Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru wa Tanganyika

Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru wa Tanganyika

Sijawahi kucheka kama nilivyocheka leo! Duh, Mohamed Said! Eti anadhani itapatikana faida kwa kumkumbuka Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru kwa kutuletea makala iliyojaa ngano ambazo kama kawaida si zaidi ya porojo zilizotawaliwa na histohisia. Hadithi, hadithi! uongo njoo utamu kolea! Nitarudi.

Mag,
Faida ndiyo kma hii ya kuwa wanajamvi wanachangia na mimi nachangia
kueleza historia ya uhuru.

Je unajua kilitokea nini 1950 pale Arnautoglo Hall wakati TAA walipoitisha mkutano
wa uchaguzi?

Je unajua Schneider Abdillah Plantan alifanya nini siku ile mbele ya maofisa Wazungu
wa kikoloni?

Je unajua kuwa Schneider alikuwa akifanya kampeni ili kumwangusha kaka yake Mwalimu
Thomas Plantan aliyekuwa rais wa TAA?

Hizi ndizo faida za kumweleza Dk. Kyaruzi kwani kwa kumueleza yeye unawafikia na wale
ambao walifutwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ukirudi katika hili kama ulivyoahidi ndiyo starehe yangu.
Karibu.
 
hizi story za abunuasi za muhamedi said huwa zinachekesha sana full upepo
 
Sijawahi kucheka kama nilivyocheka leo! Duh, Mohamed Said! Eti anadhani itapatikana faida kwa kumkumbuka Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru kwa kutuletea makala iliyojaa ngano ambazo kama kawaida si zaidi ya porojo zilizotawaliwa na histohisia. Hadithi, hadithi! uongo njoo utamu kolea! Nitarudi.

Wewe utapata hasara wengine kama kawaida twavyonza ilmu kutoka kwa mwanahistoria mzee Mohamed Said. Faida ni kubwa mno inayopatikana ila kwa vipofu kama wewe na mwenzako nguruvi3 ni vigumu kukubali hadharani ukweli mkiogopea aibu ya kujulikana historia ya kweli.
 
Last edited by a moderator:
Wameacha kule kwingine! teh teh
Tumewaambia kuwa historia haikamiliki kwa sehemu moja. Ni kitu kilichopo katika mtiririko na utaratibu.
Nguvu ya hoja muhimu sana. Sasa wametambua kuwa historia ili ikamilike lazima ishirikishe wote na si kundi fulani.Wanatambua kuwa hakuna historia 'biased'

Nguvu ya hoja! tunashukuru sana. Turudi kule kwa vijana ili waendelee kutoa kashfa sisi tukiweka mambo sawa.
Hatimaye tumevumilia majina kashfa, matusi dhalili n.k. mwisho wa yote ukweli unasimama kama ulivyo 'hakuna nusu glasi'.
Remote hakuna kukata tamaa katika kutoa elimu ya umma, ni kazi nzito lakini ni yetu sote.

Ngoja niidurusu halafu tuangalie kwa microscope, tufanye dissection n.k.

Teh teh teh
ati Nguruvi3 kumbe kachura zote zile hapa jukwaani shida yako atajwe padri hata mmoja katika historia? Sasa kama hakukuwa na padri au mkristo ulitaka mzee mohamedi saidi atengeneze historia fake kama iliyofichwa karne na karne?
 
Last edited by a moderator:
Historia hii ikiwatoa raha na bado inawanyima usingizi hadi leo.

Hakuna mahali katika historia ya uhuru wa Tanganyika maaskofu
wamekautana kuimba pambio uhuru uje.

Uwanja wa uhuru ulitawaliwa na masheikh na tawasul.
Hapa ndipo panapowatisha.

Sasa leo wataiandikaje historia hii?
Vijana watauliza ala kumbe nyie na wakoloni lenu lilikuwa moja!
Mohamed Saidi, nilidhani utaibadiri misimamo yako ya kibaguzi! bado unaendeleza uhasama ambao haupo isipokuwa ndani ya akili yako iliyojaa chuki na uozo!
Fahamu wazi kuwa vijana hao hao wanaweza kuwauliza "masheikh" aah! kumbe nyie na wafanyabiashara ya watumwa (waarabu na waswahili) lenu lilikuwa moja!
 
Natamani nisikie mnatuletea habari za askofu au wachungaji waliopigania uhuru wa Tanganyika, au Kanisa lilikuwa halipo siku hizo?
Kama vile mimi nilivyo na hamu kubwa sana Mzee Mohamed Saidi atakavyo tuletea habari za masheikh na maustaadh waliofanya juhudi ya kukomesha biashara ya utumwa kule Zanzibar!
 
This is just silly! ni habari ile ile ila kivingine! kwa kutumia Dr. Kyaruzi unataka kutuelekeza kuhusu Sykes! na kwa mgongo wake unataka kutuelezea histohisia ile ya kidini.

Wewe jamaa bado hujafa tu!?...wewe ni mmojawapo ya Wanafiki/wazandiki wakubwa humu mitandaoni wasiolitakia mema Taifa letu changa.

Huna credibility ya kuuliza suali la maana au kutoa mchango wowote watu wenye maarifa yao wakakuamini,asilan abadan!

Kwenye mnakasha wa mwisho na Sheikh Mohamed Said,tulikuomba ulete/utoe uthibitisho wenye kuthibitika juu ya yale "madai"/tuhuma aka makhanatha yako yakuwa unajua na pia una "uthibitisho" ati Sheikh Mohamed Said ni Member wa Muslim Brotherhood,na wanafanza/anafanza mipango ya kuisilimisha nchi/Tanzania iwe chini ya Islamic Sharia na utumbo mwingineo mwingi ulioandika!?

Vipi sasa yakurubia takriban mwezi wa tano tangia tukuombe uthibitishe kwayo!?

Ahsanta.
 
Kwanini tusianzie na ile Christians Slave Trade aka "Atlantic" Slave Trade!?
Ustaadh gombesugu, habari ya siku nyingi jamaa yangu! Tuanzie popote tu sina shida! wote walifanya unyama wakutisha huku wakitumia jina la Mungu wao kuharalisha uhayawani wao! wala hatuna sababu yoyote ile ya kuwakumbatia baadhi kwa vile wanatuhusu na kuwabeza wengine kwavile hawatuhusu. gombesugu, vita na ukatili mkubwa duniani unafanya kwa mwamvuli wa imani za dini. Bila imani hizo dunia ingekuwa mahali bora sana pa kuishi!
 
Wewe utapata hasara wengine kama kawaida twavyonza ilmu kutoka kwa mwanahistoria mzee Mohamed Said. Faida ni kubwa mno inayopatikana ila kwa vipofu kama wewe na mwenzako nguruvi3 ni vigumu kukubali hadharani ukweli mkiogopea aibu ya kujulikana historia ya kweli.
Ayatollah CHAMVIGA, huyu mchochezi Mohamed Said tumetoka naye mbali...kwa miaka zaidi ya 15 hadithi yake ilikuwa kama hivi, nanukuu;
Mohamed Said said:
Katika kufanya hivi msomaji wa historia hii atakutana na nyaraka za Kleist Sykes zinazoeleza hali ya siasa katika Tanganyika katika miaka ya 1920. Mwanafunzi atasoma nini kiliwapelekea wazalendo wa Dar es Salaam waliozaliwa enzi za utawala wa Kijerumani kuasisi African Association mwaka 1929, Kleist akiwa katibu muasisi na nini kilipelekea yeye tena Kleist na rais wake katika African Association, Mzee bin Sudi kuasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933 na ilikuwaje ikawa viongozi na wanachama wa vyama hivi viwili ndiyo walikuja kuasisi TANU mwaka 1954 na kuongoza harakati za kupigania uhuru. Hii ni moja ya ukweli ambao unawatisha na kuwakera baadhi ya watu na hasa viongozi wetu wa sasa ambao hawakunyanyukia na TANU. Katika maelezo haya mwanafunzi wa historia atakutana na historia nyingine kabisa ya Wazulu, Wanubi na Wamanyema walioingizwa nchini na Wajerumani kama askari mamluki. Watoto wa askari hawa kama Kleist Sykes, Ibrahim Hamisi, Mzee bin Sudi, Thomas Plantan, Schneider Plantan, Ramadhani Plantan ndiyo waliokuja kuwasha moto wa ukombozi wa Tanganyika na baadhi yao walishuhudia uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Kwa miaka zaidi ya 15 hizi hadithi zake hazikupata upinzani kwa sababu wasikilizaji wake hawakuweza kuhoji ukweli wa simulizi zake hadi pale alipojaribu kuzileta ngano zake JF. Kuna wakati nimewahi hata kujiuliza inakuwaje watu na akili zao wanaweza wakaamini madai kama haya yaliyotolewa mwaka 2012, nanukuu;
Mohamed Said said:
Mfumo kristo ni nini? Mfumo wa damu umeitwa mfumo kwa sababu damu imeenea kote mwilini. Watu wa dini ya kikristo imehodhi asassi zote za nyeti za uongozi na mamlaka katika nchi hii, sehemu zote za nguvu/maamuzi ya dola zimeshikwa na wakristo tangu uongozi wa juu ikulu mpaka kiongozi wa mtaa uongozi wote umeshikwa na mfumo kristo. Na hao walioshika hizo nyadhifa wanazitumia kuuendeleza ukristo na kukandamiza uislamu.
Wakati anaongea haya, Ikulu yupo Al Haji Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Tanzania, Kiongozi anayeunda na kuiongoza Serikali, jemadari mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa chama tawala CCM. Inakuwaje wasikilizaji wanaitikia hewala, je hawaoni, hawasikii, hawagusi na hawanusi...have they lost all sense of reality? Have the symptoms of distorted reality become so severe that they have lost touch with the world? ...That they to perceive things so differently?

Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote waliosimama kidete kumuumbua huyu adui asiyelitakia mema taifa letu kwa kuziita hadithi zake ngano (calling a spade a spade) na heshima yake mbele ya jamii yenye uelewa imeshuka kwa kiwango kikubwa. Hii ya kutuletea habari za Dr. Vedasto Kyaruzi ni katika kujitapatapa na kujikosha na kamwe haiwezi kuuzima moto unaomwakia...alilia moto na uzidi kumchoma popote alipo. Santuri yake, kwa kutumia maneno yake mwenyewe Mohamed Said, imechuja...
 
Zi wapi habari za Erica Fiah?

Udadisi,

  1. Tandon called Abdulwahid and other patriots like Chege Kibachia, Makhan Singh, Fred Kubai, James Kivu, I.K. Musazi, Erika Fiah and Gama Pinto as ‘veteran leaders of the struggle of the peoples of East Africa... whom our recent historians have forgotten'.
  2. Ramadhani Mashado Plantan broke this monopoly and unholy alliance between the colonial government and missionaries. Following the footsteps of Erika Fiah, the first African to publish a newspaper in colonial Tanganyika, Mashado registered his own paper Zuhra.
  3. Kleist was secretary of the African Association for many years with a brief period in 1933 when he resigned after clashing with Erika Fiah.
  4. But Fiah did not stay long in power; he was soon phased out by Union members and one Salum Mohamed took over the leadership from him.
  5. Fiah, Kleist's arch-enemy was elected General Secretary of the Dockworkers' Union to replace him. But Fiah did not stay long in power; he was soon phased out by Union members and one Salum Mohamed took over the leadership from him.
  6. Abdulwahid should resign and pave the way for Fiah to take over leadership of the union. This created two factions within the union. One faction wanted Abdulwahid to continue leading the union and another called for his immediate resignation.
  7. Fiah was preferred because dockworkers thought Abdulwahid was too moderate and supported Fiah's radical stand.
  8. Abdulwahid also came to learn that his former opponent for the union post and his father's political adversary of many years, Erika Fiah, was instigating the union leadership to overthrow ‘that South African son of Kleist.'
  9. A biography of Erika Fiah is in Kwetu No.11, 4 th August, 1940.
 
Ayatollah CHAMVIGA, huyu mchochezi Mohamed Said tumetoka naye mbali...kwa miaka zaidi ya 15 hadithi yake ilikuwa kama hivi, nanukuu;

Kwa miaka zaidi ya 15 hizi hadithi zake hazikupata upinzani kwa sababu wasikilizaji wake hawakuweza kuhoji ukweli wa simulizi zake hadi pale alipojaribu kuzileta ngano zake JF. Kuna wakati nimewahi hata kujiuliza inakuwaje watu na akili zao wanaweza wakaamini madai kama haya yaliyotolewa mwaka 2012, nanukuu;

Wakati anaongea haya, Ikulu yupo Al Haji Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Tanzania, Kiongozi anayeunda na kuiongoza Serikali, jemadari mkuu wa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa chama tawala CCM. Inakuwaje wasikilizaji wanaitikia hewala, je hawaoni, hawasikii, hawagusi na hawanusi...have they lost all sense of reality? Have the symptoms of distorted reality become so severe that they have lost touch with the world? ...That they to perceive things so differently?

Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote waliosimama kidete kumuumbua huyu adui asiyelitakia mema taifa letu kwa kuziita hadithi zake ngano (calling a spade a spade) na heshima yake mbele ya jamii yenye uelewa imeshuka kwa kiwango kikubwa. Hii ya kutuletea habari za Dr. Vedasto Kyaruzi ni katika kujitapatapa na kujikosha na kamwe haiwezi kuuzima moto unaomwakia...alilia moto na uzidi kumchoma popote alipo. Santuri yake, kwa kutumia maneno yake mwenyewe Mohamed Said, imechuja...

Mag3,
Try another one...
 
Udadisi,

  1. Tandon called Abdulwahid and other patriots like Chege Kibachia, Makhan Singh, Fred Kubai, James Kivu, I.K. Musazi, Erika Fiah and Gama Pinto as ‘veteran leaders of the struggle of the peoples of East Africa... whom our recent historians have forgotten'.
  2. Ramadhani Mashado Plantan broke this monopoly and unholy alliance between the colonial government and missionaries. Following the footsteps of Erika Fiah, the first African to publish a newspaper in colonial Tanganyika, Mashado registered his own paper Zuhra.
  3. Kleist was secretary of the African Association for many years with a brief period in 1933 when he resigned after clashing with Erika Fiah.
  4. But Fiah did not stay long in power; he was soon phased out by Union members and one Salum Mohamed took over the leadership from him.
  5. Fiah, Kleist's arch-enemy was elected General Secretary of the Dockworkers' Union to replace him. But Fiah did not stay long in power; he was soon phased out by Union members and one Salum Mohamed took over the leadership from him.
  6. Abdulwahid should resign and pave the way for Fiah to take over leadership of the union. This created two factions within the union. One faction wanted Abdulwahid to continue leading the union and another called for his immediate resignation.
  7. Fiah was preferred because dockworkers thought Abdulwahid was too moderate and supported Fiah's radical stand.
  8. Abdulwahid also came to learn that his former opponent for the union post and his father's political adversary of many years, Erika Fiah, was instigating the union leadership to overthrow ‘that South African son of Kleist.'
  9. A biography of Erika Fiah is in Kwetu No.11, 4 th August, 1940.

Shukrani, sasa nahitaji taarifa zaidi za yule ambaye unasema walikuwa wanamuita "Benki", shajara zake zinapatikana wapi?

Halafu katika sura iliyoandikwa na mjukuu wa Mzee Sykes, ameweka wosia unaoonesha kuwa Mzee alitaka mtoto mmojawapo kati ya watoto wake watatu awe mfanyabiashara, nahitaji taarifa za huyo jamaa, nafanya utafiti kuhusu mafanikio ya kibiashara ya Watanganyika wa enzi hizo, je yaliishia nchini tu au yalivuka hadi ng'ambo?

Pia katika katika kitabu chako kimojawapo umesema kuna nyaraka nyeti zaidi ambazo familia ya Sykes haikukupa, vipi bado hawazitoi?
 
Kama vile mimi nilivyo na hamu kubwa sana Mzee Mohamed Saidi atakavyo tuletea habari za masheikh na maustaadh waliofanya juhudi ya kukomesha biashara ya utumwa kule Zanzibar!

Na ulishasikia Askofu aliyekemea hiyo biashara?
 
Shukrani, sasa nahitaji taarifa zaidi za yule ambaye unasema walikuwa wanamuita "Benki", shajara zake zinapatikana wapi?

Halafu katika sura iliyoandikwa na mjukuu wa Mzee Sykes, ameweka wosia unaoonesha kuwa Mzee alitaka mtoto mmojawapo kati ya watoto wake watatu awe mfanyabiashara, nahitaji taarifa za huyo jamaa, nafanya utafiti kuhusu mafanikio ya kibiashara ya Watanganyika wa enzi hizo, je yaliishia nchini tu au yalivuka hadi ng'ambo?

Pia katika katika kitabu chako kimojawapo umesema kuna nyaraka nyeti zaidi ambazo familia ya Sykes haikukupa, vipi bado hawazitoi?

Udadisi,
Aliyepewa jina la utani (nickname) ''The Bank'' alikuwa Waziri Dossa Aziz lakini akijulikana zaidi kwa jina la Dossa.
Sina taarifa ya nyaraka zake.

