Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Wilbroad Slaa leo amelihutubia Bunge katika kikao chake cha kwanza cha Ufunguzi na kuelezea mikakati yake ndani ya siku 100.

Mheshimiwa Rais Slaa alisema kwamba moja kati ya mambo atakayoyafanyia kazi katika siku zake 20 za Mwanzo ni kuhakikisha kwamba anarudisha Raslimali zote zilizoporwa Mikononi mwa Wananchi, Vile vile ameagiza kuanza kutumika mara moja kwa Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba wale wote waliohusika katika kuiletea hasara Nchi hii watahukumiwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uhujumu Uchumi, vile vile ameahidi kuufanyia mabadiliko makubwa Mfumo Mzima wa Kiserikali wa Tanzania, kwa kuanzia ameahidi Katiba Mpya itakayoendana na hali halisi na kuachana na katika ya 1997 iliyosheheni viraka mpaka kufikia kiwango cha Kuji-contradict
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Wilbroad Slaa leo amelihutubia Bunge katika kikao chake cha kwanza cha Ufunguzi na kuelezea mikakati yake ndani ya siku 100.

Mheshimiwa Rais Slaa alisema kwamba moja kati ya mambo atakayoyafanyia kazi katika siku zake 20 za Mwanzo ni kuhakikisha kwamba anarudisha Raslimali zote zilizoporwa Mikononi mwa Wananchi, Vile vile ameagiza kuanza kutumika mara moja kwa Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba wale wote waliohusika katika kuiletea hasara Nchi hii watahukumiwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uhujumu Uchumi, vile vile ameahidi kuufanyia mabadiliko makubwa Mfumo Mzima wa Kiserikali wa Tanzania, kwa kuanzia ameahidi Katiba Mpya itakayoendana na hali halisi na kuachana na katika ya 1997 iliyosheheni viraka mpaka kufikia kiwango cha Kujicontradict

Tuombe Mungu ndugu yangu Dr Slaa ashinde, mimi naamini kabisa atafanya maamuzi mengi ambayo Watanzania wengi tutajivunia kwamba sasa tumempata kiongozi wa kweli anayejali maslahi ya Watanzania kama alivyokuwa Mwalimu.
 
Wenger,

Nadhani si vema kuikataa kura ya Malaria Sugu. Malaria Sugu kwenye Jamvi hili tunamjua wote kama mchokozi. Na wakati mwingine uchokozi wa aina hiyo ni mzuri. Hatuhitaji kutukanana. Kama yeye hatatoa kura yake hiyo ni haki yake wala tusimlazimishe. Na mimi nadhani hata kura yake tunaihitaji, hakuna kura ya mtanzania tunayoikataa, kura ni kura, kura haina sifa ya ubaya au uzuri bora ni kura halali. Thanksa wote, Thanks Malaria Sugu.
Asante Dr.Slaa kwa jibu zuri sana.

Jibu langu kwake nililitoa kwa kumkejeli kwani huwa anaweka hoja nyingi sana za ajabu ajabu na nimefurahi kuona msimamo wako ni tofauti sio kama ule tuliombiwa kwenye luninga ya taifa na mkuu wa nchi kwamba hana shida na kura zetu.

Nakutakia kila la kheri kwenye uchaguzi na Mungu akulinde kwenye mpambano huu mgumu wa kutuokoa watanzania na tuko pamoja kukuunga mkono kwa njia yoyote hile.
 
Wapenzi wengi wa chama chako wana sifa ya kutuweza kuvumilia mawazo mbadala hasa yanakuhusu wewe na background zako za KIKANISA na UDINI (kielimu na kimalezi)....

Naamini hustahili kura hata moja kutoka kwa MUISLAMU mwenye chembe ya IMANI kwakuwa kitakachofuata baada ya hapo ni kufunikwa kwa uislamu Tanzania na kuingiza ukatoliki maana ndiko ulikobobea (PhD) ...

Sorry nenda kanisani kaongoze kwenye urais unataka kuleta maafa na mgawanyiko mkubwa katika..ushauri tu kwa ajili ya Tanzania yetu..
kaishi somali mkuu utapata uongozi unaokufaa na unao upenda.
 
Ni huyu huyu Dr Slaa aliyeshauri wabunge wapunguzwe mishahara/posho (yeye mwenyewe included).

