Chadema wana mpango gani au wamejiandaa vipi kusimamia wizi wa kura? manake wajue wamepoteza kichwa kikubwa sana bungeni na bila kufanya mpango makini wa kusimamia wizi wa kura kitachotokea ni kama miaka ya nyuma ni kulalamika tumeibiwa kura na hakuna hatua zozote zinafanyika.
Kama wewe una uchungu na nchi, unaweza kutoa ushauri wa namna ya kulinda kura na sio kuwaachia "wengine" wafanye kazi hiyo?
nilikuwa nafuraha sana na chadema kuweka nguvu kwenye nafasi za ubunge sasa leo wanaenda kutoa kichwa chao kikubwa bungeni.
safari ndefu sana kwa wapinzani.
Mtu mmoja tu kuacha kugombea ubunge inakufanya useme kuwa chadema wameaacha kuweka nguvu kwenye ubunge? analysis yako bomba sana mkuu
Naona sasa macho yote yatakuwa kwenye hio nafasi ya uraisi kuliko kwenye wabunge.
Kwani kuna makosa kuweka nguvu kwenye vyote - uraisi + ubunge?
