Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
hata kwa waislam. nipe ushahidi?
Nimeangalia hoja za malaria sugu na Tumain. Nataka kutofautiana na Dr. Slaa. Mawazo wanayoandika Malaria sugu na Tumain hapa kwa hakika ni ya kubomoa umoja wa Watanzania. Lengo la JF siyo kuwagawanya watanzania kwa misingi ya kidini. Nilishawaomba mara nyingi Mods kuwa mijadala ya kidini ipelekwe sehemu husika yenye mijadala ya kidini ya hoja mchanganyiko au ufutwe kabisa JF. Jukwaa la siasa lisigeuzwe na Malaria Sugu na Tumain kama jukwaa la kupandikiza na kuendeleza chuki za kidini. Kwa dhati kabisa nawaomba Mods wafute hapa hoja zote za chuki za kidini. Hatuwezi kuvumilia tabia za watu kuendeleza na kupandikiza chuki za kidini na kuubomoa umoja wa Watanzania. JF sasa inasomwa na Watanzania wengi, vijana na watu wazima, ni mafundisho gani Tumain na Malaria Sugu wanayatoa kwa Watanzania. Dr Slaa kura ya yeyote ni muhimu, lakini hatuwezi kuvumilia Tumain na Malaria sugu waendelee kuitumia JF kama jukwaa la kubomoa umoja wa Watanzania. Kwa hiyo Mods naomba mtoe adhabu sitahiki kwa Tumain na Malaria sugu kwa kufuta posti zao za chuki za kidini hapa au kuwafungia kwa muda kadhaa na kutoa mwongozo mpya JF kukataza hoja za kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini.