Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
hata kwa waislam. nipe ushahidi?

Nimeangalia hoja za malaria sugu na Tumain. Nataka kutofautiana na Dr. Slaa. Mawazo wanayoandika Malaria sugu na Tumain hapa kwa hakika ni ya kubomoa umoja wa Watanzania. Lengo la JF siyo kuwagawanya watanzania kwa misingi ya kidini. Nilishawaomba mara nyingi Mods kuwa mijadala ya kidini ipelekwe sehemu husika yenye mijadala ya kidini ya hoja mchanganyiko au ufutwe kabisa JF. Jukwaa la siasa lisigeuzwe na Malaria Sugu na Tumain kama jukwaa la kupandikiza na kuendeleza chuki za kidini. Kwa dhati kabisa nawaomba Mods wafute hapa hoja zote za chuki za kidini. Hatuwezi kuvumilia tabia za watu kuendeleza na kupandikiza chuki za kidini na kuubomoa umoja wa Watanzania. JF sasa inasomwa na Watanzania wengi, vijana na watu wazima, ni mafundisho gani Tumain na Malaria Sugu wanayatoa kwa Watanzania. Dr Slaa kura ya yeyote ni muhimu, lakini hatuwezi kuvumilia Tumain na Malaria sugu waendelee kuitumia JF kama jukwaa la kubomoa umoja wa Watanzania. Kwa hiyo Mods naomba mtoe adhabu sitahiki kwa Tumain na Malaria sugu kwa kufuta posti zao za chuki za kidini hapa au kuwafungia kwa muda kadhaa na kutoa mwongozo mpya JF kukataza hoja za kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini.
 
NI UJINGA SANA NA NI UPUUZI kumuona mtu hafai kugombea kutokana na dini yake. Kama watu hawatamchagua Kikwete kwa kuwa ni muislamu itakuwa ni ujinga na akili finyu. Na kama wakimchagua kwa kuwa ni muislamu utakuwa ni ujinga zaidi. Same applies to Dk Slaa. UDINI ni UJINGA. We are Tanzanians first, baadaye ndio zinakuja dini zetu na makabila yetu. lakini kwanza baada ya kuwa watanzania.
Huo ni ukweli mtupu! waambie mzee
 
Bila kumsahau Mzee mwenye hati miliki ya CCM Yusuph Makamba. Mkuu Pasco hii PHD ya JK na Karume ni za nini kweli?
Kama ulikuwa hujajua kuwa ni za siasa basi acha kuchangia kuhusu watu hawa. hawa jamaa Ni wapotoshaji wa nchi hii
 
kwanza kura yako haitasaidia..bora ukae nayo uendelee kumkampenia kilaza wenu JK
Wewe Kigogo ni jiniasi kabisa kwanini bado upo hapo? ah!
Anyway, watu kama hawa ngoja waendelee kushangilia fisi alapo mifupa wakitegemea atawaachia kidogo.

Lazima mtoke patupu! Badilikeni mpate japo kidogo.
 
Wenger,
Nadhani si vema kuikataa kura ya Malaria Sugu. Malaria Sugu kwenye Jamvi hili tunamjua wote kama mchokozi. Na wakati mwingine uchokozi wa aina hiyo ni mzuri. Hatuhitaji kutukanana. Kama yeye hatatoa kura yake hiyo ni haki yake wala tusimlazimishe. Na mimi nadhani hata kura yake tunaihitaji, hakuna kura ya mtanzania tunayoikataa, kura ni kura, kura haina sifa ya ubaya au uzuri bora ni kura halali. Thanksa wote, Thanks Malaria Sugu.
Dr. Slaa naomba kutofautiana na wewe kidogo. Mawazo wanayoandika Malaria sugu na Tumain hapa kwa hakika ni ya kubomoa umoja wa Watanzania. Lengo la JF siyo kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Nilishawaomba mara nyingi Mods kuwa mijadala ya kidini ipelekwe sehemu husika yenye mijadala ya kidini, hoja mchanganyiko au ifutwe kabisa JF. Jukwaa la siasa na JF visigeuzwe na Malaria Sugu na Tumain kama majukwaa ya kupandikiza na kuendeleza chuki za kidini. Kwa dhati kabisa nawaomba Mods wafute hapa hoja zote za chuki za kidini. Hatuwezi kuvumilia tabia za watu kuendeleza na kupandikiza chuki za kidini na kuubomoa umoja wa Watanzania. JF sasa inasomwa na Watanzania wengi, vijana ambao bado hawajakomaa kiakili na watu wazima. Ni mafundisho gani ambayo Tumain na Malaria Sugu wanayatoa kwa Watanzania hawa?. Dr Slaa kura ya yeyote ni muhimu, lakini hatuwezi kuvumilia watu kuitumia JF kama jukwaa la kubomoa umoja wa Watanzania. Mods naomba muwafungie wahusika kwa muda kadhaa na kutoa mwongozo mpya JF kukataza hoja za kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini.
 
Huko kwenye kanisa anawaongoza kondoo wa kikatoliki wasiohoji chochote kwenye nchi kuna watu watahitaji mahakama ya kadhi na OIC si atawaua wote balaa hilo..

Tangu lini Padre akawa Rais wa NCHI aende kanisani kwao..aache TAMAA na NJAA

Wow! Sikuwa na habari hii!!!!!
 

Bwana/Bibi Malaria Sugu, kuna thread umeianzisha kisifia hotuba za Nyerer zinazorushwa na ITV. Unasema hotuba hizo zinafaa kwua funzo. Basi nakushauri endelea kuzisikiliza na kuna moja ambayo Nyerer anaonya kumchagua au kumkataa mgombea kutokana na dini yake. Nadhani utajifunza kitu unapoanza kuhoji masuala ya Dr Salaa na ukatoliki wake.
Hatuchaui Papa wala kardinali, tunachaua rais wa Tanzania
 
Wow! Sikuwa na habari hii!!!!!
Huyu jamaa anapotoosha jamii na huyo mwalimu alikuwa nani, halafu mzee wa kusini naye vipi.
Jaribu kuona watu hao walivyookuwa wakali na maisha yetu yalikuwa mazuri. Lakini siyo hilo tu tumeshasema wana JF kuwa acheni udini, Huyu jamaa nyie mshajua michango yake na mitazamo yake. kama hatuna unafiki tumpenni Dr.
 
Huko kwenye kanisa anawaongoza kondoo wa kikatoliki wasiohoji chochote kwenye nchi kuna watu watahitaji mahakama ya kadhi na OIC si atawaua wote balaa hilo..

Tangu lini Padre akawa Rais wa NCHI aende kanisani kwao..aache TAMAA na NJAA
wewe Unatupotosha, Huyo Mwalimu alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya na BWM naye hukohuko mbona hamna hoja hizo? Lakini mimi najiuliza ivi mawazo kama haya kumbe yapo!Yeye Dr. Siyo kiongozi wa kanisa, ila nchi na ameleta na kuongeza mambo chungu nzima. Hayo yalikuwa ya kanisa. Na pia mbona hatuulizi hayo yanayokuja ya Msikitini kabisa (OIC, Mahakama ya Kadhi) ni lini tena yaliwahi kutokea kama siyo kwa kambayuwayu tu.
HEBU TUACHE UDINI tucheki mtu mwenye maslahi ya Tanzania. Tuondoe ukoloni mambo leo tunufaike na raslimali zetu wenyewe. (Madini, na makampuni yetu) huku wafanyakazi wakirudisha mori wao kazini kama ENZI ZA MWALIMU. ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaa!
 
tawanyikeni mukaeleze na kuota elimu kwa watu,

ili wamchague mgombea huyu.

kuna yeyote kati yenu hapa jf bado hajarekebisha kadi yake ya kupigia?
Mimi nitatekeleza wito wako hii debate napeleka tarafa zote tarafa zangu 2 kule kyela nina vijana wangu wa kuzitawanya.Mijadala mingi nimefanya hivyo naomba wachangiaji watoe hoja zenyemaana mizaha ipunguzwe.Nashukuru mungu hata jarida la cheche nilifanya hivyo,wito kwa wanajf tumieni hii printable version kupeleka hii mijadala muhimu vijijini.Kwa kufanya hivyo utakuwa unaelemisha na kushiriki kuondoa fikra mgando kwa wapiga kura.Natoa shukrani za pekee kwa michango ya Mwanakijiji,Fieldmarshal,Invicible na wengine sifa zenu zinafahamika Ipinda na vitongoji vyake.
 
kiukweli kwenye hili tukianza leta dini tutajiuza nchi uwanja wa vita kama NIGERIA na kwingine kikubwa tumpe Dr au mmpinge kwa HOJA nasi DINI watanzani si ni wamoja dini makabila na rangi za nini leo/kipindi hiki.mkuu malaria sugu mbona mwenyekiti wako anasitiza kampeni za kistaarabu inakuaje!
 
Sipati Picha pale Rais Mteule Dr. Wilbroad Peter Slaa atakapoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akina RA, EL Nkapa na wenzake sijui watakimbilia wapi! Siewewi but nina uhakika WATAKIMBIA wapi SIJUI
 
DK SLAA NASHUKURU KWA MAJIBU
LKN NINA KISWALA KIDOGO TU

nasikia baadhi ya magazeti yansema umetumwa na wakatoliki kugombea. na mimi nikiunganisha phd yako na habari hiyo hua nahsi kuna ukweli jee kama muhusika unanitoa wasiwasi gani?

Usiwe na wasiwasi wowote MS. Dr Slaa anagombea Urais kama Mtanzania ambaye katiba ya nchi inamruhusu kufanya hivyo ali mradi tu anatimiza masharti yote ya kugombea nafasi ya Urais na pamoja Dr Slaa kuwa mkatoliki lakini wakatoliki hawajamtuma kugombea nafasi hiyo bali anafanya hivyo ili kulinda na kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania wote bila kujali dini zao au rangi ambayo kwa sasa hayana mtetezi na baadhi ya Watanzania na hata wanaojiita wawezekezaji kuifanya nchi yetu shamba la bibi katika kujichumia utajiri wa hali ya juu.

Kila la heri Dr Slaa, mwanzoni nilikasirika sana niliposikia utagombea Urais maana mimi ni mmoja wa wale ambao tulipenda ubaki bungeni lakini baada ya kutafakari sana kwa makini nikagundua halijaharibika neno. Nikakumbuka ugombeaji wa Obama, maana hakuna mtu aliyempa nafasi ya kumuangusha Hillary kaika kugombea nafasi ya Urais kupitia chama chake kutokana na kuwa na well organised people with a biggest fund raiser in America by the name of Bill Clinton lakini akafanikiwa. Kukawa na wasiwasi kwamba "American is not ready for a Black president" na ukitilia maanani kwamba population ya weusi ni ndogo ukilinganisha na Wazungu basi hitimisho likawa ni hilo kwamba Obama hatachaguliwa kwa kuwa tu ni mweusi, lakini bado akafanya miujiza na hatimaye kuustaajabisha Ulimwengu maana wengi hatukutegemea kumuona Rais mweusi wa Marekani in our life time.

Hivyo naamini na wewe unaweza kabisa kumshinda Kikwete na kuustaajabisha Ulimwengu, pamoja na kuwa kazi uliyonayo mbele yako ni nzito sana. Muombe mola wako akupe muongozo katika kipindi hiki na wale wote ambao tunapenda mafanikio yako utakuwa kwenye sala zetu kila siku iendayo kwa Mungu kukuombea afya njema na mafanikio. Ukifanya kampeni zako vizuri na kuyaweka maovu yote ya CCM yanayosababisha nchi yetu kutokuwa na maendeleo na kuweka wazi sera zako za kuinua hali ya maisha ya Watanzania walio wengi ninaamini kabisa unaweza kabisa kushinda na pia kuisadia CHADEMA kuongeza idadi ya viti bungeni.

Tufahamishe wale tunaotaka kukuchangia kama tunaruhusiwa kufanya hivyo na kama tunaruhusiwa wapi tupeleke michango yetu. Kila la heri Dr Slaa.
 
Acha hizo! kwani Dr kikwete kasomea wapi u- dakitari?, mbona kuna Profesa Mwandosya, Sarungi, na waziri wa sasa Elimu na Mafunzo ya ufundi kazi walizo fanya hazionekani wakati Dr Slaa anaonesha kunga'ra.
 
kura yangu haipati mpaka anifanulie hasa udokta wake atautumia vipi wakati yeye ni dokta wa maswala ya dini?

Ukitaka kujua udokta wake ataumia vipi angalia rekodi yake katika bunge lililomalizika. Dr Slaa ni mtanzania wa kwanza kusimama bungeni na kutamka kwa uwazi bila kumumunya maneno ufisadi unaofanywa na watendaji mbalimbali bila kujali usalama wake unawekwa katika risk. Dr. Slaa amekuwa catalyst ya bunge na watanzania kuanza kuongea maovu ya serikali bila woga. Dr Slaa amekuwa ni mwiba kwa wale wote wanaoihujumu nchi ya Tanzania, nafikiri katika haya yote sikuwahi kumsikia hata siku moja akianza na kusema "Kwa kutumia udokta wangu naweka hadharani, meremeta, EPA, Richmond et al.

Sasa wewe usiyekuwa na busara za kujua kuwa dini is nothing but a tool for people to leave with peace and harmony during and after life, basi Dr Slaa atatumia Imani yake kuhakikisha hilo linafanyika hapa duniani bila kumwogopa mtu zaidi ya mungu aliyemleta na atamwondosha pindi muda wake ukifika. Ukiona mtu anaanza kutumia dini au kabila kama kigezo cha uongozi ujue mtu huyo amefilisika na hafai kabisa kuwa katika siasa.

Propaganda si uongo bali ni kutumia mafanikio uliyopata kuonesha wananchi ili kuwashawishi wakufikirie tena. Tokea tumepata uhuru nchi yetu imeongozwa na marais wa dini zote japo hakuna tofauti yoyote kwani wote hawa walitumia dini kupatia uongozi ila wakashindwa kutumia dini kuongoza (Kwani dini inasema usiibe, usidhurumu, usizini, usipendelee, utoe haki bila kujali ni nani yupo mbele yako) haya wameyashindwa kwa nadharia ya kulindana ndani ya chama.
 
Mi baada ya kusikia Dr Slaa anagombea, Nilitoa kele na kushangilia kwa shangwe nikisema sasa mwelekeo wa nchi umebadilika.

Mungu amesha ingilia kati na kazi iliyo baki ni kufanya mapinduzi ya kura. Mi nami niko tayari kuchangia ili hii tunu ituletee mabadiliko ya kweli Tanzania tuachane na usanii wa viongozi waliopo madarakani tangu UHURU mpaka leo hamna mabadiliko! INASIKITISHA saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana
 
Slaa(13).jpg

Dr Willibrod Slaa



Having been appointed by the opposition CHADEMA’s Central Committee ( CC) to be its presidential candidate in the coming general elections, Dr Willibrod Slaa has said he will not comment on the decision through the press until the final nomination process is completed.
Speaking to The Guardian on Sunday over the weekend, the Chadema, Secretary General said his decision to keep quiet emanates from his fear of compromising the democratic process.
The Guardian On Sunday has sought to seek Dr Slaa’s comments on a wide range of political, social and economic issues, including his feelings on the decision reached by the party’s major decision-making organ.
“I understand that you are my friend but to be honest I would not say anything in press before the completion of the nomination process because if I do so I will be compromising the democratic process,’” he said.
He added that he would also be ready to give his views after meeting his voters in Karatu Constituency. But Dr Slaa’s entry into presidential race, mid this week, has been greeted with mixed feelings; some saying the decision would make him disappear from the political spotlight.
Hamad Rashid Mohammed who is the leader of the opposition camp in Parliament has been quoted mid this week as saying the decision would slap a heavy blow to the opposition team in the House.
But Chedema’s National Chairman Freeman Mbowe has said the decision to ask Dr Slaa to participate in the presidential race was reached after intensive consultations. The public now is of the view that by asking Dr Slaa to participate in the presidential race Chadema has made a glaring technical mistake since it has now literally surrendered Karatu constituency to the opposition.
However, political pundits believe Dr Slaa’s participation in the presidential race would enable CHADEMA secure a considerable number of Parliamentary seats since he is a ‘political capital’.
But Chadema’s deputy secretary general Kabwe Zuberi Zitto, this week, responded saying that CC’s decision was not final, since the candidate was to be approved by the party’s general meeting, which will be held on August 10.
If the party’s Congress endorses Dr Slaa for the presidential battle, he will take on CCM candidate President Jakaya Kikwete, CUF’s Prof Ibrahim Lipumba and TLP’s aspirant Mutamwega Mugaywa.
 
Wapinzani muungeni mkono Dk. Slaa
ban.maswali.jpg


Ansbert Ngurumo


KAULI ya Mbunge wa zamani wa Rorya, Mabere Marando, imenikuna.
Siku alipojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliwakejeli wanaopinga uteuzi wa Dk. Wilbrod Slaa kuwa mgombea urais, huku wakisisitiza kuwa ingefaa aendelee kutoa upinzani mkali bungeni kama alivyofanya katika miaka mitano iliyopita.

Hoja ya Marando ni kwamba CCM wanataka wapingwe na waendelee kukaa madarakani; na kwamba sasa wakati umefika, tuwapinge na kuwaondoa madarakani.

Na tukichunguza hoja za wanaolialia kwamba Dk. Slaa aendelee na ubunge badala ya kugombea urais, utagundua mambo kadhaa tunayopaswa kuyafanyia kazi.

Kwanza, kuna kasumba kwamba wapinzani wanapaswa wagombee ubunge, waongeze nguvu bungeni; lakini wasigombee urais.

Maana ya kasumba hii ni kwamba kuna wanaodhani wakati wa CCM kuondoka madarakani haujafika.

Na maana ya nyongeza ni kwamba wapo watu wanaofikiri kwamba kwa kuwa mgombea wa CCM ni rais aliye madarakani, tayari ameshashinda!

Huu ni ugonjwa wa akili na ujinga ambao CCM inautumia kuendelea kupuuza wananchi, kuwatumia na kuwanunua ili ibaki madarakani.

Maana laiti wangejua kuwa rais aliye madarakani mwenyewe hana uhakika wa kushinda, wasingesema hivyo. Rais Kikwete mwenyewe, licha ya dharau aliyowaonyesha wafanyakazi akisema "hata msiponichagua nitashinda", hana uhakika wa ushindi.

Bado anahitaji nguvu ya fedha nyingi (zaidi ya sh bilioni 50) na mfumo wa kiserikali kujitafutia kura.

Na wasiwasi huu ndio unawafanya wanapropaganda wake wapenyeze hoja kwamba nafasi inayomfaa Dk. Slaa ni ubunge, si urais.

Pili, inaonekana wananchi walio wengi hawajajua nafasi na dhamana anayobeba rais wa nchi. Maana watu wale wale wanaolalamikia usanii na ufisadi wa watawala waliopo, wanapaswa kuwa wa mwisho kumbeza mwanasiasa shujaa kama Dk. Slaa.

Tatu, hoja ya kumtaka Dk. Slaa abaki bungeni ni dharau au ujinga usiomithilika, kwani vigezo vyote vya kiutafiti vinabainisha kuwa katika miaka mitano iliyopita, Dk. Slaa amekuwa mbunge kinara, ambaye ameitetemesha serikali kwa hoja kali, nzito na zilizotafitiwa.

Ameonyesha umakini usiomithilika katika kujenga hoja bungeni, na ana uelewa mpana wa masuala ya kiutawala, kitaifa na kimataifa. Hata wasiompenda, wanakiri kwamba mtu asiye na akili timamu ndiye anaweza kusimama akabeza mchango wa kisiasa wa Dk. Slaa katika nchi hii.

Na ni mpuuzi pekee anayeweza kufikiri, na hata kueneza uvumi mchafu, kwamba mbunge bora hafai kuwa rais bora!

Maana unapompambanisha na rais Kikwete, unakuwa unashindanisha umakini na usanii. Itakuwa ajabu kama Watanzania watashabikia usanii na kubeza umakini.

Na hili ni moja ya masuala ambayo watu makini hatuwezi kuogopa kuyasema. Ni swali ambalo hatuwezi kusita kuhoji.

Maana, kama alivyosema Marando, kama Watanzania wamekuwa wakilialia na kuhoji yu wapi wa kupambana na kumwondoa Rais Kikwete madarakani, Dk. Slaa ni sehemu ya jibu makini.

Wale ambao wamekuwa wakisoma makala zetu na kutuhoji: "Ndiyo tunakubaliana kwamba Kikwete ameshindwa. Lakini sasa tumuweke nani?" Dk. Slaa na chama chake wameshatoa jibu.

Tusimlazimishe Dk. Slaa kuendelea na kuikosoa serikali. Tumsaidie kuiondoa madarakani.

Amekaa bungeni kwa miaka 15 mfululizo. Tumpongeze kwa kukataa usultani wa Karatu. Wanaomtaka aendelee kuwa mbunge, wanapaswa kwanza kutambua mchango wake bungeni, pia kujiuliza kama yeye binafsi anapendelea kuendelea na ubunge.

Lakini kuna la ziada. Kama Dk. Slaa amesaidia kuitetemesha serikali bungeni, basi tushikamane naye kuwatafuta kina Slaa wengine katika miaka mitano ijayo.

Na kwa kufanya hivyo, Dk. Slaa atakuwa anakuza na kujenga chama chake, akianzia pale walipoachia wenzake mwaka 2005. Maana hatutarajii chama chochote kiongeze idadi ya wabunge bila kuwa na mgombea urais aliye makini.

Nionavyo mimi, Dk. Slaa si mgombea wa urais kupitia CHADEMA tu, bali ni alama ya upinzani uliokua na kukomaa.

Na kama wapinzani walikuwa wanatafuta mgombea atakayewaunganisha na kubeba bendera dhidi ya utawala wa CCM, sasa amepatikana. Wamuunge mkono. Amepatikana mtu wa kutusaidia kuondokana na ombwe la uongozi.
 
Wachangiaji,
Mie nina swali moja muhimu sana.

Hivi kama CCM ikishinda kwenye uchaguzi wa wabunge (dalili inaonyesha hivyo) na Dr. W. Slaa akawa Rais wa Tanzania mwakani (dalili inaonyesha hivyo), nani atamchagua Waziri Mkuu? Waziri Mkuu anaweza kutoka Chadema au CCM? Nani atachagua Mawaziri?

Kama sheria inasema Chama kilichoshinda ndicho kinachotowa Waziri na wao ndiyo wanakuwa na sauti kubwa bungeni, kwa nini swala la Mahakama ya kadhi na kubadili katiba au Sheria linaletwa kwenye uhusiano na RAIS? Rais hapa yeye kazi yake si kweka Sahihi maamuzi ya BUNGE? Kama kuna utendaji mbaya, basi wakulaumiwa si SERIKALI na si RAIS?

Kusema Rais Slaa atabadili hili au katumwa na Kanisa, wakati CCM ndiyo itakuwa bungeni na Serikalini, nashindwa kuelewa "UELEWA" wa katiba ya Tanzania wa watu kama Tumain. Kuna mazoea mabaya tumeshayajenga kuwa Rais ndiye anafanya hili na lile. Imekuwa hivyo kwa sababu mara zote mwenyekiti wa CCM ndiyo Rais wa Tanzania na ndiye anakuwa Boss wa kuteuwa PM na Mawaziri wake. Kila kitu kinazunguka kwenye mwenyekiti wa CCM.

Raha pekee itakayotokea hapa sasa ni kwa mara ya kwanza, bunge la Tanzania itabidi waache uvivu na kuanza kujua sheria zao maana vinginevyo, Slaa atawaburuza. Serikali ya Tanzania itabidi waanze kufahamu sheria na uwezo wao maana vinginevyo Slaa atawaburuza. Mahakama pia itabidi hatimaye iwe mahakama.

Tumain ambaye unaona kabisa kuwa kashachanganyikiwa baada ya kusikia jina la Slaa (tuliwaonya mfanye kazi na nyie mkasema CCM FOR LIFE), anakwenda kila sehemu kutoa lugha zisizo na kichwa wala miguu. Unaweza kumchukia Malaria Sugu ila jamaa walau anaandika anachokijua na KUCHOKOZA, tofauti na Tumain. Nashukuru Malaria Sugu kwa kumpa glass ya maji huyu jamaa yako ili apowe kidogo. Inabidi kuheshimu kuwepo kwa Dr Slaa hapa JF na tena kwa jina lake. Wengi walikimbia ila yeye kabaki. Tutumie kuwepo kwake na tumpe heshima kwa kazi yake, umri wake na hapo mwakani ATAKUWA NDIYE RAIS WETU. Unaweza kuuliza swali na hata kushambulia kwa baya alilolifanya kama Mwana Siasa.

Mwisho kwa wapenzi wote wa Dr. Slaa, msomeni vizuri sana Malaria Sugu. Umdhaniaye ndiye, kumbe siye.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom