Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Hivi kweli wananchi bado mnakubali upuuzi huu kuendelea kuumiza vichwa vyetu? Huyu Mwarabu kama sikosei Mwanakijji aliwahi kuongea naye kwenye simu na akakiri kutohusika na Dowans wala haijui. Na habari zaidi ambazo siwezi kuzithibitisha ni kwamba huyu Mwarabu Mu Oman ni mzawa wa Zanzibar hata familia yake kuna Wazanzibar wanaifahamu. Na tetesi za mjini huyo mbia kutoka Kenya ni mwajiriwa kampuni ya Rostam..

Yaani madudu juu ya madudu yanazidi tu kuendelea kltk nchi ambayo kila siku tunaomba amani na usalama...hiyo amani itatoka wapi ikiwa viongozi wenyewe ndio wa kwanza kuiharibu amani kama vil;e tumetawaliwa na makaburu. Hivi kweli inaingia akilini mwenu kama hukumu ilikwisha tolewa na mahakama sisi tuwalipe Dowans hayo mabilioni ya fedha iweje leo huyo mmliki aje tena Tanzania kujadiliana na serikali yetu ili iweje?..Yaani hukumu imeacha mwanya wa mshitaki na mshitakiwa kujadiliana nje ya hukumu?..Je kama ndivyo kwa nini tuliambiwa ni lazima tulipe na haiepukiki...

Hukumu imesha toka, kinachotaka kutengenezwa hapa ni kuirudisha Dowans izalishe umeme na pengine tusameheane deni huku tukiingia mkataba wa awali ambao unatufanya tulipe mabillioi ya fedha kila mwaka kwa miaka isiyojulikana..kifedha ni faida kubwa kwa mwekezaji..hii kweli ni kuitafuta amani?..na ukisema sena utaambiwa Udini kwa sababu tu alosema alikuwa Padre na mkristu hivyo anachozungumza ni chuki binafsi ya Waislaam. Huu Uislaam jamani unatafsirika kwa majoho na Uarabu wa wahusika ama imani ya kuabudu na kutenda yaliyo mema..Hawa watu wezi hawa jamani tunawakumbatia kwa nini?

Ndugu zangu wana mapinduzi jichungeni sana na maelezo ya viongozi hasa wa dini zote.. iwe wakiislaam au Wakikristu kwani hawa viongozi wamechukua vibahasha na kunadi udini makusudi kudhoofisha nguvu za baadhi wanamapinduzi, hivyo kwa kila kinachozungumzwa na kiongozi wa dini, Wadanganyika wanachukulia kuwa ni mawazo yaliyopitia chama fulani kwani tumekwisha pandikizwa fikra za udini..lakini ukweli ni kwamba kuna mtandao ambao unaendesha udini huu kwa kupitia viongozi wa dini na majibishano yao yameandaliwa makusudi ili wajinga wengi wayakubali kwani hakuna mtu anaweza kuamini Sheikh mkuu au Kardinali fulani wanachukua vibahasha kuhamasisha udini nchini.

Nitarutuidia kusema dini na siasa ni vitu ambavyo haviwezi kwenda sambamba hata kidogo.. dini inamkataza kila mtu kushirikiana na mwenza asiyekuwa dini yake hivyo kuua kabisa uwezo wa siasa kuchagua viongozi wetu kulingana na uwezo wa mtu na sio dini yake. Na kama kuna mtu anabisha anambie yeye kama kuna dini yoyote iwe ya kikristu au kiislaam inaruhusu muumini kuongozwa na kiongozi ambaye sii dini yake?..Sidhani.. hivyo ni halali kidini kwa muumini kumchagua kiongozi wake atoke ktk dini yake lakini kisiasa ni UDINI huo..

Nawaomba sana viongozi wa dini waache mchezo huu kwani hivyo vijisenti na misamaha ya kodi wanayoipata wakijenga uhasama huu ni wao watakao iweka Tanzania ktk nafasi ya yale yaliyowakumba Rwanda..
 
hii ndiyo ile ambayo kamati ya dr. Mwakyembe alisema mengine hawakuyatoa hadharani kwa sababu za kiusalama ( wa taifa)!!!! Hivi usalama wa taifa ni usalama wa kikwete au wa wananchi? Ni usalama gani wa taifa wakati mkulu mwenyewe ndiye anayetusaliti?

watumwa wanaliwa na wanyampara chini ya mwarabu... Hongera sana watumwa kwa kukubaliana bila kupinga uamuzi wa wanyampara ccm kwa mwendelezo wa kuwekwa watumwa kwa manufaa kidogo ya tende na haluwa kwa mnyampara na mtumwa shauri yake hata akifa kwa mabomu sawa tu
 
Heshima kwako Mkandara,


Mkuu wewe ni miongoni mwawanjamvi wachache ninao heshimu na kuamini michango yao.Hakika nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana,nakumbuka maneno ya Dr W Slaa akituasa watanzania [wapiga kura] kutomchagua Rais Kikwete mara ya pili kwani kufanya hivyo ni hasara kubwa kwa taifa [Tanzania] wengi walichukulia kauli ya Dr W Slaa kama ni mkakati wake wa kujipatia kura lakini sasa tunajionea wenyewe mauza uza ya Dowans yakirejea kwa mlango wa nyuma.

Naisikitikia nchi yangu Tanzania imekabidhiwa wezi wasiokuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wa kawaida wanaoishi chini ya u$ 1 kwa siku.Hakuna mikakati ya kuwakwamua bali ipo mikakati ya kuwadidimiza kupitia mikataba mibovu.

Wezi walibaini bunge la tisa lilikuwa kimbilio na sauti pekee ya wananchi,kipindi cha uchaguzi wamehakikisha wanaliteka bunge kwa kutupachikia spika wao kwaajili ya manufaa yao.Wakaziteka kamati muhimu za bunge eg; kamati ya mambo ya nje ulinzi na usalama,kamati ya Nishati na Madini,kamati ya miundombinu na nk.Watanzania tusitegemee bunge la kumi litafanya kazi nzuri kama bunge lililopita.Masuala muhimu kwa taifa yatazimwa,sauti ya umma haitasikika tena.
 
Mitambo ya Dowans yawashwa Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:07

Waandishi Wetu
MITAMBO ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans ambayo mjadala wake bado unapasua vichwa vya Watanzania imewashwa, Mwananchi limebaini.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mitambo hiyo imewashwa kwa mkataba mpya na kampuni ya Songas kwa ajili ya kufua umeme utakaosaidia kupunguza tatizo la mgawo unaoendelea sasa nchi nzima.

Kuwashwa kwa mitambo hiyo kumekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba apendekeze kuwashwa kwa mitambo hiyo kama njia ya kuliokoa taifa na mgao wa umeme unaoendelea kote nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi katika eneo inakohifadhiwa mitambo hiyo, Ubungo jijini Dar es Salaam ulibaini kuwa baadhi ya mitambo ya Dowans ilikuwa ikiendelea kufanya kazi.

Mfanyakazi aliyekutwa katika eneo la mitambo hiyo alimweleza mwandishi kuwa mitambo hiyo imewashwa tangu juzi lengo likiwa kukabiliana na mgawo wa umeme.

"Kwa sasa tatizo la mgawo litapungua kwani mtambo mkubwa ulioko nyuma ya Jengo la Makao Makuu ya Shirika letu umewashwa, bado huu hapa mdogo," alisema mfanyakazi huyo huku akionyesha mtambo huo mdogo ambao ulikuwa haujawashwa.

Aidha, mfanyakazi huyo alimtaka mwandishi wa habari kuzunguka nyuma ya majengo na kwamba angejionea mwenyewe juu ya kweli wa kauli hiyo.

"Ndugu yangu si unataka kuona mitambo hiyo, hapa huwezi kuiona zunguka nyuma ya ile mtambo ndio utanona vizuri,"alisisitiza.

Katika eneo la karibu ya mitambo Mwandishi alishuhudia mitambo hiyo ikifanya kazi na alipouliza majirani juu ya lini imewashwa alijibiwa kuwa mara kwa mara mitambo huyo huwashwa, lakini kwa sasa imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu zaidi.

"Unajua hii mitambo bwana haileweki, mara kwa mara huwa inawashwa, lakini kwa leo naona imechukua muda mrefu zaidi, sina uhakika kama ndiyo imewashwa moja kwa moja," alisema mkazi huyo anaishi jirani na eneo ilikohifadhiwa mitambo ya umeme.

Taarifa nyingine kutoka vyanzo huru vya habari zilieleza kuwa mitambo hiyo ya Dowans iliwashwa juzi usiku kwa makubaliano baina ya Songas na Dowans, baada ya mitambo ya Songas kukorofisha hivyo kuhitaji nyongeza ya megawati 37 katika gridi ya taifa.

Kauli ya Tanesco
Meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alikanusha shirika hilo kuingia mkataba na Dowans ili kuwasha mitambo hiyo.

"Sina taarifa kuwa mitambo ya Dowans imewashwa... ni kweli ipo hapa nyuma ya ofisi zetu, lakini hatujawa na mazungumzo na kampuni hiyo kuhusiana na kuwashwa kwa mitambo hiyo," alisema.

