Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

Elections 2010 Dr. Slaa kumuwekea pingamizi Kikwete!

heading ibadilishwe wamepeleka malalamiko, hawana jeuri ya kuweka pingamizi hao.

na kwa hakika hata wale wanachama wao na viongozi kwa miaka kumi na tano wameamua kushuka kwenye boti kwa fitina na chuki na ukabila walio nao watu hawa
Pingamizi si lelemama.yaliyopelekwa ni malalamiko.wasubiri yafanyiwe kazi.ndipo watakapojiona wamechemsha mawe.
 
Mgombea wa CCM kwenye kiti cha urais, Mh JM Kikwete amewekewa pingamizi na Chama cha Demokrasia na maendeleo kwa kukiuka sheria aliyoisaini yeye mwenyewe. Imedaiwa kuwa ameongeza mishahara kwa wafanyakazi kinyume na taratibu za nchi kitu ambacho kisheria kinaonekana ni rushwa. Kwahiyo CHADEMA wamepeleka malalamiko yao kwa tume ya uchaguzi wakiomba jina lake lienguliwe kwenye mbio za kuwania uras wa JMT. Je kweli Tendwa ataweza kusimamia haki?
Sungura
Mbona unawadanganya wana JF.Au unataka wakuone unavyokurupuka.Au mategemeo ya CHADEMA yalikuwa katika pingamizi.mbona mnahaha.ahahaa si mlijiingiza wenyewe badala ya kwenda karatu mlikozoeleka mkataka makubwa.Basi kama ndivyo subiri matokeo ya wachambuzi.kumbuka kilichopelekwa kwa msajili ni malalamiko si pingamizi .Hatudanganyikiiiiiii.zipo taratibu za kufuatwa.
 
Najua tendwa anaogopa, lakini namshauri atoe uamuzi unaostahili, kama anaona usalama wake utakuwa mashakani ajiandae tutamsindikiza ubalozi wa Uingereza kama alivyofanya John Kithongo wa Kenya, aliwataja wala rushwa wote akakimilia ubalozini. Tendwa tunamuakikishia kwamba Chadema ikishaingia madarakani tutamrudisha nyumbani kama shujaa na usalama wake utakuwa guaranteed.
Naona sasa mnampa rushwa Tendwa.Tumewashtukia
 
Ndipo hapa tume huru ya uchaguzi inapohitajika, tendwa asingekuwa na kigugumizi, sasa kama ni mabosi wake unafikiri atafanyaje, mfano ametoa rushwa au kupokea kisha unampeleka kwa hosea

nafikiri Tendwa ni mtu makini,ndio maaana aliwaongezea Chadema na vyama vingine kwa ujumla siku za kurejesha fomu za maadili.Hivyo Chadema msihofu na kumpa rushwa Tendwa,atatenda haki.
Mbona mlipoongezewa siku hamkumjadili na kuhofia utendaji wake wa kazi!?
 
Source: MICHUZI

TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO





Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,John Tendwa.

Na Mary Kweka –Maelezo

Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya siku tano.

Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.

''Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya mlalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA'',Alisema Tendwa.

Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Msajili huyo wa Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya msajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi,Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.
 
Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.


Hii ngoma inaweza ikafika hadi Mahakama ya Rufaa . . . . Lissu na Marando na CHADEMA hawatakubali. Uchaguzi unaweza kuahirishwa na sheikh Yahya akapanua soko lake kwa utabiri uliotimia.

Tutaona mengi mwaka huu.
 
Acha tuone haya mambo yanaishia wapi! Ni patamu ila wanasheria wanavyojua kupindisha mambo, utasikia hiyo kona imepigwa kali watu hoi. Anyway, we need the right decision from Tendwa.
 



Hii ngoma inaweza ikafika hadi Mahakama ya Rufaa . . . . Lissu na Marando na CHADEMA hawatakubali. Uchaguzi unaweza kuahirishwa na sheikh Yahya akapanua soko lake kwa utabiri uliotimia.

Tutaona mengi mwaka huu.

Sina uhakika sana kama wafadhili watakubali kuendelea kuifadhili Tz kama vyombo vya maamuzi kwenye hili watafumba macho!
 
Hii ngoma nzito hadi kieleweke hata kama uchaguzi utafanyika mwakani. Hizo siku 5 za Tendwa ni jinsi ya kujadi na bosi wake jinsi ya kupindisha sheria kama kawaida yao
 
Mimi nimeishikilia "COUNT DOWN TIMER" yangu, kwani hizo siku tano ziko mbali?
Ya mwaka huu si mchezo!
 
Hii ngoma inaweza ikafika hadi Mahakama ya Rufaa . . . . Lissu na Marando na CHADEMA hawatakubali. Uchaguzi unaweza kuahirishwa na sheikh Yahya akapanua soko lake kwa utabiri uliotimia.

