Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

PHP:
Alisema Baada ya kampuni ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme, Septemba 2006, Bw. Aziz aliwasiliana naye akimwelezea tatizo la umeme akimshawishi awekeze kwenye umeme, akiamini kuwa mwekezaji anayetakiwa ni mwenye uwezo na anayeweza kufanya shughuli hiyo haraka.

"Mtakumbuka kuwa TANESCO iliomba kupitia kwenye vyombo vya habari mwekezaji mwenye uwezo wa kuzalisha kuanzia megawati 1 kuwasiliana nayo kuzalisha umeme wa dharura. Gridi ya taifa ilikuwa inaishiwa umeme kabisa.

"Hatimaye, Dowans ilifikia makubaliano na Richmond, kuwa kama TANESCO ingekubali kampuni yake ingechukua nafasi ya Richmond kuchukua mkataba wa kuzalisha umeme. Tuliamini kuwa Dowans ingepokewa vizuri na TANESCO, serikali na umma kama shujaa, kinachotushangaza haikuwa hivyo. 

Alisema Dowans ililipa dola za Marekani milioni 109 (kwa ajili ya mitambo, vifaa vyake na wahandisi na baadaye kuongeza mtaji wa dola milioni 20.

Al Adawi alisema kuwa watu wasiokuwa taarifa sahihi wamekuwa wakiishutumu kampuni yake wakiita ya mfukoni, lakini yeye anawapa changamoto waoneshe kampuni nyingine ya mfukoni yenye mitambo ya dola za Marekani milioni 109.

Huu ni uongo mtakatifu.........bei ya mitambo ilikuwa ni dola za marekani 7.5 na wala siyo dola 109..............................
 
Mmiliki Dowans afika kuteta na Tanesco Send to a friend Sunday, 20 February 2011 21:05
AKATAA KUONANA NA WAZIRI, AGOMA KUPIGWA PICHA
Joseph Zablon

WAKATI Mjadala wa Dowans ukibaki kwenye swali la nani mmiliki wake, raia wa Oman, Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi amejitokeza na kukiri kuimiliki kampuni hiyo inayoidai Tanzania mabilioni ya shilingi. Al Adawi alikutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini jana na kueleza ujio wake kuwa umelenga kukutana na Tanesco na kujadili suala la malipo ya Sh94 bilioni ambayo kampuni yake inaidai Tanzania.

Ujio wa Al Adawi umemaliza mjadala uliogubika umiliki wa Dowans na kuwachanganya Watanzania huku baadhi yao wakiamini kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz. Al Adawi ni mmoja wa watu ambao majina yao yako kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni nchini (Brela) waliojiandikisha kama wamiliki wa kampuni hiyo ya Dowans.

Watu wengine waliotajwa na Brela kuwa ni wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, ambao ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd na uraia wao kwenye mabano ni Andrew James Tice na Guy Picard (Canada), Gopalakrishnan Balachandaran (India), Stanley Munai (Kenya) na Hon Sung Woo (Singapore).

Akizungumza katika mkutano huo huku akigoma kupigwa picha, Al Adawi alisema yuko tayari kuzungumza na Tanesco kuhusu fidia ya Sh94 bilioni (hakutaja kiasi), baada ya kuvunjwa kwa mkataba baina ya kampuni yake hiyo na Tanesco.

"Nimekuja kwa mambo mawili; moja ni kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu kampuni ya Dowans na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwapo suluhisho la kile kilichopo hivi sasa kuhusu Dowans," alisema Al Adawi. Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, ambaye ni Mwanajeshi aliyestaafu katika ngazi ya Brigedia Jenerali, Tanzania ni nchi inayovutia kibiashara na inayofuata sheria za uwekezaji.

Lakini Al Adawi ambaye katika mkutano huo aliambatana na mwanasheria wa kimataifa, John Miles na Mkurugenzi wa fedha, Stanley Munai wa Dowans Tanzania Ltd, alisema, licha ya Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji, kampuni yake katika uwekezaji nchini imekumbwa na jinamizi.

"Nimekuwa na imani na Tanzania na nimeitikia wito wa uwekezaji katika kipindi cha matatizo yenu, lakini yote yaliyojitokeza tangu niwekeze nchini ni unyanyasaji na mnaendelea kuninyanyasa hadi leo na hii katika hali ya kawaida hamnitendei haki," alisema Al Adawi. Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa hakuwa ametaka kuishtaki Tanesco na kudai fidia ya mabilioni hayo ya shilingi, lakini alilazimika kufanya hivyo kutokana na namna alivyotendewa katika kipindi cha uwekezaji wake.

Alifafanua kuwa Tanesco ilimhakikishia usalama wa uwekezaji wake na hivyo akakubali kuingia nao mkataba lakini, shirika hilo likavunja mkataba huo na kukiuka makubaliano yaliyofikiwa chini ya sheria zake yenyewe za manunuzi. Alisema jambo hilo halieleweki katika ulimwengu wa sasa wa biashara kimataifa akieleza kuwa linaweza kuisababisha nchi hasara kubwa. Mfanyabiashara huyo aliyetumia sehemu kubwa ya taarifa yake kueleza historia ya namna alivyoingia mkataba, alisema katika ujio wake huo hana mpango wa kukutana na waziri wala kiongozi mwingine yeyote wa serikali bali Tanesco.

Alikiri kuwa na uhusiano na mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz na kusema kuwa ni rafiki yake wa siku nyingi na ndiye aliyemtaka aje kuwekeza katika sekta ya umeme nchini mwaka 2005. "Rostam ndiye aliyenipa nguvu ya kisheria za kusimamia masuala ya kampuni yangu hapa Tanzania," alisema.

"Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya sekta ya mawasiliano ya Simu Afrika Mashariki kwa hamu kubwa. Nilikusudia Dowans iwe mwekezaji katika sekta hiyo Tanzania kwa kuwekeza mkongo wa mawasiliano ya ubora wa juu nchi nzima, tumenyimwa fursa na imeenda kwa Wachina, nimehamisha uwekezaji,"alisema.

Alisema kuwa alitarajia kampuni yake iwekeze katika sekta ya mawasiliano ya simu, lakini ana taarifa kuwa serikali ya China imeikopesha serikali ya Tanzania kuwezesha kusimikwa mkongo huo wa taifa na kuwanyima wao fursa nchini. Adawi ambaye alidai kuwa yeye ni mfanyabiashara mdogo ambaye haoni sababu ya picha zake kutumia katika magazeti au vituo vya runinga, alisema ametumia mamilioni ya shilingi kukamilisha mradi huo, wenye mitambo mipya.

Dowans imekuwa ikiumiza vichwa vya wasomi, wanaharakati na wanasiasa hasa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), kuitaka Tanzania iilipe kampuni hiyo Sh94 bilioni kutokana na Tanesco kuvunja mkataba wake, kinyume na taratibu. Lakini wakati CCM na serikali yake ikibariki malipo hayo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na wanaharakati wa haki za kijinsia nchini, waliwasilisha Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, pingamizi ya malipo hayo huku CUF, ikifanya maandamano kushinikiza isilipwe.

Mvutano huo ulishika kasi tangu Desemba 27 mwaka jana, siku ambayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema aliposema kuwa ameisoma hukumu hiyo na kuridhika nayo hivyo, Serikali haitakata rufaa. Siku chache baadaye, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitoa kile alichokiita tamko rasmi la Serikali kuhusu malipo hayo akisema kuwa Serikali imekubaliana na ushauri wa Mwanasheria Mkuu.

Alisema ingawa kiwango kinachotakiwa kulipwa na Serikali kwa kampuni hiyo ni kikubwa, lakini alisema hakuna jinsi na badala yake Serikali imemua kulipa ili kuepuka kujiingiza katika matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa riba ya malipo hayo.

Akitoa ufafanuzi wa mchakato wa usajili wa tuzo hiyo, Msajili Bongole alisema tayari tuzo hiyo imeshatumwa mahakamani hapo kutoka ICC na kwamba imetumwa na Katibu wa Sekretarieti ya ICC, Victory Oraowski, lakini akasema kuwa, bado haijapokewa rasmi kisheria.

Alisema licha ya tuzo hiyo kuwasilishwa mahakamani hapo, mchakato wa usajili wake haujaanza kwa kuwa utaratibu wa kisheria bado haujakamilika kulinganga na taratibu za usuluhishi na tuzo zinazotolewa pasipo amri ya mahakama. "Sheria zinazotumika katika usajili wa tuzo hiyo ni sheria ya usuluhishi (Arbtration Act) Sura ya 15 ya Sheria za Tanzania pamoja na sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai (Civil Procedure Code- CPC), sura ya 33 jedwali la 2 kifungu cha 20.

