Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Dreamliner yaanza safari kwa kishindo: Tiketi za Mwanza na KLM tayari zimeisha mpaka tarehe 18 Agosti 2018

Hamuwezi kuendesha hili shirika kwa faida kwa kutegemea mauzo ya ticket tu hasa tukianza route za kimataifa.

Gharama za kuhudumia ndege,mafuta, mishahara ya wafanyakazi, chakula kwa abiria, hoteli kwa abiria panapotokea matatizo, charge za kupaki/kutua katika viwanja vya ndege,kulipa mainjinia wa kuihudumia, n.k kamwe haviwezi kubebwa na mauzo ya ticket tu.

Wanaofanikiwa katika hii biashara hawategemei mauzo ya ticket tu vinginevyo mashirika mengi yasingekuwa yanatangaza hasara.

Pia, eleweni tu Bombardier zilizokuwa zinatumia hiyo route sasa zinakosa abiria na ni hasara kuzipaki kwa huo mwezi mzima.
Mkuu, Umewaza nje ya box, kuna haja ya kujiuliza kwenye hili.
 
......au Tanesco watafunga waya za umeme kwenye hiyo ndege iwe inaruka nazo angani? Aagh..., huyo jamaa .....mno!
Kwa staili ya uulizaji swali, unategemea upate majibu mujarabu kweli...! Jambo inawezekana hulijui...na utaka kujua...unachanganya humo humo, kebehi, dharau, majivuno nakadhalika kwenye swali!!! Hapa unategemea nini, kama siyo 'kuchafua' hali ya hewa jukwaani.

Hivi, Mkuu, ni kweli umeshindwa kuuliza swali kirahisi na kwa staha juu ya suala hili na ukapewa jibu sahihi na la kina? Mfano, ungeweza kuuliza hivi" Ebu nifafanulie kwa kina namna ndege hii inavyotumia mafuta kidogo na huku umeme mwingi, na chanzo cha umeme huo ni kipi !?" Kwa vyovyote vile wataalamu wange'tiririka' majibu ya kutosha na ya kina. Ila kwa staili ya uulizaji swali lako...hakuna mtaalamu atajitokeza. Au umeuliza swali hilo makusudi ili watu hapa jukwaani wasifaidi elimu hiyo ya namna ndege hii inavyotumia nishati ya umeme na mafuta kwa pamoja...!? Maana, fitina zina sura nyingi siku hizi.
 
Nasubiri ripoti ya CAG ya 2018/19 nione kama hilo lindege litakuwa limeleta faida au harassa.
Nakunbuka MV Dar esalaam ilivyokuwa inasifiwa,mwishowe wakapewa Jeshi ili yasijulikane zaidi!!
 
Sasa mnatoa hongera za nini?hyo ndege imekuja iende India,China au Thailand kwa kuanzia,sasa kama ikijaza hivyohivyo safari zake za kwanza za Mumbai ndio nitasifia,sasa natunza maneno.
 
Kwa staili ya uulizaji swali, unategemea upate majibu mujarabu kweli...! Jambo inawezekana hulijui...na utaka kujua...unachanganya humo humo, kebehi, dharau, majivuno nakadhalika kwenye swali!!! Hapa unategemea nini, kama siyo 'kuchafua' hali ya hewa jukwaani.

Hivi, Mkuu, ni kweli umeshindwa kuuliza swali kirahisi na kwa staha juu ya suala hili na ukapewa jibu sahihi na la kina? Mfano, ungeweza kuuliza hivi" Ebu nifafanulie kwa kina namna ndege hii inavyotumia mafuta kidogo na huku umeme mwingi, na chanzo cha umeme huo ni kipi !?" Kwa vyovyote vile wataalamu wange'tiririka' majibu ya kutosha na ya kina. Ila kwa staili ya uulizaji swali lako...hakuna mtaalamu atajitokeza. Au umeuliza swali hilo makusudi ili watu hapa jukwaani wasifaidi elimu hiyo ya namna ndege hii inavyotumia nishati ya umeme na mafuta kwa pamoja...!? Maana, fitina zina sura nyingi siku hizi.
Hatari kubwa kwa kilaza ni kutojua kwamba ni kilaza, hivyo ni lazima azodolewe ipasavyo ili siku nyingine atafakari kabla ya kuropoka. Sasa nikuulize wewe swali,
1.) zile engine za kwenye ndege umeshawahi kusikia zinatumia umeme?
2.) Umeme unaotumika kwenye ndege, huzalishwa na nini ukiacha APU (auxilliary power unit) na engine zinazotumia mafuta?
 
Tiketi bei karibu na bure, ndio wanavyoitangaza! Mlalahoi atajazilia hasara ya uendeshaji! Kazi ipo, hapa kazi tu.
 
Ticket zaweza kununuliwa zote na kusiwe na uhalisia wowote
Kwa Serikali ya sarakasi kama hii hakuna cha ajabu kutoa hela na kutyma watu wanunue tiketi ili zionekane zimekwisha
Just thinking loudly ...
 
Kunyanyua hilo dege from Dar na kutua KIA au MWZ ni matumizi mabaya ya resources; inabidi likageuzie South Sudan kuitafuta runway. Dude ambalo uwezo wake wa "wese" ni lita 126,210 yaani zile semi-trailer tanker za mafuta zinamimina mle 3 na bado halijai. Sio mchezo.
Mkuu Dudus! Nafikiri tunakubaliana kwamba kurusha Dreamliner kwenda Mwanza "it does not make any sense". Hebu fikiria Capt kabla hajamaliza take off checklist anaanza kuaanda landing checklist. Halafu "promotional fares" ni hasara kwa shirika. Tujifunze kutoka ATC ya zamani. Walikuwa na Boeing 737 ilikuwa inatoka Dar kwenda KIA kupitia Zanzibar. Matokeo yake Boeing ilikuwa inaruka hardly 5000m inaanza kutua Zanzibar ambayo ni hasara kwa shirika.
Kama tuna nia ya dhati DAR - BEIJING ROUTE inaweza kulipa kidogo kwa kuwa "middle class" ya China inakuwa haraka sana na Serikali hao inawahimiza wananchi wake kwenda kutalii nje ya China.
 
Kama huelewi kukaa kimya nalo jibu
 
Wamesema hii ni kwa mwezi mmoja tu, wamelenga kuhudumia safari za mbali ila hiki ni kipindi cha cabin crew kuzoea mifumo ya ndege na testing ndogo ndogo. Mabasi ya mwendo kasi yalianza kwa safari za bure, lengo likiwa ni kama hili, SGR Mombasa-Nairobi nayenyewe ilianza kwa trip za bure. Unaeza usipende ununuzi wa ndege ila zilisha nunuliwa kwa pesa yetu kuombea mabaya haisaidii. Hii ni kama kumroga mtoto wako kisa kafanana na mama yake zaidi.
 
Dude lazima nipande hili, nishaanza kudunduliza.
 
Ndege mpya ya ATCL ya Dreamliner, inatarajiwa kuanza safari zake za tarehe 29 Julai 2018 kwenda Mwanza na KLM kwa kishindo baada ya tiketi kuisha mpaka za kufikia tarehe 18 Agosti 2018. Hongera sana Rais Magufuli kwa kufikiria madude kama haya.
View attachment 807780
Humo lazima mr misifa Zitto atakuwa wa kwanza kupanda ili apate la kupotosha
 
Mkuu Dudus! Nafikiri tunakubaliana kwamba kurusha Dreamliner kwenda Mwanza "it does not make any sense". Hebu fikiria Capt kabla hajamaliza take off checklist anaanza kuaanda landing checklist. Halafu "promotional fares" ni hasara kwa shirika. Tujifunze kutoka ATC ya zamani. Walikuwa na Boeing 737 ilikuwa inatoka Dar kwenda KIA kupitia Zanzibar. Matokeo yake Boeing ilikuwa inaruka hardly 5000m inaanza kutua Zanzibar ambayo ni hasara kwa shirika.
Kama tuna nia ya dhati DAR - BEIJING ROUTE inaweza kulipa kidogo kwa kuwa "middle class" ya China inakuwa haraka sana na Serikali hao inawahimiza wananchi wake kwenda kutalii nje ya China.
Imeshasemwa wazi kuwa, mipango ni kuifanya Dreamliner iende Guangzhou (China), Bangkok (Thailand) na Mumbai (India). Kuna mambo ya vibali, kujitangaza na logistics kwa ujumla. Ndiyo maana inaanza hapa Bongo Viwanja vya KIA na Mwanza.
 
Kinachonifikirisha ni runway ya mwanza na uwezo wa uwanja mwanza kuhandle abiria na ndege yenyewe kwa wakati mmoja.
Runway ya Mwanza ni nzuri sana na of course ndiyo ndefu kuliko runways zote hapa Tanzania.
IMG_4191.jpg

IMG_4192.jpg
 
Back
Top Bottom