Tunajua kwamba maji yamewafika shingoni. Mmejaribu kusomba watu na malori weee, mkawagawia khanga weee, mkawagawia tshirt, mkawagawia kofia na skafu jumlisha elfu mbilimbili lakini wapi bwana watu bado wapo kwa Dr Slaa. Mmesambaza message za uchonganishi na uchochezi, mmetumia jeshi kutishia wee, lakini hakuna kitu. Mwanzoni mlisema alifukuzwa upadre, mkaona haiuziki, sasa mmeanza tena kumwita padre wa katoliki. Hata hii haina soko kwa sasa. Mmebakiza siku nane za kuwa Ikulu.
Naamini watakaosusia mahojiano ya Dr Slaa ni mafisadi tu ambao wanajua Slaa hatasita kuwaumbua. Lakini watanzania watakuwa macho kujua Rais wao anasema nini! Au unajaribu kumlinganisha Slaa na Kikwete ambaye hotuba zake za Mwisho wa mwezi zimesusiwa? Mnatapatapa ndugu zangu, lakini msijali hiyo ni kawaida kwa mfa maji.