Alibainisha kuwa iwapo kutakuwa na jambo lolote linalohusiana na mkataba baina ya Tanesco na Dowans, shirika hilo litatoa taarifa kwa umma ili kila mmoja aelewe kinachoendelea.

Ujio wa Al Adawi
Mitambo hiyo imewashwa siku moja baada ya Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayedai kuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, kuwasili nchini na kuzungumzia sakata la fidia ambayo kampuni yake hiyo inaidai Tanesco kutokana na kukatisha mkataba wake kinyume na sheria.

Hata hivyo, ujio huo wa Al Adawi, ambaye ni raia wa Oman, umewasha upya moto wa sakata la Dowans, baada ya wasomi na wanasiasa kuuita usanii waliodai kuwa umefanywa na wajanja wachache, kuwacheza shere Watanzania.

Juzi Al Adawi aliingia nchini na kukutana na wahariri wa vyombo vya habari akieleza kuwa amekuja kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu suala la Dowans na kuangalia uwezekano wa kutafuta suluhisho kuhusu suala hilo.

"Nimekuja kwa mambo mawili; moja ni kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu kampuni ya Dowans na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwapo suluhisho la kile kilichopo hivi sasa kuhusu Dowans," alisema Al Adawi ambaye ni Mwanajeshi aliyestaafu katika ngazi ya Brigedia Jenerali.

Huku akigoma kupigwa picha, Al Adawi alisema yuko tayari kuzungumza na Tanesco kuhusu fidia ya Sh94 bilioni (hakutaja kiasi), baada ya kuvunjwa kwa mkataba baina ya kampuni yake hiyo na Tanesco.

Maoni kuhusu Al Adawi
Lakini ujio huo umeibua hasira za wasomi na wanasiasa ambao kwa nyakati tofauti jana waliuita usanii huku, mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, akiitaka Serikali imkamate Al Adawi na kumhoji.

"Nilitarajia AlAdawi angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond, lakini hakufanya hivyo. Sasa naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba vimkamate, vimpige picha na kumhoji kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans,"alisema Mnyika na kufafanua:

Kauli ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa Kahama, James Lembeli ambaye ameeleza kutilia shaka umiliki huo akihoji "muda wote, Al Adawi alikuwa wapi kama huu sio mwendelezo wa utapeli?"

"Kama kweli ni mmiliki halali siku zote alikuwa wapi, na kwa nini ajitokeze baada ya hukumu ya fidia ya malipo ambayo Watanzania wanaipinga,'' aliendelea kuhoji mbunge huyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Ni bora utembee na viraka kuliko mtu kukuvunjia heshima. Huu ni mchezo wa kundi la watu wachache wanaoichezea nchi na kuidhalilisha, huu ni utapeli mtupu,'' alisema Lembeli.

Mwanasheria maarufu nchini Profesa Abdallah Safari amemtaka Al Adawi kutoa nyaraka halisi zinazomtambulisha kuwa mmiliki wa kampuni ya Dowans vinginevyo anafanya ‘usanii'.

"Si suala la kuita vyombo vya habari na kujitangaza yeye ni mmiliki. Atoe nyaraka halisi zinazomthibitisha, kwani anaweza kuwa ni mwarabu wa Kariakoo,'' alisema Profesa Safari.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bashiru Ally alisema kinachofanyika ni mchezo wa kuigiza wenye nia ya kutuchanganya Watanzania.
Alisema jambo la msingi kuhusu utata wa kampuni hiyo na Tanesco ni kwa wote waliohusika kuliingiza taifa kwenye mkataba huo feki kujulikana na kuchukuliwa hatua.

"Kulipa au kutolipa deni hilo la Sh94 bilioni siyo hoja kwa sasa, hoja ni nani wamefikisha taifa hapo tulipo, ni pale tu Serikali kuanzia ngazi ya waziri na kushuka chini itakapotuletea msururu wa wataalamu waliosababisha taifa kuingia kwenye mkataba huo feki ndipo suala la Dowans litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Habari hii imeandaliwa na Elias Msuya, Sadick Mtulya na Geofrey Nyang'oro


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #5 kibonge 2011-02-22 08:45 naomba bwana wansakya uwe wa kwanza kuandaa andamano hilo la amani na sisi tutakuwa nyuma yako, kwa sababu wengi wanatoa mawazo ya kuandamana lakini nani wa kuanzisha??!!
Quote









+1 #4 MKWELI 2011-02-22 08:45 HII NI HATARI. SULUHISHO NI KUFANYA KAMA LIBYA, NCHI IMESHAHARIBIKA WANALOTAKA WACHACHE NDILO LINAFANYIKA KWA MASLAHI YAO NI SI KWA MASLAHI YA TAIFA. LEO UMESIKIA NI MKATABA KATI YA SONGAS NA DOWANS KESHO UTASIKIA NI UWAMUZI WA SERIKALI. WANANCHI TUSIFANYE MAKOSA TENA 2015. HAWA WATOTO WA VIGOGO WAMEWEKWA ILI KUNUSURU MASLAHI YA MAFISADI BABA ZAO.TUSIWAPE KURA HAWAFAI. KESHO UTAAMBIWA JANUARY MAKAMBA WAZIRI WA NISHATI!!!. HIVI HAWA VIONGOZI WA CCM WANAFIKIRI HII NCHI NI YAO PEKEE YAO?
Quote

 
Mitambo ya Dowans yawashwa Send to a friend Monday, 21 February 2011 21:07

Waandishi Wetu
MITAMBO ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans ambayo mjadala wake bado unapasua vichwa vya Watanzania imewashwa, Mwananchi limebaini.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mitambo hiyo imewashwa kwa mkataba mpya na kampuni ya Songas kwa ajili ya kufua umeme utakaosaidia kupunguza tatizo la mgawo unaoendelea sasa nchi nzima.

Kuwashwa kwa mitambo hiyo kumekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba apendekeze kuwashwa kwa mitambo hiyo kama njia ya kuliokoa taifa na mgao wa umeme unaoendelea kote nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi katika eneo inakohifadhiwa mitambo hiyo, Ubungo jijini Dar es Salaam ulibaini kuwa baadhi ya mitambo ya Dowans ilikuwa ikiendelea kufanya kazi.

Mfanyakazi aliyekutwa katika eneo la mitambo hiyo alimweleza mwandishi kuwa mitambo hiyo imewashwa tangu juzi lengo likiwa kukabiliana na mgawo wa umeme.

“Kwa sasa tatizo la mgawo litapungua kwani mtambo mkubwa ulioko nyuma ya Jengo la Makao Makuu ya Shirika letu umewashwa, bado huu hapa mdogo,” alisema mfanyakazi huyo huku akionyesha mtambo huo mdogo ambao ulikuwa haujawashwa.

Aidha, mfanyakazi huyo alimtaka mwandishi wa habari kuzunguka nyuma ya majengo na kwamba angejionea mwenyewe juu ya kweli wa kauli hiyo.

“Ndugu yangu si unataka kuona mitambo hiyo, hapa huwezi kuiona zunguka nyuma ya ile mtambo ndio utanona vizuri,”alisisitiza.

Katika eneo la karibu ya mitambo Mwandishi alishuhudia mitambo hiyo ikifanya kazi na alipouliza majirani juu ya lini imewashwa alijibiwa kuwa mara kwa mara mitambo huyo huwashwa, lakini kwa sasa imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu zaidi.

“Unajua hii mitambo bwana haileweki, mara kwa mara huwa inawashwa, lakini kwa leo naona imechukua muda mrefu zaidi, sina uhakika kama ndiyo imewashwa moja kwa moja,” alisema mkazi huyo anaishi jirani na eneo ilikohifadhiwa mitambo ya umeme.

Taarifa nyingine kutoka vyanzo huru vya habari zilieleza kuwa mitambo hiyo ya Dowans iliwashwa juzi usiku kwa makubaliano baina ya Songas na Dowans, baada ya mitambo ya Songas kukorofisha hivyo kuhitaji nyongeza ya megawati 37 katika gridi ya taifa.

Kauli ya Tanesco
Meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alikanusha shirika hilo kuingia mkataba na Dowans ili kuwasha mitambo hiyo.

“Sina taarifa kuwa mitambo ya Dowans imewashwa... ni kweli ipo hapa nyuma ya ofisi zetu, lakini hatujawa na mazungumzo na kampuni hiyo kuhusiana na kuwashwa kwa mitambo hiyo,” alisema.

Alibainisha kuwa iwapo kutakuwa na jambo lolote linalohusiana na mkataba baina ya Tanesco na Dowans, shirika hilo litatoa taarifa kwa umma ili kila mmoja aelewe kinachoendelea.

Ujio wa Al Adawi
Mitambo hiyo imewashwa siku moja baada ya Suleiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayedai kuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, kuwasili nchini na kuzungumzia sakata la fidia ambayo kampuni yake hiyo inaidai Tanesco kutokana na kukatisha mkataba wake kinyume na sheria.

Hata hivyo, ujio huo wa Al Adawi, ambaye ni raia wa Oman, umewasha upya moto wa sakata la Dowans, baada ya wasomi na wanasiasa kuuita usanii waliodai kuwa umefanywa na wajanja wachache, kuwacheza shere Watanzania.

