Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Sasa kazi ni moja tu nayo ni kumnadi mgombea huyu makini. Kampeni mbele kwa mbele: mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda - mpaka kieleweke mwaka huu. Hongera Dr. Slaa! Tuko nawe.

mkuu natokea mitaa ya Magu, geita, Burelesele, Nyamongo, Biharamulo na vitongoji baadhi vya huko, story ni moja tu Dr. Slaa yupo juu si kawaida - nimeongea na watu wa kawaida kabisa (Wasio wasomi) - aisee kumdai huyu wala bwana si Kazi - Anauzika. Kinachotakiwa ni kumwongezea ulinzi na kuhakikisha hawatuibii kura zetu.
 
Hata Nyerere alipoacha ualimu pugu kwenda TANU wapo waliomwambia kaingia choo cha kike.....the rest is history of course

Safari_ni-Safari na wenzako hapo juu, mnazisoma hizi news kwa makini au mnabishabisha tu tukubaliane na fikra zenu? Soma kwa makini uelewe news kama hizi. Pia pima joto halisi la nchi kwa kuangalia vijijini ambako 80% ya kura ziko. Tarime na Karatu ni wilaya moja katika zaidi ya 200 nchini, statistically insignificant. Siyo mnakaa kweye laptops/PC mnachagua Rais wenu kwa ku-type hapa JF. Comes October, we will see here at JF.

