DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

Katika kupima kipaji cha mtu watu hawaangalii kipaji chako bali watakuhukumu kwa matokeo yake unayatoa wengi wana vipaji lakini matokeo zero unadhani messi au ronaldo wana uwezo mkubwa kushinda gaucho na zidane hapana ila messi na ronaldo wameleta matokeo ambayo ni magumu kutokea that's why wanaonekana bora kwa kizazi hiki
Hivyo current form ya matokeo ya miaka hivi karibuni kwa watu huru inambeba zaidi Sisqo kushinda Noel hivyo Noel kama ana kipaji kushinda Sisqo athibitishe katika mashindano makubwa kwa kuwa bingwa lakini sio huko vijiweni kwenu mkiwa mnawaangalia Sisqo ni top kwa now kwa watu huru
 
na sisi tulio mbali na hao mabingwa tunaomba tuzishuhudie mechi zao za mara kwa mara.

itapendeza zikiwa zinapigwa online. ili online kusiwe na hila, kuwekwe limit ya dakika ambazo zitambana mshindani kufanya udanganyifu.

itanoga sana
 
EXCLUSIVE


Timu: Cr7 Vs Dogo Ally( confirmed )


Mdhamini: Shabani Sululu


Zawadi: 50,000/= (winner 40k na Looser 10k )


Lini: Jumanne tarehe 10 January 2023 Saa tisa Alasiri



Wapi: Kinondoni Manyanya


Mfumo: Ngoma 24 - Omary John + tege kumi za mzee Ngapu


Mratibu: Mkorea (5000)


Kamisaa: Chande (5000)



Note: Hakutakuwa na mshindi wa pili ila kutakuwa na nauli ya shilingi elf 10 kwa atakaefungwa



Boss Shabani ameamua kumkagua Cr7 kwa Dogo Ally ikumbukwe tu Cr7 ndie anaeng'aa kwa sasa baada ya kumzuia mkulima
 
Noel naskia ni mwalimu huko Njombe
 
na sisi tulio mbali na hao mabingwa tunaomba tuzishuhudie mechi zao za mara kwa mara.

itapendeza zikiwa zinapigwa online. ili online kusiwe na hila, kuwekwe limit ya dakika ambazo zitambana mshindani kufanya udanganyifu.

itanoga sana
Tatizo madraft yao yanachukua muda mrefu yani kama ni streaming basi ni masaa kibao
 
Wakicheza kawaida hawafungani

OKay....

wakicheza kawaida hawafungani...

kwa hiyo hizo kopi ambazo unalazimishwa kucheza zinamweka kwenye disadvantage nani, bingwa au underdog ???

Kama zinamweka bingwa kwenye disadvantage ili angalau tukaribie karibie nguvu sawa that should be my choice, kwa nini unanilazimisha ??? Unaogopa nini ? Haimuweki bingwa pabaya, lakini nikikataa kucheza hiyo copy na bingwa naye hachezi. Kwa nini ? Kuna jambo.

Au, kama hiyo kopi unayolazimisha tucheze inaniweka mimi kibonde kwenye disadvantage basi the game is rigged, it is a fraud. Ni karata tatu

Hatupaswi kulazimishwa kutumia kopi anazotaka bingwa.
 
Ile game ya jana ilichezwa kihuni. Kuna muda nilifungua Dalmax. Kwanza Cr7 kila baada ya game lazima aondoke. Game za online si za kuwekea watu pesa sababu uhuni ni mwingi. Hata mimi nisingefungwa. Dalmax linakuelekeza kila kete unayotakiwa kucheza.
 
Kuna tofauti kati ya Bingwa na kujua

Mtu anayejua draft ni yule ambaye anajua namna ya kulicheza kwa kufuata sheria na sio lazima awe bingwa

Ukiitwa Bingwa tafsiri yake ni complete package unaelewa sheria na mbinu za kiuchezaji

Na ndio wakikutana mabingwa wanacheza kete zote zile za mbele kwa maana ya kwamba kama wewe ulikuwa ni aina ya wale wachezaji unayejua copy ya major peke yake ukianishiwa pembeni lazima upotee

Mabingwa wanatakiwa wajue hiyo michezo yote

Wanakuja kufungana kwa kuzidiana tricks na hesabu kiasi thats why unaona leo kashinda huyu kesho huyu aliyefunhwa ana advantage ya kumfunga mpinzani wake kwasbabu anakuwa ameenda kuangalia wapi alifungiwa na mbinu gani ya kumshinda mpinzani wake
 
Kwa jinsi nilivyomuona Ronaldo jana akicheza na Mkulima

Nasema huyo Sisco sioni atapotokea kwenye hiyo mechi, kwasababu nimeshuhudia magemu mengi ambayo Mkulima alikuwa akitafuta sare kujinusuru

Wakati alivyocheza na Sisco hakupata ugumu huo
Hata mm jana nimeshangaa mkulima alikuwa anasakwa yaan lile lilikuwa linaitwa sako la nyani ngedere na kima huponi yaan
 
Ile game ya jana ilichezwa kihuni. Kuna muda nilifungua Dalmax. Kwanza Cr7 kila baada ya game lazima aondoke. Game za online si za kuwekea watu pesa sababu uhuni ni mwingi. Hata mimi nisingefungwa. Dalmax linakuelekeza kila kete unayotakiwa kucheza.
Dalmax program ya kawaida ukienda kwa mkulima anakupiga kama mbwa unadhani hao wakina sisqo au Noel hawaijui dalmax na pia nakuhakikishia hata yule Noel au CR7 AU SISQO anakupiga na dalmax yako mfano dalmax akianza major asilimia 100 anafungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…