Juzi Al Adawi aliingia nchini na kukutana na wahariri wa vyombo vya habari akieleza kuwa amekuja kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu suala la Dowans na kuangalia uwezekano wa kutafuta suluhisho kuhusu suala hilo.

"Nimekuja kwa mambo mawili; moja ni kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu kampuni ya Dowans na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwapo suluhisho la kile kilichopo hivi sasa kuhusu Dowans," alisema Al Adawi ambaye ni Mwanajeshi aliyestaafu katika ngazi ya Brigedia Jenerali.

Huku akigoma kupigwa picha, Al Adawi alisema yuko tayari kuzungumza na Tanesco kuhusu fidia ya Sh94 bilioni (hakutaja kiasi), baada ya kuvunjwa kwa mkataba baina ya kampuni yake hiyo na Tanesco.

Maoni kuhusu Al Adawi
Lakini ujio huo umeibua hasira za wasomi na wanasiasa ambao kwa nyakati tofauti jana waliuita usanii huku, mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, akiitaka Serikali imkamate Al Adawi na kumhoji.

“Nilitarajia AlAdawi angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond, lakini hakufanya hivyo. Sasa naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba vimkamate, vimpige picha na kumhoji kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans,”alisema Mnyika na kufafanua:

Kauli ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa Kahama, James Lembeli ambaye ameeleza kutilia shaka umiliki huo akihoji "muda wote, Al Adawi alikuwa wapi kama huu sio mwendelezo wa utapeli?"

"Kama kweli ni mmiliki halali siku zote alikuwa wapi, na kwa nini ajitokeze baada ya hukumu ya fidia ya malipo ambayo Watanzania wanaipinga,'' aliendelea kuhoji mbunge huyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Ni bora utembee na viraka kuliko mtu kukuvunjia heshima. Huu ni mchezo wa kundi la watu wachache wanaoichezea nchi na kuidhalilisha, huu ni utapeli mtupu,'' alisema Lembeli.

Mwanasheria maarufu nchini Profesa Abdallah Safari amemtaka Al Adawi kutoa nyaraka halisi zinazomtambulisha kuwa mmiliki wa kampuni ya Dowans vinginevyo anafanya ‘usanii’.

"Si suala la kuita vyombo vya habari na kujitangaza yeye ni mmiliki. Atoe nyaraka halisi zinazomthibitisha, kwani anaweza kuwa ni mwarabu wa Kariakoo,'' alisema Profesa Safari.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bashiru Ally alisema kinachofanyika ni mchezo wa kuigiza wenye nia ya kutuchanganya Watanzania.
Alisema jambo la msingi kuhusu utata wa kampuni hiyo na Tanesco ni kwa wote waliohusika kuliingiza taifa kwenye mkataba huo feki kujulikana na kuchukuliwa hatua.

“Kulipa au kutolipa deni hilo la Sh94 bilioni siyo hoja kwa sasa, hoja ni nani wamefikisha taifa hapo tulipo, ni pale tu Serikali kuanzia ngazi ya waziri na kushuka chini itakapotuletea msururu wa wataalamu waliosababisha taifa kuingia kwenye mkataba huo feki ndipo suala la Dowans litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Habari hii imeandaliwa na Elias Msuya, Sadick Mtulya na Geofrey Nyang'oro


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #5 kibonge 2011-02-22 08:45 naomba bwana wansakya uwe wa kwanza kuandaa andamano hilo la amani na sisi tutakuwa nyuma yako, kwa sababu wengi wanatoa mawazo ya kuandamana lakini nani wa kuanzisha??!!
Quote









+1 #4 MKWELI 2011-02-22 08:45 HII NI HATARI. SULUHISHO NI KUFANYA KAMA LIBYA, NCHI IMESHAHARIBIKA WANALOTAKA WACHACHE NDILO LINAFANYIKA KWA MASLAHI YAO NI SI KWA MASLAHI YA TAIFA. LEO UMESIKIA NI MKATABA KATI YA SONGAS NA DOWANS KESHO UTASIKIA NI UWAMUZI WA SERIKALI. WANANCHI TUSIFANYE MAKOSA TENA 2015. HAWA WATOTO WA VIGOGO WAMEWEKWA ILI KUNUSURU MASLAHI YA MAFISADI BABA ZAO.TUSIWAPE KURA HAWAFAI. KESHO UTAAMBIWA JANUARY MAKAMBA WAZIRI WA NISHATI!!!. HIVI HAWA VIONGOZI WA CCM WANAFIKIRI HII NCHI NI YAO PEKEE YAO?
Quote
 
Mmiliki wa Dowans azua jambo

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st February 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 450; Jumla ya maoni: 0








SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), ambalo liliamuliwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), kuilipa Kampuni ya Dowans Tanzania Limited Sh bilioni 94, limeguswa na ujio wa mfanyabiashara anayedaiwa kumiliki kampuni hiyo, Brigedia mstaafu Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi.

Al Adawi ambaye pia anamiliki Kampuni ya Dowans Holdings SA, yuko nchini na juzi alikutana na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam hasa magazeti, na kuzungumzia sakata linalohusisha kampuni yake ambalo limegusa hisia za watu wengi nchini kwa miaka kadhaa sasa.

Lakini katika ufafanuzi wake kwa mambo kadhaa kuhusu Dowans Tanzania Limited ikiwamo malipo hayo ya fidia ya Sh bilioni 94, mfanyabiashara huyo raia wa Oman, alisema yuko tayari kufuta kiasi cha deni hilo, lakini mitambo yake iachwe izalishe umeme kwa sababu ni mipya, lakini pia umeme wake ni wa bei nafuu.

Kwa msingi huo, Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipoulizwa jana kuhusu kuja kwa mmiliki huyo wa Dowans na kama wamezungumza naye, Masoud alijibu kwa kifupi, "najua unachotaka kuniuliza. Tutatoa taarifa rasmi kesho (leo)."

Hata alipoulizwa kama Tanesco wameshakutana na mmiliki huyo ambaye alisema moja ya sababu za ziara yake ni kujua kama kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano juu ya mambo yaliyopo kwa sasa, Msemaji huyo wa Tanesco, alisisitiza kwamba taarifa rasmi itatolewa leo.

Al Adawi katika mkutano wake huo na wahariri, alisema yeye ndiye mmiliki wa kampuni hizo mbili na kwamba aliteua rafiki yake wa siku nyingi, mfanyabiashara na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kufanya kazi zake nchini na kumpa nguvu kisheria ya kufanya hivyo.

Alisema aliombwa na Rostam kuja kuwekeza nchini mwaka 2006, baada ya kutokea matatizo ya umeme Tanzania; na kama alikuwa tayari kuwekeza na kwa msingi huo, alikubali mwito huo.

Aidha, katika mkutano huo na wahariri juzi, mfanyabiashara huyo inaelezwa kuwa alishangazwa na watu wanaoiponda kampuni yake na kudai ni feki, akisema inawezekanaje kwa kampuni feki kuwekeza mitambo yenye thamani ya dola za Marekani milioni 109 nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba alipoulizwa jana kuhusu kuja kwa mfanyabiashara huyo na kama wanafahamu lolote lililofikiwa kati yake na Tanesco, alisema taarifa hizo amezisoma katika vyombo vya habari,

"Nimesoma taarifa zake katika vyombo vya habari. Na amesema amewaandikia Tanesco. Lakini kesho (leo) tuna kikao na watu wa Wizara (Nishati na Madini), kwa hiyo tutaliulizia suala hili. Na keshokutwa (kesho) tunakutana na Tanesco, kwa hiyo yote tutayafahamu," alisema mbunge huyo wa Bumbuli.

Suala la Dowans limegusa hisia za watu wengi nchini na katika siku za karibuni, hukumu ya ICC inayoitaka Tanesco kulipa fidia hiyo ya Sh bilioni 94; hatua ambayo imepingwa na Watanzania wengi, lakini wapo wanaotaka mitambo yake iwashwe sasa kukabili tatizo kubwa la mgawo wa umeme nchini.

 
PHP:
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba alipoulizwa jana kuhusu kuja kwa mfanyabiashara huyo na kama wanafahamu lolote lililofikiwa kati yake na Tanesco, alisema taarifa hizo amezisoma katika vyombo vya habari, 

"Nimesoma taarifa zake katika vyombo vya habari. Na amesema amewaandikia Tanesco. Lakini kesho (leo) tuna kikao na watu wa Wizara (Nishati na Madini), kwa hiyo tutaliulizia suala hili. Na keshokutwa (kesho) tunakutana na Tanesco, kwa hiyo yote tutayafahamu," alisema mbunge huyo wa Bumbuli.

Huyu bwana mdogo kaja na pupa zake lakini ataumbulika hivi karibuni..............................This is a case of political expedience versus the rule of law......................

Swali la msingi la kujiuliza ni kwa nini JK aliwazuia Tanesco ili wasinunue mitambo yao wenyewe......................more than two years ago..........................kama lengo halikuwa ni kuwatafutia DOWANS biashara ya milele hapa nchini....................
 
PHP:
Maoni kuhusu Al Adawi
Lakini ujio huo umeibua hasira za wasomi na wanasiasa ambao kwa nyakati tofauti jana waliuita usanii huku, mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, akiitaka Serikali imkamate Al Adawi na kumhoji.
 
"Nilitarajia AlAdawi angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond, lakini hakufanya hivyo. Sasa naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola kwamba vimkamate, vimpige picha na kumhoji kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans,"alisema Mnyika na kufafanua:
 Kauli ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa Kahama, James Lembeli ambaye ameeleza kutilia shaka umiliki huo akihoji "muda wote, Al Adawi alikuwa wapi kama huu sio mwendelezo wa utapeli?"
 
"Kama kweli ni mmiliki halali siku zote alikuwa wapi, na kwa nini ajitokeze baada ya hukumu ya fidia ya malipo ambayo Watanzania wanaipinga,'' aliendelea kuhoji mbunge huyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
 
"Ni bora utembee na viraka kuliko mtu kukuvunjia heshima. Huu ni mchezo wa kundi la watu wachache wanaoichezea nchi na kuidhalilisha, huu ni utapeli mtupu,'' alisema Lembeli.
 
Mwanasheria maarufu nchini Profesa Abdallah Safari amemtaka Al Adawi kutoa nyaraka halisi zinazomtambulisha kuwa mmiliki wa kampuni ya Dowans vinginevyo anafanya ‘usanii'.
 
"Si suala la kuita vyombo vya habari na kujitangaza yeye ni mmiliki. Atoe nyaraka halisi zinazomthibitisha, kwani anaweza kuwa ni mwarabu wa Kariakoo,'' alisema Profesa Safari.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bashiru Ally alisema kinachofanyika ni mchezo wa kuigiza wenye nia ya kutuchanganya Watanzania.
 Alisema jambo la msingi kuhusu utata wa kampuni hiyo na Tanesco ni kwa wote waliohusika kuliingiza taifa kwenye mkataba huo feki kujulikana na kuchukuliwa hatua.
 
"Kulipa au kutolipa deni hilo la Sh94 bilioni siyo hoja kwa sasa, hoja ni nani wamefikisha taifa hapo tulipo, ni pale tu Serikali kuanzia ngazi ya waziri na kushuka chini itakapotuletea msururu wa wataalamu waliosababisha taifa kuingia kwenye mkataba huo feki ndipo suala la Dowans litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Habari hii imeandaliwa na Elias Msuya, Sadick Mtulya na Geofrey Nyang'oro

Tunaumisha vichwa kwa nini wakati mmiliki wa DOWANS ni JK?
 
Mmiliki Dowans utata


*Achanganya wananchi, wahoji maswali lukuki
*Mbunge ataka akamatwe apigwe picha kwa nguvu
*CTI wataka mitambo yake itaifishwe haraka


Na John Daniel

MBUNGE wa Ubungo Bw. John Mnyika ameitaka serikali kutumia vyombo vyake
vya dola kumtia mbaroni Bw. Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, aliyejitaja kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni tanzu ya Dowans Tanzania Limited.

Mbunge huyo amesema serikali inapaswa kuchukua hatua hiyo kwa madai kuwa mtu huyo alishakana kuhusika na kampuni hiyo wakati alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Dowans.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bw. Mnyika kwa vyombo vya habari jana, Bw. Al Adawi anapaswa kutiwa mbaroni kwa kuwa ametii kile alichosema katika tamko lake la Februari 16, mwaka huu la kutaka mmiliki wa mtambo huo ajitokeze.

Alisema katika tamko hilo aliitaka serikali itaifishe mitambo ya Dowans na kuiwasha kama sehemu ya kupunguza makali ya mgawo wa umeme na kuwataka wamiliki wake popote walipo duniani kujitokeza hadharani iwapo wana sababu za kuepusha mitambo yao isitaifishwe.

"Nilitarajia mmiliki wa Dowans ambaye angejitokeza angekiri hadharani kama wamedanganywa na kampuni ya Richmond na vyombo vingine katika kuhamishiwa mkataba ili kuweka msingi muhimu wa majadiliano, lakini imekuwa tofauti.

"Kutokana na hilo naomba kutoa rai kwa vyombo vya dola vimkamate vimpige picha na kumuhoji Al Adawi kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi na sheria nyinginezo kutokana na maelezo tata yaliyotolewa mpaka sasa kuhusiana na kampuni ya Dowans," alisema Bw. Mnyika katika taarifa yake.

Alidai kuwa kilichomshangaza ni kuwa siku chache baada ya tamko lake Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, alinukuliwa na gazeti moja Februari 18 mwaka huu kuwa serikali haitataifisha mitambo hiyo kwa kuwa hiyo siyo sera ya CCM.

"Ikumbukwe kwamba katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 128 la Machi 2009 Al Adawi alikanusha kuwa yeye sio mmiliki wa Dowans kama alivyonukuliwa katika Mahojiano na KLHN.

Kama amekuwa akikanusha kuwa si mmiliki lakini sasa amejitokeza kuwa ndiye mmiliki kuna kila sababu ya vyombo vya dola kumuhoji zaidi," alisisitiza Bw. Mnyika

Alitaka vyombo vya dola vimuhoji Bw. Al Adawi kuhusu utata wa kampuni ya Dowans Holdings SA ambayo kumbukumbu zake kamili hazipo Costa Rica inapoelezwa kusajiliwa na kuwa na ofisi zake.

"Kwa kuwa sasa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans wameanza kujitokeza ni muhimu pia wamiliki wa kampuni ya Portek Systems and Equipment PTE Ltd ambayo inatajwa kumiliki hisa takribani 40% kwenye Dowans wakatajwa na wakajitokeza," alisisitiza.

Alirejea ushauri wake wa kuitaka serikali kuitaifisha mitambo ya Dowans na kuchukua hatua stahiki dhidi ya ukiukwaji wa sheria uliyojitokeza ili kuepusha kasoro zingine kujitokeza katika hatua za dharura zinazokusudiwa kuchukuliwa hivi sasa.

"Kutaifisha mitambo ya Dowans sio kutekeleza sera ya chama chochote, ni kuzingatia maslahi ya taifa na kusimamia utawala wa sheria ikiwemo sheria ya uhujumu uchumi,"alisisitiza Bw.Mnyika katika taarifa yake.

Mbali na Bw. Mnyika, baadhi ya wasomaji wa gazeti walikerwa na kitendo cha mfanyabiashara huyo kukataa kupigwa picha ili Watanzania waweze kumuona, isijekuwa aliyejitokeza ni mtu mwingine asiyehusika.

"Biashara ni matangazo kama ilivyo siasa. Wafanyabiashara na wanasiasa ni watu wanaopenda kupigwa picha na kujitangaza Watanzania, Huyu Al Adawi ni mfanyabiashara wa namna gani asiyependa kupigwa picha na kuonekana? Sisi tuna walakini na biashara yake," alisema Bw. Jerome John, mkazi wa Kigilagila.

Mkazi mwingine wa Ilala ambaye hakutaka kutaja jina lake, alionesha hasira kwa wanahabari kwa kushindwa kumlazimisha Bw. Al Adawi kumpiga picha au kutunmia mbinu za kipaparazi kunasa picha yake ili iweze kuonekana.

Katika hatua nyingine, suala la Kampuni ya Dowans limezidi kuwachanganya wabunge baada ya watumiaji wakubwa wa umeme kuhoji Kamati ya Nishati na Madini, sababu za kushindwa kuishauri serikali kutaifisha mitambo ya kampuni hiyo haraka kunusuru taifa.

Pia kamati hiyo ya bunge imetakiwa kujibu iwapo nchi haikufanya makosa kuingia katika mkataba na Dowans wakati bunge liliazimia kusitishwa kwa mkataba wa Richmond baada ya kubaini mapungufu kadhaa.

Katika kikao kilichofanyika Ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam jana kati ya Kamati hiyo ya Bunge na viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Baraza la Biashara la Taifa (TNB) na Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF) wadau hao walitaka kamati hiyo kuchukua hatua za haraka kunusuru uchumi wa nchi.

Vyanzo vyetu ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa viongozi waandamizi wa taasisi hizo walionyesha wazi kukerwa na mjadala wa Dowans wakati nchi ikiwa katika hali ngumu ya umeme na kuitaka kamati hiyo kutoa majibu ya uhakika na kuweka siasa pembeni.

"Viongozi wa CTI, Bi. Esta Mkwizu, Bw. Arnold Kilewo na wale wa TPSF walituhoji ni kwa nini tunakazania tu kuzungumzia mitambo ya Dowans badala ya kuitaka serikali kununua mitambo yake.

Lakini kubwa zaidi walitaka mitambo ya Dowans itaifishwe haraka ili itumike kuzalisha umeme wa dharura kama mali ya nchi, walishangaa kwa nini nchi inapoteza mabilioni ya fedha bila sababu," kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho viongozi hao wa wafanbiashara wakubwa ambao ndio watumiaji wakubwa wa umeme kwa asilimia 8,0 waliitaka kamati hiyo kueleza iwapo si kosa kwa nchi kuingia mkataba na Dowans wakati bunge iliazimia kuwa mkataba wa Richmond haukuwa halali.

Awali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojiri katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Januari Makamba alisema wadau hao walilalamikia ukosefu wa umeme na kwamba hali hiyo imelisababishia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

"Tatizo la umeme ni kubwa kiuchumi, kwa mfano Twiga Cement pekee licha ya kutumia jenereta bado wanapoteza karibu milioni 20 kwa siku.

Kama taifa tunapoteza karibu dola za Marekani 200,000 kwa siku kutokana na ukosefu wa umeme, hii ni hali mbaya sana, ndio maana tumelazimika kuzungumza kwanza na wadau kujua ukubwa wa tatizo kiuchumi," alisema Bw. Makamba.

Alisema katika kikao hicho ambacho kilikuwa bado haijafikia mwisho CTI waliweka wazi kuwa kati ya viwanda 280 vinavyomilikiwa na wanachama wake 50 wameshindwa kuendelea na uzalishaji na kusitisha kazi kwa muda kwa ukosefu wa umeme.

"Kama mnavyojua tunatakiwa kuanza vikao vyetu wiki mbili kabla ya bunge lakini tuliomba kibali maalumu kwa Spika kufanya vikao kutokana na ukubwa wa tatizo hili, leo (jana) tumekutana na wadau, kesho (leo) tutakutana na Wizara ya Nishati na Madini na kesho kutwa TANESCO.

"Pia Jumamosi tutaitisha public hearing (mdahalo wa wazi) pale Karimjee, tutaandaa vizuri ili tupate mawazo ya wadau kwa utaratibu mzuri," alisema Bw. Makamba.

Alisema Kamati hiyo itakutana na wadau wote wanaohusika na umeme wa gesi ili kutoa mapendekezo yatakayokidhi haja ya taifa kuondokana na adha ya sasa.

Alisema Kamati yake haijatoa mapendekezo yoyote kuhusu mitambo ya Dowans na kwamba kilichonukuliwa na vyombo vya habari yalikuwa maoni yake binafsi kabla ya kikao cha kamati hiyo.

"Kamati itatoa mapendezo yake kwa serikali Jumanne ijayo baada ya kumaliza kazi yake, kwa sasa tunaendelea na vikao ili kujua nini kinachotakiwa hasa kuokoa taifa letu na ukosefu wa umeme," alisema.

Alipoulizwa iwapo Kamati yake itamwita mtu aliyejitangaza kuwa mmiliki wa Dowans anayedaiwa kutua nchini juzi na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwa sharti la kutopigwa picha alisema hawana sababu ya kufanya hivyo.

Hata hivyo alisema uamuzi wa serikali kutumia au kutotumia mtambo wa Dowans kuzalisha umeme wa dharura kwa sasa ni uamuzi tu na kwamba si jambo gumu na kufafanua kuwa kamati yake haiwezi kuishinikiza kufanya hivyo au kutofanya.

Alisema kabla ya kutoa mapendekezo yake kamati yake itafanya ziara kujionea hali halisi ya nishati hiyo katika vituo vyote vinavyozalisha umeme isipokuwa Mtera ambapo tayari wametembela.




3 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Sawa kaka Mnyika, Kaza buti na wabunge wengine wakusaidie katika hili bila kujali itikadi zao za kisiasa. Ukisikia utapeli wa kimataifa ndio huu. Sasa watanzania tuamke na tuwe makini katika hili. Hapa ndio patamu na pa kujua mbivu na mbichi katika sakata hili. mwananchi/ Mtanzania mwenzangu nina maswali kadhaa ambayo ningependa nikushirikishe katika kuyatafakari:-
1. Hivi umewahi kusikia wapi mwekezaji safi katika moyo wake (Adilifu) na mwenye nia njema katika biashara zake kukataa kuonana na viongozi wa serikali, kukataa kupigwa picha, kukataa kurekodiwa katika vyombo vya habari? Kwangu mie huyu ni mwizi na ni tapeli mzoefu, mbabaishaji na ni mtu wa kutunga umiliki wake wa kampuni.
2. Taarifa ya kamati ya bunge chini ya Uenyekiti wa Mh. Mwakyembe iliyopelekea Waziri Mkuu Lowasa kujiuzulu ilibainisha kuwa kampuni hii haijawahi kuwepo katika rekodi zozote za makampuni duniani; na hasa Costa Rica, Tanzania wala Canada. Sasa iweje leo ajitokeze kuja kuelezea umiliki na uwepo wa kampuni ya Dowans duniani na kwamba yeye ndiye mwenye hisa nyingi??
3. Katika kikao na waandishi wa habari (wakati anafafanua ugomvi wao na mzee Mengi juu ya mafisadi nyangumi na papa), Mh. Rostam Aziz - Mbunge wa Igunga alikana kuhusika kwake na kampuni zote mbili za umeme na kwamba hahusiki hata kidogo katika umiliki huo achilia mbali kusemasema na kujitokeza hivi karibuni. Je umiliki wake wa hisa ni wa aina gani? Je uongozi wake kama mbunge hauna shaka? Je uaminifu wake katika nchi yetu uko wapi? Je anafaa kuendelea kuitwa kiongozi wa watu kama aliwaficha/ aliwakana wawekezaji hapo awali? Mbunge aliyeapa kuitetea katiba, kuwa mwaminifu katika nchi yake, kutunga sheria za nchi na kutoa ushauri kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu??
4. Tapeli Adawi aliwahi kuhojiwa juu ya umiliki wake wa Dowans akakana. Leo anadiriki kujitokeza na kutaka kutuaminisha kuwa ni mmiliki halali wa kampuni ya Dowans. Hivi huu si ni ujinga na utapeli wa hali ya juu?

February 21, 2011 9:02 PM
blank.gif

Anonymous said... 5. Kwa kukataa tu kuonana na viongozi wa serikali, hatuoni kuwa kuna walakini hapa!! Kwanini mwekezaji halali wa kampuni aogope kuongea na viongozi? Ama atuambie ana watu wanaoshirikiana nao pale TANESCO au ni tapeli tu!! Kukataa kuonana na viongozi wa serikali si ni udhalilishaji na taifa (Nation Sovereignity)? Je ni halali mwekezaji kuweka masharti ya kutokuonana na viongozi ambao hiyo TANESCO inakuwepo kutokana na baraka ya viongozi?? Na hasa ukizingatia wingu kubwa lililopo katika nchi yetu kwa wakati huu? Yaani hata Waziri wa Nishati ambaye alikuwa anatetea kulipa deni naye ni adui wake?? Hapana hapa kuna jambo. Hivi Usalama wa taifa mko wapi na kwanini hamumshughulikii huyu jamaa ambaye anadhalilisha viongozi wetu?? Zoka upo au unajua kuwadhibiti wapinzani tu? Unbearable!!
6. Katika hotuba yake siku ya maadhimisho ya CCM, Mh. Rais Kikwete alisema hawafahamu wamiliki wa Dowans na kwamba haungi mkono kuwalipa Dowans. Imani yangu inaniambia kuwa Kikwete ni "baba" yetu (Nyumba ya Tanzania) na akisema deni, lisilipwe maana yake ni kuwa hatalipwa. Nilifikiri Adawi angesema anahitaji busara ya Rais ili alipwe badala yake anasema hataki kuonana na viongozi. Huu ni ubabe wa aina yake ndugu zangu watanzania na haupaswi kuachiwa kiuzembe namna hiyo. Kikwete unavumilia tu, Diplomacy?? No, No, No! Kila kitu kina ukomo wake kaka yangu Kikwete; Acha uzoba!!
7. Kuna baadhi ya wachangiaji katika matoleo yaliyopita wanashauri mwekezaji akae na TANESCO ili waone jinsi ya kupunguza au kusamehe deni. Hili ni jambo jema kabisa; lakini kwanini Taifa linyanyaswe na kudharauliwa hivyo? Mtu hataki kuonana na viongozi wetu (Hata kama walipatikana kwa kuchakachua), anawadhalilisha na kuwabeza. Hii sio haki na haihitaji kunyamaziwa hata kidogo. National Sovereignity has its space in here, we need to be a bit more serious than this otherwise we are welcoming Neo Neo Neo Colonialism in our country!!. Jambo la busara hapa ni kuitaifisha mitambo, kumtia adabu huyu mdharau viongozi wetu na tapeli wa kimataifa anayejitokeza siku za mwisho baada ya jambo hili kushika kasi.
8. Sakata hili limedumu kwa zaidi ya miaka mitano. Siku zote limewasumbua watanzania; viongozi na wanataaluma ndani na nje ya nchi. Hivi haiwezekani kuwa Rostam na wengine wamehusika kumshawishi huyu Adawi kujitokeza kuwa mmiliki halali ili malipo haya yaende kwake na wagawane na wamiliki uchwara?? Tukumbuke kuwa wote walikana kuhusika na kampuni hii; na kumbukumbu tunazo kupitia vyombo vya habari. Ikumbukwe pia matapeli huwa ni wajanja na wana mbinu mbalimbali za kutafuta fedha. Hivyo, sishangai kujitokeza kwa Adawi kuja kudai malipo hayo na ikizingatiwa udhaifu wa kisheria tulionao/ tuliouonyesha hadi sasa. Inawezekana kabisa kuwa hata viongozi wetu wamehusika kumwita huyu FISADI wa kimataifa maana watapata share yao. Ni wakati wa viongozi wetu kuonyesha misuli yao kisheria. Kikwete usikubali kudhalilishwa. Huu ni mchezo mchafu na haufai hata kidogo. Mkamateni na ashughulikiwe. Yapo mengi naweza kuyasema lakini naomba maswali yangu yaishie hapo kwe leo. "Hakuna Mjomba atakayetoka nje kuja kuwasaidia watanzania, kama yupo naomba mniambie/ mnitajie....." Mwl. Nyerere!!. Ewe mwananchi, tafakari na chukua hatua ndugu yangu Mtanzania.

February 21, 2011 9:05 PM
blank.gif

Anonymous said... Huyu mmiliki wa dowans ni mwizi inatakiwa akamatwe.

Hongera mnyika wewe ni noma hata Bana alikukubali kwenye mdahalo!!!!!!!!!!!!!!111

February 21, 2011 9:45 PM
 
Sometime you wonder if JK know his postion is about Decision Making and not Decision Supporting.

While great thinkers wengi humu tilimjua na kumjadili January makamba mtu amabye ni mdogo na hakuwa na role nyeti sana .Naona tuwafukue na tuwajue watu muhimu walioko nyuma ya pazia . Nani ni mshauri wa JK ikulu kwenye mambo ya

  • Uchumi,Uwekezaji,
  • Nishati,Mawasiliano(ICT),miundombinu
  • Viwanda , na biashara
  • Elimu
  • Afya
Mawazirini political sasa tuwajue wataalawa mambo haya amabo wako karibu na mkuu. Tujue wanasimaia upande ganiwa fani zao.

.....Ili tupate watu ambao wanaweza kufanya maamuzi magumu, kuna haja ya kuwa na somo la Decision making skills kama core katika mitalaa ya ngazi mbalimbali za elimu yetu
 
PHP:
Alitaka vyombo vya dola vimuhoji Bw. Al Adawi kuhusu utata wa kampuni ya Dowans Holdings SA ambayo kumbukumbu zake kamili hazipo Costa Rica inapoelezwa kusajiliwa na kuwa na ofisi zake.

"Kwa kuwa sasa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans wameanza kujitokeza ni muhimu pia wamiliki wa kampuni ya Portek Systems and Equipment PTE Ltd ambayo inatajwa kumiliki hisa takribani 40% kwenye Dowans wakatajwa na wakajitokeza," alisisitiza.

Huu ni uongo mwingine................kwenye affidavit ya kesi ya DOWANS versus RICHMOND ...............ambayo jana niliibandika humu kwenye thread hii DOWANS walidai wao ni wamiliki wa DOWANS kwa asilimia mia moja sasa hawa shareholders wanatoka wapi ambao yadaiwa wanamiliki silima arobaini?????????????????

Ipo siri kubwa ya kitapeli kwenye hili suala...................................na JK, EL na Rostam Aziz ndiyo waasisi wake.................
 
Mmiliki Dowans akagua mitambo Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:21

AKAGUA MITAMBO YA DOWANS KINYEMELA
Mwandishi Wetu
WINGU zito lililokuwa limetanda kuhusu picha ya mwanahisa mkubwa wa Kampuni ya Dowans, Brigedia Jenerali Mohammed Yahya Al Adawi, limeyeyuka baada ya kunaswa jana kwenye mtego wa kamera wakati alipotembelea mitambo ya kampuni hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Jenerali Al Adawi ameibua mjadala mzito nchini tangu alipotua na kufanya mkutano na wahariri wa magazeti matano Jumapili iliyopita, akigoma kupigwa picha pia akizuia televisheni na redio, huku akificha sura yake na sauti.Hata hivyo, mbio hizo za Al Adawi kukwepa kamera za waandishi jana ziliishia ukingoni baada ya kunaswa na gazeti hili akikagua mali zake zilizopo Ubungo.

Mpango mkakati wa kumnasa Al Adawi, ulipangwa na kufanikishwa kwa pamoja na duru huru za habari kutoka kwa raia wema ambao, awali walidokeza kuwa bosi huyo wa Dowans angefanya ziara kukagua mitambo ya kampuni hiyo mapema asubuhi.

Hata hivyo, mwanajeshi huyo mstaafu wa Jeshi la Oman, ratiba yake haikuwa wazi kwani duru nyingine za habari zilieleza Mwananchi kuwa, angewasili eneo hilo saa 7:00 mchana badala ya asubuhi.“Sina uhakika na ujio wa mtu huyo, lakini kwa taarifa zisizo rasmi mgeni huyo anaweza kuingia eneo hili saa 7:00 mchana. Labda kama utafika muda huo unaweza kufanikiwa kumuona, lakini sina uhakika," kilifafanua chanzo kimoja cha habari.

Lakini, kama wahenga walivyosema subira huvuta heri na hakuna marefu yasiyo na ncha, baada ya subira ya muda mrefu, bosi huyo wa Dowans alifika kwenye mitambo ya kufua umeme wa dharura saa 8:20 mchana akiongozana na watu watatu, ambao haikufahamika mara moja iwapo walikuwa wafanyakazi wa Tanesco au Dowans na kutumia dakika 22 kwenye ziara hiyo.Watu hao walifanya kazi ya kumuongoza Al Adawi kwenye maeneo ilipo mitambo hiyo, huku gazeti hili likishuhudia mmoja wao akimuonyesha bosi huyo mahali ilipo mitambo ya Dowans.

Akiwa ndani ya eneo hilo la Tanesco, bosi huyo alifanya ziara kwa dakika hizo, huku kila alipotembelea wafanyakazi walionyesha utiifu wa hali ya juu.Pia, Mwananchi ilishuhudia mmoja kati ya watu watatu alioongozana nao, akimuelekeza na kumuonyesha mitambo hiyo.

Akiwa eneo hilo, Mwananchi ilifanya mahojiano na baadhi ya wafanyakazi waliokuwamo ndani na kuelezwa kuwa, wao hawamfahamu mtu huyo ndio mara yao ya kwanza kumuona.“Mimi simfahamu kabisa mtu huyo isipokuwa nimeshangaa kuona mabosi wangu wote wakielekea huku juu aliko, kisha baadhi yao kuongozana naye,”alisema mmoja wa wafanyakazi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu za usalama.

Mwananchi ilishudia pia kila alipokuwa akipita Al Adawi, walinzi na wafanyakazi wengine waliokuwapo walisimama kuonyesha heshima hadi bosi huyo alipopita eneo hilo, ndipo walipokaa chini na kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Hali hiyo ilimsukuma mwandishi wa habari hizi kufuatilia na kuwauliza baadhi ya walinzi, iwapo wanamfahamu mtu huyo, lakini akajibiwa, "Hatumujui, lakini, ameongozana na baadhi ya mabosi wetu ndio sababu tunasimama kutoa heshima.”Al Adawi ni mmoja wa watu ambao majina yao yako kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni nchini (Brela), waliojiandikisha kama wamiliki wa kampuni hiyo ya Dowans.

Watu wengine waliotajwa na Brela kuwa ni wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd na uraia wao kwenye mabano ni Andrew James Tice na Guy Picard (Canada), Gopalakrishnan Balachandaran (India), Stanley Munai (Kenya) na Hon Sung Woo (Singapore).

Ujio wa Al Adawi ulitajwa kama njia pekee ya kuja kuweka mambo sawa, huku naye akisema yuko tayari kuzungumza na Tanesco kuhusu fidia ya Sh94 bilioni (hakutaja kiasi), baada ya kuvunjwa kwa mkataba baina ya kampuni yake hiyo na Tanesco."Nimekuja kwa mambo mawili; moja ni kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu Kampuni ya Dowans na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwapo suluhisho la kile kilichopo hivi sasa kuhusu Dowans," alisema Al Adawi.

Lakini Al Adawi ambaye katika mkutano huo aliambatana na mwanasheria wa kimataifa, John Miles na Mkurugenzi wa Fedha, Stanley Munai wa Dowans Tanzania Ltd, alisema licha ya Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji, kampuni yake nchini imekumbwa na jinamizi kwenye uwekezaji.“Nimekuwa na imani na Tanzania na nimeitikia wito wa uwekezaji kipindi cha matatizo yenu, lakini yote yaliyojitokeza tangu niwekeze nchini ni unyanyasaji na mnaendelea kuninyanyasa hadi leo na katika hali ya kawaida hamnitendei haki," alisema Al Adawi.

Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa, hakuwa ametaka kuishtaki Tanesco na kudai fidia ya mabilioni hayo ya shilingi, lakini amelazimika kufanya hivyo kutokana na jinsi alivyotendewa kipindi cha uwekezaji wake.
Al Adawi alifafanua kuwa Tanesco ilimhakikishia usalama wa uwekezaji wake,hivyo akakubali kuingia nao mkataba, lakini shirika hilo likavunja mkataba huo na kukiuka makubaliano yaliyofikiwa chini ya sheria zake zenyewe za ununuzi.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments




0 #2 POAz2 2011-02-23 07:50 MR. Moshi.
Inaonyesha wewe huijui kabisa elimu ya Historia ya Tanzania, hebu rudi shule kidogo kisha tizama uhusiano baina ya Omani na Zanzibar kisha ndio upurukuke kutoa Comment.

