Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Wale watakaopenda kumuona dr slaa live itv ambao wako nje ya nchi, mnaweza kuangalia kwenye tv4africa. nenda www.tv4africa.com then download player na ukishafanya hivyo lipia ada kidogo ya kama euro 5.58 na utapat aaccess code valid for a full month, jamaa yangu aliyepo us ananiambia hivi sasa anacheck kipindi cha watoto cha itv, so it is working perfectly lol
 
atumie nafasi hii kuwaelimisha Watanzania haki yao ya kupiga kura na umuhimu wa kujitokeza siku hiyo ya 31 oct, pia ajaribu kisisitiza amani na upendo kwa wana Chadema wote
 
Ushauri kwa Dr Slaa

Go to the point!!! Hakuna haja ya makombora, Dr Slaa anakubalika tayari na hana haja ya kutafuta zaidi, he just need to make a case kwa Watanzania, more importantly kuwaconvince independent voters kwa nini yeye anafaa kuwa raisi wa JMT.

Asikubalika kuyumbishwa na maswali ya uchokozi, ambayo yatamfanya atoke nje ya mstari na kupoteza composure yake. Kuna viswali chokozi vitaulizwa kumpima kama atahamaki na kukurupuka na kupoteza utu wake, please Dr Slaa uwe macho na maswali hayo na jaribu kuyajibu kwa uwazi na ukweli. Tafakari swali kabla ya kutoa jibu!! Kumbuka wanataka kujustify the only life line waliyobaki nayo dhidi yako kuwa "unakarupuka"!!

Jaribu kujibu kila swali utakaloulizwa, usiache au kukwepa swali, na check na muuliza swali kama atakuwa ameridhika na jibu lako.

Toa mifano na sometimes tumia parrables, na ikibidi uchekeshe wahudhuriaji. Ninachotaka hapa ni kuwaonyesha watanzania kuwa uko bold lakini pia kuna time you can be social. kucheka, funny etc

Epuka mitego ya udini ukabila na personal life. Kumbuka wewe ni mkatoliki na ni vyema ukasimamia imani yako lakini bila kuudhi au kushambulia imani za wengine.Usiwape nafasi watakouliza kuhusu ukabilia, udini, na maisha yako binafsi, wape majibu ya jumla na usiingie kwa undani.

Weka bayana na kwa njia nyepesi kueleweka ni nini dira ya taifa uatkaloliongoza, naamini kama mkatoliki dira ya kusamehe na kuanza upya ni dira itakayowaondolea hofu wale waliotenda madhambi na watafarijika na kukukubali. Ili uweze kufanya maajabu katika kipindi cha miaka mitano, nakushauri uzungumze nia ya kusamehe-reconciliation, na kuanza upya kujanga ya mbeleni kuijenga nchi upya katika mwelekeo mpya.

Wape mfano ambao Obama amekuwa anautoa huko Marekani kwenye kampeni za uchaguzi wa November. Kwamba CCM ni kama Republican ambao wamekuwa dereva wa Tanzania kwa takribani miaka 50 wametumbukiza gari la Tanzania kwenye shimo refu, sasa Chadema na wanamageuzi wengine waliamua kuingia shimoni humo kuliopoa hilo gari letu japo limepondeka pondeka lakini linafaa. Wapinzani wamesota toka kuingia mfumo wa vyama vingi kuliopoa hilo gari, Chadema na wengine wamesota huku CCM wakizidi kulisukumiza chini zaidi na kukaa pembeni kuwahadaa, kuwango'nga wapinzani na kuwaibia kura kila wakati wa uchaguzi. Wakati mwingine kuwapiga mawe na kuwanyunyuzia maji ya kuwasha ili washindwe kulitoa hilo gari shimoni. Sasa gari hili limeshatoka shimoni na limewekwa kwenye mstari ulio sawa tayari kuanza safari ndefu kukimbia kuwaletea maendeleo ya kweli Watanzania, loh , wale wale ccm waliolitumbukizamo bila aibu wala soni wanataka kuwapokonya ufunguo wa gari wapinzani hapo tarehe 31 October.

Dr Slaa , tell wananchi wasikubali kuwapa ufunguo CCM hapo October 31, with very simple reasons, ccm hawajui kuendesha gari na watalitumbukiza tena shimoni right after election. BUT wawape Chadema ridhaa ya kuongoza hili gari walipeleke kule watanzania wanakotaka kwenda, lakini Chadema wasiwanyime lift CCM , CCM wakae tu kwenye siti ya nyuma ya gari litakaloendeshwa na dereva mpa DR Slaa likiwa na plate number ya CHADEMA. Tumia huu mfano kufunga mdahalo wako. I tell you Dr Slaa kama unasoma hapa utawakoga Watanzania walio wengi na wataelewa vizuri sana with that simple example

La mwisho, waeleze Watanzania kuwa JK anawaogopa. Hata makanisani wachungaji na mapadre wana madarasa ya dini ambayo waumini wanapata fursa kuuliza maswali magumu, lakini pia wana wakati wa kuhubiri pasipo kuuliza maswali. JK amechukua njia ya kuhubiri sera, bila kuwakabili wananchi wapiga kura wake aweze kujibu maswali magumu. Huko ni kuwaogopa wapiga kura, na kiongozi wa jinsi hiyo hatufai

Alll the BEST Dr Slaa, Mungu akutie nguvu uuonyeshe ulimwengu kuwa kuna watanzania wenye akili na upako wa kuliongoza taifa letu


Natamani angekua humu ndani na akaupata ushauri huu,dah you are genius mkubwa
 
Hilo la umeme likitokea sitashangaa kabisa, na si ajabu ukakatika siku chache kabla ya uchaguzi
 
Nasikitika kusema umeme utakatika nchi nzima.


Heshima kwako KakaJambazi,

Inawezekana wewe ni pacha wangu ebu waulize wazazi wako vizuri na taratibu mkuu hata mimi nilikuwa nawaza kama wewe !.
 
Nasikitika kusema umeme utakatika nchi nzima.

Am an Engineer by professional, ninao jamaa wengi hapo TANESCO wako pamoja nasi ngoja nianze kuwatafuta ili nijue kabisa kama kuna hilo tuanze kulipuana mapema. Ahsante kwa kutukumbusha mapema hii tabia yao.
 
Mimi naitwa WAziri wa Umeme: SAsa basi Kuanzia saa moja na dkk zero mpaka lyamba hakuna umeme. sawa! Haiwezekani sisi tushindwe kujieleza halafu ninyi mko competent and confidence mtupiku NO!no? NO!no? NO!no?. hakuna cha ITv au VTI .Mbona redio ya SAUT - Mza tumeshaifunga rasmi. Msilete mchezo hapa!! Nchi ina wenyewe na wenyewe tuliozaliwa kwa ajili ya haya tupo.Msubiri TArehe 31/10 tuwape nchi kistaarabu. :smash: :smash: :smash: :smash: :smash:
 
ICHONDI nakugongea thanx mobile version haina thanx wala quotation ila hii hesabu!
Nyongeza kuna wakati dr huwa hajibu straigh mfano nakumbuka aliuzwa swali na sudi mnete doctorate yake ni ya nini! Alitoa maelezo marefu sana kiasi kwamba mtu asiyejua huweza dhania hajajibu na amekwepa swali! Namuomba ajibu maswali direct kwanza alafu atolee ufafanuzi hii itanoga!
Namwamini jenerali naamini ata u-handle mjadala!
 
Nadhani ni vizuri Dr. asibezi sana kwenye ufisadi unless aulizwe hilo na alijibu simply kama alivyofanya Star tv juzi. Nasema hili kwa sababu kuna wanaomwona Dr kama anajua ufisadi tu na hajui kuongoza, kwa hiyo aachane na makombora 20 ajikite kwenye dira ya Taifa.

Pia nadhani ni vizuri Dr. kurelax na kuonyesha tabasamu lake mara nyingi. Ni pale tu anaposisitiza na kukandamizia hoja ndio aonyeshe usiriasi wake. hii itasaidia kukonga nyoyo za akina mama wengi wanaodanganywa na tabasamu la JK na kuonyesha kuwa Dr. pia yupo social na ni celebrity pia
 
Natamani angekua humu ndani na akaupata ushauri huu,dah you are genius mkubwa
ICHONDI mimi bianfsi nimemkubali vibaya sana! Big up!
sorry kama sijasoma sehemu hii, nami niongeze mambo ambayo Dr. itabidi ayahusishe:
- kuna hii hoja ya elimu bure kama haitekelezeki, Dr. lazima aelezee kuhusu mabilioni yanayotajwa na ccm lakini kutokana na usimamizi mbovu hela hizo hazifiki kwa walengwa,
- Hoja ile ya ukubwa wa serikali na umzigo kwa watanzania kiasi kwamba kodi zimekuwa juu na zinazidi kuongezeka sasa wanaenda kwenye majengo leseni na ushuru kwa magari hata yasiyofanya biashara.
- kuongeza ukubwa wa serikali (kuongeza wakuu wa mikoa, wilaya wakatia hata waliopo wana mashangingi lakini hawafiki kwa wananchi, mishahara yao mikubwa kutokana na kodi za watanzania, na ujenzi wa majengo na samani za kiutawala zitatumika katika kuendeleza elimu na huduma bure kwa watanzania.
- Watanzania wa hali ya chini tene wenye akili kukosa shule zenye ubora huku wenye pesa wakipeleka watoto wao katika shule za Private za gharama kubwa,

wakati
hapo zamani shule za serikali waleienda watu wenye akili kwa gharama nafuu, na zikiwa na ubora mkubwa. ataje mipango ya chadema kuyatatua hayo
-Asisitize kuboresha masilahi ya wafanyakazi- afya na elimu ili waongeze ufanisi wa utendaji kama zamani maana kwa sasa wanaopanga foleni hospitali na watu masikini na shule za serikali hazina walimu wenye moyo kutokana na masilahi duni na ndizo wanazosoma watu wa kawaida.
Ajustfy sera za chama chetu kwa utulivu mkubwa maana ccm wanamtafuta sasa kumchafua
-
 
nafikiri nivizuri akiruka hewan ili watanzania bado hajawafikia wazipate sera zake kwa ufasaha katika majibu yake
 
Hata ingekuwa usiku wa manane ningeamka kuangalia tv ili nipate conclution ya oct. 31
Dr. SLAA For the president .
 
Ndugu wana Jamvi

Natambua Umuhimu wenu katika kuleta Mageuzi endelevu katika Taifa letu ambalo Kimsingi Limeshapoteza mwelekeo na sasa hivi kama ni ni jahazi linetegemea Muelekeo wa Upepo

Leo kuanzai Saa moja kamili mpaka saa tatu ITV watarusha moja kwa moja mdahalo utakaomuhusisha Mgombea wa urais kupia CHADEMA Dr. (Wa Ukweli) Wilbroad Peter Slaa.

Natambua wengi wetu humu jamvini tunafahamu kuhusu hii ratiba

Lakini nawakikishieni si wengi wanafahamu kuhusu hiii ratiba, na hii inatokana na ukweli kuwa Watanzania wengi si watu kufuatilia mambo ya msingi, wengi wanajua ratiba za vupindi vya Commedy au Tamthiliya na Pamoja na michezo ya kwenye Runinga. Kwa kweli siwalaumu kwa hili kwa sababu Serikali yao ndivyo inavyopenda wawe hivyo ili iweze kuwatawala ipendavyo.

Watu wengine TV kwao ni TBC na Star TV tu

Ni Matamanio yangu basi watanzania wengi waweze Kusikia Ujumbe wa Ukombozi utakaotolewa Leo na Mpambanani na Dr. ( wa Ukweli) Slaa.

Kutokana na hayo basi napendekeza yafuatayo

1: Sisi tunaofahamu ratiba hii tuwafahamishe na kuwakumbusha Ndugu, jamaa na marafiki zetu ambao aidha hawafahamu ratiba au hawana uhakika na Kituo gani cha TV kitaonesha Mdahalo huu

2: Kwa wale ambao muda huo utatukuta kwenye Viti Virefu basi ni vyema wakawasisitiza wahudumu wa bar au Restaurant kutune ITV ili waweze kuupata ujumbe huo

3: Chadema iwaagize wagombea wake wa ubunge na Udiwani Nchi nzima katika Kampeni zao za Leo wahamasishe au wawakumbushe watu juu Mfdahalo huu, naona njia hii itakuwa effective sana kwa sababu itafanya ujumbe huu ufikie watu wengi na kwa haraka

Narudia

Ni Muhimi watu wengi leo Wakaisikia sauti ya Mtu ambaye kwa Miaka 5 iliyopita Serikali imekuwa ikifuata Maagizo yake ama kwa kupenda au kutopenda

Ikumbukwe

Bila Slaa

Fisadi Mramba asingepajua keko pakoje ( Ingawa ni Usanii)
Fiasdi Mramba leo angekuwa hapigi Kampeni anasubiri tu Warombo wampe Ubunge(sasa hivi hali yake ni mbaya)
Fisadi Karamagi leo angekuwa kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge


Mwana JF and CHADEMA play your part so that this voice is heard by all Tanzanians hata wale Ndugu zetu wa Green Guard wanaolipwa Ujira Mdogo ili wamwage Damu za Ndugu zao

Asanteni
 
Kutumia TV ni moja nji za kuwafikishia ujumbe wantanzania. Ni vyema na haki kabisa kwa wagombea kupata fursa hii ya kujinadi hasa wenye weledi na kujiiamini. All the best Dr Slaa.
 
Shukrani kwa taarifa hii, hata EPL leo sitaangalia ili nimsikilize Dr Slaa. Natumaini Tanesco hawatafanya uhuni wao
 
Mie nitakwenda na family social centre kuwatch maana kuna dalili za mgao wa usiku
 
I suspect hawa mafisadi watakata umeme leo!! Lakini nitakwenda kwenye kijiwe chenye generator.
 
Back
Top Bottom