Watanzania, mnataka kiongozi gani tena? Vote for Dr Slaa. You will not regret!
 
You are my man. The only positive thinking missing in Tanzania
Wenger,

Nadhani si vema kuikataa kura ya Malaria Sugu. Malaria Sugu kwenye Jamvi hili tunamjua wote kama mchokozi. Na wakati mwingine uchokozi wa aina hiyo ni mzuri. Hatuhitaji kutukanana. Kama yeye hatatoa kura yake hiyo ni haki yake wala tusimlazimishe. Na mimi nadhani hata kura yake tunaihitaji, hakuna kura ya mtanzania tunayoikataa, kura ni kura, kura haina sifa ya ubaya au uzuri bora ni kura halali. Thanksa wote, Thanks Malaria Sugu.
 
Wapenzi wengi wa chama chako wana sifa ya kutuweza kuvumilia mawazo mbadala hasa yanakuhusu wewe na background zako za KIKANISA na UDINI (kielimu na kimalezi)....

Naamini hustahili kura hata moja kutoka kwa MUISLAMU mwenye chembe ya IMANI kwakuwa kitakachofuata baada ya hapo ni kufunikwa kwa uislamu Tanzania na kuingiza ukatoliki maana ndiko ulikobobea (PhD) ...

Sorry nenda kanisani kaongoze kwenye urais unataka kuleta maafa na mgawanyiko mkubwa katika..ushauri tu kwa ajili ya Tanzania yetu..
Mbona tumekuwa na rais Al haji Tanzania hatujasema kitu? Angalieni ni mbegu mbaya mnajenga na tena ukitaka kusema hivyo kwa idadi sizani kama Tz kura za kidini waislam watashinda ,so it may fire back .
 
kura yangu haipati mpaka anifanulie hasa udokta wake atautumia vipi wakati yeye ni dokta wa maswala ya dini?
Nadhani Watanzania wanamhitaji mtu mwenye uzalendo.Katiba ya Tanzania inaeleza nani ana sifa za kuwa rais wa Tanzania. Udaktari wake atautumia kama alivyoutumia akiwa mbunge. Malaria sugu anataka rais wetu awe na udaktari wa nini? Wapo walio wanasheria ktk nchi hii na ni wanasiasa lakini hawajaisaidia nchi hii kwa sababu tu hawana uzalendo. Wanasheria hao hawakusema kitu pale rais Kikweti aliposaini sheria ambayo imeongezewa vipengele tofauti na vilivyopitishwa bungeni achilia mbali hata kujadiliwa. huyo huyo ambaye malaria sugu hajui udaktari wake utamsaidia nini ndiye pekee aliyehoji hicho, je udaktari wake hauonyeshi umakini alionao kwako?

Malaria sugu usitupotezee muda wetu bure wala usitupotoshe katika mijadala ya maana. Tunachohitaji ni ukombozi wa Tanzania siyo dini au udaktari wa mtu. Hoja zenye mwelekeo wa kidini zimeanza kupenyeza hapa. Matatizo ya msingi ya Watanzani si hayo, usijaribu kutengeneza matatizo ambayo hayapo hata tukasahau yaliyopo.
 
Nimefurahi sana kusikia kuwa Dr Slaa amekubali kuingia kwenye kinyanganyiro cha usais. Watu wengi wanaopingana na uamauzi huo wanatumia hoja hafifu sana:

(1) Kwamba Dr Slaa alikuwa wa muhimu sana Bungeni, lakini hawajibu swali lakama alikuwa muhimu sana bungeni ambako hakuwa na uamuzi wa mwisho, kwa nini asiwe wa muhimu akiwa Ikulu ambako atakuwa na uamauzi wa mwisho?

(2) Kwamba CHADEMA haiwezi kushindana na CCM kwenye kiti cvha urais huku wakishindwa kujibu swali la kama Dr. Slaa aliwashinda hao CCM huko Karatu kwa nini asiwashinde huko Ikulu?

Nadhani kuwa Tanzania haijawahi kupata candidate wa upinzani ambaye ni potential kama Dr. Slaa. Namwombea afanikiwe kupata nafasi ya kuinyoseha dunia kuwa Tanzania siyo nchi ya wapuuzi kama inavyojulikana sasa. Dr Slaa ni mtu anayejua kuangalia mambo kwa kina sana kwa manufaa ya taifa kabla hajayatolea tamko; kila alilowahi kutamka akiwa bungeni lilikuwa sahihi kabisa. Kuna watu walitangaza kuwa watakwenda kumshitaki mahakamni ila wakajiona wako uchi na wakaishia kimya kimya hadi leo; hata mwanasheria maarafu na tajiri sana nchini aligwaya kumkabili Dr. Slaa mahakamani.
 
Hana jipya zaidi ya "Ukatoliki" at extreme point..Balaa hili Mungu tuepeushe nasi...lipite mbali...

Na Bado Hii Miezi mitatu Lazima Uumwe Vidonda vya Tumbo Mkuu! Na Leo anawasha Moto Karatu hakika lazima Tumbo laKuhara Damu Likuume Leo

Go Slaa, Go Slaa Watu kibao wako Pamoja na Wewe, Mafisadi Matumbo Joto
 
hapa kuna vijidudu vina nyevuanyevua na masuala ya udini.Je, wakati anagombea ubunge kwao Karatu alipigiwa kura na wakristo tu???
Je, alipokuwa anaibua mambo ya ufisadi ndani ya serikali ya rais Muislam alishangiliwa na wakristu tu katika nchi hii?
Kwa mara ya ngapi Prof Lipumba anagombea,na hamkumpa hizo kura zenu awe rais?

Kama haikuwa hivyo, sasa iweje anagombea uraisi zinaanza nongwa?????
Tuache mbwembwe za kidini na tuangalie nani atatufaa katika uongozi.
 
MS si uhamie ukatoliki tu kwasababu uislam umekushinda na uliyempigia debe amekusaliti hajaaanzisha mahakama ya kadhi kama alivyowaaidi hapo awali, mi nakushauri uachane nae msaliti JK na badala yake muunge mkono Dr. Slaa ambaye ahadi zake hazina chambechembe ya udini hata kidogo, kwake yeye waislam, wakristo na wasio na dini wote ni sawa
 
imekaa kichadema dema

UKIWEZA JINYONGE, UKICHUKIA CHUKIA , UKILIA LIA. LKN HAMNA AWEZAE KUYAPANGUA YA MUUMBA WETU "JK TU 2010

Mkuu naona kila kukicha unaikimbia statement yako mwenyewe, inaonekana umepanic sana kuona Dr. Slaa ameingia ulingoni. If the statement above is what you believe in, kwa nini huishi kuanzisha mathread yasiyo kichwa wala miguu almost 5 per day kuhusu Dr. Slaa??????
 
UKIWEZA JINYONGE, UKICHUKIA CHUKIA , UKILIA LIA. LKN HAMNA AWEZAE KUYAPANGUA YA MUUMBA WETU "JK TU 2010

Mkuu naona kila kukicha unaikimbia statement yako mwenyewe, inaonekana umepanic sana kuona Dr. Slaa ameingia ulingoni. If the statement above is what you believe in, kwa nini huishi kuanzisha mathread yasiyo kichwa wala miguu almost 5 per day kuhusu Dr. Slaa??????
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Wilbroad Slaa leo amelihutubia Bunge katika kikao chake cha kwanza cha Ufunguzi na kuelezea mikakati yake ndani ya siku 100.

Mheshimiwa Rais Slaa alisema kwamba moja kati ya mambo atakayoyafanyia kazi katika siku zake 20 za Mwanzo ni kuhakikisha kwamba anarudisha Raslimali zote zilizoporwa Mikononi mwa Wananchi, Vile vile ameagiza kuanza kutumika mara moja kwa Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba wale wote waliohusika katika kuiletea hasara Nchi hii watahukumiwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uhujumu Uchumi, vile vile ameahidi kuufanyia mabadiliko makubwa Mfumo Mzima wa Kiserikali wa Tanzania, kwa kuanzia ameahidi Katiba Mpya itakayoendana na hali halisi na kuachana na katika ya 1997 iliyosheheni viraka mpaka kufikia kiwango cha Kuji-contradict

Mkuu kuwa makini nchi hii ina rais mmoja mpaka sasa, hivyo angalia usije vunja sheria ya nchi, ukaingia kwenye kundi la watu wanotaka kumpindua raisa wetu wa Jamhuri ya muungano Mh.Dr,JK
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom