Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Chadema wanatakiwa wapige kampeni na si kulialia. Hii ni dalili ya kushindwa kabla ya mchezo.

Sina imani sana kama unajua maana ya kulia lia...
Hivi kuna anayelialia zaidi ya ccm dhidi ya CHADEMA? (naweka herufiki kubwa kumaanisha respect)
Hebu jaribu kuionea huruma nchi yako... Toka uhuru 1961 cccm wamekuwa wakiongoza kwa miaka bila mabadiliko yeyote nchi hii.
 
ingekuwa tunachagua PAPA basi Dr slaa(Daktari wa mambo ya imani ya kikristo) angetufaa, ila kwa urais wa Jamhuri ya Muungano wamchelewa na wamepwerewa pwere
 
CHADEMA jamani hawana sera na hawajiamini pamoja na mabomu yao yote hayo.
Wanataraji huruma ya Tendwa.Kosa ni la kwao wenyewe kuweka mgombea asiye na elimu inayohitajiwa na watanzania wa sasa.Mgombea wao hakubaliki kabisa hasa miongoni mwa jamii ya waislamu.
Wanalilia na huruma ya Mungu.Ati Kikwete afe,vipi nyinyi!.Kuumwa si kufa.Safari ya Dkt Slaa ni ndefu.Hata ikitokea dharura basi si Chadema watakaochukua nchi bali ni CUF.
Itakavyokuwa lakini CHADEMA wanaonyesha maana ya mkuu wa nchi kusimamia SHERIA! Kama Ukiwa na Rais kama huyu ambaye amesainisha sheria kwa mbwembwe halafu haitekelezi unatarajia nini Akishinda? Umeona aliposema kuwa WEZI WA EPA WALIORUDISHA HELA KAWASAMEHE! Kwani wewe unafikiri Dini ya KIISLAMU inaruhusu dhuluma? Wewe ni Muislam wa wapi! Unachagua mtu anayeleta usawa na sio kuangalia mambo ya kibaguzi! Kama waislam wanaikubali CUF mara zote NNE mbona hawajashinda hadi wametafuta Huruma ya CCM kuingia serekalini huko Zanzibar? Tena wamekubali kuwa Vivuli mana hawatakuwa watendaji.
Kama una akili timamu utawaunga mkono CHADEMA mana wanachotetea sio cha dini bali kinamgusa kila mtu! Wale mafidadi kwani waliiba hela za nani? Si kila mtu Mkristo kwa Muislam anateseka! sasa wewe kama unasema Kikwete anachaguliwa kwa mantiki ya Uislam kakusaidia nini? Bora Mkapa aliyetoa chuo kikuu, Nyerere aliyetaifisha shule za kidini ili watu wote wawe na usawa wa elimu.....
CHADEMA wanasimamia haki ya wote, hakuan ruhusa kwa RAIS kufunja sheria, mana ameapa tena kwa kuishika kuran kuwa watasimamia sheria!
ACHA MAMBO YA UBAGUZI WA KIDINI HAUTAKUFIKISHA POPOTE!
 
ingekuwa tunachagua PAPA basi Dr slaa(Daktari wa mambo ya imani ya kikristo) angetufaa, ila kwa urais wa Jamhuri ya Muungano wamchelewa na wamepwerewa pwere
ACHA MAMBO YA KIDINI! Uliza ndugu zako au majirani au marafiki zako wangapi wamefaidika na CCBRT? Ndio utajua kuwa dini ni imani tu, na bora mtu wa dini anayesimamia haki kuliko mtu asiyesimamia haki.

Kama propaganda zako ni kuhusu Dini ya Dr. Slaa ujue hata wakrito watampa support na uone kama hao wengine watashinda! Hujui watu wa imani gani ni wengi kwenye kupiga kura hivyo usiweke chembe za udini zitakutokea puani!
 
liganga4

user-online.png
Junior Member

reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date : Sun Aug 2010
Posts 2
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts

Watu wengine hawana kazi kazi yao kuangalia flani anapost ngapi hapa! doh
 
sasa huyu mkwere nadhani hadi uchaguzi upite atakuwa ashakufa kwa stresses!

Genekai, Siku hizi umegeuka kuombea watu wafe!!! nilidhani watu wanaombea watu wapone!!! HIZO NDO SIASA ZA TZ BWANA.
 
Itakavyokuwa lakini CHADEMA wanaonyesha maana ya mkuu wa nchi kusimamia SHERIA! Kama Ukiwa na Rais kama huyu ambaye amesainisha sheria kwa mbwembwe halafu haitekelezi unatarajia nini Akishinda? Umeona aliposema kuwa WEZI WA EPA WALIORUDISHA HELA KAWASAMEHE! Kwani wewe unafikiri Dini ya KIISLAMU inaruhusu dhuluma? Wewe ni Muislam wa wapi! Unachagua mtu anayeleta usawa na sio kuangalia mambo ya kibaguzi! Kama waislam wanaikubali CUF mara zote NNE mbona hawajashinda hadi wametafuta Huruma ya CCM kuingia serekalini huko Zanzibar? Tena wamekubali kuwa Vivuli mana hawatakuwa watendaji.
Kama una akili timamu utawaunga mkono CHADEMA mana wanachotetea sio cha dini bali kinamgusa kila mtu! Wale mafidadi kwani waliiba hela za nani? Si kila mtu Mkristo kwa Muislam anateseka! sasa wewe kama unasema Kikwete anachaguliwa kwa mantiki ya Uislam kakusaidia nini? Bora Mkapa aliyetoa chuo kikuu, Nyerere aliyetaifisha shule za kidini ili watu wote wawe na usawa wa elimu.....
CHADEMA wanasimamia haki ya wote, hakuan ruhusa kwa RAIS kufunja sheria, mana ameapa tena kwa kuishika kuran kuwa watasimamia sheria!
ACHA MAMBO YA UBAGUZI WA KIDINI HAUTAKUFIKISHA POPOTE!
Watu wengi ukiwamo wewe Mozze munasema ubaguzi wa kidini na dini ni vitu visivyo na maana,lakini kivitendo daima munaonesha kushindwa kujitenga navyo.Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwani dini ni sehemu ya ubinadamu.
Hata mgombea wenu Dkt Slaa ana hadaa kama hizo mdomoni alizorithi kwa baba yake Nyerere,lakini kivitendo anatetea dini yake na dhehebu lake la ukatoliki,ndio maana bungeni mambo yenye faida na watanzania wote lakini yanayoanzia kwenye uislamu hakutaka kuyatetea pamoja na kidomo domo chake chote.
Kuhusu kutokushinda kwa CUF sababu zinajulikana kuwa ni ubaguzi wa kidini na wizi wa kura.Kwa sababu ikiwa ni usomi wakati huo na sasa hakuna chama chenye wagombea wasomi kama CUF hata CCM hawaingii.
Kusema kwa dkt Slaa si tiketi ya kuongoza nchi.Wangapi ni wasemaji sana lakini katika utekelezaji ni sifuri.Huyu ana mwelekeo huo huo kwa sababu inasemekana katika CHADEMA kuna udikteta wa hali ya juu lakini yuko doro mno hata kuuzungumzia.
Ulipomjibu Mtu wa pwani umesema: ACHA MAMBO YA KIDINI! Uliza ndugu zako au majirani au marafiki zako wangapi wamefaidika na CCBRT? Ndio utajua kuwa dini ni imani tu, na bora mtu wa dini anayesimamia haki kuliko mtu asiyesimamia haki.
Hiyo habari ya CCBRT ni habari nyengine na ni matokeo ya ubaguzi wa kidini na kiutawala.Kwani Wakristo wangapi watafaidika pindi nchi ikijiunga na OIC au mashirika ya kiislamu ambayo hufanya kazi zake bila ubaguzi yakiachwa kufanya shughuli zake Tanzania?.
 
Chadema wanatakiwa wapige kampeni na si kulialia. Hii ni dalili ya kushindwa kabla ya mchezo.

we pandikizi la ccm? na wewe hapo huna kitu zaid ya kutumikatu
na utatumika sana mwaka huu. mgombea wenu ni mpopompo alipokuwa anasain ile sheria alizani haimlengi yeye?

tatizo hasomi bali anasaini tu. mtajibeba mwaka huu
 
Hiyo habari ya CCBRT ni habari nyengine na ni matokeo ya ubaguzi wa kidini na kiutawala.Kwani Wakristo wangapi watafaidika pindi nchi ikijiunga na OIC au mashirika ya kiislamu ambayo hufanya kazi zake bila ubaguzi yakiachwa kufanya shughuli zake Tanzania?.
Una uhuru wa kutoa maoni yako. Hujui mimi ni imani gani hivyo usikisie! Ninachojaribu kuweka hapa ni ukweli! OIC na mambo mengine hayo ni matakwa ya wananchi na sio Rais...kama katiba hairuhusu hata umweke shehe mkuu atakwama tu! Lakini wananchi wakiridhia hakuna atakayekwamisha!

Upendeleo unaosema hauna vigezo. Mkapa ametoa Chuo cha serekali Morogoro kuwa Chuo wa kiislamu matokeo yake umeyaona? Je ni Chuo ambacho hata waislam wanapenda kusoma? Mbona wanakimbilia St. Augustine, Bugando, Tumaini na sehemu kama hizo? Kuna hata mmoja ulisikia kabaguliwa?

Haya nenda Chuo cha Kiislam Morogoro, halafu uniambie mtu akitoka pale atakuwa na ushindani kwenye soko la Ajira? Kama chuo kinaacha kuajiri watu makini kwa misingi ya dini utapata wapi wataalamu? Miaka ijayo utasema waliohitimu kwenye chuo hiki hawapati ajira kwa sababu ya dini yao?

Penye haki ndugu yangu kila kitu kinasimama, wachapakazi tu ndio watafaidika na sio kukaa na kusubiri upendelewe....chagua mtu makini, anayeheshimu sheria ili hata wewe uweze kutetea haki zako! Lakini asiyefuata sheria atakukandamiza tu hata kama ni ndugu yako au mtu wa dini yako!

Jua tu kwamba UKIWA NA FIKIRA HIZO ZA UDINI UTAISHIA KULALAMIKA SIKU ZOTE! Kikwte alipopata 80% hakuchaguliwa na Watu wa dini yake tu! Na hilo halitakuja kutokea mahali popote! Kilicho akilini mwako hakiko kwa wengine! Ndio mana narudia, CUF japo wanaonekana kutaka kutumia njia ya dini hawajafanikiwa na hawatafanikiwa!

KUWA MTU WA KUPENDA HAKI! Na CHAGUA MTU ANAYESIMAMIA UKWELI NA HAKI!
 
Watu wengi ukiwamo wewe Mozze munasema ubaguzi wa kidini na dini ni vitu visivyo na maana,lakini kivitendo daima munaonesha kushindwa kujitenga navyo.Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwani dini ni sehemu ya ubinadamu.
Hata mgombea wenu Dkt Slaa ana hadaa kama hizo mdomoni alizorithi kwa baba yake Nyerere,lakini kivitendo anatetea dini yake na dhehebu lake la ukatoliki,ndio maana bungeni mambo yenye faida na watanzania wote lakini yanayoanzia kwenye uislamu hakutaka kuyatetea pamoja na kidomo domo chake chote.
Kuhusu kutokushinda kwa CUF sababu zinajulikana kuwa ni ubaguzi wa kidini na wizi wa kura.Kwa sababu ikiwa ni usomi wakati huo na sasa hakuna chama chenye wagombea wasomi kama CUF hata CCM hawaingii.
Kusema kwa dkt Slaa si tiketi ya kuongoza nchi.Wangapi ni wasemaji sana lakini katika utekelezaji ni sifuri.Huyu ana mwelekeo huo huo kwa sababu inasemekana katika CHADEMA kuna udikteta wa hali ya juu lakini yuko doro mno hata kuuzungumzia.
Ulipomjibu Mtu wa pwani umesema: ACHA MAMBO YA KIDINI! Uliza ndugu zako au majirani au marafiki zako wangapi wamefaidika na CCBRT? Ndio utajua kuwa dini ni imani tu, na bora mtu wa dini anayesimamia haki kuliko mtu asiyesimamia haki.
Hiyo habari ya CCBRT ni habari nyengine na ni matokeo ya ubaguzi wa kidini na kiutawala.Kwani Wakristo wangapi watafaidika pindi nchi ikijiunga na OIC au mashirika ya kiislamu ambayo hufanya kazi zake bila ubaguzi yakiachwa kufanya shughuli zake Tanzania?.

Kama ningepata uwezo wa kuongeza idadi ya wapiga kura wa dini yangu ningefurahi sana ili tuweze kumpigia kura rais wa dini yetu. Lakini bahati mbaya uwezo huo sina Yarabi.. sasa sina budi kusubiri tu kipenga cha mwisho ili nione matokeo.
 
Najua tendwa anaogopa, lakini namshauri atoe uamuzi unaostahili, kama anaona usalama wake utakuwa mashakani ajiandae tutamsindikiza ubalozi wa Uingereza kama alivyofanya John Kithongo wa Kenya, aliwataja wala rushwa wote akakimilia ubalozini. Tendwa tunamuakikishia kwamba Chadema ikishaingia madarakani tutamrudisha nyumbani kama shujaa na usalama wake utakuwa guaranteed.
 
Miujiza tu inasuburiwa kutimilika azima hii.....naamini kwa kuwa waliofile malalamiko ni walewale tuwajuao kwa kufatilia mabo basi naamini tutashinda kwa [pamoja nao...........
 
huko ni kupoteza muda wenu wa kampeni na pesa. pole Chadema

Hata makaburu wa South Africa walikuwa wanasema hivi hivi mkuu. Siwatofautishi walowezi wa SA na CCM, sorry kuna tofauti kubwa, makaburu walijenga uchumi imara wa taifa lile, CCM wamekalia wizi tu.
 
heading ibadilishwe wamepeleka malalamiko, hawana jeuri ya kuweka pingamizi hao.

na kwa hakika hata wale wanachama wao na viongozi kwa miaka kumi na tano wameamua kushuka kwenye boti kwa fitina na chuki na ukabila walio nao watu hawa
 
Ndipo hapa tume huru ya uchaguzi inapohitajika, tendwa asingekuwa na kigugumizi, sasa kama ni mabosi wake unafikiri atafanyaje, mfano ametoa rushwa au kupokea kisha unampeleka kwa hosea
 
Mbona vyama vingine havijaweka pingamizi??

vyama vyengine viko makini, sio kama hiki ambacho kina penda sifa na kukimbilia media. kwa ufupi wanajiangusha sio kujishusha

ukisoma ilani ya chadema utaona mkurupuko mkubwa sana hata katika uandaaaji utashangaa na kujiuliza utekelezaji wake utakuwaje ikiwa leo hawa mabwana wanapewa nchi

lkn kwa vile wanajua kama hawapati, ndio maaana wakawa wanapopowa sawa sawa na kumwambia mtoto wa mfalme nikimuoa nitampa mbingu iwe yake
 
Back
Top Bottom