Dk. Slaa awagawa wengi
• Uteuzi wake wawashtua wengi

na Waandishi wetu

UTEUZI uliofanywa juzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa kumteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, umepingwa vikali na baadhi ya watu, kwa madai utakidhoofisha zaidi kuliko kukiimarisha.
Wakizungumza na Tanzania Daima, walisema Dk. Slaa hakupaswa kuwania urais hivi sasa, kwa kuwa uwepo wake bungeni ulileta changamoto kubwa na mabadiliko ndani na nje ya Bunge kiasi cha kuifanya serikali kutetemeka kila hoja za wapinzani zinapotolewa.
Walisema uteuzi huo haukufanywa kwa kuangalia mazingira yaliyopo, ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji hoja nzito za wapinzani zitolewe bungeni, kama alivyokuwa akifanya Dk. Slaa ambaye kwa muda wa miaka mitano alishikilia hoja ya ufisadi.
Profesa Shaaban Sengo wa Chuo Kikuu Huria (OUT), alisema haoni kama Dk. Slaa amejiandaa vya kutosha kupambana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, kwa sababu alishachukua fomu za kuwania ubunge ndani ya chama.
Alibainisha kuwa maandalizi ni jambo muhimu kwa mgombea makini kama Dk. Slaa, la sivyo anaweza asitimize malengo aliyojiwekea pamoja na chama ambacho mwisho wa siku kinaweza kujuta kwa kuchukua uamuzi wa haraka haraka.
Alisema kuwa Dk. Slaa ana haki ya kuwania urais lakini ni lazima atafakari uamuzi wake ili Watanzania wamuelewe vizuri na kumuunga mkono katika hatua hii ya kuwania uongozi wa juu wa kitaifa.
"Sina shaka hata kidogo na uwezo wa Dk. Slaa, Watanzania tumeshamuona anavyojenga na kuisimamia hoja mpaka matunda yake yanaonekana, lakini sioni kama amejiandaa fresh kukabiliana na Rais Kikwete," alisema Profesa Sengo.
Baadhi ya watu ambao hawakupenda kutaja majina yao wameiambia Tanzania Daima kuwa CHADEMA wameamua kulipeleka Jimbo la Karatu mikononi mwa CCM, ambayo kwa takriban miaka mitano imekuwa ikihaha kufanya mbinu ili kulinyakua jimbo hilo.
Walisema kuwa dhana ya chama hicho kutaka wabunge wengi zaidi wa viti maalumu haitakuwa na maana kama wabunge watakaoteuliwa hawana uwezo mkubwa kama alivyo Dk. Slaa, ambaye kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa upinzani waliweza kuleta mabadiliko kwenye medani ya siasa.
"Wingi wa wabunge si hoja, tuangalie michango yao kwa jamii, unaweza ukawa na wabunge 10 lakini wakashindwa kujenga na kuzitetea hoja, unaweza ukawa na mbunge mmoja akawa anafanya kazi kuliko wao," alisema mmoja wao.
Wakati baadhi ya watu wakipinga uteuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemtangaza rasmi Dk. Willbrod Slaa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za makao makuu ya ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mbowe alisema uamuzi huo ni maazimio ya Kamati Kuu iliyomaliza muda wake juzi.
Mbowe alisema wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kwa pamoja wamekubaliana kupitisha jina la Dk. Slaa katika kinyang'anyiro cha urais ili kuziba ombwe la uongozi wa juu nchini.
"Kamati Kuu ilijiridhisha kuwa Dk. Willbrod Peter Slaa, ndiye mtu pekee anayefaa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, wajumbe wa Kamati Kuu kwa kauli moja walimuomba achukue fomu ya kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
"Tumedhamiria na hatuendi kujaribu, Dk. Slaa amekuwa mwakilishi mzuri bungeni, wote tunafahamu changamoto alizozipeleka bungeni, lakini hoja zake zinapuuzwa na serikali ya CCM, hivyo tumempeleka akawe mtekelezaji na msimamiaji wa hoja," alisema Mbowe.
Mbowe aliwaomba wananchi, mashirika na taasisi mbalimbali kuunga mkono maamuzi ya chama hicho kwa kumpigia kura za ndiyo Dk. Slaa ili kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi.
Alibainisha kuwa uteuzi wa Dk. Slaa kuwa mgombea urais wa chama hicho umezingatia taratibu zote za kichama, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanachama wa chama hicho pamoja na wadau wa masuala ya siasa.
Akijibu swali lililoulizwa kuwa ikiwa wanachama wengine watajitokeza kugombea urais kupitia chama hicho watapewa kipaumbele gani na kwanini awe Dk. Slaa tu. Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kamati Kuu imefikia uamuzi huo kutokana na umakini wa Dk. Slaa.
"Nafasi ya rais si ya kuchezea na wala si ya kukimbilia, hata hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa ukiona mtu anakimbilia urais huyo atakuwa na dosari. Dk. Slaa hakuomba kugombea, ameombwa na kamati kuu. Hivyo tumechagua mtu makini ambaye tunajua kuwa atakuwa rais wa Tanzania ifikipo Oktoba 31, mwaka huu," alijigamba.
Alisema wananchi wa Karatu watapatiwa mbunge mwingine makini kutoka CHADEMA atakayeziba kikamilifu pengo la Dk. Slaa bungeni kwa kujenga hoja zenye mashiko kwa masilahi ya Watanzania wote.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe alisema kamati kuu pia iilipokea, kujadili na kupendekeza kwa Baraza Kuu rasimu ya Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.
Alianisha kuwa wajumbe wa kikao hicho wamejadili na kupitisha taratibu zilizopendekezwa na Baraza la Wanawake (BAVICHA) za kuwateua wabunge wa viti maalumu.
Aidha, ilipokea, kujadili na kuzingatia taarifa ya utafiti kuhusu mgombea urais kupitia chama hicho kwa mujibu wa katiba yao.
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alisema Dk. Slaa si tishio kwa mgombea wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, aliyechaguliwa kwa asilimia 82 ya kura mwaka 2005.
Aliongeza kuwa Dk. Slaa ni mbunge, hawezi kufananishwa na kiongozi mkuu wa nchi aliyefanya mambo mengi makubwa katika kipindi cha utawala wake wa miaka mitano. "Dk. Slaa hawezi kuwa tishio kwa Kikwete, hayo ni matusi kwa CCM na mgombea wetu, mbunge huyo ni tishio kwako na wengine ambao si makini," alisema Makamba.
 
Hata mimi nakuunga mkono kwa hayo uliyosema tumuongezee nguvu tu na kulinda kura zetu nilidhani itakuwa shida kwa vijiji lakini nimegundua ni mpeto tu.
 
Mixed views greet Slaa's entry into October presidential race Thursday, 22 July 2010 08:29

By Frank Kimboy
THE CITIZEN

Mixed feelings have greeted the Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) decision to appoint the Karatu Member of Parliament, Dr Willibrod Slaa, as its presidential candidate in next October’s General Election.

While some hailed the move as important for strengthening the opposition in parliament, others have described it as Dr Slaa’s political suicide.

However, the ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), has welcomed the entry of the vocal MP. The CCM ideology and publicity secretary, Capt (rtd) John Chiligati, told The Citizen yesterday that they welcome Dr Slaa in the fray.

“It is the voters who are going to give the verdict on October 31... CCM is not afraid of any person as it is well prepared,” he said.

But many of those who spoke to The Citizen lauded the Chadema decision to request Dr Slaa to vie for the top post in the country’s leadership.

Nevertheless some were sceptical saying if he loses, it will deal a big blow to the opposition camp in parliament.

Mr Ayubu Rioba, a University of Dar es Salaam lecturer, lauded Chadema for the decision saying that Dr Slaa will give President Jakaya Kikwete stiff competition in the election.

“Prior to this decision by Chadema most people thought that President Kikwete will have a smooth ride in his bid to retain the seat… but now that Chadema has nominated Dr Slaa things will be very much different,” Mr Rioba said.

He added that even if Dr Slaa fails in his bid he will continue to be a very distinctive citizen because of his passion for spearheading the war against corruption.

“If he managed to stand out among more than 300 MPs, I can’t see why he cannot do the same even if he is out of the law making body,” he said.

The leader of official opposition in the parliament, Mr Hamad Rashid Mohamed, wished Dr Slaa the best of luck in his bid. However, he was quick to note that the opposition camp in parliament will be affected should Dr Salaa not bounce back.

“We should respect the decision made by Dr Slaa and his party… but it is obvious that his absence in the house will be a blow to our camp,” Mr Mohamed lamented.

The Chadema national chairman, Mr Freeman Mbowe, said the decision to ask Dr Slaa to bear the party flag was reached after extensive and thorough consultations.

He said Dr Slaa and his running mate would be confirmed by the party’s general assembly scheduled for August 12. He explained that Dr Slaa would be the party’s sole candidate for the presidential post.

Mr Mbowe said Chadema will make sure that it defends the Karatu constituency by nominating an equally competent candidate to replace Dr Slaa who has reigned in the constituency for the last 15 years.

Mr Mbowe added that Chadema will also do everything in its power to make sure that they will defeat President Kikwete in the coming election.

A renowned academician and political analyst, Mr Bashiru Ally of University of Dar es Salaam, said although many people tip CCM to win in the election, with a very popular candidate and good strategy Chadema might outdo CCM in the election.

He also commended the decision saying that even if Dr Slaa will lose the election the decision might benefit Chadema in the long run.

Prof Issa Shivji okayed the decision saying: “I don’t see anything wrong with the decision… even if he lost in his bid and is not appointed to become an MP I don’t see any gap created by his absence in the parliament.”

But the Tanzania Labour Party (TLP) national chairman, Mr Augustine Mrema, asked Dr Slaa to rethink the decision. He said rather than him vying for the presidency he should have advocated for a constitutional amendment to enable someone to vie for both presidential and parliamentary seats.

Our attempts to reach Dr Slaa for his comments did not bear fruit as his telephone went un-answered.
 
Kuna suala moja nashindwa kukubali kuamini. Bado wapinzani wana imani na kikwete. Kwa nini na wao wamesimamisha wagombea urais wakijua hawatashinda? Ni ujinga na unafiki wa wapinzani kila mtu kutaka kurarua kipande cha ikulu. Wanamwonea huruma dr. Slaa kwani ubunge walimpa wao? Hata hao wanajimbo wake hawana imani nae kuhusu urais? Wawe na mawazo endelevu tu kwani haya mambo hayahitaji subira hivyo
 
Hongera CHADEMA, Hongera DR Slaa, tupo pamoja nawe tunakuombea kwa Mungu, naamini atakupigania. Watanzania tunahitaji mtetezi wa kweli. Wachambuaji wengi pamoja na wasomi wengi wanazungumzia Ubunge Ubunge, lakini maana ya Chama Shindani ni Kushika Dola na Kuongoza nchi. Imagine mnachagua mtu asiye makini na akashida ni nani wa kulaumiwa? CCM walichagua mtu asiyemakini angalia nchi inapokwenda na mpaka leo wamekubali kuziba masikio yao wamemrudisha tena. Tuombe Mungu afungue watanzania akili zao tupate Rais Mwema. Mungu ibariki Tanzania.
 
..CCM wameshajaribu uongozi kwa kutoa maraisi 4.

..hali ya maisha ya Watanzania kipindi chote imekuwa mbaya. It is time for a change.

..kura yangu nampa Dr.Wilbrod Slaa wa Chadema.
 
Ni vema akangoja 2015 kwani jinsi hali ilivyo uwezekano wa kushinda ubunge ni mkubwa kuliko urais. Isije ikawa mbinu ya mamluki kutaka kupunguza nguvu ya upinzani bungeni

2010 ndiyo mwaka na kipindi tulichokisubiri kwa miaka 49 iliyopita. Kama Mwenyenzi MUNGU aishivyo, hatutasheherekea miaka 50 ya uhuru wa taifa ta Tanganyika tukiwa bado watumwa.
 
uwezekano wa Dr Slaa kushinda ni mkubwa, lakini kitu kikubwa kwa sasa ni kuwa na strategy inayo faa, moja ni kuigawa nchi kimkakati na kuangalia shida zao/ au mapungufu ya chama chetu tawala eg dsm hakuna sababu ya kukosa mipango bora ya mji nk, hivyo chadema itaondoa hili, Arusha, mipango miji nayo ipo duni, rasilimali za mkao hazisaidi watu, saana saana ni viongozi wa chama tawala wenye kufaidi hizo rasilimali, hivyo ccm haipo kwa ajili ya kumuendeleza mtazania wa kawaida ndio maana leo hii wachimbaji wadogo wa tanzanite wamenyanganywa maeneo na kuishia kupewa sa/ mboma/kapuya na viongozi wengine kwa kivuli cha ubinafsi shaji, njoo mkoa wa manyara nako kuna mambo yake, nenda kilimanjaro, tanga kuna nini na bandari yao, dodoma na makao makuu yao, sera ya ccm ni kuongeza idadi ya walaji badala ya hizo fedha kuendeleza shule/zahanati nk, nenda mtwara na gesi yao, sasanA sana wafaidikaji ni viongozi na hivyo vivuli vya artumas, nenda kilwa, tanesco , reli, dhahabu, alamasi maliasili ya uwindaji, manunuzi hadithi ni hiyo hiyo, kiwanda cha nyama shinyanga, kagera na uwanja wao wa ndege na kahawa na mifugo, kigoma na reli ya kati na bandari yao, tabora na reli ya kati na dhahabu na tumbaku wanaotajirika ni makampuni ya nje, rukwa aliye faiika ni dr majiyatanga na si wananchi wa kawaida wa pale rukwa, njombe imekuwa kama ni nchi ya makweta na makinda, faida kwa locals hakuna, iringa imekuwa ya lukuvi, monica mbega na mungai, mbinga na msanii komba , tunduru songea to mbambA BAY na michoro ya barabara isiyo isha NA hadithi ya millinium goal challenge na hela za bush, umeme ziro mpaka pale kila kiongozi wa ccm anapokuwa na share kwa wawekezaji ndio umeme utakuja
 
Ni vema akangoja 2015 kwani jinsi hali ilivyo uwezekano wa kushinda ubunge ni mkubwa kuliko urais. Isije ikawa mbinu ya mamluki kutaka kupunguza nguvu ya upinzani bungeni
kipindi hiki ndio kizuri maana mapungufu ya ccm ni makubwa na watu wengi wanayajua, come 2015 watakuwa wameisha funika funika mapungufu yao mengi kwa kuibinafsisha nchi kwa watoto wao kwa fedha walizo tuibiwa, kama walivyo funika funika richmond, buzwagi, rites, netgroup, nakuishia kutupa kapelo, t-shirt, kanga na nauli zakuhudhuria ikutano ya kampeni.
 
Karibu Dr. Slaa. Huu ndo muda mwafaka wa kudodosha kuta za JERICHO (Chama Cha Mafisadi). Naahidi kutumia nafasi yangu kuhakikisha ushindi wenye kishindo kikuu unapatikana kwako na kwa CHADEMA na kwa watanzania wote wanaochukia ufisadi
 
Safari_ni-Safari na wenzako hapo juu, mnazisoma hizi news kwa makini au mnabishabisha tu tukubaliane na fikra zenu? Soma kwa makini uelewe news kama hizi. Pia pima joto halisi la nchi kwa kuangalia vijijini ambako 80% ya kura ziko. Tarime na Karatu ni wilaya moja katika zaidi ya 200 nchini, statistically insignificant. Siyo mnakaa kweye laptops/PC mnachagua Rais wenu kwa ku-type hapa JF. Comes October, we will see here at JF.

Dk. Slaa awagawa wengi
• Uteuzi wake wawashtua wengi

na Waandishi wetu

UTEUZI uliofanywa juzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa kumteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, umepingwa vikali na baadhi ya watu, kwa madai utakidhoofisha zaidi kuliko kukiimarisha.
Wakizungumza na Tanzania Daima, walisema Dk. Slaa hakupaswa kuwania urais hivi sasa, kwa kuwa uwepo wake bungeni ulileta changamoto kubwa na mabadiliko ndani na nje ya Bunge kiasi cha kuifanya serikali kutetemeka kila hoja za wapinzani zinapotolewa.
Walisema uteuzi huo haukufanywa kwa kuangalia mazingira yaliyopo, ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji hoja nzito za wapinzani zitolewe bungeni, kama alivyokuwa akifanya Dk. Slaa ambaye kwa muda wa miaka mitano alishikilia hoja ya ufisadi.
Profesa Shaaban Sengo wa Chuo Kikuu Huria (OUT), alisema haoni kama Dk. Slaa amejiandaa vya kutosha kupambana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, kwa sababu alishachukua fomu za kuwania ubunge ndani ya chama.
Alibainisha kuwa maandalizi ni jambo muhimu kwa mgombea makini kama Dk. Slaa, la sivyo anaweza asitimize malengo aliyojiwekea pamoja na chama ambacho mwisho wa siku kinaweza kujuta kwa kuchukua uamuzi wa haraka haraka.
Alisema kuwa Dk. Slaa ana haki ya kuwania urais lakini ni lazima atafakari uamuzi wake ili Watanzania wamuelewe vizuri na kumuunga mkono katika hatua hii ya kuwania uongozi wa juu wa kitaifa.
“Sina shaka hata kidogo na uwezo wa Dk. Slaa, Watanzania tumeshamuona anavyojenga na kuisimamia hoja mpaka matunda yake yanaonekana, lakini sioni kama amejiandaa fresh kukabiliana na Rais Kikwete,” alisema Profesa Sengo.
Baadhi ya watu ambao hawakupenda kutaja majina yao wameiambia Tanzania Daima kuwa CHADEMA wameamua kulipeleka Jimbo la Karatu mikononi mwa CCM, ambayo kwa takriban miaka mitano imekuwa ikihaha kufanya mbinu ili kulinyakua jimbo hilo.
Walisema kuwa dhana ya chama hicho kutaka wabunge wengi zaidi wa viti maalumu haitakuwa na maana kama wabunge watakaoteuliwa hawana uwezo mkubwa kama alivyo Dk. Slaa, ambaye kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa upinzani waliweza kuleta mabadiliko kwenye medani ya siasa.
“Wingi wa wabunge si hoja, tuangalie michango yao kwa jamii, unaweza ukawa na wabunge 10 lakini wakashindwa kujenga na kuzitetea hoja, unaweza ukawa na mbunge mmoja akawa anafanya kazi kuliko wao,” alisema mmoja wao.
Wakati baadhi ya watu wakipinga uteuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemtangaza rasmi Dk. Willbrod Slaa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za makao makuu ya ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mbowe alisema uamuzi huo ni maazimio ya Kamati Kuu iliyomaliza muda wake juzi.
Mbowe alisema wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kwa pamoja wamekubaliana kupitisha jina la Dk. Slaa katika kinyang’anyiro cha urais ili kuziba ombwe la uongozi wa juu nchini.
“Kamati Kuu ilijiridhisha kuwa Dk. Willbrod Peter Slaa, ndiye mtu pekee anayefaa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, wajumbe wa Kamati Kuu kwa kauli moja walimuomba achukue fomu ya kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
“Tumedhamiria na hatuendi kujaribu, Dk. Slaa amekuwa mwakilishi mzuri bungeni, wote tunafahamu changamoto alizozipeleka bungeni, lakini hoja zake zinapuuzwa na serikali ya CCM, hivyo tumempeleka akawe mtekelezaji na msimamiaji wa hoja,” alisema Mbowe.
Mbowe aliwaomba wananchi, mashirika na taasisi mbalimbali kuunga mkono maamuzi ya chama hicho kwa kumpigia kura za ndiyo Dk. Slaa ili kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi.
Alibainisha kuwa uteuzi wa Dk. Slaa kuwa mgombea urais wa chama hicho umezingatia taratibu zote za kichama, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanachama wa chama hicho pamoja na wadau wa masuala ya siasa.
Akijibu swali lililoulizwa kuwa ikiwa wanachama wengine watajitokeza kugombea urais kupitia chama hicho watapewa kipaumbele gani na kwanini awe Dk. Slaa tu. Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kamati Kuu imefikia uamuzi huo kutokana na umakini wa Dk. Slaa.
“Nafasi ya rais si ya kuchezea na wala si ya kukimbilia, hata hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa ukiona mtu anakimbilia urais huyo atakuwa na dosari. Dk. Slaa hakuomba kugombea, ameombwa na kamati kuu. Hivyo tumechagua mtu makini ambaye tunajua kuwa atakuwa rais wa Tanzania ifikipo Oktoba 31, mwaka huu,” alijigamba.
Alisema wananchi wa Karatu watapatiwa mbunge mwingine makini kutoka CHADEMA atakayeziba kikamilifu pengo la Dk. Slaa bungeni kwa kujenga hoja zenye mashiko kwa masilahi ya Watanzania wote.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe alisema kamati kuu pia iilipokea, kujadili na kupendekeza kwa Baraza Kuu rasimu ya Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.
Alianisha kuwa wajumbe wa kikao hicho wamejadili na kupitisha taratibu zilizopendekezwa na Baraza la Wanawake (BAVICHA) za kuwateua wabunge wa viti maalumu.
Aidha, ilipokea, kujadili na kuzingatia taarifa ya utafiti kuhusu mgombea urais kupitia chama hicho kwa mujibu wa katiba yao.
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alisema Dk. Slaa si tishio kwa mgombea wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, aliyechaguliwa kwa asilimia 82 ya kura mwaka 2005.
Aliongeza kuwa Dk. Slaa ni mbunge, hawezi kufananishwa na kiongozi mkuu wa nchi aliyefanya mambo mengi makubwa katika kipindi cha utawala wake wa miaka mitano. “Dk. Slaa hawezi kuwa tishio kwa Kikwete, hayo ni matusi kwa CCM na mgombea wetu, mbunge huyo ni tishio kwako na wengine ambao si makini,” alisema Makamba.

tunajua strategy ya ccm, mojawapo ni kutumia baadhi ya wasomi/wachambuzi wa kisiasa kupunguza makali ya upinzani/mpinzani/mgombea yoyote awe wa uraisi au wa ubunge, kutumia rasilimali fedha walizopata kwa njia zisizo halali kuwa ghilibu wapiga kura na wasimamizi wa kura, kupandikiza watu wao kwenye vyama vya upinzani, kutumia vyombo vya habari ikiwemo kununua waandishi wa habari ili wapotoshe habari, pia kutumia vibaraka wao kupotosha uongo kuwa kweli na kweli kuwa uongo, naona safari hii wameshikwa vibaya, sasa strategy ya kujitoa wanataka mpaka kutumia udini ili kuwagombanisha wananchi wa tanzania kwa kuandika kwamba Dr ana mkataba wa siri na maaskofu, hii ni kuonyesha mafisadi wapo tayari kuingiza nchi katika migogoro ili kutetea maslahi binafsi, naona mwishowe hata barabara wata binafsisha tuwe tunawalipa kuzitumia
 
Mi naona CHADEMA wamechezea karata jimbo lao la karatu lililokuwa likisakwa kwa udi na uvumba na CCM,kumsimamisha silaa kugombea urais ni imani yangu CHADEMA wamejiandaa na yafuatayo,
Kwanzawatapoteza jimbo tete la Karatu ambalo ni miongoni mwa ngome tanzu za CHADEMA!
Pili CCM ina rasilimali nyingi na imejiandaa kikamilifu kushinda urais na watashinda kwa kishindo.
Sipati picha bunge lijalo kumkosa mwenyekiti wake wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma..Buriani Dr. Slaa,Buriani CHADEMA.
 
Kweli mbuzi wa masikini hazai na akizaa anazaa mchanganyiko wa kiziwi na mwendawazimu kipofu. Waliomteua Dr Slaa kuwa mgombea urais huku wakijuwa fika kwamba atashindwa na hivyo kutokuwa mbunge hawakuitendea haki Tz hata kidogo. Kadhalika Dr Slaa ameingia kwenye mtego wa CCM kwa kukubali kujitoa kwenye ubunge na kujiunga na safu ya akina Lipumba, Mrema, na wagombea wengine wanaoishi kwa ruzuku. Imenikatisha tamaa na imenisikitisha sana. CCM kwa makosa ya wapinzani imelamba dume tena. Badala ya kumwacha Mbowe aendelee kubwabwaja na kuwaacha Zitto na Dr Slaa bungeni waendelee kutoa chachu ya maendeleo, bunge lijalo halina mpizani mwingine isipokuwa Zitto ambaye sasa midomo yake imepigwa nchi 12 za ulimbo. Swali langu kwa Dr Slaa na CHADEMA: Inaingia akilini kuuza pikipiki ili mnunue fimbo?
 
Napenda nikupe taarifa kuwa hata ugonjwa wa ukimwi ulioshindikana hivi sasa umepatiwa dawa na wagonjwa ukimwi wanapata ahueni, hivyo usijidanganye. In the meantime ngoja kampeni zianze MgonjwaUkimwi, utashuhudia moto ambao haujaonekana toka tupate uhuru ! Mimi kwa hivi sasa sina hata wasi wasi na ninapata usingizi mwororo nikisubiri siku Dr.Slaa atakapouwasha - CCM kwa mara ya kwanza itajikuta uchi kabisa kwani macho ya wananchi yatafunuliwa, we subiri.
 
Mi naona CHADEMA wamechezea karata jimbo lao la karatu lililokuwa likisakwa kwa udi na uvumba na CCM,kumsimamisha silaa kugombea urais ni imani yangu CHADEMA wamejiandaa na yafuatayo,
Kwanzawatapoteza jimbo tete la Karatu ambalo ni miongoni mwa ngome tanzu za CHADEMA!
Pili CCM ina rasilimali nyingi na imejiandaa kikamilifu kushinda urais na watashinda kwa kishindo.
Sipati picha bunge lijalo kumkosa mwenyekiti wake wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma..Buriani Dr. Slaa,Buriani CHADEMA.

Wacha woga, hayo ni maneno ya mwana CCM - sasa wewe Izack, utampigia kura nani ? Kama unampigia kura Kikwete sawa lakini kama humpigii Kikwete, wasi wasi wa nini ?
 
Huwezi jua. Kuna majimbo yenye watu "walioelimika" wasiozuzuka na uongo wa mafisadi wa CCM. Adha, lazima tu-appreciate changamoto zinazotolewa na CHADEMA na akina Slaa katika siasa zilizodumaa za nchi hii. Hawa angalau wanaonyesha dalili za kujiweka juu ya ubinafsi na hivyo kutupa mada za kujadili kuhusu hatma ya nchi. I just wish the people (Tanzanians) would wisen up to their reality!
 
Mi naona CHADEMA wamechezea karata jimbo lao la karatu lililokuwa likisakwa kwa udi na uvumba na CCM,kumsimamisha silaa kugombea urais ni imani yangu CHADEMA wamejiandaa na yafuatayo,
Kwanzawatapoteza jimbo tete la Karatu ambalo ni miongoni mwa ngome tanzu za CHADEMA!
Pili CCM ina rasilimali nyingi na imejiandaa kikamilifu kushinda urais na watashinda kwa kishindo.
Sipati picha bunge lijalo kumkosa mwenyekiti wake wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma..Buriani Dr. Slaa,Buriani CHADEMA.

Kutumia neno Buriani kavukavu kwa mtu aliye hai ni kitu kibaya sana, usilete uchuro. Hata wewe hautapenda kuambiwa Buriani Izack.
 
Izack uoga wako hautusaidii katika kuleta mabadiliko yanayohitajika. Wanakaratu wana msimamo wanajua wanachokifanya, ni hoja gani CCM itumie kushinda Karatu. Mimi natoka katika jamii ya Kiiraq, tukkishabadilika huwa haturudi nyuma kwa hiyo mawazo yako hayana nafasi Karatu.

Unafikiri Dr Slaa na Dr JK nani anafaa kuwa rais waTz? Kwa watanzania wenye nia njema na nchi yao, ni Dr Slaa anayaefaa. Kwa wana CCM ni JK anayefaa kwani ndani ya CCM ni ufisadi tu; mawazo yao ni kwenye tumbo.

Na wasiwasi wewe ni CCM damu damu
 
Mi naona CHADEMA wamechezea karata jimbo lao la karatu lililokuwa likisakwa kwa udi na uvumba na CCM,kumsimamisha silaa kugombea urais ni imani yangu CHADEMA wamejiandaa na yafuatayo,
Kwanzawatapoteza jimbo tete la Karatu ambalo ni miongoni mwa ngome tanzu za CHADEMA!
Pili CCM ina rasilimali nyingi na imejiandaa kikamilifu kushinda urais na watashinda kwa kishindo.
Sipati picha bunge lijalo kumkosa mwenyekiti wake wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma..Buriani Dr. Slaa,Buriani CHADEMA.

Huna lolote zaid ya unafiki. Watu wa aina yako ndiyo wameifanya nchi hii iliwe na watu wachache. Hivi lini utaacha kujiona kuwa wewe ni panzi na huwezi kuyakabiri majitu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom