Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru wa Tanganyika

Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru wa Tanganyika

My name is wayne palmer not john wayne...nipo hapahapa kaka yangu...

Nakukubali sana...ila unapo-turn radical haah...nasikitika sn..kwa sababu najua unavitu vingi...

Kama nchi hii inakuwa institution..basi wewe ni kati ya wale tunawaita...institutional memories...watu muhimu sana..

Wayne,
Mie kukuita John Wayne ni katika maskhara tu.
John Wayne alikuwa muigizaji mashuhuri wakati mie nakua Dar.

Nimeona filamu zake nyingi Empire Theatre.

Ikiwa hupendi nikuuite hivyo nitaacha.
Nimefurahi kuwa kuna baadhi ya mambo unayapenda.
 
Remote,Inaelekea hujasoma kitabu changu.Kitabu kimewataja wote walioshiriki katika harakati za kupigania uhuruDk. Kyaruzi akiwa mmojawapo.Usifanye haraka ya kulaumu kabla hujasoma yaliyoandikwa.
Mkuu nadhani uliwahi kuwataja akina Dk.Kyaruzi na Dk.Mutahangarwa kama sikosei, hapa baadhi ya wana JF wanataka kukuchemsha tu MkuuMS, sikumbuki kama uliwahi kusema Dk.Kyaruzi alisilimu(not sure of the term) na kujulikana kama Alhaji Dk.Kyaruzillah bin Iwe bin Bojo!! Mkuu ninacho kiona mimi nafikili baadhi ya members wanaona katika simulizi zako, wakina Dk.Kyaruzi na wenzake hawakupewa uzito wa kutosha in othewords walitajwa in a watered down format - tatizo ndilo hilo mkuu, I might be wrong.
 
Kwani huyu ni wa gerezani, kipata na aggrey. Naona sasa unaanza kuwa objective sio kila siku gerezani kana kwamba Tanganyik ilkuwa hapo tu.

We mdini kweli kweli kwahiyo sababu kataja vedasto ndo kaanza kua objective?!! Angesema ali au hamisi sio?!!
 
Tatizo humu watu wengi hawasomi makala kwa umakini wanakimbilia kucomment
 
Mkuu nadhani uliwahi kuwataja akina Dk.Kyaruzi na Dk.Mutahangarwa kama sikosei, hapa baadhi ya wana JF wanataka kukuchemsha tu MkuuMS, sikumbuki kama uliwahi kusema Dk.Kyaruzi alisilimu(not sure of the term) na kujulikana kama Alhaji Dk.Kyaruzillah bin Iwe bin Bojo!! Mkuu ninacho kiona mimi nafikili baadhi ya members wanaona katika simulizi zako, wakina Dk.Kyaruzi na wenzake hawakupewa uzito wa kutosha in othewords walitajwa in a watered down format - tatizo ndilo hilo mkuu, I might be wrong.

Bukyanagandi,
Kama ungenipatia majina ya hao ''watered down format'' In Sha Allah mimi ningechambua
na kuwekajamvini jinsi nilivyowaandika katika kitabu.

Natoa changamoto kwako na kwa yoyote yule alete majina.

Dk. Kyaruzi baada ya kuchaguliwa rais wa TAA 1950 hakudumu kwani 1951 akapewa uhamisho
kwenda Kingolwira kisha Nzega.

Kwa siasa za pale New Street huo ndiyo ukawa mwisho wake.
Ikiwa kama kuna mtu ana taarifa zake zaidi jamvi ndilo hili na atuletee maneno tufaidike.
 
sasa ni kwa nini historia ifichwe??

Historia hii ikiwatoa raha na bado inawanyima usingizi hadi leo.

Hakuna mahali katika historia ya uhuru wa Tanganyika maaskofu
wamekautana kuimba pambio uhuru uje.

Uwanja wa uhuru ulitawaliwa na masheikh na tawasul.
Hapa ndipo panapowatisha.

Sasa leo wataiandikaje historia hii?
Vijana watauliza ala kumbe nyie na wakoloni lenu lilikuwa moja!
 
Tumempa barabara hadi Kibaki lakini tuna wazalendo lukuki hata barabara za huko mikoani tunashindwa kuwapa. Itabidi akina Amani wa bukoba tuwaambie wampe Kyaruzi hata ile barabara ya Kashai kama kumbukumbu.
 
Bukyanagandi,Kama ungenipatia majina ya hao ''watered down format'' In Sha Allah mimi ningechambua na kuwekajamvini jinsi nilivyowaandika katika kitabu.Natoa changamoto kwako na kwa yoyote yule alete majina.Dk. Kyaruzi baada ya kuchaguliwa rais wa TAA 1950 hakudumu kwani 1951 akapewa uhamishokwenda Kingolwira kisha Nzega.Kwa siasa za pale New Street huo ndiyo ukawa mwisho wake.Ikiwa kama kuna mtu ana taarifa zake zaidi jamvi ndilo hili na atuletee maneno tufaidike.
Samahani mkuu nilikuwa sijasoma attachment yako, nimeipitia inaeleweka. Hivi Dk.Kyaruzi hakuacha popote copy ya manuscripts ya kitabu alicho taka ku-publish nasikia hata baadhi ya manuscripts za historia ya Sykes ziliwahi kupotea kimihujiza kuan ukweli gani katika hilo - tujuze mkuu. Kitu kingine Je, Dk. Mutahangarwa and Dk.Tsere walihishia wapi? Inaelekea Dk. Michael Lugazia na Dk.Kyaruzi waliendelea na mambo ya Uganga wa binadamu, in fact katika kukua kwangu sikuwahi kusikia Dk.Lugazia kujihusisha na mambo ya siasa. Mengine ntakuhuliza kadri tunavyo kwenda. CHEERS.
 
Sijawahi kucheka kama nilivyocheka leo! Duh, Mohamed Said! Eti anadhani itapatikana faida kwa kumkumbuka Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru kwa kutuletea makala iliyojaa ngano ambazo kama kawaida si zaidi ya porojo zilizotawaliwa na histohisia. Hadithi, hadithi! uongo njoo utamu kolea! Nitarudi.
 
Tumempa barabara hadi Kibaki lakini tuna wazalendo lukuki hata barabara za huko mikoani tunashindwa kuwapa. Itabidi akina Amani wa bukoba tuwaambie wampe Kyaruzi hata ile barabara ya Kashai kama kumbukumbu.
Mkuu napendekeza barabara karibu na Posta imepakana sana na ilipokuwa Hospitali yake. R.I.P Dk.Kyaruzi.
 
Mkuu napendekeza barabara karibu na Posta imepakana sana na ilipokuwa Hospitali yake. R.I.P Dk.Kyaruzi.

Ingelikuwa ni Abdu Sykes, Sheikh Hassan Bin Ameir na Mshume Kiyate nao ungelipendekeza wapewe barabara?????
 
Mzee karudi na hekaya za abunuasi, pumzika ulee wajukuu au wafate wenzio kwenye jukwaa la wastaafu utamkuta sir alex kule.
 
Nguruvi,
Mbona unajipongeza kwa silo?

Kwani hujasoma kitabu changu?
Hayo unayojisifia kuwa nimerekebisha mbona sihabadili kitu?

Yote hayo yamo kwenye kitabu changu.

Sasa wewe na Remote hiyo elimu mnayojipongeza mmetoa
kunibadili ni elimu ipi?

Huo ukweli ni ukweli upi?
Hiyo nguvu yako ya hoja iko wapi?

Ala hata kabla hujadurusu unaingia ulingoni na Mohamed Said!
We unataka kufia ulingoni?

Nguruvi una kichwa kigumu sana wewe mtu.
Nimekuwekea habari za Dk. Kyaruzi tena kwa namba kuanzia 1-...

Nikakueleza kuwa haya yametoka katika kitabu changu na juu
ya haya yote unakuja na hayo hapo juu...

Au ile post imekupita hukuisoma?

Sasa si unamtafuta undani Faiza bila ya sababu?

Akhiy Mohamed Said, huyu Nguruvi3 ni mfa maji haishi ...

Maana hana alijualo yeye mradi ababie hapa na pale na hata umpe jibu lipi yeye hatoridhika, na unajuwa kwanini> kwa sababu Hakuna askofu hata mmoja wala mchungaji tunaemsikia kwenye hizi harakati za kudai Uhuru. Basi hata kwa kusahauliwa pia hayumo? hapo sasa!
 
Sijawahi kucheka kama nilivyocheka leo! Duh, Mohamed Said! Eti anadhani itapatikana faida kwa kumkumbuka Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru kwa kutuletea makala iliyojaa ngano ambazo kama kawaida si zaidi ya porojo zilizotawaliwa na histohisia. Hadithi, hadithi! uongo njoo utamu kolea! Nitarudi.

Natamani nisikie mnatuletea habari za askofu au wachungaji waliopigania uhuru wa Tanganyika, au Kanisa lilikuwa halipo siku hizo?
 
This is just silly! ni habari ile ile ila kivingine! kwa kutumia Dr. Kyaruzi unataka kutuelekeza kuhusu Sykes! na kwa mgongo wake unataka kutuelezea histohisia ile ya kidini.
 
Ingelikuwa ni Abdu Sykes, Sheikh Hassan Bin Ameir na Mshume Kiyate nao ungelipendekeza wapewe barabara?????

Mdondoaji,
Hiyo ni fikra nzuri ya kuwaenzi mashujaa wetu.

TAA ilikuwa na madaktari watano na wote walichangia katika kuupigania uhuru wa
Tanganyika:

  1. Dk. Luciano Tsere
  2. Dk. Vedasto Kyaruzi
  3. Dk. WEB Mwanjisi
  4. Dk. Michael Lugazia
  5. Dk. Joseph Mutahangarwa
 
This is just silly! ni habari ile ile ila kivingine! kwa kutumia Dr. Kyaruzi unataka kutuelekeza kuhusu Sykes! na kwa mgongo wake unataka kutuelezea histohisia ile ya kidini.

MM,
Unavyopenda kuchambua hakuna wa kukukataza huu ukumbi ni
wa kubadilishana fikra.

Lakini elewa huwezi kumtaja Dk. Kyaruzi bila kumtaja Abdu Sykes.

Uongozi wao ndiyo uliotengeneza TAA Political Subcommittee 1950
kamati iliyokuja kuasisi TANU 1954
 
Back
Top Bottom