DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

Dogo Sisco na kundi lake Walikuwa na Mpango wakubali Mechi ila ichezwe Jumanne ili Cr7 asifanye zoezi Kidogo la kushtua ila dogo Mwenyewe amegoma na kusema anahitaji angalau Siku 4 za kumkagua Cr7 Maana hajacheza nae Muda na hajui huko alikokuwa alikuwa anatengeneza ngoma au la!
 
TAARIFA KUTOKA KWA MKULIMA [emoji89]

KUELEKEA MECHI YA NDULI VS MKULIMA



_*Barua ya wazi kwa RAISI WA WATU HURU




Tunashukuru sana kwa mpambano uliotuwekea na NDUGU NDULI NDULIMA... Hakika litakuwa pambano lenye Mvuto saana.



Kitendo cha sisi kupata Pesa ya BANDO tu baada ya ushindi kinatunyong'onyesha sana! Kwa vigezo vifuatavyo.....!!!!

1} Mkataba tunaotoa ni Mgumu sana, sawa na Mkataba wa kuvua Mamba.[emoji17]

2} Lazima tutumie nguvu kubwa kufanya Utafiti wa michezo mipya ili kumfunga mchezaji Mkubwa kama Nduli, Sisco, Noel, Mamba au Ronaldo

3} Tunatumia mda mwingi kucheza hizi game takribani masaa 6

4} It deteriorates the Quality of our Brand



HIVYO TUNAOMBA ULIANGALIE HILI KWA MTAZAMO WA KIPEKEE
 
Dalmax program ya kawaida ukienda kwa mkulima anakupiga kama mbwa unadhani hao wakina sisqo au Noel hawaijui dalmax na pia nakuhakikishia hata yule Noel au CR7 AU SISQO anakupiga na dalmax yako mfano dalmax akianza major asilimia 100 anafungwa
Dalmax kawaida huku mnakolifunga, nenda kule kwenye game analysis uone kete zake. Nilikuwa nafuatilia game yao kwa kuangalia suggestions za Dalmax, walikuwa wanatembea mulemule. Hapa bongo hakuna mtu wa kumfunga anayetumia game analysis. Ni sare au kufungwa.
 
Mabingwa huko mbele kete tatu za mwanzo hauchezi kama unavyotaka. Kuna makubaliano kuwa kete tatu za mwanzo zitakuwaje kisha wanaendelea.
 
Chukua dalmax nenda kacheze na mkulima uone
 
Si ndiyo wote walikuwa wanatumia jana na Cr7. Unafikiri alikuwa anatokatoka kwa ajili gani. Ukicheza game moja lazima uiseti upya. Walipata sare zote sababu wote walikuwa wanaitumia.
inaonekana ww mgeni kabisa dalmax hafui dafu nakupa offer kama upo dar es salam njoo manyanya jumanne na tunakupa mchezo utumie dalmax halafu ucheze na mabingwa uone
 
playok unatumia account gani nije nikufunge?
Wewe ndiyo mkulima mimi nikicheza nitacheza na mkulima tu ...wengine mtanipotezea muda wangu bure chukua hata dalmax ucheze nalo michezo 10 ukiweza kulifunga 7 bila ya kurudisha kete nyumq basi unaweza kunishawishi nikutafute live na pesa nitaweka kwa upande wangu tu siitaji yako nitakupa michezo kumi ukifanikiwa kunifunga 4 kati ya kumi nakulipa pesa
 
Tamko rasmi lini bado
 
upo mkoa gani kwanza maana kila mkoa kuna mabingwa tunawajua
 
Timu: Cr7 Vs Dogo Ally( confirmed )

Zawadi: 50,000/= (winner 40k na Looser 10k )

Mratibu: Mkorea (5000)

Kamisaa: Chande (5000)
Wakuu....

Kuna kitu kinani-dissappoint hapa.

Mbona hizi zawadi naona kama ni ndogo sana kulinganisha na brand za hawa mabingwa?

Yaani bingwa wa draft Tanzania nzima anacheza game 24 mfululizo (zingine usiku wa manane), anatumia akili nyingi, halafu akishinda anaambulia 40,000 tu?
 
Hio manyanya saa 9 na pia inategemea na ukubwa wa mechi
 
Tatizo madraft yao yanachukua muda mrefu yani kama ni streaming basi ni masaa kibao
hiyo ndiyo changamoto, michezo 24 inachukua muda mrefu.

lakini mbona michezo mingine inachukua muda mrefu na bado watazamaji wanabaki kuangalia wanaona burudani. na sisi watazamaji wa mchezo wa draft tunaona sawa tu.
 
inaonekana ww mgeni kabisa dalmax hafui dafu nakupa offer kama upo dar es salam njoo manyanya jumanne na tunakupa mchezo utumie dalmax halafu ucheze na mabingwa uone
Dalmax yule wa kucheza naye hata mimi humfunga. Hapa nazungumza wewe tumia kichwa halafu mimi nitumie game analysis ya Dalmax. Huingizi goli. Hata huyo Mkulima na Ronaldo jana ndiyo waliyokuwa wanatumia. Ile inakuonyesha kabisa hiyo kete ina nguvu kiasi gani kwa namba. Positive na negative. Mtu yeyote mwenye idea ya bao hawezi kufungwa akitumia Dalmax.
 
Umenichekesha na kunikumbusha kitu. Yaani niliona ukimfunga bingwa wanaitana mabingwa wachache wanajifungia ndani Ili wengine msione wanalipanga draft upya na kulicheza kuanzia mwanzo hadi pale kwenye kete iliyotoa ushindi kwa mpinzani na wanazama kufikiri na kutafuta kete mbadala ya kujinusuru na droo au kushinda hii Ina maana huwezi kumfunga bingwa wa manyanyà Draft moja mara Mbili! Ukimfunga Leo Hilo draft Kesho ukija kichwa kichwa na kopi yako hiyo unapasuka!

Matula Tula wa Manyanya na boss wao Mangwelele si wa polepole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…