Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

Mbita aionya serikali

na Datus Boniface

amka2.gif
BRIGEDIA Jenerali mstaafu Hashim Mbita ameionya serikali kama hakutakuwa na majadiliano baina yake na wananchi uwezekano wa kuvunjika kwa amani ni mkubwa.
Mbita alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam katika kongomano la uundwaji wa jukwaa la taifa la Asasi za Kiraia (AZAKI) la kitaifa na la kikanda.
Alisema tatizo kubwa lililopo katika serikali na utawala wa nchi nyingi za ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania ni kutokuwa na majadiliano ya pamoja kati yao na wananchi.
"…Shida kubwa iliyopo ni kukosa majadiliano ya pamoja kati ya watawala na raia, amani na utulivu inaweza kutoweka kwenye ukanda wa nchi za Afrika endapo majadiliano hayo hayatakuwepo," alisema Jenerali Mbita.
Akitolea mfano kwenye nchi zilizokumbwa na machafuko zikiwemo za Libya na Tunisia, alisema nchi hizo zimefika katika hatua hiyo kutokana na kutokuwa na majadiliano kati ya watawala na raia wake.
Alisema kwa miaka ya hivi karibuni nchi nyingi za Afrika zikiwemo zile za Uarabuni zimekumbwa na matukio ya uvunjifu wa amani, hivyo hali hiyo inaweza pia kutokea katika nchi nyingine za Afrika kama hakutafikiwa kwa hatua hiyo.
"Kukosekana kwa majadiliano kati ya raia na watawala hawa kunaweza kuzaa malumbano na kutoweka kwa amani," aliongeza.
Jenerali Mbita ambaye pia ni Balozi mstaafu na Mdhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alisema lengo la AZAKI ni kufaya kazi kwa pamoja na serikali katika kutekeleza mipango mbalimbali na kuleta maendeleo ya nchi.
 
Mimi natibu ukimwi, umaskini na mgawo wa umeme
ban.jicho.jpg

Mpayukaji wa Msemahovyo​

amka2.gif
MUNGU anatupenda hasa walevi Eimeeen. Bongolalaland imebarikiwa kupata tabibu asiye na kifani dunia nzima, Amiin. Baada ya kutokewa na God na kuniamuru nianzishe dhehebu la The Holiest and Highest Mighty Tarbenacle (THHMT), nimeamua kutoa huduma ya utatuzi wa matatizo mbali mbali bure.
Kuna wahuni wamelipa jina la utani dhehebu langu tukufu lililodhamiria kuondoa matatizo ya walevi. Wanaliita Tuamke Haraka Haraka Matatizo Tuondoshe. Kwa kiasi fulani hawajakosea. Maana dhehebu hili ndiye mkombozi wa pekee awezaye kuwafikisha walevi kwenye nchi ya ulabu na bangi bila wasi wasi baada ya wasanii kuwaahidi hili wakaishia kuwauza utumwani mwa wachukuaji, wachakachuaji na mafisadi. Tuachane na haya ya watani.
Seriously, nimejitenga na wivu, chuki na njaa kama Zaa-kalia Ka-Tortoise ambaye amenukiliwa akilalamika kuwa usanii wake umekosa walaji baada ya kuibuka kwa babu. Babu kakonga roho yangu kuwafichua matapeli wanaomtumia Mungu kuwaibia walevi. Mie nasema wazi. Simchukii babu. Maana wajinga ndio waliwao. Akinipiku kwa kuvuta umati wa wachovu, sitalalamika bali kwenda kuuza nyanya.
Mimi ni tofauti na hawa waota ndoto. Nimemuenga God kwa maninga yangu mawili. Hivyo, tiba yangu si ya kubangaiza wala nini, niaminini.
Baada ya kuona watu hasa vigogo wanavyohenyeka kwenda Loriyondo na ugogoro na utata uliojitokeza kutokana na tiba wanayofuata kule, hatimaye, God amesikia kilio chenu.
Amenituma niwasaidieni. Msiulize tuliongea au kukutana linin a wapi. Hili haliwahusu. Amenipa mamlaka niyatumie lau kujipatia raha hata senti kidogo nikitaka.
Vigogo msiogope kuja kwangu. Hata kama mmeishaikanyaga miwaya nitatunza siri zenu ilmradi tukatiane chochote kitu. Mie siruhusu mle peke yenu ndiyo maana God amenituma kwenu.
Nimeamua kutibu matatizo yote ili kuwaonea hasa huruma vigogo ambao wameonekana wakihaha kwenda kule. Anwani yangu ni simpo. Alhaj, mtakatifu, maulana, nguli, gwiji,mchunaji, sorry mchungaji wa wachungaji, daktari wa madaktari, shehe wa mashehe, mtakatifu Mpayukaji Msemahovyo mjukuu wa mzee Waambie Waelewe, MB, MBA, MSc, DM, PhD, DD, LLD, MPHDM, kwa Mfugadog Bongo, Bongolalaland.
Mnaziona shahada zangu? Si za kughushi. Mie nimesoma sana na si mchunaji bali mchungaji wala si shehena bali shehe.
Mungu amenipa karama hii baada ya kugundua kuwa wabongolalaland ni wagonjwa wa roho, akili na mwili. Hivyo aliona ni bora kumtafuta mtu muadilifu na mwelevu kama mimi.
Mimi siyo kama wale matapeli wanaojivisha uchungaji na ushehena wa kujipachika na uombezi wa kuibiana na kuhadaana. Mimi sitibii njaa wala kutaka sifa. Situmii luninga, magazeti ya udaku wala radio kutangaza huduma yangu. Pia ninayo dawa ya kuzuia TAKUKURU kukukamata hata ukichukua kitu kikubwa. Nina zindiko la kuwazuia walevi kukustukia unapowaliza.
Mie si mpenzi wa kujisifu. Mimi ni kama brigedia Al Adui wa Duwanzi, sipendi sifa. Ila ukweli ni kwamba ni mimi yule yule aliyewapa zindiko kina Dowans, Kagoda, Richmond, IPTL, Net Group, EPA, Zumbe wa mauaji ya Kirosa na wengine wengi tu.
Mjapo kwangu mnatoka ukiwa kile Wajapani huita shin Jin Rui au viumbe wapya. Mie silazimishi uwe na imani. Wala sitaki uwe na kile wahindi huita satyagaraha. Uje ukiwa dasht e kavir au dasht e lut (chumvi au mchanga) mie nitakutibu uwe binadamu. Samahani kwa kuongea kijepu na ki*********. Nimewahi kuishi kule. Au niongee kihawaii?
Anyway, mkitoka kwangu mtakuwa wapya na kuambiana heri ya mwaka mpya au Hau'oli Makahiki Hou. Nasema "Uyavutha Umlilo" kwa wale ndugu zangu wazulu au moto wawaka; mtakuja. Tuachane na lugha za watu.
Natenda miujiza ambayo haijawahi kutendwa na yeyote popote juu ya nchini, chini ya bahari na angani. Kwa mfano, nina dawa ambayo ukiinyunyizia nyumbani umeme unawaka na unaepukana na kulanguliwa na Tanidowanesco.
Natibu ukimwi, umaskini, mgao wa umeme, ugumba wa aina zote hata wa mawazo, hofu, matatizo ya kupata mume, kuongeza upendo, kuondosha nuksi na mikosi, kushinda uchaguzi, kukinga maandamano, kuzuia kuvunjika kwa amani, msongo wa roho, presha na chuki dawa hiyo moja.
Nina uwezo wa kuongeza uwezo wa kufikiri, kujiamini, kuridhika, kuvumilia hata kama unaliwa, kuona visivyoonekana na kupanua utajiri.
Pia natibu magonjwa ya migawanyiko, mitandao, msongo wa mawazo, kuzuia kushitakiwa ukighushi vyeti, kuzuia kustukiwa ukichakachua iwe pesa au uchaguzi na mengine kama hayo.
Kuhakikisha praivesi (faragha) yenu inatunzwa, nitatibia vigogo na akina mama uani na chumbani. Nifafanue.
Vigogo wa kiume nawatibia uani na akina mama wawe vigogo au la natibia Guest House. Hili ni sharti nililopewa na God. Najua bila kutoa maelezo mtaanza kuguna na kuuliza kunani.
Kwa akina mama, kama una sura mbaya au ni mzee utatibiwa na vigogo uani. Kama ni kidosho, nimeagizwa nikutibie Guest House ili kuondoa nuksi. Nadhani naeleweka. Pia tiba hii lazima ifanyike usiku kizani ili shetani asiweze kukuona na kukuweka alama na kulipiza kisasi.
Sababu nyingine ya kutibia uani ni kuepuka wezi kuiba teknolojia yangu, pia kuhakikisha wadaku wa magazeti na runinga hawapati picha za vigogo wanaoumwa hasa Ukimwi na ufisadi na kuwaanika. Pia akina mama wazee hawaogopi kiza ni watu wazima.
Wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wanaotaka kupata mikopo haraka na kushinda mitihani yao waje kwangu haraka. Wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wanaohofia mikataba yao au ukwepaji kodi wao kugunduliwa na kushitakiwa hata kufilisiwa njooni haraka.
Wale walioshindikana yaani ambao wanahisi hawawezi kuolewa au kuzaa waje haraka. Wanasiasa hawana haja ya kwenda Bwagamoyo kwa mambo ya uchaguzi. Waje kwangu watashinda hata kama hawana sifa. Chama kinachotishiwa kunyang'anywa ulaji kifanye haraka.
Sitaki niseme mengi. Nadhani mmeona ukweli wangu. Hivyo nategemea mtamiminika kwangu badala ya kwenda Loriyondo.
Wajinga ndio waliwao. Naona kinokia kinalonga. Huenda wameanza kujiingiza. Haloo profesa mtakatifu hapa!
 
Kikwete aelezwa makali ya mgawo

Na Edmund Mihale

WAZIRI wa Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo amemweleza Rais Jakaya Kikwete jinsi makali ya mgawo wa umeme yanavyoathiri uzalishaji katika sekta ya
uchumi na kijamii nchini.

Akitoa taarifa ya Rais Kikwete alipotembelea wizara hiyo jana, Bw. Mkulo alisema, "Athari kubwa ni kupungua kwa mapato ya ndani kutokana na kushuka kwa uzalishaji. Bajeti ya serikali imebidi kutumika kusaidia ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura," alisema Bw. Mkulo.

Alisema kuwa hali hiyo imesababisha kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa na huduma.

Sababu nyingine iliyosababisha ugumu wa maisha, alisema kuwa ni kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia iliyosababishwa na hali mbaya ya kisiasa katika nchi za kiarabu.

Akitoa majumuisho ya taarifa hiyo, Rais Kikwete hakuzungumzia suala hilo bali masuala mengine, huku akiitaja wizara hiyo kuwa moyo wa nchi katika uendeshaji, hivyo inatakiwa kuwa makini katika utendaji wake.

