Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hahaaaa wiwiwwwwiiii.. Tembo usingizi umepaaa.. go baba Slaa Mungu akutangulie.
 
Sina Uhakika kama hiyo namba inafanya Kazi maana last time nilituma Ujumbe nikaishia kuktwa pesa ya SMS yaani Shilingi 58
 
Kilichobaki ni kwetu sisi kuwashauri jirani zetu (wenzetu) wasituangushe siku ya kura....
 
DSC00085.JPG

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akitangaza rasmi leo kuwa Kamati Kuu ya Chama hicho imemteua Katibu Mkuu wao Dk. Wilbroad Slaa kuwa mgombea wao wa Urais katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano na wanahabari makao makuu ya chama huko Kinondoni jijini

DSC00086.JPG


Waandishi na baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakimsikiliza Mh. Mbowe

DSC00101.JPG


Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe akitoa ufafanuziw a jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi Saeed Kubenea baada ya mkutano huo leo

MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MH. FREEMAN MBOWE LEO AMETANGAZA RASMI KWAMBA CHAMA HICHO KITAMSIMAMISHA KATIBU MKUU WAKE DK. WILBROAD SLAA KUGOMBEA KITI CHA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.

MH. MBOWE AMESEMA MCHANA HUU KWENYE MAKAO MAKUU YA CHADEMA YALIYOKO KINDONDONI JIJINI DAR KWAMBA KWA KAULI MOJA KAMATI KUU YA CHADEMA ILIYOMALIZA VIKAO VYAKE JANA IMEKUBALIANA KWA KAULI MOJA KUMUOMBA DK. SLAA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS, NA KWAMBA NAYE AMEKUBALI.

MBOWE AMEPANGUA HOJA KIBAO ZILIZOKUWA ZIKIPIGIA UKOPE UAMUZI WA CGHADEMA KUMPA DK. SLAA NAFASI HIYO AMBAYO MOJA KWA MOJA ATAKUWA HATETEI TENA KITI CHAKE CHA UBUNGE CHA KARATU, NA KWAMBA ENDAPO ATAKOSA URAIS ATAKUWA KAMALIZIKA KISIASA.

"OCTOBA 31 DK. SLAA ATAKUWA RAIS WA NCHI HII SASA UNAPOSEMA ATAKUWA AMEJIMALIZA KISIASA UNA MAANA GANI AMA NDIO UNAJIMU WENU AMBAO MMESHAUANZA.

"DK. SLAA NI MTU MAKINI NA MWENYE SIFA ZOTE ZA SIO TU KUWA RAIS BALI PIA KULETA MABADILIKO MAKUBWA AMBAYO NCHI HII INAYAHITAJI LAKINI HAKUNA WA KUTEKELEZA", ALISEMA MH. MBOWE KWA KUJIAMINI HUKU AKISHANGILIWA NA BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHRIA MKUTANO HUO NA WANAHABARI.

MWENYEKITI HUYO WA CHADEMA PIA AMEKANUSHA VIKALI UVUMI KWAMBA DK. SLAA AMETUMWA NA KANISA LA DINI FULANI KUGOMBEA HUO URAIS, NA KUDAI HUO NI UMBEA WA BAADHI YA MAGAZETI AMBAYO KADAI AIDHA WAANDISHI AMA WAMILIKI WANATUMIKA KUKIPAKA MATOPE CHADEMA.

"kUNA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINABAKA WANANCHI KWA KUANDIKA HABARI ZA UMBEA NA KUPOTOSHA KWA MANUFAA YAO (WAANDISHI BINAFSI) AMA WAMILIKI WA VYOMBO HIVYO.

"NAOMBA BAADHI YA WAANDISHI WENYE TABIA HIYO WAIACHE WASIJE WAKAIPELEKA NCHI PABAYA", ALISEMA MH. MBOWE HUKU MEZA KUU WALIYOKETI VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHADEMA AKIWEMO NAIBU KATIBU MKUU MH. ZITTO KABWE, WAKITIKISA VICHWA KUUNGANA NA KAULI ZAKE.

KUHUSU UBUNGE JIMBO LA KARATU ATALOACHA WAZI DK. SLAA MWENYEKITI WA CHADEMA KASEMA WAO HAWANA WASIWASI KWANI HAKUNA CHAMA CHENYE YBAVU WA KUTWAA KITI KATIKA JIMBO HILO AMBALO ALIONGEZEA KWAMBA HALMASHAURI YAKE YA WILAYA IMEKUWA IKONGOZWA NA CHADEMA KWA MIAKA 10 SASA.

