Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Hiyo Ndege Inahusu Nini Wananchi Walio Wengi ? Kwanza Hawana Habari Ya Uwepo Wake, Na Hata Kama Ipo Kuipanda Ni Miujuza. Hiyo Ndege Inahusu Daraja Fulani La Watu Wachache Na Si Wananchi Wote.
 
Kunyanyua hilo dege from Dar na kutua KIA au MWZ ni matumizi mabaya ya resources; inabidi likageuzie South Sudan kuitafuta runway. Dude ambalo uwezo wake wa "wese" ni lita 126,210 yaani zile semi-trailer tanker za mafuta zinamimina mle 3 na bado halijai. Sio mchezo.
Ndio maana wakati linatua lilienda mbali sana tukasubiri litue wapi wakati tumeliona limetupita hapa juu kipawa kumbe ngoma ilienda karibu na mafia ndio likageuza kuitafuta run way
 
Naomba kuuliza hilo dude lina bima ? Mfano likianguka Leo je tutalipwa jipya?
 
Tatizo liko wapi si zinakuwa zimenunuliwa Na shirika limeingiza pesa? Chadema magwanda ya chadema Huwa mnawauzia CCM? Si mnajiuzia wenyewe?
Lakini si Huwa mumeuza? Very poor argument
Achana nao hao!
Kwishney habari yao!
 
Mmmmh imejaaje wakati ukifanya booking huambiwi ni ndege ipi itatumika na ukiwauliza hawakujibu na wamesema inaanza mwezi wa nane hapo siku ya safari unakuta ni bombadia ndo unapanda na gharama za kurudishiwa nauli Wanakata asilimia karibia 90.
Fanya hivi waulize hao agents wao ni flight ipi itatumika? Maana kuna route zaidi ya moja kwenye booking sasa flight ipi itatumika kwenye route ipi?
 
Hamuwezi kuendesha hili shirika kwa faida kwa kutegemea mauzo ya ticket tu hasa tukianza route za kimataifa.

Gharama za kuhudumia ndege,mafuta, mishahara ya wafanyakazi, chakula kwa abiria, hoteli kwa abiria panapotokea matatizo, charge za kupaki/kutua katika viwanja vya ndege,kulipa mainjinia wa kuihudumia, n.k kamwe haviwezi kubebwa na mauzo ya ticket tu.

Wanaofanikiwa katika hii biashara hawategemei mauzo ya ticket tu vinginevyo mashirika mengi yasingekuwa yanatangaza hasara.

Pia, eleweni tu Bombardier zilizokuwa zinatumia hiyo route sasa zinakosa abiria na ni hasara kuzipaki kwa huo mwezi mzima.

Wafanye hivi. Deploy one bombardier to serve lake zone. Dreamliner inamwaga abiria Mwanza Bombadier inawapeleka Bukoba, Kigoma, Musoma. Na shinyanga
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa chadema
Adui wako ni chadema tu...mtanyoka tu ngoja liingize hasara na kujaa linajaza.
Tuliwaambia mradi wa mabasi haufai una hasara mlikataa hivihivi ikawa chadema chadema yako wapi kituo kinajengwa kwenye maji ccm buana. Ndege hizo haziwezi kuinua shirika, jifunze kwa wenzio
 
TRA watakapokuwa wabakufata ofisini kwako pia usiwakimbie mpe Hongera Rais Magufuli, maana hilo dude linaingiza hasara, na ili kufidia itabid mwananch wa chini Aumie,

Kwahiyo sitarajii kuona Ukileta uzi humu kuwa TRA inakubana na kodi zimeongezeka
Aiseeee""" ndio yale Yale ya wasanii na makampuni '' kupeleka pesa BASATA
 
watu ukiwaambia kuwa hizi ndege zinajaa hawakubali sijui wanatakaje?

hivi katika tanzania yenye watu zaidi ya millioni 50 hakuna watu wenye uhitaji wa kupanda ndege 3000 kwa siku? hii ni hesabu rahisi tu wakati ndege zote zikijaza za shirika hilo hawafiki watu 1000?

tumekazana kuwa watapata wapi wateja kweli? yaani unazaa mtoto lakini sala zako unaomba mtoto afe haraka do! sijatembea na kuvuka mpaka lakini tujifikirie upya kwa maslahi ya taifa vinginevyo tusema kuwa tunayopinga tuna furahisha ubongo kupunza stress zetu.
Siku zote uzinduzi hujaza watu hasa wenye shauku ya kujionea tukio lakini safari inapopamba moto mnaanza kupungua mwisho mtafika wachache.
 
Back
Top Bottom