Drafti: Ronaldo kaisha tangu arudi kutoka ughaibuni, kesho atacheza na Simba Dom kwa aibu atakayoipata hatokaa asahau

Drafti: Ronaldo kaisha tangu arudi kutoka ughaibuni, kesho atacheza na Simba Dom kwa aibu atakayoipata hatokaa asahau

Huu mchezo unapoteza muda mwingi sana wa kazi:
mtu anashinda draftini siku nzima na wengine Hadi wanakesha kwa kusukuma kete tu:
Ni mchezo wa kuhamasisha uvivu, kupoteza nguvu kazi na uzalishaji mali:
Mchezo ambayo haujawahi kumtajirisha Kijana na hautawahi:
Wachezaji wengi wanaishia kukosa ajira rasmi na kuishia kufa katika umaskini:
Amkeni vijana hamna muda wa kupoteza kwenye mchezo usio na faida kwa maendeleo yenu na ya taifa kwa ujumla wake, mchezo wa Drafti:
Huu mchezo ni ajira tosha kuliko unavyofikiri.
 
nikienda hapo nmevaa AI glasses si hakuna atakaenishinda?

Checkers ilishakuwa solved kitambo, ukikariri moves unamla kila mtu, tukutane kwenye chess, checkers waachie watoto wa mama
Watu wanambonda Dalmax , farasi nk.
 
Huu mchezo ni ajira tosha kuliko unavyofikiri.
Nitajie mchezaji mmoja anaye endesha maisha yake kwa kutegemea mchezo wa Drafti tu:
Na nieleze anayaendeshaje maisha yake na familia yake kwa kutegemea mchezo wa Drafti:
Huo mchezo unapoteza muda mwingi sana kwa vijana na hauna faida yoyote:
Dunia ya Leo yenye fulsa nyingi za kazi, sio ya kukaa kwenye benchi (kijiweni) siku nzima na kusukuma kete:
Ukienda katika vijiwe vya Drafti vijana wengi wamechoka kwa kuchosha akili na kushindwa kutafuta pesa:
 
kuna wakuitwa Mkulima, alitisha sana kwenye playok dot com, sijui yuko wapi
 
Hii uzi imekaa poa sana mzee . Nadhani nikipiga tizi vizuri angalau majina 20 hapo natia mguu . Kwa dar kijiwe ni wapi weekend nije kupiga raketi?
 
Back
Top Bottom