"DK SLAA PAMOJA NA KUWA CHACHU KUBWA YA USHINDI WA CHADEMA KARATU LAKINI SI YEYE PEKEE MWENYE UMUHIMU MKUBWA KULE JIMBONI. KUNA VIONGOZI WENZIE NA WANANCHI AMBAO KWA PAMOJA NDIO WALIOIFANYA CHADEMA ISIMAME.

"HIVYO KAA UKIHJUA TAYARI KUNA MGOMBEA MAKINI AMESHAANDALIWA NA ATAFANYA MAKUBWA KAMA ALIYOFANYA DK. SLAA", ALIFAFANUA.
 
Jamani tuungane pamoja kwa wale waliopo nchni na wenye uchunu wa mali zetu tulizojaliwa na Mwenyezi Mungu zinavyoibiwa na mafisadi waungane na wahakikishe wanajiandikisha na wanapiga kula ili kumwondoa JK ambae kashindwa kwa kila kitu. Sanasana aichofanikiwa ni safari na kukaa kimya wakati nchi inamhitaji! Mie nilitegemea nisirudi kupiga kura, kwa sasa najiandaa kuja lazima nimpigie SLAA. VIVA SLAAA VIVA.
 
Kura yangu nimepata wa kumpigia.I believe in miracle, Go slaa.
 
Source: Mtanzania

Dr. Slaa ana sifa zote za kuwa rais wa nchi. Wakati wagombea wengine wanakimbilia kujaza form za kugombea urais yeye amepinga sana, alikataa kugombea. Waone wasiokuwa na sifa kama Kikwete anavyolilia kuwa rais. Watu wanaotaka kukimbilia ikulu hawana kitu. Dr Slaa ametumia silaha zote kukataa kugombea urais ikiwemo mambo ambayo mwingine asingeyasema, mambo ya siri ya mume na mke. Lakini pamoja na kuwa hakutaka kugombea urais ameacha ubinafsi akanyoka akakubali kugombea. Chadema wameonyesha wako tayari kumpa uenyekiti wa chama Dr. Slaa. Huu ni mtazamo mzuri wa Chadema. Kuna vyama ambavyo wagombea wameng'ang'ania uenyekiti wa vyama vyao na kugombea urais kila uchaguzi unapokuja. Chama ni taasisi siyo mtu mmoja, mtazamo wa kubadilishana nafasi katika uongozi ni mzuri mno kwa chama. CCM wameshindwa, wameamua kumrudisha Kikwete agombee ingawa ameshindwa kuongoza nchi. Badala ya kumwambia ukweli umeshindwa kuongoza ondoka, kaa pembeni wao wanampamba kwa unafiki. Hongera Chadema, Hongera Dr. Slaa kwa kuonyesha njia.

Mwandishi wa Mtanzania naye anashangaza alivyomaliza habari yake. Sijui shule yake ya alienda wapi. Hivi Dr. Slaa kugombea urais hadi aombe baraka za Maaskofu? Sijui hii ni akili gani, mwandishi anashindwa kupambanua sifa za kiongozi anayegombea anaanza kukimbilia habari za maaskofu. Ameripoti mlolongo wa namna alivyokataa kugombea halafu anamaliza kwa pumba. Namsubiri Kiranga amwajibishe mwandishi huyu.
 
duh! Mpo wengi hapa JF wa sampuli ya kukomalia kitu!. Unauliza swali la wazi hivi? Mimi nadhani Slaa kaingia choo cha kike. Mshaurini arudi kiumeni. Bungeni
naona umeishiwa hoja unaishia kutuo lugha zisizofaa, haya bw/bi tunashukurui kwa kauli yako, na hii inaonyesha ulikuwa unatetea kitu sio kwa kuwa na hoja bali kwa kuwa hupendi wapinzani washinde, ndio maana unakuja na hoja mfuu, kwamba oh wapinzani bado wachanga , oh karatu/bunge litakosa msemaji (dr Slaa) nk nk, lakini mwisho wa siku umeona hoja zako hazina mshiko unaishia kutumia maneno ya ******.
 
Dr slaa ni mpambanaji wa kweli!Asante sana,TUKO NYUMA YAKO!
 
