Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
mimi ninamaswala haya kwa dk slaa
1)endapo atashinda uchaguzi na kuwa rais nini atafanya katka kurudisha mahakama ya kadhi
2) vipi kuhusu swla la oic
3) vipi kuzibadilisha kuwa siku za mapumziko kuwa j3 na j4 badala ya j1 na j2 au kuongeza ijumaa?

Hivi huyu jamaa huwa anaandika kwakuwa ana lakusema au anaandika kwakua anataka kuandika?
 
Kwa kila kiwango katika medani ya siasa na uelewa wa mambo, Dr Slaa amempita kwa mbali mno, tena sana, ni kama umbali wa anga na nchi kavu. Tangu Dr. Slaa alipotangaza majina ya watuhumiwa wa ufisadi Mwembe yanga Dar es Salaam, hadi bungeni ambapo ameweka sawa masuala mbalimbali katika vifungu vya sheria na bajeti ya nchi. Hivi karibuni Dr. Slaa ndiye yeye pekee aliyeona madudu katika sheria ya uchanguzi ambayo JK yeye alimwaga wino bila hata kusoma. JK hatilii maanani kusoma katika misitari ndiyo maana ana uelewa mdogo wa mambo ukilinganisha na Dr Slaa. Kituko cha mwaka ni pale JK alipoulizwa akiwa nje ya nchi kwa nini nchi yako ni maskini wakati inamaliasili kibao. Yeye akajibu kwa mbwembwe kwamba hajui anashangaa. Sasa mtu anakuwaje rais kama hajui matatizo ya nchi? Dr. Slaa alishaona tangu mwanzo kwamba nchi yetu inakwamishwa na ufisadi ndio maana yeye na Tindu Lisu wakajitoa mhanga kuwakabili watuhumiwa wa ufisadi 11. CCM msiwe wanafiki, Dr. Slaa yupo juu sana, ameongoza nchi kwa mawazo mazuri japo alikuwa bado Mbunge. Akiwa rais neema imewashukia Watanzania.
 

You are spot on.........mgombea urais ana influence sana kwenye wagombea ubunge.....na mambo yalivyo mwaka huu weneye hela watapiata CCM hivyo CHADEMA ijipange mapema kupick up potential candidates watakaoachwa CCM....my take ni zaidi ya 50.....hatuhitaji tu rais wa upinzani bali idadi ya kutosha ya wabunge kuibana serikali maana sasa JK atakuwa anashuka mlimani (2010-2015) kama atashinda....sadly hiki huwa kipindi kibaya sana maana marais hawana woga tena wa kutochaguliwa....Mwinyi(1990-1995) madudu kibao CHAVDA,CIS,etc....Mkapa(2000-2005) RADA,JET,EPA,KIWIRA,NYUMBA ZA SERIKALI etc.....Kikwete??????
 
Ndugu Wanajamii forum,

Kwanza napenda kumpongeza mheshimiwa Slaa kwa uamuzi wake,

Lakini nimesikitika kwa uamuzi huo kwa hali halisi ya siasa za Tanzania hawezi kushinda na tutakuwa tumempoteza mchangiaji mzuri sana kwenye bunge lijalo,ninani atakuwa na ujasiri wa Dr.Slaa wa kukosoa sera mbovu za CCM na kuibua maovu akiwa nje ya Bunge,na pia atakuwa hajawatendea haki wapiga kura wake wa Karatu,angesubiri mwaka 2015 hapo angekuwa amecheza kete nzuri,

Ninahofia Slaa asije akaja kufilisika kisiasa kama Mheshimiwa Mrema,

Elisante Yona
 
Source: Mtanzania
 
habari zilizopatikana sasa hivi zinasema kwamba dk. Slaa ndiye mgombea urais wa chadema mwaka 2010.


kikao kilichomchagua dr. Slaa kuwa mgombea urais wa chadema

more to come
hongera dr slaa kwa maamuzi yaliyo sahii kwa wakati sahii
 
Mimi nazani kadri siku zinavyokwenda Dr Slaa atafafanua yote. Tusubiri tuone
 

Slaa kugombea na kushinda au kutoshinda karatu ni matakwa ya wananchi wa karatu.Wananchi wa Karatu wanaweza kuamua kuwa na msimamo uleule na kuwashangazeni.Kinachokuhakikishia karatu kuchukuliwa na CCM ni nini endapo Slaa atagombea Uraisi?

Kuacha kugombea Urais na kubaki kugombea ubunge ili hali wananchi wa Tanzania na wanazuoni wanamwomba agombee Uraisi utakuwa ni ubinafsi na Uchoyo.

Dr. slaa amesikiliza kilio cha watanzania na amechagua fungu lililo jema!

Bila shaka hii siyo habari njema kwa CCM kwa upande wa Urais na Slaa anaweza kuwashangaza wengi kwa kushinda Uraisi, kwani hata uwizi wa kura una kikomo chake!
 
yaani kama kweli viongozi ni chaguo la mungu, basi naamini dr. slaa ndio chaguo sahihi na tumuombe mungu atupe slaa wetu.
 
