Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Elections 2010 Dr. Slaa kujibu maswali "Live" ITV saa moja Usiku Jumamosi Hii

Ina maana " Dr" Jakaya Kikwete hataudhuria? Oooh nimesahau hana experience ya kufanya presentation!!Si ubajua U-dr ameupata jukwaani? How can he lead the people he is scared of facing?
 
Hongera Dada Rose Mwakitwange kwa jitihada zenu za kuikomboa nchi hii kwa mbinu mbalimbali ikiwemo hiyo ya mdahalo. Watanzania wana haki ya kuwafahamu vema wagombea hususan wa urais namna wanavyoweza kujenga hoja wanapokabiliana na maswali ya waajiri wao (wananchi).

Tabia ya kifisadi ya kukataa mdahalo itaendelea kuiumbua sisi m na hiyo ni fursa kwa Rais Mtarajiwa wetu mpendwa Dr. Slaa kuuonyesha umma namna atakavyoikomboa nchi hii. Sisi wazalendo wapenda maendeleo na wenye imani tunaendelea kumwombea Dr. Slaa Mungu ampe hekima ya kuongea ili hatimaye tuikomboe nchi yetu kutoka kwenye makucha ya mafisafi.

Wanaodhani kuwa kikwete atahudhuria waondoee mawazo hayo. Unadhani yeye na timu yake hawajitambui?? Thubutuuuu!! Wanajitambua kuwa uwezo wao ni mdogo. Wao wanapenda wahojiwe peke yao tena na tido mhando au marin hasan.
 
Ni saa ngapi.

Watu watoe wasiwasi, Dr atavuta kura za kutosha kwa kuwa live.

Mitaani mijadala itaibuka sana.
 

Jumamosi, 23 Octoba 2010

Kipindi kitaanza kurushwa kuanzia saa 1.00 jioni

Waalikwa wawe wamekaa ifikapo saa 12.00jioni

Ukumbi ni Moven Pick Hotel-Kivukoni Hall

**Ukumbini kwa walio na mwaliko wa kadi pekee
 
Good move! kuna undecided wengi ila ndo wale wasioenda mkutanoni na hawajui value of vote. May be watamega!
 
Naunga mkuno Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla kutumia kila njia kuelezea sera zao. TV facility ni nzuri kwa kuelezea sera. Acha CCM na Kikwete wao wanaoogopa midahalo. Chadema /Dr. Slaa kaza uzi songa mbele tumia kiola chance mnayoipata kwenye TV na Radio na magazeti na vipeperushi.
 
Jumamosi, Oktoba 23 Mgombea Urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa atajibu maswali ya wananchi moja kwa moja (live) kupitia ITV Televisheni, kuanzia saa moja jioni hadi tatu usiku.

Mwambie rafiki yako na wadau wote wa uchaguzi wasiokuwa kwenye mtandao huu, kwa njia ya simu au ujumbe mfupi wa maandishi, ni wakati murua wa kumuuliza maswali na kumbana kujua anataka kuifanyia nini hasa nchi hii, maana midahalo ndio kama hiyo ya urais hatuoni kama itakuwapo tena.


Tufunge huo mjadala wote tumeletwa na mwenyezi mungu hapa duniani. Mungu awajua walio wake na atawapigania katika mabaya yote. Tuendelee kumtumaini mungu tutashinda tu kwa uwezo wake.

Mengine tutajiumiza vichwa bure tufikirie kulinda kura kwa kwa akili zetu zote na kwa msaada wa mungu.

tutavuka salama Dr.Slaa ni Musa wetu.
.

Hatumchagui Askofu wala Sheikh kwenda Ikulu ni makosa kunukuu vifungu vya kitabu kimoja cha dini na kusema Dr Slaa ni Musa wetu.Unapomfananisha Dr Slaa na Musa wa kwenye Biblia unataka wapiga kura wa dini zingine wamfananishe na nani kutoka kwenye vitabu vyao vya dini? Au Hussein mjukuu wa Mtume Muhammad .Ni muhimu kuelewa na kutenganisha kwamba wapiga kura ni wa dini zote lakini Mungu ndiye mmoja kwa wote.
 
Nashauri asifanye hivyo kabisa atajimaliza,hakuna sababu ya kuendelea kutia chumvi Dr.Slaa tayari amekubalika hana haja ya kuendelea kujiuza, hiyo strategy haitakuwa tofauti na ya JK ya kueneza mabango nchi nzima, SLAA ni bidhaa inayouzika kwa wateja ni bidhaa adimu, anatakiwa aendelee na za majukwaa zinatosha sana, magazeti yanafanya kazi kubwa sana pia.

Chonde chonde asifanye hivyo nawaomba washauri wake wabadilishe, the strategy is not healthy, ile aliyofanya juzi pale ITV na Masako inatosha sana wa watu waliizungumzia karibu nchi nzima.TAFADHALIU TUSIZIDISHE CHUMVI MBOGA ITAHARIBIKA.

Namna kuna chembechembe ya busara kwenye post yako. Mdahalo wa kwanza wamesema alifanya vizuri, nani anajua je akiharibu katika mdahalo wa pili si utafuta uzuri wa mdahalo wa kwanza?
 
Ina maana " Dr" Jakaya Kikwete hataudhuria? Oooh nimesahau hana experience ya kufanya presentation!!Si ubajua U-dr ameupata jukwaani? How can he lead the people he is scared of facing?

Tusisahau kwamba, kampeni za sisi waafrika hazina ustaarabu wa kutosha kama za wenzetu wa nchi zilizoendelea ambapo kampeni hazigeuzwi uwanja wa vita vya kutupiana kejeli, matusi na maneno ya kumshusha mtu hadhi. Katika nchi zinazoendelea kama hilo litatokea ni kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na huku kwetu. Mazingira haya ya kampeni za kudhalilishana hayatoi nafasi ya wagombea kuingia kwenye mdahalo kwa amani.
 
kwenye ITV ya wachaga???? hakyanani stazami


Wale wale wanaopandikiza mbegu za udini na uakabila. Humu ndani kuna wachaga unafikiri watakuewa vipi kwa maneno yako ya kibaguzi. Mchaga kumiliki ITV basi imekuwa ya kabila la wachaga? Unakotupeleka siko,tafuta nchi nyingine ya kuishi yenye kuenzi ukabila. Nawachukia na siwapendi watu wanaosukumwa na udini au ukabila kujadili hoja. Ninakusihi kuepuka kurusha makombola aina ya udini na ukabila ni silaha za maangamizi kwetu sote ukiwemo wewe na mimi. Tukosoe lakini huku tukikwepa kutumia udini na ukabila kama ushawishi wa nyongeza kukoleza hoja zetu. Udini una madhara kwa wote CCM na chadema
 

Jumamosi, 23 Octoba 2010

Kipindi kitaanza kurushwa kuanzia saa 1.00 jioni

Waalikwa wawe wamekaa ifikapo saa 12.00jioni

Ukumbi ni Moven Pick Hotel-Kivukoni Hall

**Ukumbini kwa walio na mwaliko wa kadi pekee

Muda mbaya sana Kitila. Tulio wengi tunatulia vitini saa 3 usiku. Tutaukosa uhondo huu. Waombeni ITV muanze saa tatu. Mbona vipindi maalum vya Mengi na wengine vinawekwa saa 3? Nawaomba pia JF waangalie uwezekano wa kuwaleta Dr Slaa na Prof Lipumba "live" humu.
 
Kesho Jumamosi Oktoba 23 Mgombea Urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa atajibu maswali ya wananchi moja kwa moja (live) kupitia luninga ya ITV ya jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki
 
Naona uko uptodate. Tunaomba tarehe na muda wa kujibu maswali LIVE ya Mzee wa Boma, Dr. JK
 
Back
Top Bottom