Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Huyu Izak ni mawazo yake na yana ukweli wake japo maneno katumia maneno ambayo mimi sijayakubali. Lakini kwanza sisi wenyewe tulio na Imani na Dr. slaa, siku ya kupiga kura tuende tukampigie, na pia tuwaelimishe "WADANGANYIKA" wanaoshabikia CCM huku wakinusa harufu tu ya mipesa iliyojaa mifukoni mwa "MAFISADI" vigogo wa CCM. Wati kama Izak jamani badilikeni hii nchi haitafunwi tena ila inamezwa nzimanzima.
Tumepewa chance ya kubadilisha mwaka huu, tumepewa yule "MKOMBOZI" Je, Tutafumba macho tuendelee kuchagua mtu anayewadharau wafanyakazi na kuwafanya wajinga na hawana maana.?
PLEASE WAKE UP!!!
CHANGE PLEASE!!!!!
 
Kama wewe unaona Dr. Slaa kama M/kiti wa kamati ya bunge ya kudumu alifaa sana na aliwafaa sana wana-Karatu basi sasa umefika wakati wa yeye kushughulikia mambo yote na wananchi wote tukiwemo sisi wana-Bukoba mjini. Yaani atufae katika nyanja zote na watanzania wote.

Nikiombwa nitoe sifa zako, nitasema: you are a coward, chickenhearted, perssimistic, myopic, not pragmatic, traitor, hypocrite, litmus paperlike, chameleon, a branch of tree to be pruned!! Lakini una bahati sijaombwa kufanya hivyo!!!!
 
Huna lolote zaid ya unafiki. Watu wa aina yako ndiyo wameifanya nchi hii iliwe na watu wachache. Hivi lini utaacha kujiona kuwa wewe ni panzi na huwezi kuyakabiri majitu.

binafsi sikutegemea kama slaa atagombea urais,lakini na heshimu maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA, ila naona Dr.Slaa na Chadema walikuwa bado kujipanga kumsimamisha DR Slaa,karata wameicheza pabaya kweli,ndio maana hata wanachi wa Jimbo la Karatu wanapanga kupeleka malalamiko makao makuu ya chadema ikiwezekana watengue uamuzi huu,changamoto na vita dhidi ya ufisadi Bungeni zitapungua bila Mh.Dr.Slaa
 
Well hii sio habari njema kwa Chadema kihivyo. Jimbo la Karatu linarudi CCM believe me. Na kwa taarifa tu ni kuwa kweli Dr. Slaa hawezi kupata urais kwa sasa. Kama yuko kupima anakubalika vipi ili agombee 2015 sawa.

Kwa nini tumeweka fikra hasi mbele zaidi? hebu fikiri kama tunamkiri kuwa Dr. Slaa ni mtu muhimu kwenye Bunge kwa nini basi tusimuunge mkono kwenye kugombea urais? watu weeengi wanalalamika kwamba Bunge litamkosa mtu muhimu wakati mtu muhimu huyohuyo anatuomba tumuunge mkono kwenye nafasi ya uraisi ili apate fursa ya kulitumikia taifa hili kwa ufanisi zaidi, lakini sisi tunamvunja nguvu kuwa hatopata kitu, umuhimu wake uko wapi bbasi!

Kuhusu jimbo la Karatu kwenda CCM sina hakika sana kwana hawa jamaa wanasifa moja na historia nzuri sana ya kuwa na msimamo. Wambulu wanayo historia ya kumpinga Nyerere (marehemu) wakati fulani huko nyuma. Labda na wao waamue kuzira na kuipigia kura CCM kwa lengo la kuikomoa CHADEMA.
 
Ninazindua kampeni rasmi, Dr. Slaa, anaifaa nchi hii iliyofikishwa hapa ilipo, ninaomba aungwe mkono, kwani ninauhakika kabisa kwa kura atakazopata si haba . Viti maalumu vya ubunge pia vitaongezeka sana kupitia Dr. Slaa.
 
jamani jmani mawazo yake ni sawa sawa,hapa kupata uraisi inataka matayarisho thabit, watz wengi nje ya miji hawajui kitu chochote zaidi ya nyerere na chama chake, hivyo kuwin urais kwa asie ccm kwa sasa ni vigumu jamani, huyu bwana hajakosea hata, maana wengi ndivyo wasemavyo huku mitaani. pia msisahau wezi wa kura wa ccm wao ni mahiri kwa hilo je chadema na wapenda mapinduzi wengine wako nchi nzima kusimamia wizi wa kura? mfano mzuri 2005 felix alishindwa arusha na upinzani je mliona matokeo ya wizi?
mimi nimesikitika sana kwa uamuzi huu, wa dr. slaa maana atarudi mtaani sasa nafasi yake ilikuwa bungeni tu, sasa waliemsimika hawezi toboa ngo' kwa ccm na vitimbi vya.
jamani mi naona chadema mmoja amepewa kitu ili wamdanganye dr. aweze tyu kuondoka bungeni na wamefanikiwa, jamani jamani sikutegemea dr.slaa atadangwanywa
 
Kwa taarifa yenu wote mliona na mashaka kuwa jimbo la karatu linarudi ccm baada ya dr.slaa kugombea urais, mfute hayo mawazo, anakuja mtu ambaye atashinda kwa kura zaidi ya alizopata dr. Mwaka 1995. Mimi ni mkazi wa karatu tunajua mbunge wetu ni nani kama chadema watampitisha basi ushindi wa chadema hapa ni hakika na jk hapati diwani wala mbunge hapa karatu. Msituone wairaqw wa karatu hatuna cha kusema mtusemee. Tuna watu wengi wenye sifa kama slaa, tunaomba mpigieni kura slaa tubadili nchi kiuchumi. Tumesikia mengi kuwa anaundiwa zengwe kuwa ana udini katumwa na katoliki jamani mnasahau wosia wa baba wa taifa? Dini ya mtu inatuhusu nini? Ni mtanzani mchango wake ameuonyesha kwa miaka 15 mnataka nini kwenye dini yake? Wengine wanahoji mbona mkewe ccm kwani nyie mwataka nini kwa mkewe. Siasa siyo vita jamani, tunajenga nchi moja tusigombee fito.
Nawasilisha mwenyekiti kwa niaba ya wana karatu.
 
Mie nafikiri kuna tatizo la kimsingi juu ya uelewa wa watu wa mjini na sehemu za vijijini. Nasema haya kwa kuangalia hasa zaidi ya mjini japo tunapenda kusema sana watu wa vijijini kuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na siasa za nchi hii, lakini kwa hili napenda niwasifu Watanzania wote waishio vijijini kwa kuleta mabadiliko katika siasa za TZ. Tuangalie Bunge lililopita wabunge wote wa vyama vya upinzania wametokea majimbo yasiyo ya mjini. Kwa mfano Karatu, Tarime, Kigoma nk. Dar es Salaam ambako watu wanajidai wanaelewa mambo wabunge wao wote ni CCM, na inaelekea watu wa Dar wanafurahia hali hii hali ikiwa jiji linanuka kwa uchafu na foleni kibao bila ufumbuzi makini toka kwa Madiwani na Wabunge wa CCM.
Kwa hivyo mara nyingine tukujadili siasa za Bongo tusiwabeze watu wa vijiji kuwa hawana uelewa wa kutosha ilihali sisi wa Mjini ndo mbumbu wa siasa na hatutaki kuonyesha mabadiliko kwa vitendo.
Big Up Dr. Slaa you have my Vote!!
 
JAMANI WATANZANIA, TUMPE KURA ZETU DR.SLAA NI MTANZANIA WA KWELI NA ANAOUCHUNGU NA MAENDELEO YA NCHI HII. SI MTU BINAFSI. NIMWONAVYO MIMI ANATUFAA KAMA KWELI TUNATAKA MAENDELEO YA KWELI KWA WATANZANIA.

DR. SLAA, GO AHEAD!

Nimeambiwa na Mabere Marando pia yupo nyuma yako. Tupo nyuma yenu pia!!!!!!!!
 
Kweli mbuzi wa masikini hazai na akizaa anazaa mchanganyiko wa kiziwi na mwendawazimu kipofu. Waliomteua Dr Slaa kuwa mgombea urais huku wakijuwa fika kwamba atashindwa na hivyo kutokuwa mbunge hawakuitendea haki Tz hata kidogo. Kadhalika Dr Slaa ameingia kwenye mtego wa CCM kwa kukubali kujitoa kwenye ubunge na kujiunga na safu ya akina Lipumba, Mrema, na wagombea wengine wanaoishi kwa ruzuku. Imenikatisha tamaa na imenisikitisha sana. CCM kwa makosa ya wapinzani imelamba dume tena. Badala ya kumwacha Mbowe aendelee kubwabwaja na kuwaacha Zitto na Dr Slaa bungeni waendelee kutoa chachu ya maendeleo, bunge lijalo halina mpizani mwingine isipokuwa Zitto ambaye sasa midomo yake imepigwa nchi 12 za ulimbo. Swali langu kwa Dr Slaa na CHADEMA: Inaingia akilini kuuza pikipiki ili mnunue fimbo?

Sijui kwa nini watu wanafikiria sana kuwa mtu kuwa bungeni ndipo mahali pa kubadilisha mambo. Dr Slaa kwa miaka mitano yote amesema Bungeni kuhusu Meremeta, Tangold, Kagoda na mengine, nikuulize ni lipi limefanyiwa kazi. Dr Slaa huyo huyo alipoona kuwa bungeni mambo hayaendi akaenda mwembe Yanga akaanika ufisadi wa EPA na ukafanyiwa kazi. Zitto Kabwe alizungumza kuhusu Buzwagi akiwa bungeni mpaka akfungiwa vikao, leo niambie suala la Buzwagi limefanyiwa nini? ni mpaka alipotoka bungeni na kwenda kwa wananchi ndipo athari ikatokea, mawaziri wakaanza kuzomewa. Siasa si ndani ya bunge, siasa ziko nje ya Bubge. Go Slaa, tuko nawe, hata akiwa nje ya Bunge Slaa ni moto, nani asiyekumbuka swala la sheria ya uchaguzi JK aliposaini bomu? Slaa alikuwa BUngeni? hapana, huku nje ndiko kunako peleka hija Bungeni. Kwa Slaa kuwania Uraisi, kwanza atashinda, kama uwanja utawekwa sawa, pili idadi ya wabunge wa upinzani bungeni itakuwa kubwa na nchi itakombolewa kutoka kwa mafisadi.
 
Napenda nikupe taarifa kuwa hata ugonjwa wa ukimwi ulioshindikana hivi sasa umepatiwa dawa na wagonjwa ukimwi wanapata ahueni, hivyo usijidanganye. In the meantime ngoja kampeni zianze MgonjwaUkimwi, utashuhudia moto ambao haujaonekana toka tupate uhuru ! Mimi kwa hivi sasa sina hata wasi wasi na ninapata usingizi mwororo nikisubiri siku Dr.Slaa atakapouwasha - CCM kwa mara ya kwanza itajikuta uchi kabisa kwani macho ya wananchi yatafunuliwa, we subiri.

Mkuu Mg3,
Be realistic na acha siasa za JF za kwenye internet....wala sio siri kwamba CHADEMA haija enea nchi nzima na itachukuwa karne kadhaa kuenea. Hili halipingiki. Kampeni za miezi kadhaa kamwe haziwezi kuwashawishi wanavijiji wampigie kura Dr Slaa ambapo kwao neno CHADEMA ni msamihati wa kichina.

Nasikitika sana kwamba CHADEMA wanaishi katika Tz yakufikirika. Tz ya internet, Tz ya JF. Inasononesha kuona kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wanakesha JF badala ya kukesha mikoani na haswa vijijini wakijaribu kumomonyoa nguvu ya CCM. Wala sitashangaa kusikia kwamba uamuzi wa CHADEMA wa kumuua Dr Slaa kisiasa ulikopwa hapa JF.

Tatizo sio kwamba CCM haiwezi kuondolewa madarakani, tatizo ni kwamba HAKUNA UPINZANI wa kuiondoa. Upinzani wa kweli unaanza na kuimarika bungeni na sio IKULU kama CHADEMA wanavyotaka tuamini. Cha ajabu vyama vya upinzani tangu vianze vimekuwa "vikiua" wabunge makini kwa kuwafanya wagombee urais, na matokeo yake CCM inaendelea kujiimarisha. Ebu fikiria bunge ambalo lingekuwa na watu kama Lipumba, Seif Sharif, Mrema, Dr Slaa, Zitto, Mbowe, Marando, na vigogo wengine wa upinzani CCM ingekuwa katika wakati gani? CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinasahau kwamba umaarufu na ukomavu wa viongozi wao umetokana na kushiriki kwao katika Bunge na sio vinginevyo.

Kama kweli wana JF tupo hapa kwa maslahi ya kujenga nchi yetu na sio kujenga interests zetu, na kama kweli tunataka kuiondoa CCM madarakani kwa kuleta upinzani wa kweli ni lazima tuupinge uamuzi wa CHADEMA kumtoa Dr Slaa Bungeni. Kwasababu upinzani bado hauna nguvu katika maeneo mengi ya nchi silaha pekee tuliyonayo ni kuwa na wabunge wengi na makini Bungeni.
 
Huu ni mtizamo wako tu na wala hauwezi kuwa ukweli. Eti itachukua karne kadhaa (yaani miaka zaidi ya mia moja) kwa chadema kuenea nchi nzima? Ama kweli ccm mna guts za kuropoka

Nasikitika sana kwamba CHADEMA wanaishi katika Tz yakufikirika. Tz ya internet, Tz ya JF. Inasononesha kuona kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wanakesha JF badala ya kukesha mikoani na haswa vijijini wakijaribu kumomonyoa nguvu ya CCM. Wala sitashangaa kusikia kwamba uamuzi wa CHADEMA wa kumuua Dr Slaa kisiasa ulikopwa hapa JF.

Kukesha JF?

Nilijua tu utaenda kwenye porojo kama kawaida yako. Yaani Tanzania ambayo kuna mitandao ya mawasiliano karibu nchi nzima (nikimaanisha mikoani) itamzuia nani kutokwenda mikoani akiwa na laptop yake na bado akawa anapost JF

Inaonekana kinakuuma sana kuona wana chadema hapa JF - hasa ukichukulia kuwa waropokaji wa ccm kina makamba hawana uwezo wa kuandika chochote hapa.

Tatizo sio kwamba CCM haiwezi kuondolewa madarakani, tatizo ni kwamba HAKUNA UPINZANI wa kuiondoa. Upinzani wa kweli unaanza na kuimarika bungeni na sio IKULU kama CHADEMA wanavyotaka tuamini. Cha ajabu vyama vya upinzani tangu vianze vimekuwa "vikiua" wabunge makini kwa kuwafanya wagombee urais, na matokeo yake CCM inaendelea kujiimarisha. Ebu fikiria bunge ambalo lingekuwa na watu kama Lipumba, Seif Sharif, Mrema, Dr Slaa, Zitto, Mbowe, Marando, na vigogo wengine wa upinzani CCM ingekuwa katika wakati gani? CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinasahau kwamba umaarufu na ukomavu wa viongozi wao umetokana na kushiriki kwao katika Bunge na sio vinginevyo.

kama kawaida ya mafisadi, always dismissive.

Mkapa alisema wapinzani wana wivu wa kike, Kikwete akasema kuwa ni kelele za chura mlangoni. Lini wanaccm mtatoa credit kwa upinzani?

Kama kweli wana JF tupo hapa kwa maslahi ya kujenga nchi yetu na sio kujenga interests zetu, na kama kweli tunataka kuiondoa CCM madarakani kwa kuleta upinzani wa kweli ni lazima tuupinge uamuzi wa CHADEMA kumtoa Dr Slaa Bungeni. Kwasababu upinzani bado hauna nguvu katika maeneo mengi ya nchi silaha pekee tuliyonayo ni kuwa na wabunge wengi na makini Bungeni.

Wewe interest zako zinajulikana hapa, una maslahi yapi ya kujenga nchi na wana JF? BTW ni wana JF wapi hao unaowajumuisha kwenye hili?

Kisha ona unavyojigonga mwenyewe, kwanza unasema kuwa itachukua karne kwa chadema kuenea nchi nzima, na kisha unasema kuwa tuongeze wabunge wengi bungeni. Hao wabunge wengi wataingia kutokea maeneo "machache" tu ambayo upinzani ni maarufu?

Spin hizi zilizopitwa na wakati zinafaa sana pale lumumba na sio hapa.
 
Watanzania wote mnaoona CHADEMA wamefanya makosa kumchagua Rais wa Tanzania mwaka 2011 yaani NDUGU W. Slaa basi kwenu leo nina ujumbe mmoja mfupi sana.

Kama Komeo ndiyo limeshafungwa. Mtalia, mtaimba, mtacheka, mtaweweta, mta..... wala hakitaeleweka.

Kama Mnawivu, MKAJINYONGE.

Kama mna wasiwasi basi nendeni mkafanye kampeni kali sana ili Dr. Slaa ashinde.

Vingine, mnachoandika ni heri msubiri kwanza hadi matokeo ya uchaguzi yatoke.

Mwisho wa siku, Dr. Slaa hata asipokuwa Rais, atakuwa na muda wa kupitia Tanzania nzima akitangaza operation SANGARA na wakati huo, John Walker kwa kufahamu hahitaji tena kuchaguliwa, nina imani atakuwa anaishi ANGANI huku akitua tu kujaza mafuta kwenye ndege na kutalii nchi moja baada ya nyingine.....
Na nyie mnaomshangilia mtaungana na sisi kusota pale Temeke siku mama zenu, dada zenu, shangazi zenu, wake zenu nk watakuwa wanazalia kwenye SAKAFU kama kukuna kulazwa kwenye kitanda mzungu wa pili na watoto wao (kitanda watu wanne). Fly-over zitapotea kama Rapid busses ambazo zilikuwa zianze sijui mwaka gani?
Kama wewe baba yako ni FISADI au KIGOGO wa CCM, basi una kila HAKI ya kuanza kuhaha maana nina uhakika, chini ya utawala wa Dr. Slaa basi watu kama Mama Mkapa na kigenge chake na MAFISADI, watapanda KIZIMBANI na kujibu wizi wao wote walioufanya. Katika hao, CCM wataongoza kwa kushushwa SEGEREA. Wakilifahamu hili, ndiyo maana MATUMBO MOTO wakisikia Slaa. Wanajifanya eti "Jimbo la Karatu litapotea, atapunguza upinzani bungeni na upupu mwingine kibao - WE DON'T BUY......"

Kama Dr (?!?!?!) Malecela John alivyosema miaka hiyooooo..... ".......YOU CAN GO TO HELL."
 
SLOGAN YA Rais wa Tanzania mwaka 2011, NDUGU W. Slaa.

UKO NA DR. SLAA AU UKO NA MAFISADI

King of Kings, huyu mtu (MS) usipoteze naye muda wako bure......mimi nilishaachana naye tayari. Ni mtu wa kuleta upepo wa kuchafua tu. Nakushauri uwaachie ****** wenzake ndio wawe wanajibizana naye.
 
Mkuu Mg3,
Be realistic na acha siasa za JF za kwenye internet....wala sio siri kwamba CHADEMA haija enea nchi nzima na itachukuwa karne kadhaa kuenea. Hili halipingiki. Kampeni za miezi kadhaa kamwe haziwezi kuwashawishi wanavijiji wampigie kura Dr Slaa ambapo kwao neno CHADEMA ni msamihati wa kichina.

Nasikitika sana kwamba CHADEMA wanaishi katika Tz yakufikirika. Tz ya internet, Tz ya JF. Inasononesha kuona kwamba viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wanakesha JF badala ya kukesha mikoani na haswa vijijini wakijaribu kumomonyoa nguvu ya CCM. Wala sitashangaa kusikia kwamba uamuzi wa CHADEMA wa kumuua Dr Slaa kisiasa ulikopwa hapa JF.

Tatizo sio kwamba CCM haiwezi kuondolewa madarakani, tatizo ni kwamba HAKUNA UPINZANI wa kuiondoa. Upinzani wa kweli unaanza na kuimarika bungeni na sio IKULU kama CHADEMA wanavyotaka tuamini. Cha ajabu vyama vya upinzani tangu vianze vimekuwa "vikiua" wabunge makini kwa kuwafanya wagombee urais, na matokeo yake CCM inaendelea kujiimarisha. Ebu fikiria bunge ambalo lingekuwa na watu kama Lipumba, Seif Sharif, Mrema, Dr Slaa, Zitto, Mbowe, Marando, na vigogo wengine wa upinzani CCM ingekuwa katika wakati gani? CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinasahau kwamba umaarufu na ukomavu wa viongozi wao umetokana na kushiriki kwao katika Bunge na sio vinginevyo.

Kama kweli wana JF tupo hapa kwa maslahi ya kujenga nchi yetu na sio kujenga interests zetu, na kama kweli tunataka kuiondoa CCM madarakani kwa kuleta upinzani wa kweli ni lazima tuupinge uamuzi wa CHADEMA kumtoa Dr Slaa Bungeni. Kwasababu upinzani bado hauna nguvu katika maeneo mengi ya nchi silaha pekee tuliyonayo ni kuwa na wabunge wengi na makini Bungeni.
Katika red nenda kaulize Tarime,Busanda na Biharamuro ndiko utakako pata majibu yake. Kama unadhani watu wanazungumzia mambo kwa kusoma kwenye internet, labda nikueleze kuwa hao wanaweza kuwa na data zinazokaribia ukweli kuliko kuchukua takwimu toka katika majalada ya akina Tambwe Hiza.
 
Katika red nenda kaulize Tarime,Busanda na Biharamuro ndiko utakako pata majibu yake.

Yaani Tanzania ya CHADEMA inaundwa na Tarime, Busanda, Biharamuro, na JF. Tuna safari ndefu kuiondoa CMM madarakani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom