu katika udhibiti na uwajibikaji katika eneo zima la manunuzi," alisema Ndugai na kuwataka wabunge kuwa makini na kutumia mjadala huo kuishauri serikali kwa sababu asilimia 70 ya bajeti yake inatumika kwa manunuzi na asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo nayo hutumika katika suala hilo hilo.
"Fedha nyingi za Serikali zinapotea katika manunuzi. Ni changamoto kwetu sisi wabunge kuishauri ipasavyo Serikali katika eneo hili. Muswada wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2010 unategemewa kujadiliwa na kupitishwa na Bunge lijalo," alisema Ndugai.
Hata hivyo, alisema kabla ya kupelekwa bungeni, Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi itawashirikisha wadau mbalimbali kuuboresha.
Comments
0
#13 enkine kitok 2011-03-15 17:12 Naomba tu niseme mgawo wa umeme haujaanza leo na sio jana karibu miaka nane sasa. Hivyo dharura haihitajiki tena mana pia ndo iliyotufikisha hapa tulipo!
Sheria/kanuni za PPRA zisibadilishwe na hakuna sabab ya kununua vyuma chakavu. serikali ina hela nyingi ambazo zinztumika indirectly kuwanufaisha wachache!
Mitambo mipya inunuliwe na sio mitambo ya Dowans.
Quote
0
#12 mahenge emmanuel 2011-03-15 16:50 Nirahisi sana kuchagua maembe mengi lakini kumbuka nivigumu sana kutambua kama lipi ni tam na lipi ni chungu.Pia mwenye nyumba aweza kusikia radio mda wote kwa sauti ya juu na anapo amua kununua radio nyingine kwa bei ya juu hata kama imetumika nivigumu sana kwa mpangaji kupinga.Utaaminije kama mwenye nyumba anamahusiano na muuzaji?Hii ndo TANZANIA nchi yenye udongo wenye dhambi.
Quote
0
#11 kidaruini 2011-03-15 14:07 Hapa ninashindwa kuelewa kinachoendelea
ina maana walizima umeme ili wabunge wanaojadili kubadili sheria ya kununua
vitu kukuu vilivyotumika wafanye haraka kuipitisha hiyo sheria?
Takwimu za hali ya hewa zinasemaje kuhusu hali ya mvua kwa wakati huu?
Rada tuliyonunua haiwezi kutabiri kama mvua ziko za kutosha kujaza mabwawa ya mtera na mengineyo ili kutuepusha kununua
hii mitambo ya dowans?
Kwa huu muda mimi bado kabisa siungi mkono wa kununua hii mitambo kwa wakati.
ni bora serikali ikanunua mafuta ya kutosha kwa ajili ya IPTL wakati
tukisubiri mvua za masika na huku tukihangaikia mitambo yetu mipya
Quote
+1
#10 mkweli 2011-03-15 13:53 hatuna haja ya kufanya mambo kwa dharura, hatuhitaji dharura tena, kama taabu tumeshataabika, Eeeh mola waache DOWANS waede zao hatuwataki tena. Sheria ya manunuzi ikibadilishwa ni kwa manufaaa ya MAFISADI WACHACHE,kina DOWANS na Viongozi watumwa wa DOWANS, naomba wakumbuke mambo haya yana mwisho tu,Egypt na Libya kumepatikana nini? Kwa nini hadi leo DOWANS?Hivi BUNGE lililopita la Baba Sita lilikuwa bunge hewa au MAFISADI wameliuuwa?
Quote
+1
#9 D.F Masao 2011-03-15 13:18 Tatizo la Mgawo wa umeme nimeanza kuliona Mwaka 1994, kuanzia wakati huo hadi leo ni miaka 17, kwa nini serikali isianzishe mradi mkubwa wa kuzalisha Megawatts 3000, hata kama utachukua muda mrefu kukamilika lakini tuwe na matumaini kuwa kuna jambo tunasubiri, kuliko hii mipango ya dharura kila mwaka ambayo matokeo yake hayadumu.