Kleist alisema kuwa huwezi kutajirika katika kazi ya kuajiriwa.
Njia nzuri ya kuboresha maisha ni kufanya kazi na kuwa na biashara.

Katika wanae aliyefanya biashara ni Ally Sykes.

Msome hapa chini Ally Sykes akizungumza na mimi takriban miaka 20 iliyopita:

''We (with Peter Colmore) represented, promoted, and were consultants to Coca
Cola (East Africa) Ltd; Cooper Motors Corporation Ltd; Allsopp (EA) Ltd; Shell
Company of East Africa Ltd, Aspro Nicholas Ltd; Gailey and Roberts Ltd; Bata
Shoes Company Ltd; Kenya Broadcasting Service, Cotton Lint and Seed Marketing
Board, Raleigh Industries of East Africa Ltd; we were also commercial representative
in Kenya for Tanganyika Broadcasting Corporation.

The head office of this massive sales promotion venture was in Nairobi, Delamere
Avenue, now Kenyatta Avenue. Peter Colmore built some products into household
names in East Africa.

The best musicians East Africa had ever known were used to promote these products.

After independence and following the Arusha Declaration of 1967 which intended to
turn Tanzania into a socialist state the government passed the Leadership Code.

The code prohibited civil servants to engage in business, draw more than one salary;
own property or hold shares in a private company.

The code even prevented a civil servant from renting out property.

I had a feeling that the Arusha Declaration would be the turning point in my career
and business relationship with Colmore because as a civil servant I had property and
was an established entrepreneur.

In 1971 the government passed the Acquisition of Building Act.

By a stroke of a pen all buildings with the value of more than a hundred thousand
became government property.

We lost some property through nationalisation including the office, which at that time was
owned by Colmore.

The moral behind all this was Nyerere's belief that Arusha Declaration
and nationalisation would establish an agrarian society in Tanzania.

Colmore who could not stand the political climate wound up sold the company to me and
returned to Nairobi.''

Kuhusu nyaraka nyeti kama unavyoziita kwa uhakika ni shajara (diaries) za Abdu Sykes alizokuwa
akiandika katika uhai wake.

Hizi ingawa niliziona kwa macho yangu lakini hawakuniruhusu kuzisoma na nyingi zimeandikwa
kwa hati mkato.
 
alikuwa ni The Bank Dossa Aziz aliefungua kinywa chake na kumwambia Nyerere aache kuvaa makaptula yake, maana sasa ameingia TANU hivyo atakutana na watu wazima na hilo sio vazi la watu timamu.

Ndipo Dossa alichukua baadhi ya Suruali zake na kumpa Nyerere...lakini waapi, haikusaidia kwani Still Nyerere alikuwa anazikunja Suruali hizo...
 
Na ulishasikia Askofu aliyekemea hiyo biashara?
Bi mkubwa, hakuna hata askofu aliyewahi kukemea biashara hiyo, mbaya zaidi kule "west Africa" wakati wa "Trans Atlantic Slave" baadhi yao walisafiri na wafanyabishara haramu ya watumwa na kuwabatiza baadhi ya watumwa hao. Je, unajua kuwa baadhi ya masheikh na maustaadh kule Zanzibar walikuwa wanawamiliki na kuwauza watumwa?
 
alikuwa ni The Bank Dossa Aziz aliefungua kinywa chake na kumwambia Nyerere aache kuvaa makaptula yake, maana sasa ameingia TANU hivyo atakutana na watu wazima na hilo sio vazi la watu timamu.

Ndipo Dossa alichukua baadhi ya Suruali zake na kumpa Nyerere...lakini waapi, haikusaidia kwani Still Nyerere alikuwa anazikunja Suruali hizo...
Ustaadh Mohamed Saidi ebu tupe darsa, maneno haya yana ukweli kiasi gani? Kwanini Dossa alimpa Nyerere suruali badala ya kumpa musuli?
 
Sijawahi kucheka kama nilivyocheka leo! Duh, Mohamed Said! Eti anadhani itapatikana faida kwa kumkumbuka Dr. Vedasto Kyaruzi daktari mpigania uhuru kwa kutuletea makala iliyojaa ngano ambazo kama kawaida si zaidi ya porojo zilizotawaliwa na histohisia. Hadithi, hadithi! uongo njoo utamu kolea! Nitarudi.
Wewe endelea kucheka Watanzania wanafyonza Ilm.
 
Back
Top Bottom