Quote









0 #1 issa moshi 2011-02-22 22:44 huyu si muoman huyu ni mtanzania aliye pewa paspoti ya omani kwa watu ambao wamefika au kuishi oman kitu hicho wanakijuwa fika ndio maana anajificha kama picha yake itachapiswa watu wengi watakuwa wanamfahamu mpaka kazi anayo fanya ikumbukwe kalibu nusu ya waoman wote ni watanzania wenye paspot za oman wengi wakiwa kutoka huko mikowani hasa shinyanga na mikowa ya pembeni maafisa wengi wa serikali ya omani ni watanzania hicho kitu kinajulikana na kiko wazi huyu adawi sio muoman huyu ni mtanzania jizi sema limepewa paspot ya oman kama ilivyo kwa watanzania wengine kwa hiyo si ajabu kuwa kitu kimoja na hawa vigogo wa serikali huyu ni mtanzania siyo muoman
Quote

 
PHP:
Mpango mkakati wa kumnasa Al Adawi, ulipangwa na kufanikishwa kwa pamoja na duru huru za habari kutoka kwa raia wema ambao, awali walidokeza kuwa bosi huyo wa Dowans angefanya ziara kukagua mitambo ya kampuni hiyo mapema asubuhi.

Kosa lenu Mwananchi ni kuwa picha za huyu njemba mbona hamziweki humu kwenye mtandao ili tuzifanyie kazi???????????
 
Wabunge wafungua kesi kupinga Dowans


*Wananchi wengine waunga mkono

Na John Daniel

KATIKA hali inayodhihirisha Watanzania kukerwa na malipo ya Kampuni ya Dowans, Mahakama Kuu ya Tanzania imepokea na
kusajili kesi ya kikatiba kupinga malipo hayo.

Kesi hiyo ya kikatiba ilifunguliwa mahakamani hapo jana na Watanzania saba wakiwemo wabunge watatu na kupewa namba tano ya mwaka 2011 chini ya Kampuni ya Mawakili ya Mpoki na Lukwaro.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, msingi wa kesi hiyo ni kwamba malipo ya Dowans ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sehemu ya tatu kifungu cha 27 Ibara ya kwanza na ya pili.

Katika kesi hiyo Watanzania hao wanaiomba Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa malipo hayo kwa kuwa yanakwenda kinyume na katiba ya nchi.

"Sisi kama Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, tunahurumia taifa letu na watu wake masikini wanaokosa hata huduma muhimu kutokana na hali ngumu, tumeamua kwenda kuomba haki Mahakama Kuu," alisema Bw. Senkoro Nzoka mmoja wa Watanzania hao.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 27 Ibara ya kwanza na ya pili malipo ya Dowans ni uvunjaji mkubwa wa katiba ya nchi kwa kuwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

"Kifungu cha 27 Ibara ya kwanza na ya pili inataka kila mwananchi kulinda rasilimali za nchi, sisi kama Watanzania tuna wajibu kuhakikisha rasilimali za nchi hazichezewi," alisema Bw. Senkoro.

Kifungu hicho cha Katiba kinasomeka- "27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, Kulinda mali ya umma, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao," inasema sehemu hiyo ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977.

Alisema kifungu hicho ndio msingi wao wa kufikia maamuzi ya kufungua kesi hiyo wakiwawakilisha Watanzania.

Hata hivyo Bw. Nzoka alisema hawezi kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kesi hiyo kwa kuwa ni suala la kisheria na kuweka wazi kuwa anachoweza kukiri ni kwamba wamejitolea kuwawakilisha wanannchi wasio na uwezo watakaoathirika kukosa huduma muhimu.

"Kama unavyojua hili ni suala la kisheria kwa sasa, siwezi kusema zaidi lakini tambua kuwa wabunge wa CCM walikataa na kuitaka serikali kutafuta njia ya kuepusha malipo hayo, huo ndio mwongozo wetu," alisema Bw. Nzoka bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Uchunguzi wa Majira ulibaini wabunge watatu wanaowakilisha wenzao katika kesi hiyo kuwa ni Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene, Bi. Anjela Kairuki pamoja na Bw. Gosbert Blandes.

Naye Bw. Hassan Nassoro ambaye ni kijana msomi Mtanzania aliyekuwa nchini Uingereza alisema atazungumzia kesi hiyo baadaye kwa kuwa ni suala la kisheria huku akithibitisha kuwa yeye ni mmoja kati ya walioifungua.

Sakata la malipo kwa Kampuni ya Dowans limekuwa kero kubwa kwa Watanzania tangu ilipoibuka kupitia vyombo vya habari na bungeni.

Awali ilidaiwa kuwa malipo hayo yalikuwa ni bilioni 195 lakini baadaye ilibainika kuwa taarifa hizo zilipikwa na watu wenye manufaa na kampuni hiyo kwa lengo la kuwaibia Watanzania.

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa kuwa ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara ICC) malipo hayo ni sh. bilioni 94.

Katika hatua inayoonyesha suala hilo kukumbwa na giza nene juzi mtu aliyedai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo alitingwa nchini na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari kwa masharti ya kutopigwa picha.

Sharti hilo limezua utata mzito huku Watanzania wengi wakidai kuwa mtu huyo si mmiliki wa kampuni hiyo na kuwa uenda amenunuliwa na wahusika ili wafikie lengo lao la kuvuna jasho la Watanzania la sh. bilioni 94.

Hii ni kesi ya pili kupinga malipo ya Dowans, kesi ya kwanza ilishafunguliwa na asasi za kiraia zipato 50 zikiwakilishwa na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC).
 
PHP:
Uchunguzi wa Majira ulibaini wabunge watatu wanaowakilisha wenzao katika kesi hiyo kuwa ni Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene, Bi. Anjela Kairuki pamoja na Bw. Gosbert Blandes.


Welcome to the party............................
 
TANESCO tayari kuzungumza na Dowans


Na Grace Michael

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema liko tayari kukutana na mmliki wa mitambo ya Dowans kwa ajili ya mazungumzo ili kuinusuru
nchi na janga la mgawo wa umeme ambalo linatishia kuporomoka kwa uchumi.

Hatua hiyo ilifikiwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa shirika hilo, Bw. William Mhando wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kujua kama shirika hilo limeshakutana na mmiliki wa mitambo hiyo au kama mitambo hiyo imeshawashwa.

Sisi hatujakutana na huyo mmiliki wa mitambo na wala hiyo mitambo hatujaiwasha...kumbukeni hili suala ni la kisheria na sisi tusingependa kuvunja sheria zilizopo lakini kama atakuja kwa ajili ya mazungumzo tuko tayari kuzungumza naye kwani lengo ni kuinusuru nchi na janga hili ambalo sasa linatishia kupomoa uchumi wetu,� alisema Bw. Mhando.

Hata hivyo, Kamati ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, Bw. January Makamba ilithibitisha kuwa TANESCO imepokea barua ya mwaliko wa mazungumzo kutoka kwa mmiliki huyo.

Kutokana na hatua hiyo, Bw. Makamba alisema kuwa wao kama kamati wangesisitiza TANESCO kufanya mazungumzo na mmliki huyo wa Dowans ili kupunguza tatizo la umeme ambalo linaikabili nchi kwa sasa.

Unajua hata jana (juzi) tulikutana na wamiliki wa viwanda nao walisema namna tatizo la umeme linavyokwamisha kazi zao na linavyotishia ajira za wananchi, hivyo kama kuna uwezekano wa hiyo mitambo kusaidia basi wafanye mazungumzo ili kunusuru hiyo hali,� alisema Bw. Makamba.

Akitoa taarifa ya kilichozungumziwa na kamati hiyo, alisema kuwa mjadala mkubwa ulijikita katika suala la umeme pamoja na mafuta ambapo wengi walihoji kuwepo kwa mfumuko wa mafuta na ubora wake.

Aidha alisema kuwa kamati iliweka msisitizo kwa wizara kuharakisha upatikanaji wa umeme ili tatizo hilo limalizike kwa kuwa limekuwa kero kubwa kwa nchi.

Kwa kweli kamati inachotaka ni umeme kuwaka...tumechoka na mipango ya kila siku...na kama mipango hiyo inachelewa kwa urasimu basi ishughulikiwe haraka ili lengo lifikiwe, tunajua kuna mpango wa kukodisha majenereta, mradi wa Dar es Salaam na Mwanza wenye jumla ya megawati 160 hivyo michakato hiyo ifanywe haraka ili miradi hiyo ikamilike, alisema Bw. Makamba.

Kwa upande wa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja alipohojiwa kuhusu kuwashwa kwa mitambo ya Dowans alisema hana jibu la suala hilo kwa kuwa liko mahakamani hivyo hawezi kulizungumzia.

Kamati ya Nishati na Madini leo itatembelea TANESCO kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo.

 
Maandamano makubwa CHADEMA Mwanza


*Ni kupinga malipo Dowans, kupanda gharama za maisha

Na Waandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuanza kutekeleza agizo la Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kufanya maandamano na
mikutano kesho, ikiwa ni ishara ya kupinga mambo kadhaa, ikiwemo mgawo na ongezeko la bei ya umeme kwa kuwa yameongeza ugumu wa maisha ya kila siku kwa Mtanzania.

Kwa mujibu wa viongozi wa juu wa CHADEMA, Mwenyekiti wa taifa, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa pia watazungumzia matukio kadhaa yanayotokea nchini ikiwemo suala la milipuko katika kambi za jeshi, hasa tukio la karibuni la mlipuko katika kambi ya Gongolamboto.

“Kwa kifupi niseme tunatarajia kuanza kampeni yetu ya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima wiki hii kama tulivyoahidi. Tunaanzia mikoa ya Kanda ya Ziwa na kituo cha kwanza kitakuwa Mkoa wa Mwanza na baadaye mikoa mingine. Tutazungumzia mambo mengi yenye maslahi kwa taifa letu,� alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya kufanya kusanyiko bila kibali inayowakabili viongozi kadhaa na wanachama wa Chama hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Dkt. Slaa alisema watatumia mikutano hiyo kuwaeleza wananchi
ukweli wa tukio la mauaji ya Arusha ili kuzuia upotoshaji unaofanywa na serikali kupitia vyombo na idara zake mbalimbali.

Wakati serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka zingine imekuwa ikielezea tukio hilo na kukitupia lawama chama hicho kwa vurugu zilizosababisha mauaji hayo Januari 5, mwaka huu, CHADEMA nao kwa upande wao wamedai kukusanya ushahidi ukiwemo wa kielektroniki kuthibitisha kuwa mauaji hayo yalipangwa na kutekelezwa na polisi kwa makusudi kwa shiniko la wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa pande wake, Bw. Mbowe alisisitiza kuwa CHADEMA haitapumzika katika kudai mabadiliko na mambo ya msingi yanayohusu maisha ya Watanzania na kutamba kuwa hakuna nguvu yoyote, iwe ya dola, mabomu wala risasi itakayozuia hamu ya mabadiliko inayotakiwa na umma wa watanzania.

“Hakuna njia ya kuzuia mabadiliko yanayotakiwa wa umma, CHADEMA kama tulivyoanza tutaongoza kampeni kudai mabadiliko yenye tija na maslahi kwa nchi bila kujali tofauti za kiitikadi za vyama. Maisha magumu yanayowakabili Watanzania kwa sasa haubagui, wote wamepigika sawa sawa. Lazima tuungane sote kudai maisha bora
tunayoahidiwa kila siku bila utekelezaji,� alisema, Bw. Mbowe.

Akifafanua alisema mateso wanayopata Watanzania yanasababishwa na viongozi walioko madarakani kukosa utashi wa kisiasa kuyakabili na kutolea mfano mfumuko wa bei unaosababisha bidhaa kupanda bei kila kukicha wakati uwezo wa kununua kwa mwananchi wa kawaida ukipungua huku viongozi wakipita na kutamba kuwa uchumi umekua na
kuimarika.

“Watanzania hawahitaji uchumi unaokuwa kwenye makaratasi na takwimu za wataalamu. Kinachotakiwa ni ukuaji huo kuonekana katika maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida na hii inahusu uwezo wa kununua bidhaa na mahitaji muhimu. Uchumi utakuaje wakati mtu hana uhakika wa bei ya sukari dukani kwani inapanda kila siku licha
kujengwa viwanda vingi vya sukari nchini kuliko kipindi kingine chochote?.

"Mwaka 2005 wakati rais Kikwete anaingia madarakani, bei ya kilo moja ya sukari ilikuwa sh. 600. Lakini kiasi hicho kwa sasa kinauzwa kati ya sh. 1,700 hadi 2,000 ambayo ni karibia ongezeko la asilimia 150 ndani kipindi cha miaka sita tofauti na kipindi cha awamu ya tatu chini, Bw. Benjamin Mkapa ambapo bei ya bidhaa
ilidhibiti kwa karibu miaka yote kumi aliyokaa madarakani.

"Pamoja na sukari baadhi ya bidhaa zingine za mahitaji ya kila siku zilizopanda bei mara dufu na bei za zamani na mpya kwenye mabano ni pamoja na paketi moja ya kiberiti (sh. 20 hadi 50), kipande cha sabuni (sh. 100 hadi 350), pakiti moja ya chumvi (sh. 50 au 100 hadi sh. 200 au 300), kilo moja ya nyama ya ng’ombe (sh.
2,000 hadi 4,000 au 5,000). Hii ni mifano michache kwani orodha ni ndefu," alisema.

Wakati hali ikiwa hivyo, makusanyo ya serikali kutokana kodi mbalimbali imeongezeka kutoka sh. bilioni 250 kwa mwezi hadi zaidi ya bilioni 400 na hivyo kuipa nguvu hoja kuwa tatizo siyo fedha bali utashi wa viongozi na mipango ya vipaumbele vya taifa katika matumizi ya serikali na haya ni baadhi ya mambo ambayo CHADEMA wameahidi kufafanua na kuyahainisha katika kampeni yao nchi nzima.

Hivi karibuni akitoa taarifa ya CC kwa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema kuwa mbali ya kuwahimiza wana-CHADEMA, wabunge na wananchi kwa ujumla kuendelea kupinga kwa nguvu zote malipo ya Dowans, CC ya chama hicho pia iliagiza sekretarieti kuanza maandalizi ya maandamano ya nchi nzima kupinga ongezeko la bei ya umeme, gesi na malipo kwa Dowans yatakayoanzia jijini Mwanza, Februari 24, mwaka huu.

"Kamati kuu imesikitishwa na kupanda holela kwa bei ya nishati muhimu ya umeme na gesi, pamoja na kushindwa kwa serikali ya CCM katika kuwekeza kikamilifu katika sekta ya nishati hapa nchini," alisema Dkt. Slaa.

Akizungumza na Majira jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw. Erasto Tumbo, alisema wataanza kwa maandamano jijini Mwanza, yatakayofuatiwa na mkutano katika viwanja vya Furahisha, kisha katika wilaya za mkoa huo.

"Kesho yake tutasambaa na kufanya mikutano katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza. Mikutano hiyo itafanyika pia kwa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, baada ya Mwanza, itafuata Shinyanga, kisha Mara halafu Kagera, kwa staili hiyo hiyo ya kufanya mkutano makao makuu ya mkoa kisha katika wilaya zote za mkoa husika," alisema Bw. Tumbo.

Aliongeza "tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi katika kila eneo husika, tutafanya maandamano ya amani, tayari tumeshatoa taarifa kwa polisi, hivyo hatuna mgogoro nao tena, na kwa sababu tumetoa muda mrefu bila shaka taarifa za kiintelijensia watakuwa wameshafanyia kazi ili kuhakikisha kuwa raia na mali zao wanalindwa."

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha, imeamuru kesi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA isijadiliwe nje ya mahakama hata kama inawahusu viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Bw. Charles Magesa alisema hayo jana wakati akizungumzia hoja zilizotolewa mahakamani hapo na mawakili wa upande wa utetezi na upande wa washtakiwa.

Bw. Magesa alikubaliana na hoja ya wakili wa upande wa utetezi na kutoa onyo kwa wale wote wanaoeleza masuala ya mahakamani nje ya mahakama.

“Mahakama hii, inatoa onyo kuacha mara moja kwa mtu yoyote kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani, kwani wanaofanya hivi wanajua wazi sheria zinakataa na hata wale wanaotoa vielelezo kwenye vyombo vya habari, nao waache mara moja, kwa kuwa wanavunja sheria,� alisema Bw. Magesa.

Imeandikwa na Tumaini Makene, Peter Saramba na Glory Mhiliwa

 
Nimeshangazwa sana na magazeti ya Habari leo na Daily News kukwepa kuzungumzia au hata kuripoti ujio wa huyu anayedai ni mmiliki wa DOWANS............................
 
Watu wa Uhamiaji, Airport, Tanesco na waandishi mliohudhuria mkutano wa huyo Al-Adawi tunaomba mtujuze nani walihusika ama kuratibu ujio wake na mambo yote anayofanya hapa nchini. Kuna siri kubwa imefichwa ndani ya ujio wake.
 
ETI "serikali haitataifisha mitambo hiyo kwa kuwa hiyo siyo sera ya CCM". -Ngeleja on 18th Feb 2011.
HUU NI UKICHAA UNAOZIDI WA KUTIBIWA MIREMBE (Hospitali ya magonjwa ya Akili Dodoma).

"Ikumbukwe kwamba katika gazeti la Mwanahalisi toleo namba 128 la Machi 2009 Al Adawi alikanusha kuwa yeye sio mmiliki wa Dowans kama alivyonukuliwa katika Mahojiano na KLHN.. Leo (two days ago) anakuja na kusema eti yeye ni Mmiliki...
HUU NAO NI UKICHAA UNAOZIDI WA KUTIBIWA MIREMBE (Hospitali ya magonjwa ya Akili Dodoma).

hivi huyo DO-ONCE (Al Adawi) anawezaje kuanzisha kampuni kubwa inayomuingizia mahela mengi hivyo nje ya nchi yake? Kwa uelewa mdogo ni kuwa ingekuwa imeanza nchini kwake Oman then ndio iwe na matawi Costa Rica, Tz n.k.

I'm sure hata kama WaTZ hawaamki, kusikia wala kuona haya maigizo, "they feel it". In a very short time we haki itapatikana tu.
 
Back
Top Bottom