Alisema baada ya tuzo hiyo kuwasilishwa mahakamani, mshinda tuzo anapaswa kuwasilisha maombi ya maandishi akiambatanisha na hati ya kiapo ili tuzo yake iweze kusajiliwa. Alisema baada ya mshindi wa tuzo kuwasilisha maombi hayo, Mahakama itatoa taarifa kwa mshindwa tuzo atoe sababu kwa muda maalumu atakaopewa na Mahakama aeleze kwa nini tuzo hiyo isisajiliwe.

"Kama mshindwa tuzo akisema hana pingamizi tunaisajili na akisema ana pingamizi basi tunasikiliza kwanza pingamizi hilo na kulitolea uamuzi. Baada ya taratibu hizo ndIo tunaweza kuisajili sasa na kuwa nguvu ya kumlazimisha mdaiwa kulipa deni," alisema Bongole. Alisema mbali na mshindwa, mtu mwingine yeyote ambaye pia ataona maslahi katika tuzo hiyo ana haki ya kuwasilisha pingamizi lake ambalo pia litasikilizwa na kutolewa uamuzi kabla ya tuzo kusajiliwa.

"Kwa hiyo kwa sasa tumeletewa tu, hiyo tuzo ili tuihifadhi tukisubiri mwenye tuzo hadi atakapoleta maombi na wala si kwamba sisi ndio tunakwenda kumtafuta, mahakama haiwezi kwenda kutafuta kesi," alisema Bongole. Hata hivyo akizungumza kwenye semina ya wabunge jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema serikali iko katika mchakato wa kuangalia namna itakavyoweza kutumia njia za kisheria kuondoa mzigo wa kuilipa mabilioni ya shilingi kampuni ya kufua umeme ya wa dharura ya Dowans.

"Suala hili ni la kisheria kwa maana kwamba limetokana na kitu kinaitwa mkataba, jambo hilo limepelekwa mpaka kwenye chombo hicho cha kisheria chombo kile kimetoa maamuzi yake maamuzi yake yamerudiswa hapa nyumbani kwa ajili ya utekelezaji.

Aliendelea,"kwa hiyo katika mazingira ya kawaida hatuna namna nyingine ya kusema hapana kimabavu bavu hivi, hebu tutazame kama vipo vyombo au watu wanaosema upo uwezekano wa kujiondoa katika hili basi tujaribu kushirikiana nao ili tuone kama wanaweza kutusaidia namna ya kutoka pale bila kuvunja sheria zinazotakiwa kuzingatiwa."
 
Hivi DOWANS waliwezake kumpa Rostam Aziz powers of Attorney kama wao siyo kampuni ya mfukoni???????????????

RostamAziz.jpg
 
Huyu aliyehojiwa ni kanyaboya....ndio maana hataki kupigwa picha

Kabisa! Anaogopa picha zikitoka kule Oman watamuumbua! Jamani haka kabwana RA! Katatutesa sana, kameshtukia hoja yenye mnaso wa nguvu ya Kijana Mnyika, kakabidi kafanye mauza mauza mengine!
 
Affidavit hii inawakana huyu tapeli na wenzie juu ya umiliki wao wa DOWANS:-

Sasa huyu tapeli anatokea wapi??????????????????????????????????????????????

DOWANSOwners1.jpg

DOWANSOwners2.jpg

DOWANSOwners3.jpg
 
Huu ni utapeli mwingine wa hali ya juu.

Rostam Aziz anazidi kumaintain kuwa juu ya sheria.

Fedha ina akili kuliko akili za Watanzania wote.

Huyu Basha Rostam ataendelea kutufanyizia mpaka Tuseme ENOUGH is ENOUGH.
 
PHP:
[B] [IMG]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon1.png[/IMG] Re: Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS... [/B]

    Huu ni utapeli mwingine wa hali ya juu.
 
Rostam Aziz anazidi kumaintain kuwa juu ya sheria.
 
Fedha ina akili kuliko akili za Watanzania wote.
 
Huyu Basha Rostam ataendelea kutufanyizia mpaka Tuseme ENOUGH is ENOUGH.

Can't agree more....................................
 
PHP:
Kabisa! Anaogopa picha zikitoka kule Oman watamuumbua! Jamani haka kabwana RA! Katatutesa sana, kameshtukia hoja yenye mnaso wa nguvu ya Kijana Mnyika, kakabidi kafanye mauza mauza mengine!

Unapoona mtu hata picha hataki apigwe ujue huyo nit apeli wa kimataifa........................na huenda hata INTERPOL wan taarifa zake..................huyo ni mwajiriwa wa JK na Rostam Aziz....................................yupo kutuchezea shere na kuufunika ukweli................
 
Kama Brigedia ndiye mmiliki halali wa DOWANS mbona MEMARTS imeibiwa BRELA? Mbona Dowans (T) Ltd haimtaji kawa owner? Pamoja na huyu TAPELI kujitokeza hadharani bado maswali ni mengi kuliko majibu. TUNAHITAJI NGUVU YA UMMA kukemea uovu na ujanja ujanza wa RA na rafiki zake (2) wawili waliojificha kwenye kuvuli chake.
 
Hivi watanzania tutaendelea kufanywa wajinga mpaka lini? JK, RA&EL eleweni kuwa mtailipua nchi hii kwa ufisadi wenu.
 
PHP:
Kabisa! Anaogopa picha zikitoka kule Oman watamuumbua! Jamani haka kabwana RA! Katatutesa sana, kameshtukia hoja yenye mnaso wa nguvu ya Kijana Mnyika, kakabidi kafanye mauza mauza mengine!

Unapoona mtu hata picha hataki apigwe ujue huyo nit apeli wa kimataifa........................na huenda hata INTERPOL wan taarifa zake..................huyo ni mwajiriwa wa JK na Rostam Aziz....................................yupo kutuchezea shere na kuufunika ukweli................

tech.jpg

Huyu hapa kulia
 
The partnership of Brigadier-General (Retd.) Suleiman bin Mohammed Al-Adawi and Mr. P.N.C Menon has created a multi billion dollar international conglomerate over the past decades. Aside of construction and property development they have very successfully built an international technology enterprise. In a joint statement they expressed "The entry of IMTAC into our group allows us to target market leadership in the booming MEA region from Oman. We have always strongly believed in the vision of His Majesty Sultan Qaboos in terms of striving for global quality and service delivery benchmarks, without losing focus on our Omani heritage, culture and social commitment. Imtac, its people, its customers and its positioning in both Oman and the region represents an institution of excellence through which we will deliver our regional aspirations."

Mbona hasemi DOWANS?
 
DOWANS ni kampuni iliyoko TEXAS Marekani....kwa hiyo hawa waarabu hawahusiki......................ila DOWANS inatumika kuhalalisha ulaji wa watu wachache hapa nchini...................
 
Thibitisha hizi tuhuma....................................

tech.jpg

PHP:
[IMG]http://www.renaissanceoman.com/UploadedFiles/UserMedia/image/News/2008/tech.jpg[/IMG]
 
Huyu hapa kulia
 
Jakaya Mrisho KIWETE a.k.a Mcheka onyoooooooooooooooooooooooo
 
PHP:
The partnership of Brigadier-General (Retd.) Suleiman bin Mohammed Al-Adawi and Mr. P.N.C Menon has created a multi billion dollar international conglomerate over the past decades. Aside of construction and property development they have very successfully built an international technology enterprise. In a joint statement they expressed "The entry of IMTAC into our group allows us to target market leadership in the booming MEA region from Oman. We have always strongly believed in the vision of His Majesty Sultan Qaboos in terms of striving for global quality and service delivery benchmarks, without losing focus on our Omani heritage, culture and social commitment. Imtac, its people, its customers and its positioning in both Oman and the region represents an institution of excellence through which we will deliver our regional aspirations."

Mbona hasemi DOWANS?

DOWANS ni kampuni iliyoko TEXAS Marekani....kwa hiyo hawa waarabu hawahusiki......................ila DOWANS inatumika kuhalalisha ulaji wa watu wachache hapa nchini...................

Richmond ndiyo iko TEXAS. DOWANS wanasema (mimi sijui) ni ya COSTA RICA
 
Kwan mmesahau kauli ya mwakyembe kuwa kuna mambo mengi ameyaacha ili kuitunzia heshima serikali by any alikua ni jk ndiye ambae hakutajwa kwenye ishu ya richmond na richmond na dowans ni m2 na mdogo wake na baba yao ni serikli ya jk!!
 
PHP:
Richmond ndiyo iko TEXAS. DOWANS wanasema (mimi sijui) ni ya COSTA RICA

Kamati ya Maakumu ya Bunge iliyoongozwa na Mwakyembe ilienda marekani hadi kwenye ofisi za DOWANS sasa iweje zisiwe marekani?????????????????

Ofisi za Richmond ndizo hazijulikani zilizpo lakini za DOWANS zinajulikana..................................
 
Back
Top Bottom