Dr Slaa na mchumba wake watakiwa kufika mahakamani

Dr Slaa na mchumba wake watakiwa kufika mahakamani

Hadi amezaa na Josephine, Dr Slaa yuko kimya sana angetoka kufafanua hili jambo litamchafua pasipo sababu. Kama ameamua kuishi na huyo mama hana sababu za kukaa kimya wakati jamii inaumba maneno mengi juu ya uhusiano huo wa kimapenzi.

Wewe unatakam limchafue mara ngapi? Bila Kashfa hii nakuhakikishia hata CCM wangeiba vipi wasingeweza kupiku kura zake/ Likini imagne watu wa ngazu za chini ambao ndio wengi burudani pekee waliyonayoo ni katika ndoa zao asa anatokea mtu wa CCM anadai mgombea huyu kapor mke wa mtu, unafikiri mpiga kura huyu alichukua uamuzi gani?
 
sawa, wako wengi lakini unataka kuwa na kiongozi mzizi sijui muasherati, la hasha.

Nilidhani Dr Slaa angetenda yale anayohubiri, kwamba tuwe wasafi; usafi sio kwenye ufisadi tu usafi hata kwenye maisha yetu na matendo yaetu ya kila siku. Huwezi kuishi, kuwa na mchumba au kuzaa na mwanamke ambaye ni mke wa mtu hatafu useme mbona kila mtu anaye, this is unacceptable kwa kweli.

Nimependa signature yako sana,
Ebu rudia tena nizidi kucheka
Umenifanya nimecheka sana na mpaka sasa nacheka.
 
Hizi hila za hawa magamba,
ila mwisho wao ushaanza kuonekana ,
 
Naelewa wengi wenu mmejikita kwenye upande wa "mkataba" wa ndoa kuliko uhalisia wa ndoa yenyewe.

Sidhani kama huyu ndugu Mahimbo alinyang'anywa mke, huyu alimtelekeza na baada ya kujuwa yuko na Slaa akaona hapo ndo pa kutokea.

Hata hivyo kwa upande mwingine najiuliza kama Dr Slaa mwenyewe ana washauri ama vipi?
Ni wazi kuna taswira alitaka kuijenga kabla ya uchaguzi mkuu, lakini strategically, something went wrong somewhere...
 
Mungu kaumba wanaume kwa mfano wa pekee kumbe katika umri huo bado machine ni bomba kiasi cha kumtosheleza binti mdogo.

Ha ha ha haaaaa wataka kusema Slaa amejaaliwa kwa mashine ? ha ha ha haaaaaaaaaa

 
Naelewa wengi wenu mmejikita kwenye upande wa "mkataba" wa ndoa kuliko uhalisia wa ndoa yenyewe.

Sidhani kama huyu ndugu Mahimbo alinyang'anywa mke, huyu alimtelekeza na baada ya kujuwa yuko na Slaa akaona hapo ndo pa kutokea.

Hata hivyo kwa upande mwingine najiuliza kama Dr Slaa mwenyewe ana washauri ama vipi?
Ni wazi kuna taswira alitaka kuijenga kabla ya uchaguzi mkuu, lakini strategically, something went wrong somewhere...

Kwa hiyo wewe upo upande wa Slaa, kwenye suala ili utaangaika sana kumtetea Slaa, suala la Slaa kuchukuwa mke wa mtu wala haliitaji kuwa na PhD watu wote wanajua.

Mwisho wa siku utaona watu wanamchafua Slaa, lakini sio kweli, yeye kama kioo cha jamii ndio anajichafua mwenyewe!
 
Kwa hiyo wewe upo upande wa Slaa, kwenye suala ili utaangaika sana kumtetea Slaa, suala la Slaa kuchukuwa mke wa mtu wala haliitaji kuwa na PhD watu wote wanajua.

Mwisho wa siku utaona watu wanamchafua Slaa, lakini sio kweli, yeye kama kioo cha jamii ndio anajichafua mwenyewe!
Mkuu Ritz mbona jamaa amemaliza hapo mwisho. Kwamba kabla ya uchaguzi Dr. Slaa alitaka kujenga sura kwamba ana mke lakini washauri wake wakamshauri vibaya na kujikuta amemchukua mke wa mtu; strategically something went wrong!
 
Mkuu Ritz mbona jamaa amemaliza hapo mwisho. Kwamba kabla ya uchaguzi Dr. Slaa alitaka kujenga sura kwamba ana mke lakini washauri wake wakamshauri vibaya na kujikuta amemchukua mke wa mtu; strategically something went wrong!

Mkuu Kimbunga,
Ni kweli walimshauri vibaya!
 
huh..hivi kumbe inawezekana?yasser arafat alipooa akiwa na miaka 75 nilishangaa ila slaa amenifumbua macho na vile mademu wanazengua zama hizi i gonna wait till i hit 60.then i find maself a fiancee of 20.hongera dr for your inspiration.

Jamaa bado anamchumba dah!
 
Ngoja tuchokonoe kidogo;

Hivi huyu Josephine alikuwa akifanya kazi pale ofisini chadema kabla Dokta wa ukweli hajafanya vitu vyake au alimvua gamba kutokea CCM akamvisha gwanda, kazi na tumbo mbwii, all in one?

Hapo inabidi mje na vina , msikurupuke maana kuna watu wanasota huko hawakaribishwi hata ofisi za kata wacha makao makuu.
 
headline_bullet.jpg
Vinginevyo hati ya kumkamata itatolewa



SlaaChadema(7).jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa


Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa, amemuonya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad

Slaa na mchumba wake, Josephine, kwa kushindwa kufika mahakamani jana.
Kutokana na hali hiyo, amewaamuru kufika leo asubuhi kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao vinginevyo atatoa hati ya kuwakamata.

Mshitakiwa mwingine ambaye alionywa na Hakimu Magesa kwa kutofika mahakamani hapo jana ni Aquline Chuwa.
Washtakiwa wengine 16 walifika mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka 13

badala ya manane na kesi dhidi ya yao itaanza kusikilizwa leo.
Dk. Slaa na wenzake wanatakiwa kusomewa mashtaka yao leo saa 2:00 asubuhi na baada ya hapo wataungana na wenzao wakati kesi yao itakapoanza kusikilizwa.

Hakimu Magesa alisema endapo washtakiwa hao watashindwa kufika leo, atalazimika kutoa hati ya kuwakamata.
Wakili wa washtakiwa hao, Albert Msando, akiwatetea Dk. Slaa na wenzake kwa

kutofika mahakamani, alidai kuwa wamechanganya tarehe ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

Awali, Wakili wa Serikali, Edwin Kakolaki, aliiomba mahakama kutoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao na kuwapeleka mahakamani kwa nguvu kwa kudharau mahakama.

“Hawa washtakiwa si kweli kama anavyodai wakili wao kuwa wamechanganya tarehe ya kesi kutokana na wingi wa kesi walizonazo, kwa kuwa wana wadhamini wao, wangepaswa kufanya nao mawasiliano pamoja na wakili wao hivyo naomba mahakama kutoa hati ya

kuwakamata na kuwaleta hapa kwa nguvu ili wasipate mkanganyiko wa kuchangaya tarehe,” alidai.
Aidha, aliiomba mahakama kuendelea na usikilizaji wa kesi hiyo kama walivyokubaliana na washitakiwa ambao hawakuwepo, wasomewe mashitaka yao leo.

Hata hivyo, Hakimu Magesa aliamuru kusomwa kwa mashtaka ya awali kwa washtakiwa hao, ambayo yameongezwa hadi 13.
Wakili Kakolaki alidai washitakiwa wote 19 wanashitakiwa kwa kosa la kwanza la kupanga njama Januari 3 na 5, 2011 kutenda kosa la kufanya fujo na kosa la pili linawahusu washitakiwa 18, ambao wameshtakiwa kwa kufanya kusanyiko lisilo halali.

Katika shitaka la tatu, washitakiwa 18 wameshitakiwa kula njama kutenda kosa kwa kufanya kusanyiko lisilo halali.
Aliendelea kusoma shitaka la nne kuwa, washitakiwa 18 isipokuwa Samson Mwigamba, wanashitakiwa kuwa siku hiyo ya tukio walikula

njama ya kufanya vurugu baada ya katazo halali.
Shitaka la tano linawahusu Dk. Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo, la kula njama ya kutoa matamshi yenye lengo la kuleta uchochezi.

Shitaka la sita walisomewa washitakiwa watatu, ambao ni Ndesamburo, Dk. Slaa na Mwigamba, wakidaiwa kula njama kutenda kosa kwa kushawishi watu wengine kutenda kosa.
Shtaka la saba walisomewa washitakiwa 18 kwamba, walikataa amri halali iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji, iliyoelekeza jinsi ya kufanya maandamano na kuainisha njia za kupita wakati wa maandamano.

Akisoma shitaka la nane kwa washitakiwa 18, ilidaiwa walifanya kusanyiko lisilo halali, ambapo siku ya tukio watu zaidi ya watatu walikusanyika kwa ajili ya kutekeleza lengo moja na kukataa kutii amri ya OCD iliyowataka watawanyike.

Shitaka la tisa lilisomwa kwa washtakiwa 18 isipokuwa Mwigamba, la kufanya fujo, ambapo ilidaiwa kuwa wakiwa zaidi ya watatu walikusanyika kwa nia ya kufanya kusanyiko hata baada ya amri ya OCD kutolewa ya kuwataka watawanyike.
Shtaka la 10 linamhusu Dk. Slaa, la kutoa matamko yenye lengo la uchochezi.
Hata hivyo, kwa kuwa hakuwepo mahakamani, hakusomewa mpaka atakapofika leo mahakamani. Shtaka la 11 la kutoa matamshi ya

uchochezi lilisomwa dhidi ya Ndesamburo, ambapo ilidaiwa kuwa alitamka kuwa: “Nakuambia Kikwete leo hii umenitia saini ya vurugu nchini Tanzania, Polisi Arusha watapiga risasi zitaisha na tutawakamata, Kikwete kama huna baba Ndesamburo anapigwa na vichangachanga vyako.”

Katika shitaka la 12, washitakiwa wanadaiwa kutaka kuwatoa watu chini ya ulinzi halali na shitaka la 13 ni la kufanya fujo na kusababisha uvunjifu wa amani na kutia hofu wananchi wa maeneo hayo.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo.



CHANZO: NIPASHE

 
Ndo tunavyoila nchi yetu taratibu...kufanya mambo yasiyo na tija tuonekane tuko serious na tunajua tunachofanya.
 
Back
Top Bottom