Tutaona mengi mwaka huu.
Kwa nini uchaguzi uahirishwe mbona kuna wagombea ubunge wamewekewa pingamizi na kunawaliopita bila kupingwa na uchaguzi unaendelea.

Jina la JK likitolewa uchaguzi unaendelea kama kawaida hata kama kungekuwa hakuna wagombea wengine na akabaki mmoja still huyo angepita bila kupingwa.

Ila kwa hili I can guess heat kwa Msajili otherwise tungesikia pingamizi amelitupilia mbali from day one kama ilivyozoeleka.
 
Mzee Tendwa safari hii wamemkamata pabaya, ingekuwa malalamiko hayo yametolewa na ccm kwa chama kingine, Tendwa angemwaga ung'en'ge hapo mpaka watu wakashangaa. Sasa Mkwewe CCM ndiye mtuhumiwa Mzee Tendwa anatafuta namna ya kupiga propaganda then changa la macho then usije shangaa kibao kikageuziwa hao CHADEMA. Nimjuavyo mzeeTENDWA atasema sheria ya gharama ya uchaguzi haijakiukwa.samahani sana mzee Tendwa kama huo sio uamuzi wako utakaoutoa baada ya siku 5.
 
Hii ngoma inaweza ikafika hadi Mahakama ya Rufaa . . . . Lissu na Marando na CHADEMA hawatakubali. Uchaguzi unaweza kuahirishwa na sheikh Yahya akapanua soko lake kwa utabiri uliotimia.

Tutaona mengi mwaka huu.

Hakuna utabiri wowote hapo, ila itakuwa mbinu mkakati nyingine ya CCM ili wapumue na kisha kupata ushindi. Si unakumbuka 2005, walibanwa kwenye kona hasa nafasi za ubunge. Lakini apokufa Mar Mzee Jumbe, na uchaguzi kuahirishwa ndiyo ikawa ahueni kwa CCM.

Kwasasa hivi wamebanwa kwenye kona haina mfano. Ndiyo maana wanatumia mbinu zote ikiwa kuwadanya watz kwa habari za uongo, kuzuia vyombo vya habari kuhujumu mitandao ya simu mpaka ya internet ambayo wanajua itawasaidia CHADEMA kwa namna moja au nyingine kupata ushindi.
 
hii ni sawa na kesi za mafisadi zilizofunguliwa kwa ajili tu ya uchaguzi baada ya hapo hutakuja kusikia kamwe kama kunma kigigi wa kweli aliyechukuliwa sheria yoyote.....kamwe
 
Au Chadema wakubali yaishe tu?

Ya nini malumbano; Ya nini maneno;
Najiweka pembeni; Naepuka msongamano;
Bora nitulie; Ningoje chakula nile;
Mola nijalie; Yasijirudie tena.

 
Kwa nini uchaguzi uahirishwe mbona kuna wagombea ubunge wamewekewa pingamizi na kunawaliopita bila kupingwa na uchaguzi unaendelea.

Jina la JK likitolewa uchaguzi unaendelea kama kawaida hata kama kungekuwa hakuna wagombea wengine na akabaki mmoja still huyo angepita bila kupingwa.

Ila kwa hili I can guess heat kwa Msajili otherwise tungesikia pingamizi amelitupilia mbali from day one kama ilivyozoeleka.

Hawawezi kulitupa hilo pingamizi from day one kwasababu wanajua reaction ya wanachi itakuwa kubwa wakati ukweli upo.
Wanachofanya ni kusikilizia hali ikoje(delaying tactic), huku majukwaani wakimwaga upupu butu kisha waje na maamuzi waliyojadili Tendwa + CCM (I guess Msekwa, maana Makamba hapo ni maamuma)
 
Tendwa kazi unayo tunangoja maamuzi yako !
 
Chadema hawana hoja na nina imani hawataridhika na nimegundua chuki zenu ni za kidini mnamchukia JK kwa dini yake nilikipenda sana chama chenu ila ubaguzi wenu wa kidini umenifanya niwasikitikie nyie sio watu wazuri mnaweza kusababisha mauaji ya kimbari ANGALIENI SANA
 
Amini amini nakuambieni, kuna watanzania wanatuona wasaliti sisi tunaokesha kusaka uhuru wa kweli na ukombozi halisi dhidi ya wakoloni weusi.

Chama Cha Mapinduzi kimepoteza dira na mwelekeo. Huo ndo msimamo wa katubu wao mkuu aliyepita (RIP H. Kolimba). Na tangu siku hizo mpaka leo hakijapata mwelekeo zaidi ya kupapasa gizani na kupiga kelele kuwa kimeuona mwanga
 
Back
Top Bottom