Inakuwa hivi, kuna program za computer zimemezeshwa kila copy ya draft na mbinu, hakuna kipya utachofanya ambacho haijui, kwa kifupi ni kwamba hakuna mwanadamu anaeweza kushinda, na hata zikicheza computer 2 ni droo.
mfano wa hizi program ni kama chinook iliyoweza kuzimeza kopi zote za kushinda na kutoa sare. HAIFUNGIKI !! achana na hizo games za kwenye simu, hazifikii hata theluthi ya kilichomo kwenye chinook.
Kwa mtu anaecheza mtandaoni anaweza kuzitumia program hizo kujimwambafai, upande moja anakuwa na laptop yenye hiyo program upande wa pili ndio anakuwa na simu anayochezea draft mtandaoni.
Mpinzani akisukuma kete, nae anaigiliza hio move anaiweka kwenye program ya computer, computer ikicheza yeye anaigilizia anacheza hivyo hivyo kwenye simu yake mtandaoni,
nimestuka sana pale imefikia hatua huyo mkulima hataki kajiamini kiasi kuviomba vikundi vya draft viwe vinahangia kwa mpigo wawe wanaunganisha vichwa, yawezekana ni mtaalam ila kwenye hili ndipo nilipomtilia shaka huenda ana kichwa kama computer ama anatumia program ya computer.
Wanaocheza drafti yawezekana wanachojua zaidi ni drafti ila wasisahau kwamba teknolojua imekuwa kubwa sana, wawe makini !! wao wanaweza kudhani kwa kuwa anaecheza ni mtu basi wanamwamini kumbe mtu wanaecheza nae anaigilizia kwenye computer.
Nasikia kuna sponsor analipa pesa... Awe makini.