Quote
+2
#8 MBILIGI 2011-03-15 11:01 Bora wananchi twende kuichoma moto mitambo ya DOWANS kukata mzizi wa fitina.
Quote
+3
#7 Mzalendohalisi 2011-03-15 09:23 Binafsi nimefurahi wabunge kuka[NENO BAYA] umeme. Na huyo Mbunge anayesema kuwa TANESCO haiheshimu Bunge ni mbinafsi haangalii hospitali zinavyoka[NENO BAYA] umeme. Binafsi napinga kununua mitambo ya DOWANS kwa kuwa wameshachukua fedha nyingi bila ya kutoa huduma. Serikali inunue mitambo yake toka kiwandani. Hivi kila siku DOWANS, DOWANS mpaka lini? Kuna njia nyingi tu za kupata umeme wa dharura bila ya kununua mitambo ya DOWANS (Mradi wa vigogo)
Quote
-1
#6 Gigi wa Sao Paulo- B 2011-03-15 06:37 hata hao tuliwapa dhamana wanafanya masihala eti CCM.....! CCM....! Kukatika kwa umeme bungeni di hii kali tena ya mwaka. kubadilishwa sheria ni kwamba mafisadi wameshinda kwa kuwa sheria itaruhusu serikali kununua kitu chochote kilichotumika hata magari,mitambo na vifaa vya ofisini. Du....!!!!kweli hiI Tanzania namaliza kwa kusema CCM Oyee....!!!! aaaah!!!!ehkhee eeee!!!!????
Quote
-5
#5 hezron Lus 2011-03-15 05:38 Wawekezaji wa nje watakimbia sasa hivi kama nchi haina umeme. uchumi utaporomoka. tushabikie kukua kwa uchumi sio hoja za kisiasa. sheria ibadilishwe ili tununue hiyo mitambo. ishu ni kukosekana kwa umeme. mnataka mgao uwepo mpaka lini? hela za kununua mitambo mipya zipo wapi?
Quote
0
#4 jangala 2011-03-15 05:17 safi kabisa. wakome kuchukua maamuzi ya kizumbukuku. si mlipiga makofi bungeni kubariki dowans?. sasa inawatoeni jasho. natamani kama ile tsunami iliyotokea japan ingewakuteni humo ndani iwasambaratishe ni maana hamna mnalofanyia nchi hii zaidi ya kupitisha hoja za kutunyonga sie wananchi. TANESCO SAFI SAAAAAAAAAANA. "well done"
Quote
+1
#3 mapinduzi 2011-03-15 04:54 safi sana tanesco. mmefanya la maana sana. hawa wanasiasa wa[NENO BAYA] sana. wanapenda kuingilia ishu ambazo ni technical huku hawajui lolote. inabidi mkate hadi magogoni na mjengoni ili wawe na heshima na wanataaluma.
Quote
+2
#2 elibariki yerald 2011-03-15 04:45 hatutaki hiyo mitambo ya DOWANS hizi i biashara za kihuniiiiiiiiii iiiiiiiiiiiii
mbona mnaendeshwa hivyooooooooooo oooo1 , mbona mnatumiwa hivyo hivi ROSTAM AZIZ anawayumbisha kiasi hicho mnunue mitambo yake badala ya kutafuta suluhisho la kudumu,,,, tunataka njia nyingine kama vipi mitambo itaifishwe na si kununua
Quote
+3
#1 vuvuvzela 2011-03-15 04:11 Mafisadi wanaendesha nchi jinsi wanavyotaka.Kwa nini hii sheria ijadiliwe kipindi hiki wakati kila mahali ni DOWANS?
Serikali inajali maslahi ya Mafisadi zaidi ya wananchi waliyoingiza madarakani. Je tutafika?
Tuungane kuwaombea Wabunge wazidishiwe ufunuo kuliokoa Taifa letu dhidi ya Mafisadi.
Quote