"Wizara ya fedha ni kama moyo kwa binadamu, ni kiungo muhimu katika uendeshaji wa serikali ikizembea shughuli zote za serikali zinasimama," alisema Rais Kikwete.

Mbali na hilo, alizungumzia Sheria ya Manunuzi ya Umma kuwa ndiyo inayotoa mianya ya rushwa, na kuitaka wizara hiyo kuhakikisha inasimamia eneo hilo kwa umakini makubwa.

Hata hivyo Rais Kikwete alisema pamoja na kuwa sheria hiyo ni nzuri lakini ni ngumu katika utekelezaji, aakaitaka wizara hiyo kuagalia namna inavyoweza kuiboiresha kuwa tija katika jimii.

"Jamani sheria hii ni nzuri lakini ina ugumu wake, nakumbuka nilikwenda Halmashauri ya Mahenge wakanimbia kuwa iwapo watasimamia wao ujenzi nyumba zao watajenga moja kwa sh. milioni 15 lakini wakitumia sheria hiyo watajenga moja kwa sh. milioni 46, hapa mtaona kuwa kuna nyumba tatu kama watasimamia wao.

"Katika sheria hii ndipo watu wanapokula wanaibia serikali sasa hilo mliangalie," alisema.

Rais alizungumzia sheria hiyo wakati kuna mjadala miongoni mwa wabunge kuwa kuna mpango wa kubadili sheria hiyo na kuondoa kifungu kinachozuia kununua bidhaa zilizokwishatumika, ikiwamo mitambo ya Dowans.

Uhamisho wa wafanyakazi

Rais Kikwete aliwataka watendajiwa serikalia kutowahamisha wafanyakazi iwapo ofisi zao hazitakuwa na fedha.

Alisema hali hiyo inachangia kuongezeka kwa deni la serikali na hatimaye kusababisha migomo isiyo na lazima katika sehemu za kazi.

Ukuaji wa uchumi

Rais Kikwetea aliitaka wizara hiyo kuhakikisha kuwa inaelekeza katika maeneo yanayosababisha ukuaji wa uchumi ili kuongeza mapato ya serikali.

Wazee wa Afrika Mashariki

Aliagiza wizara kufanya utaratibu wa kuwalipa haraka wazee hao kwa kuwa limekuwa suala la muda mrefu.

1 Maoni:

blank.gif

Göttingen said... Kazi ya uwaziri ni pamoja na kumshauri raisi. Si vema raisi kupewa taarifa hii baada ya kutembelea wizara. Ilibidi tangu mapungufu haya yaanze kujitokeza, yangepelekwa kwenye baraza la mawaziri ili kujadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi mapema. Kama ilikuwa inajulikana kwa raisi tayari, basi hii si taarifa ya kumpatia raisi baada ya kutembelea wizara zake. TUWAJIBIKE KWA MAKINI NA UADILIFU KATIKA DHAMANA TULIZOPEWA.
March 16, 2011 12:15 AM

Post a Comment
 
Tiba ya Liliondo ‘isizike' mjadala wa Dowans
ban.blank.jpg

Joseph Sabinus​

amka2.gif
p>KATIKA moja ya makala zangu, niliwahi kuandika kuhusu tatizo la Watanzania kuvutwa na kuyumbishwa kwa hoja za msimu kadiri zinavyojitokeza. Kwamba hali hiyo, imewapa nguvu hata watawala wazembe kuongeza juhudi za kumuomba Mungu wao ili liibuke suala jipya linaloweza kuzima lile la moto linalokuwa likichemka kwa nguvu ya moto wa kasi au bungeni, kwenye vyombo vya habari na katika jamii kwa jumla.
Kama ilivyo ada, shilingi inazo pande kuu mbili; upande wa mwenge na upande wa kichwa. Ndivyo ilivyokuwa hata katika makala hiyo. Kwamba wapo walioniunga mkono na kukiri kuwa kweli, jamii yetu inaumwa ugonjwa huo wa kuvutwa na kuyumbishwa na hoja za msimu na matukio ya msimu.
Kwamba hili linapovuma, wanaliacha hili hata kama bado "changa"; wanalifuata lingine la wakati huo huo ambalo nalo hawalifikishi tamati na kujua limekwisha vipi.
Kadhalika, wapo waliosita kukubaliana na mimi na wengine wakasema nami kama mwandishi wa habari, ninayo sehemu kubwa ya kulaumiwa kwa kutokuwa chachu ya kuendeleza hoja hizo.
Nianze tu kwa kusema kwamba mimi sio malaika. Nami pia ninayo madhaifu kama walivyo wanajamii wenzangu hivyo, ninapoikosoa jamii, maana yake ni kwamba nami ninajikosoa pia maana Wazungu wanasema ‘Charity begins at home', yaani wema huanzia nyumbani.
Nipende tu kusema kuwa, takriban wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimetawaliwa na habari kutoka Loliondo inapotolewa tiba mbadala ya Mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu.
Babu ambaye anatoa tiba mbadala kwa msingi wa imani kwa Mungu, amekuwa gumzo kubwa na kimbilio kwa watu mbalimbali kwa kuwa jamii yetu inaumwa magonjwa mbalimbali yakiwamo hasa ya kimwili yanayosababishwa na mambo mbalimbali kama ugumu wa maisha na mienendo michafu ya kimaisha.
Ndani ya matatizo yanayoshuhudiwa na mashuhuda mbalimbali wa "tiba ya Babu", ni pamoja na udhaifu wa kinga mwilini, kiharusi, kisukari na magonjwa ya moyo ambayo hakika ni tatizo sugu kwa Watanzania na chanzo cha matatizo mengine ukiwamo umaskini katika jamii.
Hivi vitapatikana endapo kila mmoja atapaza sauti ya unyenyekevu na kumlilia Mungu aliponye Bara la Afrika kwa namna na njia aitakayo Mungu.
Hayo ndiyo yametokea Tanzania. Vyombo vya habari zaidi ya wiki nzima sasa vinatawaliwa na habari za tiba mbadala inayotolewa Liliondo mkoani Arusha na Mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapile.
Tiba hiyo inayokwenda sambamba na imani ya uponyaji utokao kwa Mungu, imekuwa kivutio cha maelfu ya watu toka ndani na nje ya nchi, na inadaiwa kutoa matunda makubwa yanayoshuhudiwa na watu mbalimbali waliokuwa na mgonjwa mbalimbali. Hawa, ni watu wa kada mbalimbali.
Hilo hatukatai kujadiliwa kwa kina maana tunahitaji usalama wetu kwanza ili mambo mengine yajadiliwe kwa hoja na kwa kina, maana amani na usalama au tuseme uzima, ni mtaji wa kila jambo jema.
Hata hivyo, kuibuka kwa "uponyaji" huo ambao ni kazi ya Mkono wa Bwana unaowashukia Watanzania, ambao kamwe haupaswi kuwa mtaji wa kuacha mambo mengine muhimu na badala yake, kuganda juu ya Loliondo.
Ieleweke mapema kabisa kwamba nami ninaunga mkono na wala sipingi watu kwenda kutafuta tiba hiyo mbadala ambayo ina upekee zaidi wa kutumia nguvu ya Mungu, na si kupiga ramli hivyo ni vyema na haki watu waizungumze na huku pia, wakipanga taratibu nzuri za kuendelea na uzalishaji mali na mijadala mingine muhimu kwa taifa.
Mambo yanayolikumba taifa kama ugumu wa maisha unaowatafuna wananchi kiasi kwamba kila siku inaonekana ngumu kuliko jana, bahati mbaya au basi tuseme uzembe uliosababisha takriban watu 40 kupoteza maisha katika milipuko ya mambo iliyotokea katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 511KJ cha Gongo la Mboto na hata tatizo la mgawo wa umeme ambao umekwenda sambamba na nyongeza ya bei, ni mambo ambayo katu hayapaswi kuzikwa kwa njia ya tiba ya Loliondo.
Watanzania bado wanahitaji majibu ya maswali mengi kutoka kwa watawala, ikiwa ni pamoja na kujua hatima ya malipo ya mabilioni ya pesa za wavuja jasho kutokana na mikataba mibovu na kampuni za ajabuajabu ikiwamo ile ya kufua umeme wa dharura ya Dowans. Wanataka kujua what is up; and what is next (kuna nini na nini kinafuatia).
Watanzania wanayo kiu kubwa kusikia tena "ahadi zile na kama zile" za Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kama bado tatizo la umeme nchini litaendelea kuwa historia ya kukosekana au litabadilika na kutoka hapa ili sasa mgawo wa umeme na kupanda ovyovyo kwa bei yake vibadili mfumo wa masimulizi na kuwa unaoanza kwa maneno, "Hapo zamani za kele, palikuwa na mgawo wa umeme na kupanda kwa bei kila siku…"
Watanzania wanayo hamu ya kusikia Waziri Ngeleja akiendelea "kuuimba wimbo huu" japo hawaoni mchezaji wake katika uwanja ulio wazi.
Watanzania wanahitaji kujua kuna sababu gani za msingi zinazovisukuma baadhi ya vyama vya siasa kutaka kufanya maandamano na kuna sababu gani za msingi za kuwafanya walaumiwe na wasifanye hivyo.
Watanzania wanahitaji mapema kujua mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaanzaje, utafanyikaje na utamalizika vipi ili Katiba ya nchi iwe ya wananchi wote na isiwe inayowabeba "watoto wa mama" huku wengine ambao labda ndio "watoto wa mama wa kambo, wakiachwa watembee kwenye kokote bila viatu".
Yapo mambo mengi muhimu kujadiliwa bila kuuawa kwa agenda yoyote ikiwamo agenda ya tiba ya Babu kule Loliondo.
Tiba ya Babu iheshimiwe na watu waendelee kupata huduma hiyo ili kwa mapenzi yake Mungu, mwenye kupona apone na mwenye kushindwa, ashindwe maana Bwana ndiye aliyetoa na ndiye anayetwaa.
Watanzania waende kutafuta huduma ya tiba hiyo mbadala kwa imani ya kupata nguvu za Mungu huku wakijua kuwa, imani ndiyo inayopnya na kwamba, hata kabla ya huduma hiyo, magonjwa kama malaria yalikuwapo yakiwa na tiba za kidaktari kutoka kwa wasomi waliobobea, lakini Tanzania tumezika ndugu zetu wengi hivyo, hata tunapopona, tusipone ili turudi "kuanza upya mashambulizi" ya uzembe dhidi ya kanuni za afya.
Tuache hayo, tuendelee kujadili masuala mengine ya msingi pia ikiwa ni pamoja na kwanini watoto wetu waliohitimu kidato cha nne katika mtihani wa mwaka 2010, walifeli katika kiwango cha kutisha.
Tuendelee kutafuta majibu halisi ya kwanini wafeli kiasi hicho ilihali kuna serikali? Kwanini wafeli kiasi hicho ilhali kuna wizara inayohusika na masuala ya elimu; kwanini ilhali kuna walimu na takwimu zinazoonyesha idadi ya majengo ya shule zinazidi kuongezeka?
Tusihamishe hoja na kuishia Loliondo; bali tujiulize na kutaka kupewa majibu kwamba, walimu wanatosha katika shule hizo za sekondari? Walimu wanafanya kazi katika mazingira ya kiutu yanayoonesha wanaheshimiwa na kwamba wanapaswa kutiwa moyo?
Bado tujiulize vitendea kazi kama vitabu vya ziada na kiada vipo, mishahara wanapata kwa wakati na kwa njia isioyowapa usumbufu? Kama hakuna, tujiulize kwanini baadhi ya shule zimekuwa mapango ya popo na nyingine zikikosa walimu?
Yapo mambo mengi ikiwa ni pamoja na tatizo lingine linalozidi kuibuka la ukosefu wa maji safi na salama hata katika maeneo ya mijini ambako eti kuna mabomba. Jamii ijiulize, kina mama kule vijijini watajifungua kwa kutumia mwanga wa vibatari hadi lini?
Ndiyo maana ninasema, Watanzania watumie tiba mbadala ya Loliondo, lakini wasiue wala kusahau mambo mengine muhimu ili hata hao wanaopona, Mungu awajalie wapone na kuja kuishi katika Tanzania inayofaa kuishi.
Majibu kama matatizo ya milipuko katika kambi za majeshi, bado yanahitaji kutolewa ili mzembe ajulikane na ajibu kwanini uzembe wake uwe bei ya mauti ya wengine.
 
Mimi natibu ukimwi, umaskini na mgawo wa umeme
ban.jicho.jpg

Mpayukaji wa Msemahovyo​

amka2.gif
MUNGU anatupenda hasa walevi Eimeeen. Bongolalaland imebarikiwa kupata tabibu asiye na kifani dunia nzima, Amiin. Baada ya kutokewa na God na kuniamuru nianzishe dhehebu la The Holiest and Highest Mighty Tarbenacle (THHMT), nimeamua kutoa huduma ya utatuzi wa matatizo mbali mbali bure.
Kuna wahuni wamelipa jina la utani dhehebu langu tukufu lililodhamiria kuondoa matatizo ya walevi. Wanaliita Tuamke Haraka Haraka Matatizo Tuondoshe. Kwa kiasi fulani hawajakosea. Maana dhehebu hili ndiye mkombozi wa pekee awezaye kuwafikisha walevi kwenye nchi ya ulabu na bangi bila wasi wasi baada ya wasanii kuwaahidi hili wakaishia kuwauza utumwani mwa wachukuaji, wachakachuaji na mafisadi. Tuachane na haya ya watani.
Seriously, nimejitenga na wivu, chuki na njaa kama Zaa-kalia Ka-Tortoise ambaye amenukiliwa akilalamika kuwa usanii wake umekosa walaji baada ya kuibuka kwa babu. Babu kakonga roho yangu kuwafichua matapeli wanaomtumia Mungu kuwaibia walevi. Mie nasema wazi. Simchukii babu. Maana wajinga ndio waliwao. Akinipiku kwa kuvuta umati wa wachovu, sitalalamika bali kwenda kuuza nyanya.
Mimi ni tofauti na hawa waota ndoto. Nimemuenga God kwa maninga yangu mawili. Hivyo, tiba yangu si ya kubangaiza wala nini, niaminini.
Baada ya kuona watu hasa vigogo wanavyohenyeka kwenda Loriyondo na ugogoro na utata uliojitokeza kutokana na tiba wanayofuata kule, hatimaye, God amesikia kilio chenu.
Amenituma niwasaidieni. Msiulize tuliongea au kukutana linin a wapi. Hili haliwahusu. Amenipa mamlaka niyatumie lau kujipatia raha hata senti kidogo nikitaka.
Vigogo msiogope kuja kwangu. Hata kama mmeishaikanyaga miwaya nitatunza siri zenu ilmradi tukatiane chochote kitu. Mie siruhusu mle peke yenu ndiyo maana God amenituma kwenu.
Nimeamua kutibu matatizo yote ili kuwaonea hasa huruma vigogo ambao wameonekana wakihaha kwenda kule. Anwani yangu ni simpo. Alhaj, mtakatifu, maulana, nguli, gwiji,mchunaji, sorry mchungaji wa wachungaji, daktari wa madaktari, shehe wa mashehe, mtakatifu Mpayukaji Msemahovyo mjukuu wa mzee Waambie Waelewe, MB, MBA, MSc, DM, PhD, DD, LLD, MPHDM, kwa Mfugadog Bongo, Bongolalaland.
Mnaziona shahada zangu? Si za kughushi. Mie nimesoma sana na si mchunaji bali mchungaji wala si shehena bali shehe.
Mungu amenipa karama hii baada ya kugundua kuwa wabongolalaland ni wagonjwa wa roho, akili na mwili. Hivyo aliona ni bora kumtafuta mtu muadilifu na mwelevu kama mimi.
Mimi siyo kama wale matapeli wanaojivisha uchungaji na ushehena wa kujipachika na uombezi wa kuibiana na kuhadaana. Mimi sitibii njaa wala kutaka sifa. Situmii luninga, magazeti ya udaku wala radio kutangaza huduma yangu. Pia ninayo dawa ya kuzuia TAKUKURU kukukamata hata ukichukua kitu kikubwa. Nina zindiko la kuwazuia walevi kukustukia unapowaliza.
Mie si mpenzi wa kujisifu. Mimi ni kama brigedia Al Adui wa Duwanzi, sipendi sifa. Ila ukweli ni kwamba ni mimi yule yule aliyewapa zindiko kina Dowans, Kagoda, Richmond, IPTL, Net Group, EPA, Zumbe wa mauaji ya Kirosa na wengine wengi tu.
Mjapo kwangu mnatoka ukiwa kile Wajapani huita shin Jin Rui au viumbe wapya. Mie silazimishi uwe na imani. Wala sitaki uwe na kile wahindi huita satyagaraha. Uje ukiwa dasht e kavir au dasht e lut (chumvi au mchanga) mie nitakutibu uwe binadamu. Samahani kwa kuongea kijepu na ki*********. Nimewahi kuishi kule. Au niongee kihawaii?
Anyway, mkitoka kwangu mtakuwa wapya na kuambiana heri ya mwaka mpya au Hau'oli Makahiki Hou. Nasema "Uyavutha Umlilo" kwa wale ndugu zangu wazulu au moto wawaka; mtakuja. Tuachane na lugha za watu.
Natenda miujiza ambayo haijawahi kutendwa na yeyote popote juu ya nchini, chini ya bahari na angani. Kwa mfano, nina dawa ambayo ukiinyunyizia nyumbani umeme unawaka na unaepukana na kulanguliwa na Tanidowanesco.
Natibu ukimwi, umaskini, mgao wa umeme, ugumba wa aina zote hata wa mawazo, hofu, matatizo ya kupata mume, kuongeza upendo, kuondosha nuksi na mikosi, kushinda uchaguzi, kukinga maandamano, kuzuia kuvunjika kwa amani, msongo wa roho, presha na chuki dawa hiyo moja.
Nina uwezo wa kuongeza uwezo wa kufikiri, kujiamini, kuridhika, kuvumilia hata kama unaliwa, kuona visivyoonekana na kupanua utajiri.
Pia natibu magonjwa ya migawanyiko, mitandao, msongo wa mawazo, kuzuia kushitakiwa ukighushi vyeti, kuzuia kustukiwa ukichakachua iwe pesa au uchaguzi na mengine kama hayo.
Kuhakikisha praivesi (faragha) yenu inatunzwa, nitatibia vigogo na akina mama uani na chumbani. Nifafanue.
Vigogo wa kiume nawatibia uani na akina mama wawe vigogo au la natibia Guest House. Hili ni sharti nililopewa na God. Najua bila kutoa maelezo mtaanza kuguna na kuuliza kunani.
Kwa akina mama, kama una sura mbaya au ni mzee utatibiwa na vigogo uani. Kama ni kidosho, nimeagizwa nikutibie Guest House ili kuondoa nuksi. Nadhani naeleweka. Pia tiba hii lazima ifanyike usiku kizani ili shetani asiweze kukuona na kukuweka alama na kulipiza kisasi.
Sababu nyingine ya kutibia uani ni kuepuka wezi kuiba teknolojia yangu, pia kuhakikisha wadaku wa magazeti na runinga hawapati picha za vigogo wanaoumwa hasa Ukimwi na ufisadi na kuwaanika. Pia akina mama wazee hawaogopi kiza ni watu wazima.
Wanafunzi hasa wa vyuo vikuu wanaotaka kupata mikopo haraka na kushinda mitihani yao waje kwangu haraka. Wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wanaohofia mikataba yao au ukwepaji kodi wao kugunduliwa na kushitakiwa hata kufilisiwa njooni haraka.
Wale walioshindikana yaani ambao wanahisi hawawezi kuolewa au kuzaa waje haraka. Wanasiasa hawana haja ya kwenda Bwagamoyo kwa mambo ya uchaguzi. Waje kwangu watashinda hata kama hawana sifa. Chama kinachotishiwa kunyang'anywa ulaji kifanye haraka.
Sitaki niseme mengi. Nadhani mmeona ukweli wangu. Hivyo nategemea mtamiminika kwangu badala ya kwenda Loriyondo.
Wajinga ndio waliwao. Naona kinokia kinalonga. Huenda wameanza kujiingiza. Haloo profesa mtakatifu hapa!

h.sep3.gif
 
Yaani hawa serikali they claim our wealth without our consent!
Wananchi si washapinga hatutaki dowans tunulieni umeme wa jua au hata wa upepo au hata mawimbi ya bahari..
Dharura dharura tuko gizani miaka 20 sasa ndo wanatuletea zarura zao leo wanataka watupige changa la macho la mwisho wa awamu ndo waondoke?!
 
Mitambo ya Downs ilinunuliwa na CIP Send to a friend Wednesday, 16 March 2011 21:23

Sadick Mtulya
MITAMBO ya kuzalishia umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans, ilinunuliwa na Cyprus Independent Power Cooperation (CIP) kwa Dola za Kimarekani milioni 70 mwaka 2009, imefahamika.Habari hizo zinakuja wakati serikali ikiwa mbioni kurekebisha sheria ya manunuzi ya umma kwa kile kinachoelezwa ni mkakati wa kutaka kuinunua mitambo hiyo.

Mitambo hiyo ililetwa nchini baada ya Dowans kurithi mkataba wa Kampuni ya Richmond wa kuzalisha umeme wa kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wakati taifa lilipokumbwa na upungufu wa umeme mwaka 2006.

Hata hivyo baadaye ilishindwa kuondolewa nchini kufuatia hatua ya Tanesco kufungua shauri la pingamizi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ikidai mitambo hiyo kuwa ndiyo dhamana ya Dowans katika kesi ya msingi ya kudai fidia iliyotokana na hasara iliyoipata kutokana mkataba utata.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, katika shauri hilo Tanesco ilidai kama Dowans ingeshindwa kesi na kama isingekuwa na fedha za kulipa, mitambo hiyo ingefidia fedha hizo.

Hata hivyo kinachosubiriwa sasa ni kumalizika kwa taratibu za kimahakama katika kesi ya Dowans dhidi ya Tanesco iliyoko Mahakama Kuu ya Tanzania.Kwa mujibu wa habari, CPI imeilipa Dowans lakini, kampuni hiyo haitachukua fedha hiyo hadi itakapotimiza masharti makuu mawili.

Masharti hayo ni pamoja na mnunuzi wa mitambo hiyo kuitaka Dowans kuhakikisha kuwa mitambo hiyo inapata mkataba wa kuzalisha umeme nchini ambao si chini ya miezi sita, lakini ikishindwa hilo, ihakikishe kuwa imepakiwa ndani ya meli ili isafirishwe kutoka nchini ndipo iruhusu kuchukuliwa kwa fedha hizo.Juzi Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania, Stansalus Munai, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, hakukana wala kukubali.

Alisema "mitambo yetu haijakosa soko. Wanaihitaji wengi wa kuisafirisha nje ya nchi."Kwa mujibu wa Munai, kila siku wanapokea watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaotaka kununua mitambo hiyo."Wanakuja wengi kila siku wa ndani na nje, mazingira ya huko nyuma yalizuia tusiuze sasa hilo linaelekea kwisha," alisema.

Alipotakiwa kueleza kama watakuwa tayari kuiuza mitambo hiyo kwa serikali, Munai alisema hawatalazimisha biashara na serikali, lakini wakienda kwa nia ya kuinunua watawasikiliza."Hatutalazimisha biashara na serikali, hawajaja ila wakija tutawasikiliza. Tutawafikiria kama watu wengine, bei inategemea," alisema Munai.

Chini ya sheria ya mwaka 2004, inayotumika sasa, serikali hairuhusiwi kununua bidhaa au mitambo ambayo tayari imetumika.Lakini kama sheria hiyo ikirekebishwa, itatoa nafasi kwa serikali kununua mitambo iliyokwishatumika kama inayomilikiwa na Dowans.
Sheria ya sasa inayoizua serikali kutonunua bidhaa au vitu vilivyotumika ilitafsiriwa katika sheria ya manunuzi ya Benki ya Dunia (WB), inayolenga kuepuka mazingira ya ufisadi.Mwaka 2008 Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd ilitangaza zabuni ya kuuza mitambo yake ya kuzalisha umeme ikiwa ni miezi mitatu baada ya serikali kusitisha mkataba wake na (Tanesco).

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #1 Bakari 2011-03-17 03:45 Sarakasi zinaendelea, maswali yanazidi majibu:

1. TZ ikikubali kuingia mkataba wa kutumia mitambo hii, nani atakuwa anapokea malipo, Dowans au CPI?

2. Kama CPI ndio watapokea malipo, iweje Dowans iifanyie biashara; kwanini wameliki wa CPI wasije kufanya 'deal' wenyewe (au CPI pia inamilikiwa na Rostam aka Al-Hadaiwi)?

3. Al-Hadaiwi alikuja nchini kama nani ilhali mitambo ni mali ya kampuni nyingine?
 
Mradi wa Stiegler's Gorge wazinduliwa

na Mwandishi wetu

amka2.gif
WIZARA ya Nishati na Madini imezindua kamati ya kusimamia utelekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kutokana na maporomoko ya maji ya ndani ya bonde la Mto Rufiji.
Uzinduzi wa kamati hiyo inayoundwa na wataalamu kutoka wizara mbalimbali nchini ikiwemo Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ulifanywa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Jairo alisema mradi huo utakaosimamia mambo matano ukiwemo uzalishaji wa umeme wa megawati 6,000 na kwamba hatua hiyo ni mkakati wa kuiondoa nchi gizani.
Kwa mujibu wa Jairo, mradi huo utakaotekelezwa kwa awamu tatu utagharimu dola za Marekani bilioni tano na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitano.
Shughuli nyingine za mradi huo utakaoongozwa na Kamishna wa Nishati na Petroli, Mhandisi Bashir Mrindoko,
zitahusu kilimo cha umwagiliaji, usambazaji wa maji majumbani na viwandani, uvuvi na utalii.
Wajumbe ni mhandisi Theophillo Bakwea, Mhandisi Leonard Masanja na Joram Kengeta - wote kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Evodia Pangani wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Mhandisi Hamza Singano (Wizara ya Maji), Bonaventure Midala na John Mbwilizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wengine ni mhandisi Katinda Kamando wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhandisi Wenslaus Lambaleki (Wakala wa kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Mhandisi Lewanga Tesha (TANESCO) na Anastaz Mbawala wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).
Aliitaka kamati iliyoundwa kukutana mara moja kwa lengo la kuandaa hadidu za rejea kuhusu mradi huo na kusisitiza kuwa mradi huo utatekelezwa ipasavyo.
 
Zitto airarua serikali
• Abeza Rais kulalamikia matatizo badala ya kuyatatua

na Bakari Kimwanga

amka2.gif
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, ameitaka serikali ichukue maamuzi ya haraka ya kulinusuru taifa na tatizo la umeme nchini, kwani uzoefu unaonyesha ndiyo imekuwa ikichelewesha na wakati mwingine kukwamisha uwekezaji wa miradi mikubwa ambayo ingeweza kulipatia taifa umeme wa uhakika.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (CHADEMA), aliyasema hayo wakati akisoma ripoti ya mapendekezo ya kamati yake kuhusu tatizo la umeme, ambayo kwa kiasi kikubwa imeonyesha kuwa uzembe na urasimu ndani ya serikali umechangia kwa kiasi kikubwa taifa kukosa umeme wa uhakika na kujikuta likiingia gizani mara kwa mara.
Akisoma maazimio hayo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alilitaka Baraza la Mawaziri chini ya Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi ya haraka ili kukamilisha miradi ya umeme wa makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma, aliyosema ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha na wa uhakika.
Alisema wakiwa katika ziara ya siku tano ya kukagua mradi wa Liganga na Mchuchuma, walibaini kuwa ipo haja ya haraka kwa serikali kutimiza wajibu wake kufanikisha utekelezwaji wa haraka wa miradi hiyo na kwamba wanaunga mkono hatua zilizofanywa na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kwa kukamilisha hatua za kumpata mbia kutoka nchini China.
Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutaifanya nchi inufaike kwa kupata umeme wa Megawati 1500 KV ndani ya kipindi cha miaka mitano na kuendelea, ambao unaweza kuzalishwa kwa takriban miaka 150 kabla ya makaa ya mawe kwisha.
"Hatuwezi kuwa na taifa la walalamikaji kila mara…. rais, wabunge na wananchi wote sasa tumekuwa walalamikaji lakini muhimu ni kwa baraza la mawaziri kufanya uamuzi wa haraka ili kuinusuru nchi na tatizo la umeme.
"Hata kampuni tanzu itakayoundwa ili kuendesha miradi hii ifuate taratibu zote za uchimbaji ikiwamo kusainiwa kwa mkataba wa uendelezaji wa mgodi kwa madhumuni ya kulinda masilahi ya taifa na watu wa Ludewa," alisema Zitto.
Alisema NDC wameingia ubia na Kampuni ya Atomic Resources ya Australia na kuunda Kampuni tanzu ya TANCOAL Energy wilayani Mbinga kwa lengo la kuzalisha umeme wa megawati 450, ambapo shirika hilo litakuwa na hisa ya asilimia 30 na uwekezaji wake utakuwa ni dola za Marekani milioni 350.
"Mkataba wa ubia kati ya NDC na Kampuni ya Sichuan Honga kutoka nchini China ili kuendeleza mradi wa Mchuchuma na Liganga ni vema ukasainiwa haraka na serikali," alisisitiza Zitto.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema Wizara ya Nishati na Madini inatakiwa kuharakisha utoaji wa leseni ya uchimbaji wa makaa ya mawe kama ilivyokuwa imeombwa na Kampuni ya TANCOAL ambayo inamilikiwa kwa ubia na NDC ili uchimbaji huo uanze na umeme uzalishwe.
Kwamba, umefika wakati kwa TANESCO kuanza kuwekeza katika msongo wa kusafirisha umeme kuelekea kwenye miradi hii ili iwe ya maana, ikiwa ni pamoja na suala la msongo wa umeme kuwa chini ya TANESCO.
Akifafanua kuhusu mradi wa umeme wa makaa ya mawe wa Kiwira, alisema kamati yake inaunga mkono hatua ya mashirika ya umma kuwekeza katika sekta ya uzalishaji wa umeme na Shirika la Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF), kujitokeza kuendesha mgodi huo.
"Kamati yetu mwaka 2009 ilikwenda nchini Malaysia na kukuta mashirika ya mifuko ya hifadhi za jamii yamewekeza na kuzalisha umeme megawati 27,000 huku wakiwa na akiba ya megawati 12,000 ya umeme katika nchi yao, je, Tanzania tunasubiri nini?" alihoji Zitto.
Alisema kamati hiyo itakuwa na mkutano na wadau wa kujadili miradi ya umeme ambapo mkutano huo utawakutanisha NDC, STAMICO, TANESCO,NSSF na CHC pamoja na makatibu wakuu wa wizara na wenyeviti wa kamati za Bunge za Viwanda, Biashara, Nishati na Madini ili kujadiliana kwa pamoja na kupata njia mbadala zaidi.
Akijibu maswali, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe, alisema kamati yao imefuatilia na kubaini kuwa mchakato wa kurejesha umiliki wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira na kubaini kuwa mchakato huo bado haujakalimika kama ilivyokuwa imeelezwa awali.
 
Tanzania bila Dowans haiwezekani?
ban.nundu.jpg

Deus Bugaywa​

amka2.gif
DHARURA, dharura! Kuliokoa taifa lisiingie katika hali mbaya zaidi, hakuna jinsi ni lazima mtu fulani afanye maamuzi magumu mahali fulani ili taifa liweze kuokolewa na hatari ya kuingia gizani kabisa, ndiyo maana ni lazima bila kujali chochote au lolote lile uje mchana, uje usiku, lazima hatua zichukuliwe. Na kwa kweli zimeanza kuchukuliwa, Dowans.
Serikali sasa iko katika harakati kubwa za ‘kuliokoa' taifa lisitumbukie gizani, imeandaa muswada wa sheria ambao utategua sheria iliyopo ya manunuzi ya mwaka 2004, ambayo pamoja na mambo mengine inakataza serikali kununua mitambo, magari, au vipuri vilivyotumika (vikuukuu /mitumba).
Sheria hiyo inataka kupitishwa ili kuiwezesha serikali katika hali ya dharura iweze kununua vitu hivyo bila kulazimika kufungwa na sharti ka kununua vitu vipya, hasa kama ununuzi wa vitu hivyo vipya (kwa kutumia sheria ya sasa) unaweza kuchukua muda mrefu kiasi kwamba wakati vinapatikana madhara yatakuwa yametokea na havitakuwa na maana tena.
Bila shaka nia ya serikali kwa kuiangalia juu juu ni njema sana, tena ina madhumuni safi kabisa kwa ajili ya kuwatumikia watu wake, kwamba haitaki taifa liingie katika matatizo kwa sababu tu ya urasimu wa sheria ambazo tunazitunga wenyewe na ambazo ziko kwa ajili ya ustawi wetu.
Kwa msingi huo ni rahisi kabisa kujenga hoja kwamba, watu au taifa si kwa ajili ya sheria isipokuwa sheria ni kwa ajili ya watu. Kwamba sheria zimetungwa ili zitutumikie na sio sisi tuzitumikie, kwa hiyo ni lazima ziwepo kwa mujibu wa manufaa yake kwa watu hao.
Lakini pia katika mstari huo huo, ni vyema kujiuliza maswali muhimu na ya msingi. Moja likiwa ni, je, mgawo wa umeme bado tunaweza kuliita ni tatizo la dharura kwa taifa hili? Maana ya dharura ni nini kwa wataalamu na viongozi wa taifa hili linaloitwa Tanzania ?
Si kweli kwamba matatizo ya upungufu wa maji katika mabwawa yetu tunayoyategemea kwa umeme tumeyajua zaidi ya miaka kumi sasa? Na mgawo wa umeme si umekuwa ni sehemu yetu kwa zaidi ya miaka kumi? Tunaweza kweli kuwa na ujasiri wa kusema tatizo la mgao wa umeme ni la dharura kwa kiwango hicho mpaka tutafute visingizio vya kubadili sheria ili kukabili dharula hiyo yenye umri wa zaidi ya muongo mmoja?
Na hata kama ni dharura, kwa jicho la tafakuri, inaonekana kana kwamba Dowans ndiyo ‘Kikombe cha Babu wa Loliondo' kwa matatizo ya umeme ya taifa hili. Kwamba wataalamu wetu waliobobea, viongozi wa serikali na hata Bunge (kamati ya nishati na madini) uwezo wao wa kukabiliana na tatizo la umeme umeishia katika Dowans.
Kwamba kama taifa hatuwezi kufikiri namna ya kutatua matatizo yetu ya umeme isipokuwa kujiviringisha kwa Dowans tu, ni jambo ambalo si tu linasikitisha isipokuwa linatia mashaka pia kama taifa bado lina uwezo wa kitaalamu na kiuongozi kukabiliana na changamoto zinazolikabili.
Ndiyo, hivi pamoja na matatizo na tuhuma zinazoiandama Dowans, bado viongozi wetu wanazidi kubuni mbinu mpya na za kisasa kuhakikisha kwamba Dowans wanafaidika kwa namna na gharama yoyote ile na matatizo haya ya umeme yanayolikabili taifa.
Ni kama vile kuna watu wamekula kiapo kwamba, nikikopa maneno ya vijana wa siku hizi, ‘piga, ua, garagaza', ni lazima kampuni hii ifaidike kwa namna moja ama nyingine na tatizo hili la umeme.
Kwa taifa makini na viongozi waadilifu wanaoujua vyema wajibu wa dhamana zao kwa jamii wanayoingoza, Dowans isingekuwa mojawapo ya hoja zinazojadiliwa sasa kwa mtazamo huu, wa kutaka kufanya biashara tena na serikali.
Kanuni ya kawaida na nyepesi kabisa ya maadili yawataka viongozi wetu, bila kujali hali ikoje, lakini mradi tu kwamba kampuni hii inasikika kwa ukakasi masikioni kwa Watanzania, ilitosha kutoihusisha kabisa na mikakati yoyote ile ya serikali.
Imani ya wananchi kwa serikali yao ndiyo kitu cha msingi na muhimu ambacho serikali makini itakitazama kabla ya kufanya kitu chochote, serikali inayojali na kuheshimu wajibu wake kwa umma, haitataka kuingia katika mgongano usiokuwa na sababu na wananchi wake.
Tayari Dowans, kwa Watanzania imekuwa ni kampuni ambayo inatiliwa mashaka kwa kila namna, uhalali wake wa kurithi mkataba wa Richmond, uhalali wa uwepo wake Costa Rica inakodaiwa imesajiliwa, zaidi sana utata wa mtangulizi wake Richmond, phantom Company, kama ambavyo Rais Kikwete aliizungumzia wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya CCM.
Mashaka haya, iwe ya kweli au ya kutunga, yawe halisi au ya kufikirika, yalitosha sana kuifanya serikali isijihusishe tena na kampuni hii, achilia mbali kuthubutu kubadili sheria ili kupata mwanya wa kuweza kununua mitambo ya kampuni hiyo.
Kwa hatua hii serikali inatuma ujumbe mmoja tu kwa wananchi kwamba, Tanzania bila Dowans haiwezekani, njoo masika, njoo kiangazi. Bila kuwepo Dowans Tanzania labda ingeweza kushindikana kuzalisha umeme.
Mtu mzima unajiuliza, baada ya harakati zote hizi za kutaka kununua mitambo ya Dowans tutakuwa tumemaliza kabisa tatizo la umeme nchini? Wakati wa ile dharura ya mwaka 2006, iliyoleta Richmond, pamoja na hatua kuchukuliwa za haraka kukabiliana na dharula hiyo, lakini mpaka udharura unakwisha hakuna umeme uliokuwa umewaka badala yake ikawa ni dharula ya kutafuta dhahama hii ya Dowans tunayokumbana nayo sasa, Je, hatuwezi kujifunza kitu kutokana na hili.
Hata kama mabadiliko haya ya sheria ya manunuzi yana nia njema na nzuri kama tunayotaka kusadikishwa lakini, kwanini sasa hivi? Katika filamu ya Gold finger, moja ya filamu zake nyingi, James Bond ananukuliwa akisema "Once is happenstance, Twice is coincidence, the third time its enemy action", kwa ufupi anamaanisha jambo likitokea mara ya kwanza ni la kawaida, ya pili ni kama ajali, na mara ya tatu si bure kuna kitu.
Waswahili wanasema hakuna kitu kinatokea kwa sababu ya kutokea tu, hasa ukizingatia wakati jambo hilo linatukia, kila jambo linatokea si kwa nasibu tu, isipokuwa kunakuwa na sababu za msingi zinazolifanya litokee, ziwe zinajulikana au zimefichika, lakini kila jambo kama lilivyo na wakati wake lina sababu zake pia.
Mungu ibariki Tanzania
 
Tangu hili sakata lianze kama serikali ingekuwa na nia ya kulitatua TANESCO tayari wangekuwa na majenereta yao lakini kwa sababu Dowans ni ya JK na anataka kula mpunga wa walipa kodi basi ndio hivyo tena inasuasua. Watanzania tuamke na kuanza maandamano mapya ya kushinikiza TANESCO kupewa uwezo wa pesa zetu za kodi wanunue majenereta mapya na katika wiki mbili yawe yametua Dar Es Salaam tena yaletwe kwa ndege haraka inavyowezekana. JK kama hawezi hilo afurumushwe kutoka Magogoni. We are sick and tired of these losers ambao wamekulia msoga na akili zao zinaishia msoga.
 
'Tatizo CCM ni mafisadi, si kukosoa nje ya vikao'

Na John Daniel

VIONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wametakiwa kujifunza historia ya chama hicho kabla ya kuzungumza na kutambua kuwa kila
mwana CCM wakiwemo viongozi wastaafu au waliopo sasa wana haki ya kuhoji mwenendo wa chama hicho kwa kuwa huo ndio msingi uliojengwa na muasisi wa chama hicho, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Pia viongozi hao wa UVCCM wametakiwa kujihoji kwanza wao kama mali walizonazo ni halali ikilinganishwa na vipato vyao kabla ya kutoa maneno ya kejeli kwa viongozi waastafu na kutambua kuwa kama wamenunuliwa kutumikia kundi fulani, macho ya Watanzania yanayowatazama yatawahukumu hata kabla ya maneno.

Akizungumza na Majira kwa sharti la kutotajwa jina Dar es Salaam jana, kigogo mmoja wa CCM alisema suala la kujikosoa ni la msingi kwa viongozi waastaafu na waliopo na kwamba Mwalimu Nyerere alipoona badhi ya viongozi wanakwenda kinyume alionya hadharani na kutunga kitabu cha wajisahihishe.

"Ni jambo la kusikitisha na la ajabu sana kuona watu wanakataa katiba, kanuni na utaratibu wa chama, ni sawa na mkiristo kumkemea Mchungaji au padre pale anaposema uzinzi au uasherati ni dambi wakati biblia ndivyo inavyosema.

"Baba wa Taifa aliweka utaratibu wa kutuita mara kwa mara na kutuuliza mambo yanayoendelea kwa wananchi, alipoona baadhi ya watu wanaenda kinyume alitunga kitabu 'cha tujisahihihishe, hakujificha," alisema kiongozi huyo bila kutaka kutajwa jina ili kuepuka malumbano yanayoendelea.

"Inabidi hawa vijana wakajifunze kwanza historia ya chama, hawaijui. Kuonyana ni jambo la kawaida ndani ya CCM na mwazilishi wa utaratibu huo alikuwa Baba wa Taifa mwenyewe.

"Watu wanapewa fedha kununua mitambo ya umeme badala yake wanakodisha mtambo kwa gharama ya juu mara dufu kisha wenye uchungu na nchi hii watulie tu! Haiwezekani, ni kwa nini hao UVCCM wasikemee ufisadi kama wanataka ukweli?," alihoji.

Alisema chanzo cha malumbano yote yanayoendelea ndani ya CCM ni chama hicho kuwakumbatia watu waliochafuka na ufisadi badala ya kuwachukulia hatua ikiwemo kuwaondoa katika nafasi ndani ya chama hicho.

Alisema kwa mujibu wa historia ya chama hicho tangu enzi za TANU na baadaye CCM, kazi kubwa ya UVCCM ilikuwa ni kukishauri na si chombo cha kukiamulia chama mambo ya kufanya kama inavyofanyika sasa.

"Hao vijana wanatakiwa kujifunza sana, kazi za jumuiya hizi za chama ni kushauri na ushauri wenyewe si hadharani. Matusi wanayotoa kwa viongozi waadilifu wastaafu ndio sasa wanakimaliza chama chetu.

"Huu ndio mfumo mpya ulioanza sasa, ni hatari sana, ni utaratibu mpya ambao haukuwepo na unalenga kuimaliza CCM. Kama watu wanatakiwa wasisema ukweli maana yake ni kuwataka kuwadanganya Watanzania hawa wenye akili kuliko hao vijana, kamwe hatutakubali," alisisitiza.

Alisema mpango wa viongozi wanaofaidika na msimamo wa UVCCM kuwachukuliwa hatua wakosoaji wa chama katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya (NEC) mjini Dodoma mwenzi ujao ndio itakisambaratisha kabisa CCM.

"Kama watathubutu kufanya hivyo maana yake wanataka tuwadanganye Watanzania na hatutafanya hivyo. Sisi tunata wakemee ufisadi na si kutuhamisha kwenye ajenda ya msingi, haya yote chanzo chake ni ufisadi, kama wangeshughulikia mzizi huo haya yote yasingekuwepo," alisema kiongozi huyo.

Habari zilizoifikia Majira kutoka ndani ya CCM zilisema kuwa vikao vya Kamati Kuu (CC) na baadaye NEC vinavyotarajiwa kufanyika Dodoma mwezi ujao vitawaka moto baada ya kundi linaloaminika kuwaunga mkono UVCCM kutaka vigogo wote waliohusika katika kukosoa CCM hadharani wachukuliwe hatua kali.

"Kama viongozi waliohusika katika malumbano wakati wa awamu ya kwanza ya Rais Kikwete hawakuchukuliwa hatua unategemea nini kama si kuendeleza tabia hiyo ya kusemasema nje ya vikao?

Subiri Kamati Kuu na NEC mwezi ujao utaona, watafukuzwa wote waende wanakotaka, baada ya hapo chama kitatulia, maana kuanzia hapo kila mtu ataogopa," kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Hata hivyo uwezekano wa kuchukua hatua hiyo dhidi ya watu hao ni mdogo kwa kuwa hatua kama hiyo inaweza kukiwepa pabaya zaidi CCM katika uchaguzi Mkuu ujao.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema njia pekee inayoweza kuchukuliwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, ni kukemea watu wanaokwenda kinyume na maadili na miiko ya uongozi na kufumua uongozi wa chama hicho ili kukijenga upya pamoja na kuvunja makundi yote ya urais mwaka 2015, bila kuwaonea haya wenye tuhuma za ufisadi.

Vigogo wanaotajwa kukosoa CCM hadharani bila kuogopa ni mawaziri wakuu wastafu, Jaji Joseph Warioba, Bw. Frederick Sumaye, Bw. Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Spika wa Bunge sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samwel Sitta.

Hivi karibuni viongozi wa UVCCM walinukuliwa wakiwashambuliwa viongozi hao bila kuwataja majina, huku wakiwahusisha baadhi yao na mpango wa kusaka urais mwaka 2015, hatua ambayo imeibua malumbano na watu wa mada mbalimbali kujitokeza kuwatetea, na baadhi yao kujitetea.

5 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... DU mimi naiogopa ccm, namna inavyo endelea hebu tuone kama tutufika na vile mi naona upinzani ungekua makini ungeweza kutwaha hatamu kwani kule zanzibar washaipunguza makali
March 29, 2011 2:07 AM
blank.gif

Anonymous said... CCM kama inataka kuwa mahali salama inatakiwa ihakikishe kuwa ufisadi unakemewa kama baadhi ya viongozi wanavyofanya na kama hawa viongozi wanaokemea ufisadi wataonekana hawafai ndani ya CCM ujue hilo ndiyo litakuwa anguko la chama cha mapinduzi, hivi kwa sasa nani ataweza kukiokoa chama cha mapinduzi mafisadi wapo kila pande ya chama na serikali,ccm iwatimmue wote mafisadi ndiyo itakuwa salama lakini nani anaweza kufanya hayo? tusubiri kikao cha mwezi ujao tuone.
March 29, 2011 3:08 AM
maisha dunia ngumu said... TATIZO LA UVCCM NI UDUNI WA ELIMU DUNIA, HATA UKIONA MANENO WANAYOSEMA NIKAMA VILE MTU HAJAENDA SHULE!NAKAMA WALIMALIZA SHULE BASI WALIMALIZA KWA KUDRA YA MWENYEZI MUNGU MWENYE REHEMA ZOTE.
KINACHO NISHANGAZA ZAIDI NI KWA NINI MWENYEKITI WA CCM AMEKAA KIMYA NA KURUHUSU HAYA MAJIBIZANO YAKIENDELEA? BILA SHAKA SASA TUNAWEZA KUONA UDHAIFU WA HUYU MWENYEKETI WA TAIFA WA CCM.
March 29, 2011 6:41 AM
blank.gif

Anonymous said... yetu macho,tuone km kuna mwenye kumfunga paka kengele
March 29, 2011 6:43 AM
maisha dunia ngumu said... BARUA YA WAZI KWA WANA-CCM.
Hivi haya maneno na malumbambano ya kila siku hamuoni kuwa badala ya kujenga chama chenu mnakibomoa chama hiki kikongwe? Hivi mwenyekiti wa chama hiki mheshimiwa J.kikwete yuko wapi? hivi kweli anafurahia hali hii ya malumbano yasiyo na tija? hivi mzee makamba kwa hekima ya uzee wake anaona busara kupayuka kila siku kwa mambo yale yale? Sumaye akisema kitu wanamjibu, lakini chadema wakirusha dongo la CCM wanakaa kimya kiasi kwamba wananchi wanafikiri ni kweli yale chadema wanayosema ni kweli! mbona kama katibu wa chama hujibu mapigo ya chadema? mie naona mzee makamba husitahili cheo hicho!ni muda wako mzuri wa kujiuzuru nafasi hii, hapo ulipofikisha chama inatosha!!! unajenge uswahili sana katika chama na sasa umemuambukiza mwenyeketi wa CCM mh. J kikwete uswahili huo.
Ebu tukumbushane kama siyo mageuzi haya batiri ndani ya CCM ya sasa,enzi ya uwenyekiti wa baba wa taifa hali hii ya kutukanana kada wa CCM kwa kada wa CCM ingeweza kutokea? kwa mtazamo wangu chama cha CCM kimekosa mvuto tena na jinsi kinavyoendeshwa ni ibilisi tu ndiye anayejuwa chama kinatumia dira gani! NINI KINAFANYA KIKWETE KUKAA KIMYA??? bila shaka anahusika na kile kinachoendelea sasa hivi ndani ya chama chake, vinginevyo kikwete ameshindwa kuongoza chama ni bora aachie ngazi kama mwalimu nyerere alivyoachia ili chama hiki kirudiwe na hadhi na heshima kama ilivyokuwa mwanzo.
March 29, 2011 6:44 AM

Post a Comment
 
Deni TANESCO laishtua Kamati ya Bunge

Na Tumaini Makene

DENI linalokadiriwa kuwa kati ya sh. bilioni 67 na 96 linaloonekana kulielemea Shirika la Umeme nchini (TANESCO) umeishtua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mahesabu ya
Mashirika ya Umma (POAC) na kulazimika kuiita wizara za Nishati na Madini pamoja na Fedha na Uchumi, kujadili kwa kina suala hilo.

Habari hizo zimekuja wakati ambapo Kwa muda mrefu sasa imekuwa ikidaiwa kuwa shirika hilo limeelemewa na mzigo mkubwa wa madeni, unaoliweka katika hali mbaya kiuchumi kiasi cha kushindwa kukopesheka, huku mapato yake kwa mwezi yakiwa hayaendi sambamba na gharama kubwa za uendeshaji wa shughuli zake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Bw. Murtaza Mwangunga alisema kuwa wajumbe wa POAC walishindwa kupitisha hesabu za TANESCO mpaka watakapopata maelezo ya kina juu ya deni hilo kutoka wizara hizo mbili.

"Wizara hizo mbili yaani ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Fedha na Uchumi zitakuja hapa, tumeagiza watendaji wake, makatibu wakuu wa wizara hizo waje hapa siku ya Jumatano, ili tujadili kwa kina sababu ya tatizo hilo," alisema Bw. Mwangunga.

Akizungumza kwa tahadhari akisema kuwa hataki kuiingia kwa kina katika suala hilo, kiasi cha kuathiri kanuni za bunge, alisema kuwa inaonekana hakuna taarifa za kutosha, hasa uhusiano kati ya taarifa za wizara hizo mbili na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"...hata TANESCO wenyewe wako puzzled (wanashangaa) hawajui nature ya madeni haya yanayokadiriwa kuwa kati ya sixty seven bilion hadi ninety six bilion shillings, wameshindwa kuyatolea maamuzi," alisema Bw. Mwangunga, akisisitiza hawezi kusema masuala mengi kwa kina mpaka watakapoweza kusikiliza pande zote husika.

Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imetangaza 'hali ya hatari' ikisema kuwa haitaachia uozo unaoendelea katika halmashauri za wilaya hasa katika ufisadi wa fedha za serikali, ambapo zimekuwa zikitumika vibaya katika matumizi 'feki'.

Akitangaza hilo jana mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa LAAC, Bw. Agustine Mrema alisema "ama zao ama zetu...haponi mtu hapa", akisema kuwa kamati hiyo imemwagiza CAG kufanya ukaguzi maalumu kwa baadhi ya halmashauri za wilaya zilizoonekana kutapanya fedha katika maeneo kama vile manunuzi na mishahara hewa.

Alisema kuwa katika wilaya takribani kumi pekee ambazo zimeitwa na kamati hiyo, Rorya, Kilosa, Morogoro, Rungwe, Mbeya, Sumbawanga, Msoma Vijijini, Tarime na Kisarawe, kumegundulika upotevu wa sh. milioni 792 katika mwaka mmoja wa fedha 2008/209, kwa kuwalipa wafanyakazi ambao hawapo.

"Tulichokiona ni kuwa kuna uozo mkubwa ndani ya halmashauri, hasa katika suala la mishahara hewa, fedha za serikali zinatumika kulipa watu waliokwisha kufa, watoro ambao hawako kazini, wengine walikwisha fukuzwa siku nyingi, hili ni jambo linalotisha.

"Mambo haya si kwamba hayafahamiki, yanafahamika sana, wapo watu wanahosika kuidhinisha malipo hayo, kwa mfano Wilaya ya Morogoro wametumia sh. milioni 19.4 katika mishahara hewa...Serengeti milioni 39.4, Tarime milioni 89.1, Kilosa 84.1," alisema Bw. Mrema.

Alisema kuwa wameagiza uchunguzi maalumu wa CAG ufanyike, kisha taarifa zitolewe kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili wahusika wachukuiwe hatua za kisheria, ikiwemo kutiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani.
 
Serikali yatangaza kiama kwa mafisadi Send to a friend Monday, 28 March 2011 21:35

Ramadhan Semtawa
KATIKA kile kinachooonekana ni kusikia kelele za umma, serikali inatarajia kupeleka muswada bungeni wa mabadiliko ya sheria mbalimbali, licha ya mambo mengine kosa la rushwa litakuwa ni uhujumu uchumi.
Siku za karibuni nchi imejikuta ikitiswa na vitendo vya rushwa kubwa, ikiwamo mikataba ya kampuni za Richmond na Dowans, huku wananchi wakitaka hatua zaidi kubana watuhumiwa.

Hata hivyo, katika hatua inayoonyesha serikali kusikia matakwa hayo ya umma jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, aliwasilisha muswada huo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali 14, mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala.

Katika mapendekezo hayo yaliwasilishwa mbele ya kamati hiyo na wadau kwa ajili ya kupata maoni, Werema alisema wameamua kufanya hivyo baada ya kung'amua rushwa ni tatizo.Werema alifafanua kwamba, mabadiliko hayo yamo kwenye sehemu ya saba katika Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi sura ya 200.

Alisema mapendekezo hayo ya marekebisho yanatoa pia mamlaka kwa mahakama za hakimu mkazi kupokea kesi za uhujumu uchumi.

Aliongeza kuwa kama muswada huo utakubalika, mahakama hizo sasa zitakuwa na mamlaka ya kupokea na kusikiliza kesi hizo, tofauti na sasa ambako husikilizwa na mahakama kuu pekee.

"Sehemu ya saba ya marekebisho katika Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi, sura ya 200. Sehemu hii inapendekeza marekebisho katika kifungu cha 29 ili kuzipa mahakama za hakimu mkazi kuwa na uwezo wa kupokea na kusikiliza kesi za uhujumu uchumi," alisisitiza Werema na kuongeza:
"Makosa ya rushwa sasa yanafanywa kuwa ni miongoni mwa makosa ya uhujumu uchumi."
Katika hatua nyingine, muswada huo pia unatarajia kuongeza adhabu kwa watu wanaokutwa na makosa ya uchawi, ikiwamo kutozwa faini ya Sh1 milioni na kifungo jela.

Pia, Werema alisema sehemu ya muswada huo, umeweka kipengele cha marekebisho kwenye kifungu cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16, yanayolenga kutoa adhabu mahsusi kwa mtu mwenye umri wa miaka chini ya 18 anayetuhumiwa kubaka.

Muswada huo wa serikali ambao umegusa sekta mbalimbali, umeweka bayana kwamba kifungu cha 192, kinapendekeza marekebisho ili kuipa mahakama kuu uwezo wa kusikiliza awali, mashauri ya jinai pale ambako mshtakiwa atakuwa amekana shtaka dhidi yake kama ilivyo kwa mahakama ya wilaya.

Akichangia maoni yake, Mbunge wa Singida Kusini, Tundu Lisu, alionyesha wasiwasi kama kuna umuhimu kwa sasa kuweka sheria ya uchawi wakati ilitajwa kwenye Tume ya Jaji Nyalali miaka 20 iliyopita kama sheria mbaya.

Tundu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alionyesha shaka pia kipengele cha sheria ya uchawi, akisema kitakuwa na madhara makubwa, kwani kitamnyima haki mtuhumiwa ya kujieleza na kujikuta akitupwa jela na kulipa faini.
 
tatizo la ****** ajui biashara ata kuiba kwa kutumia akili ajui kazikuta mali anaparamia.anataka kuchukua vyote kwa pupa. kuna miradi mingi sana pamoja na biashara anazomiliki ****** bila kujificha, ni kwa sababu anahasili ya biashara na kushika pesa ndiyo maana anakurupuka vibaya na mdomo kimya. muda umekwisha ccm na ****** out
 
Mbivu, mbichi Dowans kujulikana leo Send to a friend Wednesday, 30 March 2011 11:20

mangungu-murtaza.jpg
Murtaza Mangungu

Mwandishi Wetu
MBIVU au mbichi kuhusu malipo ya Dowans zitajulikana leo wakati kamati Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), itakapowahoji makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha, Uchumi na Nishati na Madini ili kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

Mbali na watendaji wakuu wa wizara, kamati hiyo pia itawahoji watendaji wa Tanesco kuhusu sakata hilo.

Suala la malipo ya deni la Dowans limesababisha mjadala mkubwa kwa kipindi kirefu sasa huku wanasiasa na viongozi mbalimbali wakipinga Dowans kulipwa mabilioni ya shilingi na wengine wakitaka ilipwe haraka.

Tangu Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), iiamuru Tanesco kuilipa Kampuni ya Dowans, suala la malipo kwa kampuni hiyo limezua utata kutokana na viongozi pamoja na Tanesco kushindwa kutoa ufafanuzi unaoeleweka juu ya deni hilo.

Juzi POAC ilishindwa kuthibitisha deni la zaidi ya Sh96 bilioni la Tanesco ambalo wameiomba serikali kuwasaidia kulipa kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu akizungumza na waandishi wa habari alisema kutokana na hali hiyo kamati hiyo imewataka Makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco watoe ufafanuzi juu ya kuwapo kwa deni hilo kubwa.

"Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili, na kwamba tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa maamuzi ya kulipwa au la,"alisema Mangungu.

Comments

+1 #2 Bulugu 2011-03-30 11:35 Hapa naona tunazinguana tu, serikali iliingia mkataba na kampuni ya RICHMOND ambayo baadae serikali hiyi hiyo ikaja kutuambia kwamba ni kampuni hewa. DOWANS waliingia mkataba na RICHMOND waende wakamdai, sasa sisi Watanzania tunahusika vipi na deni????????????
Quote

+2 #1 CAROLINE 2011-03-30 11:26 WATANZANIA TULISHAFUNGA MJADALA HUU KUWA HAKUNA KUWALIPA DOWANS NA SEREKALI IKILIPA IONDOKE YENYEWE MADARAKANI WALA ISINGIJE BAKORA.
Quote
 
Kamati ya Bunge yaitwisha Serikali mzigo wa Dowans Send to a friend Wednesday, 30 March 2011 21:29

Patricia Kimelemeta
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imeibebesha Serikali mzigo wa deni la kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikisema ndiyo iliyohusika na mkataba wake. Serikali imekuwa ikidai kwamba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), ndilo linalopaswa kulipa deni hilo.Agizo hilo la POAC lilitolewa jana katika kikao cha pamoja baina ya Kamati hiyo na makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi na Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco.

Juzi, Kamati hiyo ilishindwa kuthibitisha deni hilo la zaidi ya Sh96 bilioni kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake na nani anastahili kuilipa kati ya Serikali na Tanesco.Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha juzi zililidokeza gazeti hili kuwa tangu kutolewa kwa hukumu iliyotaka Dowans ilipwe fidia kutokana na mkataba wake wa kuzalisha umeme kuvunjwa kiholela, Serikali na Tanesco wamekuwa wakitupiana mpira wa nani anayepaswa kulipa deni hilo.

"Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili na tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa uamuzi," aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu, aliwaambia waandishi wa habari.

Baada ya mahojiano ya muda baina ya viongozi hao wa Serikali na Tanesco, Kamati hiyo iliitaka Serikali kuilipa Dowans ikiwa mahakama itatoa hukumu ya deni hilo kulipwa.Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema jana kuwa kwa mujibu wa vitabu vilivyotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), deni la Dowans lilitakiwa kuingizwa kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco.

"... Kwa sababu wao (Serikali) ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo (Dowans) ya kuwalipa gharama za ununuzi wa umeme," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema). Zitto alisema Serikali ilipinga suala hilo na Katibu Mkuu (Hazina) alimwandikia CAG, Februari 9, mwaka huu kuwa Tanesco inapaswa kulipa deni hilo. Tanesco nayo iliandika barua ya kupinga kulipa deni hilo jambo ambalo lilisababisha CAG kukataa kusaini vitabu hivyo.

"Ripoti ya CAG iliyotolewa kwenye kamati hii imeonyesha kuwa deni hili linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco kwa sababu wao (Serikali), ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Hivyo deni lake halipaswi kulipwa na Tanesco. Utata huo ulimfanya CAG aombe mwongozo," alieleza Zitto jana.

Kwa mujibu wa Zitto, baada ya malumbano hayo, POAC iliomba kukutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi; na Nishati na Madini ili wajadili suala hilo na kufikia muafaka."Muafaka ni kuwa deni hilo linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali hivyo wao ndiyo wenye jukumu la kulipa deni hilo ikiwa mahakama itatoa hukumu ya kulipwa," alisema Zitto.

Alisema Tanesco haiwezi kulipa deni hilo kwa sababu wao siyo walioingia mkataba na Dowans... "Tanesco haiwezi kubebeshwa mzigo usiowahusu, badala yake Serikali itawajibika yenyewe katika suala hilo ikiwa hukumu yake itatoka."Zitto alisema Tanesco linajiendesha kwa hasara kila mwaka na hiyo inatokana na wadaiwa kushindwa kulipa madeni yao ipasavyo, hivyo kulibebesha mzigo wa kulipa deni kubwa kama la Dowans ni sawa na kulifilisi au kuliua kabisa.

"Mwaka jana, Tanesco lilipata hasara ya Sh5 bilioni. Hii inatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya wadaiwa wao kushindwa kulipa madeni yao. Jambo hilo limesababisha shirika lijiendeshe kwa hasara na kutokana na hali hiyo, hawawezi kubebeshwa mzigo huo wa Dowans," aliongeza.

Sakata la malipo kwa kampuni ya Dowans limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii hasa ya wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali baadhi yao kupinga na wengine kukubaliana nayo.

Mjadala ulipamba moto baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kueleza kuwa Serikali haina pingamizi na malipo hayo na kwamba tayari imewaagiza wahusika kutekeleza mara moja.

Kauli hiyo ya Werema na ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kuunga mkono malipo hayo ziliwafanya wanaharakati wa haki za binadamu kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.

Last Updated on Wednesday, 30 March 2011 21:30 Comments

0 #6 mtu kwao 2011-03-31 05:33 wizi mtupu hii Dowans kila siku danadana sijui itaisha lini serilkali iliyopo si ijiuzuluuuuuuuu uuu?!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!!
Quote

0 #5 Bakari 2011-03-31 05:31 Chadema mmekuwa mkidai mitambo inafaa kutaifishwa, haya ya kulipa Dowans yanatoka wapi?

Nilitegemea Zito usimamie msimamo wa chama chako au wewe uko CCM?
Quote

0 #4 ay 2011-03-31 05:26 Haijuzu hata kidogo kuita deni hilo feki au kuwa mmiliki wa Dowas hajulikani. Vipi hajulikani na huku mkataba uli[NENO BAYA] sahihi baina ya Serikali na mmiliki wa mitambo hiyo Al Adawi na mitambo ikaletwa na ikawashwa, umeme ukazalishwa na ingali ipo na baadae mkataba ukavunjwa na kila kitu kilichukuwemo ndani ya mkataba kinajulika na leo hii mnasema deni hilo lisilipwe. Deni hilo limehalalishwa na wapatanishaji wa mataifa na kutakiwa serikali ilipe au na uamuzi huo wa kitaifa vilevile feki? Jee yupo mwenye ubavu wa kuukanya uamuzi huo? Jee mikataba haiheshimiwi?
Quote

0 #3 mwamba 2011-03-31 03:05 HILO DENI HALIELEWEKI HATA KAMA WATATAFUTA VITABU HAVITAPATIKANA KWANI NYARAKA ZA KAGODA ZIKO WAPI..SERIKALI INAJUA KILA KITU ISITAKE KUTUONA SISI NI [NENO BAYA] KIASI HICHO.HILO SIYO DENI LA TAIFA NI LA CCM NA KIKWETE WALIPE WENYEWE NA MAFISADI WENZAO.
Quote

0 #2 Burton Jorde 2011-03-31 02:15 Najua hapa ndio wananchi tutaamka kupinga kuwa hatuna imani na serikali iliyopo madarakani kwa serikali kulipa deni hili.
Quote

0 #1 ALOYCE DONATH 2011-03-31 02:03 hii ni ya majuha na kiongozi wetu ni mfalme juha,
Quote

Refresh comments list
 
Kamati ya Bunge yaitwisha Serikali mzigo wa Dowans Send to a friend Wednesday, 30 March 2011 21:29

Patricia Kimelemeta
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imeibebesha Serikali mzigo wa deni la kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikisema ndiyo iliyohusika na mkataba wake. Serikali imekuwa ikidai kwamba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), ndilo linalopaswa kulipa deni hilo.Agizo hilo la POAC lilitolewa jana katika kikao cha pamoja baina ya Kamati hiyo na makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi na Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco.

Juzi, Kamati hiyo ilishindwa kuthibitisha deni hilo la zaidi ya Sh96 bilioni kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake na nani anastahili kuilipa kati ya Serikali na Tanesco.Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha juzi zililidokeza gazeti hili kuwa tangu kutolewa kwa hukumu iliyotaka Dowans ilipwe fidia kutokana na mkataba wake wa kuzalisha umeme kuvunjwa kiholela, Serikali na Tanesco wamekuwa wakitupiana mpira wa nani anayepaswa kulipa deni hilo.

“Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili na tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa uamuzi,” aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu, aliwaambia waandishi wa habari.

Baada ya mahojiano ya muda baina ya viongozi hao wa Serikali na Tanesco, Kamati hiyo iliitaka Serikali kuilipa Dowans ikiwa mahakama itatoa hukumu ya deni hilo kulipwa.Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema jana kuwa kwa mujibu wa vitabu vilivyotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), deni la Dowans lilitakiwa kuingizwa kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco.

"... Kwa sababu wao (Serikali) ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo (Dowans) ya kuwalipa gharama za ununuzi wa umeme," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema). Zitto alisema Serikali ilipinga suala hilo na Katibu Mkuu (Hazina) alimwandikia CAG, Februari 9, mwaka huu kuwa Tanesco inapaswa kulipa deni hilo. Tanesco nayo iliandika barua ya kupinga kulipa deni hilo jambo ambalo lilisababisha CAG kukataa kusaini vitabu hivyo.

"Ripoti ya CAG iliyotolewa kwenye kamati hii imeonyesha kuwa deni hili linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco kwa sababu wao (Serikali), ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Hivyo deni lake halipaswi kulipwa na Tanesco. Utata huo ulimfanya CAG aombe mwongozo," alieleza Zitto jana.

Kwa mujibu wa Zitto, baada ya malumbano hayo, POAC iliomba kukutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi; na Nishati na Madini ili wajadili suala hilo na kufikia muafaka."Muafaka ni kuwa deni hilo linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali hivyo wao ndiyo wenye jukumu la kulipa deni hilo ikiwa mahakama itatoa hukumu ya kulipwa," alisema Zitto.

Alisema Tanesco haiwezi kulipa deni hilo kwa sababu wao siyo walioingia mkataba na Dowans... "Tanesco haiwezi kubebeshwa mzigo usiowahusu, badala yake Serikali itawajibika yenyewe katika suala hilo ikiwa hukumu yake itatoka."Zitto alisema Tanesco linajiendesha kwa hasara kila mwaka na hiyo inatokana na wadaiwa kushindwa kulipa madeni yao ipasavyo, hivyo kulibebesha mzigo wa kulipa deni kubwa kama la Dowans ni sawa na kulifilisi au kuliua kabisa.

"Mwaka jana, Tanesco lilipata hasara ya Sh5 bilioni. Hii inatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya wadaiwa wao kushindwa kulipa madeni yao. Jambo hilo limesababisha shirika lijiendeshe kwa hasara na kutokana na hali hiyo, hawawezi kubebeshwa mzigo huo wa Dowans," aliongeza.

Sakata la malipo kwa kampuni ya Dowans limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii hasa ya wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali baadhi yao kupinga na wengine kukubaliana nayo.

Mjadala ulipamba moto baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kueleza kuwa Serikali haina pingamizi na malipo hayo na kwamba tayari imewaagiza wahusika kutekeleza mara moja.

Kauli hiyo ya Werema na ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kuunga mkono malipo hayo ziliwafanya wanaharakati wa haki za binadamu kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.

Last Updated on Wednesday, 30 March 2011 21:30 Comments

0 #6 mtu kwao 2011-03-31 05:33 wizi mtupu hii Dowans kila siku danadana sijui itaisha lini serilkali iliyopo si ijiuzuluuuuuuuu uuu?!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!!
Quote

0 #5 Bakari 2011-03-31 05:31 Chadema mmekuwa mkidai mitambo inafaa kutaifishwa, haya ya kulipa Dowans yanatoka wapi?

Nilitegemea Zito usimamie msimamo wa chama chako au wewe uko CCM?
Quote

0 #4 ay 2011-03-31 05:26 Haijuzu hata kidogo kuita deni hilo feki au kuwa mmiliki wa Dowas hajulikani. Vipi hajulikani na huku mkataba uli[NENO BAYA] sahihi baina ya Serikali na mmiliki wa mitambo hiyo Al Adawi na mitambo ikaletwa na ikawashwa, umeme ukazalishwa na ingali ipo na baadae mkataba ukavunjwa na kila kitu kilichukuwemo ndani ya mkataba kinajulika na leo hii mnasema deni hilo lisilipwe. Deni hilo limehalalishwa na wapatanishaji wa mataifa na kutakiwa serikali ilipe au na uamuzi huo wa kitaifa vilevile feki? Jee yupo mwenye ubavu wa kuukanya uamuzi huo? Jee mikataba haiheshimiwi?
Quote

0 #3 mwamba 2011-03-31 03:05 HILO DENI HALIELEWEKI HATA KAMA WATATAFUTA VITABU HAVITAPATIKANA KWANI NYARAKA ZA KAGODA ZIKO WAPI..SERIKALI INAJUA KILA KITU ISITAKE KUTUONA SISI NI [NENO BAYA] KIASI HICHO.HILO SIYO DENI LA TAIFA NI LA CCM NA KIKWETE WALIPE WENYEWE NA MAFISADI WENZAO.
Quote

0 #2 Burton Jorde 2011-03-31 02:15 Najua hapa ndio wananchi tutaamka kupinga kuwa hatuna imani na serikali iliyopo madarakani kwa serikali kulipa deni hili.
Quote

0 #1 ALOYCE DONATH 2011-03-31 02:03 hii ni ya majuha na kiongozi wetu ni mfalme juha,
Quote

Refresh comments list
 
Dowans yawawekea pingamizi wanaoipinga mahakamani

na Happiness Katabazi

amka2.gif
HATIMAYE Kampuni ya Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Ltd, zimeweka pingamizi dhidi ya Shirika la Umeme (TANESCO), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) (LHRC) na mwandishi wa habari mwandamizi, Timoth Kahoho, katika kesi yake ya kuomba tuzo waliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) isajiliwe na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Kesi hiyo ambayo jana ilitajwa mbele ya Jaji Emilian Mushi katika Mahakama Kuu, wakili wa mlalamikaji (Dowans), Keneddy Fungamtama, aliiambia mahakama kuwa tayari ameshawasilisha mapingamizi matatu kwa pande zote tatu katika kesi hiyo, ambazo ni TANESCO inayotetewa na Dk. Evi Sinare, Dk. Angelo Mapunda, Alex Nguruma, Profesa Paramaganda Kabudi na Lugano Mwandamba, LHRC na Dk. Sengondo Mvungi na Harold Sungusia na Kahoho ambaye anajiwakilisha binafsi. Wote watatu wanapinga tuzo ya Dowans isisajiliwe.
Jaji Mushi alisema anaitaka TANESCO ijibu pingamizi lililowekwa kwake na Dowans Mei 27, LHRC na Kahoho nao wajibu mapingamizi waliyowekewa na Dowans Mei 20, mwaka huu, na kwamba majibu yote hayo yajibiwe kwa njia ya maandishi na aliiahirisha kesi hiyo hadi Julai 28, mwaka huu, ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
"Kama nilivyoamuru hapo juu kwamba katika tarehe hizo basi pande zote ziwe zimejibu mapingamizi ya Dowans kwa njia ya maandishi na ninaiahirisha kesi hii hadi Julai 28 mwaka huu ambapo kesi itakuja kwa ajili ya kutajwa…..lakini hata hivyo ninayo furaha kuona ndugu zangu wa vyombo vya habari wamepunguza kasi ya kuiandika kwa mitizamo wanayoijua tuzo ya Dowans," alisema Jaji Mushi na kusababisha jopo la mawakili zaidi ya kumi kuangua vicheko mahakamani hapo.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilitajwa mbele ya Jaji Mushi Mei 2, mwaka huu, ambaye alitoa siku 21 kwa pande zote kuhakikisha zinakabidhiana nyaraka zote zinazohusu kesi hiyo ambayo hadi kufikia jana ilikuwa imetekelezwa na pande zote katika kesi hiyo.
 
‘TANESCO iondolewe ukiritimba'

na Angelica Sullusi, Mbeya

amka2.gif
SERIKALI imeshauriwa kuruhusu mashirika mengine yanayojihusisha na ufuaji wa umeme kwa ajili ya kuleta ushindani wa kibiashara ili kuwanusuru Watanzania kuondokana na ukiritimba uliokithiri wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Ushauri huo ulitolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Kanisa la Reedemed Assembles of God (RAGT) lililoko mjini Tunduma, Obeid Sichembe, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Askofu Sichembe alisema TANESCO ina uwezo mdogo wa kuhimili kugawa umeme kwa wananchi ndio maana hadi sasa wameshindwa kuyafikia hata maeneo ambayo kimsingi yalipaswa kupata umeme haraka ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo.
"Hali hii ya kukatikakatika kwa umeme inaathiri sana maendeleo ya wananchi kwa kuwa kazi nyingi zinahitaji matumizi ya umeme.
"Ifike wakati serikali yetu ilione hili na iruhusu mashirika kama haya yashindane kibiashara ili kuboresha hali nzuri ya upatikanaji wa nishati ya umeme nchini tena kwa gharama nafuu," alisema.
 
Back
Top Bottom