Hata Nyerere alipoacha ualimu pugu kwenda TANU wapo waliomwambia kaingia choo cha kike.....the rest is history of course
Safari_ni-Safari na wenzako hapo juu, mnazisoma hizi news kwa makini au mnabishabisha tu tukubaliane na fikra zenu? Soma kwa makini uelewe news kama hizi. Pia pima joto halisi la nchi kwa kuangalia vijijini ambako 80% ya kura ziko. Tarime na Karatu ni wilaya moja katika zaidi ya 200 nchini, statistically insignificant. Siyo mnakaa kweye laptops/PC mnachagua Rais wenu kwa ku-type hapa JF. Comes October, we will see here at JF.
Dk. Slaa awagawa wengi
• Uteuzi wake wawashtua wengi
na Waandishi wetu
UTEUZI uliofanywa juzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wa kumteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, umepingwa vikali na baadhi ya watu, kwa madai utakidhoofisha zaidi kuliko kukiimarisha.
Wakizungumza na Tanzania Daima, walisema Dk. Slaa hakupaswa kuwania urais hivi sasa, kwa kuwa uwepo wake bungeni ulileta changamoto kubwa na mabadiliko ndani na nje ya Bunge kiasi cha kuifanya serikali kutetemeka kila hoja za wapinzani zinapotolewa.
Walisema uteuzi huo haukufanywa kwa kuangalia mazingira yaliyopo, ambayo kwa kiasi kikubwa yanahitaji hoja nzito za wapinzani zitolewe bungeni, kama alivyokuwa akifanya Dk. Slaa ambaye kwa muda wa miaka mitano alishikilia hoja ya ufisadi.
Profesa Shaaban Sengo wa Chuo Kikuu Huria (OUT), alisema haoni kama Dk. Slaa amejiandaa vya kutosha kupambana na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, kwa sababu alishachukua fomu za kuwania ubunge ndani ya chama.
Alibainisha kuwa maandalizi ni jambo muhimu kwa mgombea makini kama Dk. Slaa, la sivyo anaweza asitimize malengo aliyojiwekea pamoja na chama ambacho mwisho wa siku kinaweza kujuta kwa kuchukua uamuzi wa haraka haraka.
Alisema kuwa Dk. Slaa ana haki ya kuwania urais lakini ni lazima atafakari uamuzi wake ili Watanzania wamuelewe vizuri na kumuunga mkono katika hatua hii ya kuwania uongozi wa juu wa kitaifa.
"Sina shaka hata kidogo na uwezo wa Dk. Slaa, Watanzania tumeshamuona anavyojenga na kuisimamia hoja mpaka matunda yake yanaonekana, lakini sioni kama amejiandaa fresh kukabiliana na Rais Kikwete," alisema Profesa Sengo.
Baadhi ya watu ambao hawakupenda kutaja majina yao wameiambia Tanzania Daima kuwa CHADEMA wameamua kulipeleka Jimbo la Karatu mikononi mwa CCM, ambayo kwa takriban miaka mitano imekuwa ikihaha kufanya mbinu ili kulinyakua jimbo hilo.
Walisema kuwa dhana ya chama hicho kutaka wabunge wengi zaidi wa viti maalumu haitakuwa na maana kama wabunge watakaoteuliwa hawana uwezo mkubwa kama alivyo Dk. Slaa, ambaye kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge wa upinzani waliweza kuleta mabadiliko kwenye medani ya siasa.
"Wingi wa wabunge si hoja, tuangalie michango yao kwa jamii, unaweza ukawa na wabunge 10 lakini wakashindwa kujenga na kuzitetea hoja, unaweza ukawa na mbunge mmoja akawa anafanya kazi kuliko wao," alisema mmoja wao.
Wakati baadhi ya watu wakipinga uteuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemtangaza rasmi Dk. Willbrod Slaa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za makao makuu ya ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Mbowe alisema uamuzi huo ni maazimio ya Kamati Kuu iliyomaliza muda wake juzi.
Mbowe alisema wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kwa pamoja wamekubaliana kupitisha jina la Dk. Slaa katika kinyang'anyiro cha urais ili kuziba ombwe la uongozi wa juu nchini.
"Kamati Kuu ilijiridhisha kuwa Dk. Willbrod Peter Slaa, ndiye mtu pekee anayefaa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, wajumbe wa Kamati Kuu kwa kauli moja walimuomba achukue fomu ya kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
"Tumedhamiria na hatuendi kujaribu, Dk. Slaa amekuwa mwakilishi mzuri bungeni, wote tunafahamu changamoto alizozipeleka bungeni, lakini hoja zake zinapuuzwa na serikali ya CCM, hivyo tumempeleka akawe mtekelezaji na msimamiaji wa hoja," alisema Mbowe.
Mbowe aliwaomba wananchi, mashirika na taasisi mbalimbali kuunga mkono maamuzi ya chama hicho kwa kumpigia kura za ndiyo Dk. Slaa ili kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi.
Alibainisha kuwa uteuzi wa Dk. Slaa kuwa mgombea urais wa chama hicho umezingatia taratibu zote za kichama, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanachama wa chama hicho pamoja na wadau wa masuala ya siasa.
Akijibu swali lililoulizwa kuwa ikiwa wanachama wengine watajitokeza kugombea urais kupitia chama hicho watapewa kipaumbele gani na kwanini awe Dk. Slaa tu. Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kamati Kuu imefikia uamuzi huo kutokana na umakini wa Dk. Slaa.
"Nafasi ya rais si ya kuchezea na wala si ya kukimbilia, hata hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa ukiona mtu anakimbilia urais huyo atakuwa na dosari. Dk. Slaa hakuomba kugombea, ameombwa na kamati kuu. Hivyo tumechagua mtu makini ambaye tunajua kuwa atakuwa rais wa Tanzania ifikipo Oktoba 31, mwaka huu," alijigamba.
Alisema wananchi wa Karatu watapatiwa mbunge mwingine makini kutoka CHADEMA atakayeziba kikamilifu pengo la Dk. Slaa bungeni kwa kujenga hoja zenye mashiko kwa masilahi ya Watanzania wote.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe alisema kamati kuu pia iilipokea, kujadili na kupendekeza kwa Baraza Kuu rasimu ya Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.
Alianisha kuwa wajumbe wa kikao hicho wamejadili na kupitisha taratibu zilizopendekezwa na Baraza la Wanawake (BAVICHA) za kuwateua wabunge wa viti maalumu.
Aidha, ilipokea, kujadili na kuzingatia taarifa ya utafiti kuhusu mgombea urais kupitia chama hicho kwa mujibu wa katiba yao.
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, alisema Dk. Slaa si tishio kwa mgombea wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, aliyechaguliwa kwa asilimia 82 ya kura mwaka 2005.
Aliongeza kuwa Dk. Slaa ni mbunge, hawezi kufananishwa na kiongozi mkuu wa nchi aliyefanya mambo mengi makubwa katika kipindi cha utawala wake wa miaka mitano. "Dk. Slaa hawezi kuwa tishio kwa Kikwete, hayo ni matusi kwa CCM na mgombea wetu, mbunge huyo ni tishio kwako na wengine ambao si makini," alisema Makamba.