Hamuwezi kuendesha hili shirika kwa faida kwa kutegemea mauzo ya ticket tu hasa tukianza route za kimataifa.
Gharama za kuhudumia ndege,mafuta, mishahara ya wafanyakazi, chakula kwa abiria, hoteli kwa abiria panapotokea matatizo, charge za kupaki/kutua katika viwanja vya ndege,kulipa mainjinia wa kuihudumia, n.k kamwe haviwezi kubebwa na mauzo ya ticket tu.
Wanaofanikiwa katika hii biashara hawategemei mauzo ya ticket tu vinginevyo mashirika mengi yasingekuwa yanatangaza hasara.
Pia, eleweni tu Bombardier zilizokuwa zinatumia hiyo route sasa zinakosa abiria na ni hasara kuzipaki kwa huo mwezi mzima.