Lol! kazi ipo hapo Itabidi mama ajivue usisiemu hapo hana jinsi inabidi awe begakwabega nu mumewe....:welcome: CHADEAMA Mama Slaa
 

Ndugu Elisante,
Mimi naamini kabisa kuwa kwa hali ya maisha yalivyo sasa, Dr Slaa atakuwa changamoto kubwa, kamwe hajafanya makosa, na wala hajawaangusha wana Karatu, CHADEMA itashinda tena huko. Kwa Slaa kugombea urais kutaongeza idadi ya wabunge wa upinzani Bungeni kwa hiyo chama tawala ccm (kama kitashinda) kitakuwa na wakati mgumu sana bungeni. Na pia tukumbuke ukweli kuwa masuala ya ufisadi yalilipuliwa kwenye viwanja vya Mwembe Yanga na si bungeni, kwa hiyo Slaa anaweza kuwafanyia watanzania akiwa popote. Nenda Slaa! Nenda Watanzaia tuko bega kwa bega, kuibwaga CCM inawezekana hata sasa, wananchi tuamke tuikomboe nchi yetu kutoka kwenye makucha ya ukoloni wa mafisadi. PAMOJA TUTASHINDA
 
Jamani huu ni muda wa dhahabu tuliokuwa tunausubiri,piga simu sasa,kama uko nje piga simu sasa,kama uko humu humu bongo ongea na jamaa na ndugu,kila mpenda mabadiliko tupatie kura 20++ kutoka vijijini,ni muda wa vitendo sasa,waelimishe,wapige kura ya mabadiliko,this is what we have been longing for for a long long time,we are always slow at taking chances but let's take this one!...Go go slaa Go go wind of change!
 

Nadhani umefafanua vizuri alipofilisika Mrema akaja Slaa....basi atakuja mwingine kwa hiyo tumwache agombee
 
Source: Mtanzania

Hivi hili gazeti "mtanzania" huwa watu wanatoa hela kulinunua au linatolewa bure???????? Why it is this low?????

Habari za ndani zilisema Dk. Slaa aliingia makubaliano yasiyo rasmi na baadhi ya maaskofu Katoliki alikokuwa kifanya kazi kwenye Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na anategemea kutumia ukaribu wake na maaskofu hao kupigiwa ndogo ndogo aingie Ikulu

Hivi waziri Mkuchika yuko wapi kwenye hili, je ingeandikwa na gazeti kwamba JK aliingia makubaliano yasiyo rasmi na baadhi ya mashehe kupigiwa ndogo ndogo kuingia ikulu serikali ingekaa kimya????

Kwa nini mitizamo ambayo inaonekana ni binafsi na habariz zisizothibitiswa zenye nia na sumu mbaya kabisa ya udini zinazidi kuwa popular siku hizi????????

SHAME ON YOU "GAZETI LA MTANZANIA"
 
I WISH DR SLAA AWE RAIS WETU,MUNGU MTANGULIE NA AFANYE MIUJIZA, Halafu tufanye yafuatayo:
1. Tuishinikize tume ya uchaguzi kutoa majina ya wapiga kura mapema kwa kila eneo walilojiandikisha ,make wana mchezo wa kupeleka jina sehemu nyingine( hasa sehemu ambazo ni tishio kwa CCM)ukienda kuangalia jina lako unakuta halipo, wanasema watashughulikia mara saa kumi na mbili inafika muda wa kupiga kura unaisha unakuwa umekoswa haki yako ya kupiga kura, hivyo watoe majina mapema na kwa usashihi ili wapiga kura wajue mapema kama majina yao yapo kwenye kituo walichojiandikishia.
2.Serikali iruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wapige kura za kumchagua Rais majumbani kwao kwani wengi wamejiandikisha kwenye vyou vyao( DSM,Morogoro,Dodoma ,Iringa na mahala pengine) lakini Vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi hivyo watashindwa kupiga kura huko majumbani kwao watakapokuwa likizo.
3.CUF na NCCR Mageuzi viunganishe nguvu na CHADEMA,Lipumba amuachie Dr Slaa kwani kwa sasa nyota ya Dr Slaa inang'ara sana kuliko Lipumba,Dr anakubalika sana kwa sasa, tuachane na vyama vingine waganga njaa( TLP,UDP na vingine vilivyopo tu kwenye orodha ya msajili wa nyama,havijulikani kabisa nchini).
4. Sisi wenye uelewa na machungu ya nchi hii tuwahamasishe ndugu zetu(Kila mmoja ahamasishe ndugu zake huko vijijini )waache woga kwamba vyama vya upinzani vikiongoza nchi kutatokea ukosefu wa amani.Hizo ni propaganda tu za akina makamba na CCM yake.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…