Mimi nashangaa wameenda Voda! sijui vipi tena jamani. Tigo naiaminia
 
Tuwekeeeni na mitandao mingine..
Tuko pamoja...
 
Since I was born about four decades ago, now I see the light at the end of the tunnel. Liberation of Tanzanians of today is now around the corner! Chadema's NEC has shown their wisdom. I remember in the past the late Nyerere commended Chadema as a strong and serious opposition party in Tanzania. I now nickname Dr. Wilbroad Slaa as Dr. W. Silaha (a weapon) that will soon help us to get rid of our enemies of better life in Tanzania.

Nyerere seconded the idea of Plato of letting philosophers to be heads of their state because they have two qualities: 1. they have a capacity to lead 2. they do not like to lead. Plato's state would drive philosophers to lead in short periods of time, and they would like that since they would go back to their philosophy business after their terms or phases (Nyerere, 1990s, p. 8). Dr. Slaa is a philosopher, that is, holding a PhD and he has already shown two qualities like that of those of Plato's state - he is capable of leading and he dislikes leading as he was not ready to accept NEC's decision; in short, he is a right guy based on his history in a political arena.

Nyerere (1990s, p. 8) said that our country is led by politicians who are not philosophers (non PhD holders) who love to lead though they do not have that capacity, and once they are in power they do not like to leave that power! We have witnessed this in CCM - why presidential candidate aspirant was alone, why Sheick Yahya was used to scare other aspirants like Shibuda, we have already observed poor performance of incompetent president JK.

Tanzanians, there is a saying that OPPORTUNITY NEVER COMES TWICE! This year Britons (UK with David Cameron) and recently the Cowboys (US with Obama) have made it in their general elections why not us? Why should we eat ugali with beans all these years while we can go for pilau with Tanzanian chicken easily?

VOTE FOR THE REAL WEAPON THAT BRINGS LIBERATION TO ALL ASPECTS OF OUR LIFE IN TANZANIA - WHAT IS THAT WEAPON? Dr. WILBROAD SLAA aka SILAHA (I give CHADEMA a permission to modify and use this slogan in their election campaign this year - you have my vote already!)

God loves Tanzania since Dr. Slaa is almost an alternative to an independent candidate!!! God bless and protect you, Dr. Slaa (Silaha) and live longer

Reference: Nyerere, J.K. (1990s). Uongozi Wetu na hatima ya Tanzania. Harare: Zimbabwe Publishing House.
 
Umefika wakati wa watu kusimama wahesabiwe kwani msitari tayari umechorwa, ama uko upande wa status quo au mabadiliko. Sasa sio muda tena wa kulialia au kutanguliza hofu, ni muda wa kila moja wetu kusema hapana imetosha na hatuwezi kuendelea kuwa watazamaji na huku taifa linateketea. Humu JF tunashuhudia wapiganaji wa kweli wakijitokeza wazi wazi na kuchukua msimamo huku wenzao, wale asilimia 70%, wakisubiri waone kwanza upepo unaelekea wapi. Hongera Dr. Slaa, sisi wengine hatuna hata wasi wasi kwani twajua Mkwere kenda na maji na huko Uspania saa hizi madaktari wako kazini kumzindua mtu kwani kimbunga chastua ati !
Don't underestimate CCM!
 
Well my point is ni jukumu letu sote hata ss tulio nje kumkampenia Dr. Slaa. Inanishangaza pale watu wanaposema kwa nini asigombee ubunge ambao ana uhakika kushinda kuliko uraisi eti ambao ni obviousd JK atashinda.
Urais hauna hati miliki!Kwanini agombee kitu ambacho anauhakika wa kushinda ni bora agombee kitu amabacho ataweka ushindani na Urais ndiyo nafasi yake! Congrats Dr Slaa ,naomba nafasi ya Uwaziri ukipata ,nami nianze kujipigia kampeni kwa Mtarajiwa!
 
[U said:
Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu[/U];995884]Urais hauna hati miliki!Kwanini agombee kitu ambacho anauhakika wa kushinda ni bora agombee kitu amabacho ataweka ushindani na Urais ndiyo nafasi yake! Congrats Dr Slaa ,naomba nafasi ya Uwaziri ukipata ,nami nianze kujipigia kampeni kwa Mtarajiwa!

Kweli slaa kiboko katoa nyoka pangoni kuna watu sijawai kuwaona hapa JF tokea nijiunge karibu mzeeeee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom