Msengapavi
JF-Expert Member
- Oct 23, 2008
- 8,819
- 7,638
Sikuelewi mkuu kwa hiyo kwa sababu Dr. Slaa anahitaji kura za wafanyakazi basi ndo anyamazie uozo eti wafanyakazi hawatamuelewa.Wafanyakazi wa Tanzania hawako hivyo unavyowafikiria. Hawajui kugoma. Ni watiifu sana. Wengi wao wanaridhika sana anapopewa nafasi inayomwezesha kufanya ubadhirifu. Hawatamwelewa Dr Slaa hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inaweza kucheza rafu yoyote ile ikiwemo hiyo nyongeza kinyemela ya mishahara. CCM wanajua marefa wote ni wao. NEC, RPP na vyombo vya DOLA.
Mimi naendelea kuomba kuwa Dr Slaa na CHADEMA washinde uchaguzi. Mungu atufanyie muujiza huu ili katiba cha nchi irekebishwe. Kwa sasa hivi kwa serikali hii hii ya JK huyu huyu, na tume ya uchaguzi isiyo huru hapawezi kuwa na haki.
kama ungekuwa wewe.....Kama ningekuwa mimi, ningemuwekea JK pingamizi kwa kuwa afya yake ina utata. Anaanguka ovyo ovyo jukwaani. Hana nguvu tena ya kutembea kwa magari, ndio maana sasa anatembea kwa helikopta!
2011-2015 atatumia muda wake mwingi kwa matibabu, kuliko kuongoza nchi. Hamuoni kwamba itawagharimu Watanzania na Serikali yao fedha nyingi za matibabu yake, pia, kutokuwapo kwake ofisini, nani ataongoza nchi? BILAL? Masikhara haya!
Lipumba nawe weka pingamizi lako!
Kama kweli ameongelea tetesi la pingamizi basi Tendwa kachemka vibaya mno.
Nimegundua member wengi humu JF uwezo wao wa kufikiria ni mdogo sana au wana mtindio wa ubongo kiasi cha kushindwa kujua hali halisi ya watanzania.Mtu anashabikia tuu hata akiambiwa padre Slaa kammega mke wake!Slaa kadondoka ****** alipokuwa anapiga.....watu wakamshangilia wakati wanajua hilo ni dhambi kwa bwana Yesu,inabidi mtubu kabla muda wenu wa kurudi kwa Bwana haujafika!
...Wewe Ndio Namba MOJA.
Huyu Slaa na network yake sasa anazidi ku boa!!! Issue iko wazi kabisa kuipeleka mahakamani ni kujidhalillisha wenyewe, huu ni wakati aeleze sera za chama chake, hawawezi kushinda kwa kuonewa imani na watanzania wala hawawezi kushinda kwa maombi
Kinachotakiwa chadema yeye kama kiongozi aondoe image ya ukabila na udini ndani ya chama chake, Hakuna atae mpigia kura kuongoza nchi wakati anashindwa kusafisha chama cha kidini. Mchungaji usidharau malalamiko ya wapiga kura
Geofrey Nyang'oro na Lilian Mazula-Mwananchi
SHERIA ni msumeno na sasa mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete atalazimika kufanya kazi ya ziada isimdhuru baada ya Chadema kumwekea pingamizi rais huyo wa serikali ya awamu ya nne.
...................................................................[deleted]
"Sehemu ya tano ya sheria hiyo sura ya 21.-(1) inaweka bayana vitendo vinavyokatazwa wakati wa uteuzi wakati wa kampeni za uchaguzi na inasomeka:
"(a)Kila mtu ambaye kabla au wakati wa kipindi cha kampeni, moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote, kupitia kwa mtu mwingine yeyote au kwa niaba yake, anatoa, anakopesha au anakubali kutoa au kukopesha, au anatoa, anaahidi au kumpatia au anajaribu kumpatia fedha yoyote au kitu chochote chenye thamani, mpiga kura au kwa ajili ya mtu yeyote kwa niaba ya mpiga kura yeyote au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote kwa nia ya kumshawishi kupiga kura, au kuacha kupiga kura au kumrubuni mtu yeyote kutendo hicho kwa niaba ya mpiga kura huyo kupiga kura au kuacha kupiga kura katika kura za maoni au uchaguzi wowote;
.................................................[deleted]
"CCM wametumia Sh1.5 bilioni kutengeneza mabango nje ya nchi kwa kutumia fedha za serikali pia ankara ya malipo "invoice" inaonyesha imeandikwa 'VAT INVOICE' kitu ambacho hakieleweki," alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa ni muhimu CCM kutoa ufafanuzi juu ya hilo kwa kuwa ushahidi upo na unaonyesha kuwa kuna mchezo mchafu umeanza kufanywa.
Huyu Slaa na network yake sasa anazidi ku boa!!! Issue iko wazi kabisa kuipeleka mahakamani ni kujidhalillisha wenyewe, huu ni wakati aeleze sera za chama chake, hawawezi kushinda kwa kuonewa imani na watanzania wala hawawezi kushinda kwa maombi
Kinachotakiwa chadema yeye kama kiongozi aondoe image ya ukabila na udini ndani ya chama chake, Hakuna atae mpigia kura kuongoza nchi wakati anashindwa kusafisha chama cha kidini. Mchungaji usidharau malalamiko ya wapiga kura
Nimesoma pia leo ktk Jambo Leo kwamba Chadema wameahirisha kuwasilisha pingamizi lao dhidi ya JK le ili kuwapa nafasi wanasheria wake walinoe zaidi. lakini habari kutoka kwa swahiba wangu katika uongozi wa ndani ya Chadema zinasema kuwa wanasheria hao wanataka kuhakikisha kwamba Tendwa hapati escape route yoyote ya ki-hoja ya kulitupilia mbali pingamizi hilo -- isipokuwa tu ibakie ile ya kuibeba tu CCM!
Kajiita mwenyewe mgonjwa wa ukimwi sasa hapo ni tusi? shida ni kwamba sisi m hamna tofauti kati ya ukweli na matusi. Ukilaza umewazidiHaaa haaa haaa.. hamna nyimbo, zaidi ya matusi! Slaa kapelekwa mkenge na akina Mbowe na Zito, na sasa anajuta!