DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

DRAFT ONLINE: Sisco vs Mkulima

Huyo mkulima ni undisputed player hivyo mabingwa wa draft tanzania hakuna anaweza kumfunga hivyo yeye anakupa sare michezo 24 maana yake katika michezo iyo asipokufunga wewe ni bingwa
Kwa nini game 24 ? Ukishatoa sare mara 10 your head is fried, unafungwa kwa kuchoka akili, kwa hiyo hapo mnapimana stamina, na sio tena uwezo wenu akili zikiwa fresh and zippy. Kwa nini hili hawalioni?
 
Kitambo sana hii mambo sijafatilia. Kifupi ni kwamba wakali wa draft wapo wengi. Na ikipigwa mbungi ni makosa madogo sana yanapelekea mtu kufungwa.
Kati ya mabingwa wa draft nimebahatika kumwona Cr7, wa sinza, Mangwelele, Marehemu Jumah Mchafu na mkali wa vipande Gadzilla.

Japo sijacheza muda mrefu sana ila mimi kete najua kusukuma sana tu.
Huyu Juma Mchafu ni yule wa Mwanza?
 
Ujue mimi siwaelewi elewi unapaswa upate sare ngapi umshinde
Eti sare 24! RIdiculous.

Baada ya sare 10 kichwa kishakuwa deep fried. Yeye kakariki kopi za yeye kutoka droo, humfungi na haumizi kichwa. Ukichoka kichwa anakung' oa kama Alli alivyompiga Foreman walipokuja Congo.

Halafu droo zenyewe sasa, nishaona kijiwe cha mabingwa Buguruni Chama, wewe unaepewa mteremko wa kutafuta droo wanakuanzishia kete yako ya kwanza, you have no choice japo zamu ni yako. Kwa hiyo mnacheza kopi ambayo YEYE BINGWA ndo kai master. So crazy yani.
 
Sisco anasema Simu iliisha chaji akatumia ya mtu

Matokeo ALIPIGWA 2-0

Akakimbia

Kundi la WATU HURU lenye wachezaji Kama NDULI ,NOEL ,SISCO na mafundi wengine wa Draft TZ

Wanaanda marudiano na MKULIMA


PIA LEO KUTAKUWA NA MTANANGE

WA NOEL BINGWA KUTOKA NJOMBE NA MKULIMA

View attachment 2467722
Hii Tanzania draughts naipatJe
 
Nimefurahi nilitaka kuuliza sare 24 inakuaje..pia fafanuzi kidogo kama hutojali tege,john na Omary ni nini
Omari John hawa ndio waanzilishi walipenda kucheza michezo yote ya mwanzo kwa kucheza kila kete ambayo ndio inatoa michezo 7 kwa kuwaenzi tunasema tunacheza omari John ok
Na tege ni mchezo wa kumuanzisha mpinzani ambapo yeye anaamini unacheza kete dhaifu
 
Omari John hawa ndio waanzilishi walipenda kucheza michezo yote ya mwanzo kwa kucheza kila kete ambayo ndio inatoa michezo 7 kwa kuwaenzi tunasema tunacheza omari John ok
Na tege ni mchezo wa kumuanzisha mpinzani ambapo yeye anaamini unacheza kete dhaifu
mkulima na noel. babaaskofu matokeo yalikuaje?
 
Back
Top Bottom